Wazanzibari wacheza ngoma wasioijua – vyama vya siasa

Kupitia mkutano huu tunawaomba sana Wananchi wa Zanzibar, Unguja na Pemba na wale wanaoishi nje ya Visiwa hivi kuwa makini sana na kundi hili. Tunawatanabahisha akinamama wasikubali kutumiwa namna hiyo kwani hatua hiyo inaweza kuwaletea maafa. Dalili zinaonesha kuwa viongozi hao wako tayari kusababisha maafa na kuwatupia lawama watu wengine mradi tu waweze kufikia malengo yao. Ninawasihi sana wasicheze ngoma wasiyoijua. Sehemu nyengine duniani, vikundi kama hivi vimesababisha matokeo mabaya sana na kusababisha maafa makubwa. Kwa mfano Alkayda, Bokoharam kule Nigeria, na Al-Shabab kule Somalia. Hali za nchi zenye makundi haya zinasababisha kuondoka kwa hali ya usalama na amani.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAONI YA VYAMA VYA UPINZANI VYA TADEA, SAU, NLD NA AFP KUHUSU TUKIO LA VURUGU LILILOTOKEA HIVI KARIBUNI.
Ndugu waandishi wa habari na wananchi,
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana nanyi leo tukiwa katika hali ya uzima na afya. Pili napenda kushukuruni nyinyi kwa dhati kwa kukubali mualiko wetu na kuhudhuria kwa wingi kwenye mkutano wetu huu muhimu kwa wananchi wa Zanzibar hasa wale wenye kuitakia amani, utulivu na maendeleo nchi yetu hii.
Ndugu waandishi na wananchi,
Mtakumbuka kuwa Mei 26, mwaka huu, Zanzibar tulishuhudia tukio lisilo la kawaida la uvunjwaji wa amani lililofanywa na wenzetu ambao tumekuwa nao katika harakati mbali mbali za maendeleo. Wananchi hawa walisababisha maduka kuvunjwa, nyumba za ibada kuchomwa moto, mipira ya gari kuchomwa barabarani na kusababisha uharibifu wa miundo mbinu ambayo imejengwa na wageni waliokuwepo nchini. Watu walishindwa kufanya shughuli zao hasa maeneno ya mjini. Mitandao na vyombo vyote vya habari vilijaa habari mbaya kuhusu Zanzibar. kwa ufupi hali ilikuwa ni ya kutia aibu na mbaya sana kwa upande wetu hasa ukizingatia taswira nzuri iliyojengeka chini ya uongozi wa pamoja wa Serikali yetu. Tunahisi ushirikiano bado unahitajika sana katika kuweka hali ya utulivu sambamba na juhudi kubwa ambazo Serikali imekuwa ikizichukua. Kwa moyo safi kabisa, leo hii tumeamua kuitisha mkutano wetu huu maalum kuzungumzia hali halisi iliyojitokeza ndani ya nchi yetu.
Hatuna lengo la kulaumu upande wowote kutokana nay ale yaliyotokea, lakini ili kuepuka masuala yale yasitokee tena, ni vyema tukaangalia chanzo cha tukio lenyewe na mazingira yake ili baadae tuweze kuchukua hatua zinazofaa. Sote ni mashahidi kwamba sababu ya vurugu ni mihadhara na maandamano yaliyokuwa yakiendeshwa na Jumuiya ya Uamsho. Harakati za muda mrefu za Jumuiya hiyo ndizo hatimaye zilitoa mianya kwa watu wengine kuifikisha pabaya nchi yetu, ambayo mwelekeo wake kiuchumi ilishaanza kuonesha mafanikio makubwa. Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislam yenye kuzungumzia Uamsho ni Jumuiya ya Kidini kwa mujibu wa usajili wake.
Mimi binafsi nashangaa kuona kwamba pamoja na taratibu nzuri zilizowekwa za watu kutoa maoni yao kwa salama na amani, Jumuiya hii inahamasisha watu kufanya mambo kinyume na utaratibu uliowekwa. Harakati za Jumuiya hii zilianza kwenye Misikiti, kuingia mitaani na sasa viwanjani. Hii inaonesha dhahiri kwamba kundi hili lina agenda ya siri na lieltwa makusudi kuchafua hali ya siasa, amani na utulivu na nchi yetu, na dalili za vurugu zimeanza kuonekana.
Sisi kama wanasiasa tunafahamu kwamba jina la Jumuiya hii linatumika kama kivuli, lakini harakati hizi zinaendeshwa na viongozi ambao wamo ndani ya Serikali na ndani ya vyama vya siasa. Tunalaani vikali vitendo vya Jumuiya hii kwani havina maslahi ya nchi yetu. Aidha, tunafahamu kwamba Jumuiya hii inapata ufadhili wa kifedha kutoka nje ya nchi.
Ndugu Waandishi,
Ushahidi wa haya ninayoyazungumza hauhitaji taaluma kubwa kuweza kujua chama kipi cha siasa kinahusika. Harakati za Jumuiya hii zinaendeshwa kwenye maeneo na wafuasi wa Chama hicho ninachokizungumza. Lakini hata viongozi wake wanashindwa kuzilaani hadharani harakati za Jumuiya hii, licha ya athari zilizojitokeza za kuharibu vibaya jina na sifa ya visiwa hivi, vinavyoendelea kujijengea umaarufu katika maendeleo. Nchi nyingi zimevutiwa sana na hatua zinazochukuliwa na nchi yetu katika kuleta maendeleo.
Kupitia mkutano huu tunawaomba sana Wananchi wa Zanzibar, Unguja na Pemba na wale wanaoishi nje ya Visiwa hivi kuwa makini sana na kundi hili. Tunawatanabahisha akinamama wasikubali kutumiwa namna hiyo kwani hatua hiyo inaweza kuwaletea maafa. Dalili zinaonesha kuwa viongozi hao wako tayari kusababisha maafa na kuwatupia lawama watu wengine mradi tu waweze kufikia malengo yao. Ninawasihi sana wasicheze ngoma wasiyoijua. Sehemu nyengine duniani, vikundi kama hivi vimesababisha matokeo mabaya sana na kusababisha maafa makubwa. Kwa mfano Alkayda, Bokoharam kule Nigeria, na Al-Shabab kule Somalia. Hali za nchi zenye makundi haya zinasababisha kuondoka kwa hali ya usalama na amani.
Ndugu Waandishi wa Habari na Wananchi,
Tumepata taarifa kuwa kundi jengine la wananchi wa Zanzibar linalopendelea Muungano tayari linaanzisha harakati dhidi ya wale wanaoupinga Muungano, wakidai kuwa udongo uliochanganywa katika kuunganisha nchi mbili hizi ulitoka Unguja na Tanganyika na sio Pemba. Kwa msingi huo basi wananchi wa Pemba hawahusiki na Muungano, kundi hilo linadai kuwa wasiotaka Muungano ni Wazanzibari kutoka kisiwa cha Pemba. Kutokana na sababu hizo, kundi hilo linawaomba wasioutaka Muungano waondoke Unguja kwa hiyari yao warudi kwao walikotoka.
Ndugu Waandishi wa Habari,
Hizi ni athari za ubaguzi na kwa kweli ni hatari kwa hatma ya nchi yetu. Tunapaswa tukumbuke kuwa Zanzibar kwa muda mrefu tulikuwa tumefarikiana kwa sababu za kisiasa. Mungu ametujaalia miaka miwili iliyopita tumekaa pamoja na tumeondosha tofauti zetu na matunda yake yameonekana kwa kipindi kifupi sana katika kuinua pato letu la Taifa sote tumeshuhudia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta ya Kilimo na hasa Karafuu na utalii nchini.
Taarifa za uchumi zinaonesha kuwa tumepata mafanikio makubwa ya kukuza uchumi wetu ndani ya kipindi kifupi. Kwa mujibu wa bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2012/2013, pato la mtu mmoja limeongezeka kutoka wastani wa Tsh. 782,000 mwaka 2010 na kufikia Tsh. 960,000 mwaka huu.
Haya ni mafanikio makubwa ambayo hayakupatikana katika nchi nyengine duniani. Kwa wenzetu wa Chama Tawala – CCM tayari wameshavuka lengo lao la miaka mitano katika muda wa miaka miwili tu. Wao walilenga pato la mwananchi lifikie wastani wa Tsh. 884,000 ifikapo 2015.
Ndugu Wanahabari,
Hapa ndipo inapokuja hofu kwamba kuna mkono wa siasa kuvuruga mafanikio haya hasa kwa vile hayo ni matunda yanayotokana na hali ya amani, utulivu na mshikamano wa Wazanzibari, ambapo wananchi waliweza kuendelea na shughuli zao za uzalishaji na biashara bila ya sumbufu, wageni waliendelea kufurika nchini na wawekezaji wameedelea kuwekeza.
Ndugu Waandishi,
Mafanikio ya kukua kwa uchumi wetu yanaendelea kutupa funzo juu ya umuhimu wa kuilinda amani, utulivu na mshikamano wetu ambao umetujengea sifa kubwa. Hivyo napenda kuitumia fursa hii kwa niaba ya vyama vya upinzani kusisitiza mambo yafuatayo:-
1. Tunaiomba Serikali kuangalia usajili wake Jumuiya ya Mihadhara ya Kiislam kutokana na kwenda kinyume na masharti ya usajili wao na kwamba mwelekeo wake ni kuirejesha Zanzibar kwenye mafarakano, vurugu, siasa za chuki na uhasama miongoni mwa Wananchi.
2. Serikali ichukuwe juhudi maalum kuhakikisha kuwa vurugu zilizotokea hazitokei tena, na vyombo vya sheria viwachukulie hatua kali za kisheria wale wote watakaohusika katika kuanzisha na kuendeleza harakati za uamsho za kupinga Muungano.
3. Tuweke mbele maslahi ya nchi yetu kwa maslahi yetu na vizazi vijavyo. Kwa kufanikisha hili, tujitahidi kadri tuwezavyo kuepuka vitendo vyote ambavyo hatimaye vitavuruga mshikamano wetu, amani na utulivu uliopo.
4. Tunawasihi Masheikh na Maulamaa wote wasitumie dini kama ngao ya kuwapotosha wananchi na kusababisha vurugu ndani ya nchi.
5. Tunawaomba Wananchi walioanza harakati za kutaka kuigawa nchi misingi ya uzawa, kuachana na kasumba hizo kwani hazina hatma njema miongoni mwa Wazanzibari.
6. Tunawaomba viongozi wote wa kisiasa kulaani vikali harakati za Uamsho na vitendo vyote vyengine kuashiria uvunjifu wa amani kama ambavyo amekuwa akifanya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu wa Pili wa Rais.
7. Tunaungana na viongozi wetu wa vyama siasa na Serikali waliojitokeza hadharani kulaani matukio yenye mwelekeo wa uvunjifu wa amani na tunatoa wito kwa wale ambao bado hawajafanya hivyo wafanye kwa haraka na kwa nguvu zote kwani hatua hiyo itaonesha nia yao ya dhati katika kuleta maendeleo ya nchi yetu.
8. Tunapongeza kwa dhati juhudi za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa chini ya Uongozi wa Dkt. Ali Mohammed Shein kwa mafanikio makubwa ya kiuchumi, kijamii na kimaendeleo katika kipindi kifupi tokea Serikali hiyo iingie madarakani.

DAIMA TADEA UMOJA NA AMANI
Tunawashukuru sana kwa kutusikiliza

Advertisements

19 responses to “Wazanzibari wacheza ngoma wasioijua – vyama vya siasa

 1. Muheshimiwa tunakushukuruni kwa hotuba yenu,lkn hotuba yenu inanipa wasiwasi kidogo,mnanipa mshangao kidogo kwa nini munatetea maslahi ya chama kuliko maslahi ya wananchi?nakushangaeni kuwafananisha uamsho na vikundi vyengine bila ya kuangalia hoja za muamsho zinataka nini?hebu tuelezeni basi hivi mnategemea ni siku za uchaguzi kupata wakati hampo close na wananchi?maajabu ni kwamba hata kwenye serekali yenyewe(GNU)hammo halafu ndio kwanza mnatetea ujinga wenu vipembeni atakusikilizeni nani?

 2. HUU NI UPUMBAVU WA VYAMA HIVI VINAVYOOJIITA VYA UPINZANI. WAPUMBAVU WAKO WENGI NA HAWA NI WAPUMBAVU WA KISIASA. NYINYI KAMA WANASIASA TULITEGEMEA MTAUNGA MKONO IUNDWE TUME HURU NA BAADAE IJE NA MATOKEO NA BAADA YA HAPO WAHUSIKA WACHUKULIWE HATUA LAKINI MNAKUJA NA UJINGA AMBAO UNAONYESHA WAZI MMETUMWA NA NANI. NAPONGEZA VIONGOZI WALIOSITA KUILAUMU UAMSHO KWANI NI MAKOSA KUFANYA HIVYO BILA YA USHAHIDI. HIVI VYAMA NDO MAANA VINAKOSA HATA KURA ZA WAKE ZAO KWA UJINGA KAMA HUU. VYAMA VILIVYOJIZUIA KULAANI UAMSHO VINASTAHILI PONGEZI ZA WAZANZIBARI WOTE WANAOITAKIA MEMA ZANZIBAR KWANI HAWAKUKURUPUKA KAMA VYAMA VYENGINE KUTOA KAULI BILA HATA KUFANYA UCHUNGUZI KWANZA. HII ILIFANYWA NA KAMISHNA MUSA WA POLISI NA SERIKALI NA SASA HIVI VYAMA VYA WAPUMBAVU KAMA HAWA. MUNGU ANAANZA KUWALAANI NA WATAJIONYESHA WAZI WANAOPINGA HARAKATI ZA WAZANZIBARI. KWA HILI HAKUNA KURUDI NYUMA MPAKA KIELEWEKE.

 3. Upumbavu na ujinga kama huu wenu tumeshauzoea na wala hautozuia wimbi hili la mabadiliko. Hivi ni nani asiejua nyinyi mnatumiwa? Endeleeni na upumbavu wenu sisi usanii wenu na vyombo vya habari vya Tanganyika tumeshauzoea. Njaa zenu ndio adui yenu. Wezeni njaa zenu mnatutia aibu watu watu wa Pemba wanasifika kwa kuweza njaa ila nyinyi sijui ni wapemba wa wapi msioweza njaa zenu.

 4. Njaa si masihara ndio ukaambiwa adui yako muombee njaa, sasa hawa wafuasi wakanisa njaa zao ndizo zilizowafikisha hapa wanashindwa kuutetea masikiti uliovunjwa kwa kutetea kanisa.

  Na ishaallah M/mungu atakuadhibuni hivyo hivyo kwa njaa muadhirike.

  • Waarabu wana msemo wao unosema جــــوِع كلبــــك يتـــــــــــبـعك Yaani mueke na njaa mbwa wako atakufata tu. Sasa hicho ndicho kinachowaponza hawa viongozi wetu kwa kutoweza kuzistahmilia zile njaa zao kwa kutamani kile walichoahidiwa kupewa na Madikteta wao hua hawaoni hawasikii kwa njaa ya hivyo walivyoahidiwa, hatimae hufata tu kila wanachoimbishwa, na kufanya chochote kwa wananchi ndugu zao, na kutojali hata kuiuza nchi. Na linalonishangaza mimi ni kua hawafkirii kua huo UONGOZI wenyewe ni wa mda mchache tu. Miaka mitano kitu gani..!!? Hatimae unamkuta mtu alokua kiongozi anauza nyanya na kumsikia nae kusikitikia maisha magumu, au kuadhirika kwa bakora ya Mungu kupita madukani au kwa majirani wale wale alokua anawafanyia kejeli na kuwadharau kwa kuwatuana anaanza kuwaomba bila hata aibu. Jamani Viongozi zindukeni..!! Hapa hatuna utawala wa kifalme kama utakaa kwenye madaraka hadi ufe. Miaka mitano musiione Mingi. Au mnasubiri mpaka mustaafu ndio muwe na hikma. Manake kila kukicha hua tunaskia masikitiko na majuto ya ndugu zetu walokua ni wakubwa wa jeshi au Polisi au wengineo.
   Namalizia kwa msemo mwengine wa kiarabu unaosema أحــــــــــسن على الناس تــــــــــــستعبد عقــــــــــولهم (Wafanyie mazuri watu uzitawale akili zao) Basi eleweni nyi viongozi kua hilo ndilo liliopo kwa watanganyika kujidai kukufanyieni Ihsani nyie wachache ili wazitawale akili zenu ili mcheze kila wimbo wanaokuimbieni, na kwa hilo wamefanikiwa…….Kwa hio tahadharini sana.! Ndugu zenu mlotoka tumbo moja wanaumia na dhulma ya hao wanaojidai kukufanyieni Ihsan nyinyi wachache.

 5. Kwanza nyie mnaojiita umoja wa vyama tafuteni angalau hao wafuasi wenu mpate angalu wafuasi 200 ndio hapa Z’bar ndio mtuletee upumbavu wenu hapa Z’bar.

  Halafu itisheni mikutano kama nyny ni wanaume wa kweli na kama mna hoja kama za Uamsho.

  Njaa zenu mtaishia kwenye ushoga nyieee kama Joyce Banda wa Malawi, subirini mataona.

  Hawa jamaa wa vyama hivi ni wahuni tuu, tutawagonga watatafutana hapa Zenji.

 6. Akitokea m2 akiku2kana ww uliyesema haya ni haki kabisa. Lakini ilikuwa ujitangaz ww ni nani 2jue sio CHADEA inasema.
  Ww unasema UWAMSHO ni kama Al-shabab na makundi mengine maovu lakin ni wazi kwmb hujui unachokisema. Kw sbb hao BOKO HARAM,AL-SHABAB Serikali zao hazilali kw kuwatafuta kw hali na mali lakin UWAMSHO wapo mitaani wanaranda na km kwl ww ni mzanzibar bac hadi wanapolala unapafaham ni kw nn huwendi mahakaman ukapeleka kesi ili wakamatwe? Hebu wa2 wawache ujinga wa kisiasa hivi ww CHADEA ujiitae Mzanzibar upo radhi kuiona Zanzibar inapotea na kuondosha hadhi yke kw mfano leo Zanzibar haina fedha,bandari huru na jeshi hali hii inayopiganiwa irejee Zanzibar uko wapi ww mbn unakataa ukwli.
  Halafu unanasibisha chama cha CUF hku unaona aibu kukitaja. Cc wanzibar 2naamini ka2 chama cha CUF hakiwezi ku2takia mabaya. Fikiria ww Zanzibar kulikuwa na uhasama wa hali ya juu waliokaa na kurejesha hali ya amani ni CUF na nyny ndio mliokuwa wapingaji wa kuu wa serikali hii iliyopo. Ilifika hadi kumwita Mh. Aman Karume kwmb ni CUF eti sbb karidhia Serikali iliyopo acheni fitna bado 2po macho. Nyny ndio wachafuzi wa Amani wakubwa kwn kuna dhambi gani kuufanya MUUNGANO wa Demokrasia kw kuwauliza wananchi wanautaka au hawautaki kw kupiga kura ya maoni?
  Kw hili 2naomba msisumbuke kuwatisha wa2 2natangaza waz kwmb HATUUTAKIIII MUUNGANOOOO.

 7. DUA ZA WAISLAM ZITAWAFICHUWA WANAFIKI WENGI.
  Wanafiki walianza kubainika wakati Mtume alipohamia Madina kutoka Makka . Wakati huo kule Makka kulikuwa na Makafiri na Waumini tu,hakukuwa na unafiki . Lakini walipofika Madina ndipo walipokuwa Wanafiki na Washirikina.
  Ilikuthibitisha haya Mwenye ez Mungu huwa anatuonyesha ni wepi hao wanafiki na makafiri hapa hapa Duniani.
  Mwamsho na Jumiki ni watetezi wa Haki za Wazanzibari waliodhulumiwa na hata Dunia inalijuwa hilo pia ni jumuia zilizo jisajili kisheria .Lakini kwa sababu kuna watu niliowaeleza hapo juu kwa kujijua wao ninani ndio hufanya Fitna za Kijinga na kwa kutumiliwa kwa dhiki zao za maisha hukubali kuwasaliti wenzao bila kujua Athari zake na za familia zao.
  Hawa hawana tofauti na Maadui wa Wazanzibari wote. tusiwasikilize hawa ni Njaa zinawasumbua .

 8. Hao wajiitao wacheni waropokwe hamjui Kama siasa kazi wache wapeleke porojo lao mrima wazanzibari wanajua wakitakacho waacheni jawabu Lao liko tayari sikilizeni next mhadhara uamsho ndio ugom ozi wetu

 9. Nimeacha kusoma makala nzima, nilipoona kuwa taarifa inalinganisha bokoharam na uamsho.Hizi ni propaganda za kipumbavu, sishangazwi na vyama vinavyotoa taarifa hii kukosa kiti hata kimoja visiwani Zanzibar.Pumba tupu!

 10. Asalam alykum warahma tul llahi wabarakatu!

  KWANZA KABISA NAPENDA KUMSHUKURU ALLAH (SW) KWA KUMJAALIA BUSARA RAISI WETU MPENDWA Dr. SHEIN ZA KUAMUA KUKUTANA NA VIONGOZI WETU WA DINI (WAPIGANIA HAKI NA MASLAHI YA ZANZIBAR NA WATU WAKE)

  MUNGU MZIDISHIE HEKMA NA BUSARA ZAIDI RAIS WETU, aaamin rabbilaalamina!

  PILI, NAWAOMBA MASHEKHE ZETU, NDUGU ZETU WAPENDWA, (SHEKH FARID, SHEKH MUSSA, SHEKH AZANI, NA WENGINEO WOTE ITIFAKI INAZINGATIWA!)

  TUKUOMBENI KIKAO HIKI CHA KESHO NDIO TURUFU YENU (YETU) YA KUWEZA KUFIKISHA UJUMBE WETU MOJA KWA MOJA MBELE YA Mh. RAIS.

  SIKU ZOTE TULIKUA TUNAONGEA NA WAWAKILISHI WETU(MRs) ILI WATUFIKISHIE UJUMBE WETU KWA RAIS. WAKATI MWINGINE TULIFISHA UJUMBE KWAKE TUKIWA MBALI NAE, YAWEZEKA KABISHA UJUMBE ULIMFIKA ILA ULIMFIKA KATIKA MAZINGIRA GANI? JE NIVILE TULIVYOKUSUDIA UMFIKE? JE KUMEONGEZWA MAJI? JE KUMEPUNGUZWA MAJI? JE KUMETIWA FITNA?

  NADHANI MWENYE UWEZO WA KUYAIBU MASWALI HAYO NI YULE TU ALIEMFIKISHIA UJUMBE WETU Mh. RAIS SI VYENGINEVYO!

  TAUFIQ YA ALLAH IMEMFIKA Mh. RAIS AMEAMUA KESHO J3 KUONGEA NA VIONGOZI WETU WA DINI.

  HAKIKA NIDHAMU YA WOGA HAITA SAIDIA KITU KTK KUKOMBOA ZANZIBAR KTK MAKUCHA YA TANGANYIKA.

  TUNAWAOMBA MASHEKH MUONGEE YOTE TULIKWISHA KUYAONGEA TUKIWA MBALI YA Mh. RAIS, ILI AYASIKIE NA AONE HISIA ZA WAZANZIBARI.

  WALA KIKAO HIKI KISIWE NI CHA KUTAFUTA SULUHU YA KUINGIA KTK MCHAKATO WA KATIBA,( NAFAHAMU MASHEKH HAMLIKUBALI HILI ILA NIMESEMA KAMA TAHADHARI TU!)

  Mh. RAIS ATAKUEPO KUWASIKILIZENI NINI MAWAZO YENU, NINI MNATAKA, NA SISI TUNACHOSUBIRI KUSIKIA KTK MATUNDA YA MKUTANO NI:-

  1)MAKUBALIANO YA KUPANGWA TAREHE YA KURA YA MAONI TUUUU SI CHENGINE.
  2) BAADA YA KIKAO TUPATE TAMKO LA JUMUIYA KUHUSIANA KIKAO.

 11. ushamaliza?nenda kachukue hilo fungu lako kisha waambie hao waliokutuma kwamba mara hii hawa jamaa washaamka na hawalali tena mpaka waikamate JAMHURI YA WATU WAZANZIBAR

 12. AMA KWELI CHUI HAACHI MAPAKU YAKE! NAMUULIZA HUYU TAPELI MUUZA MANENO ANATAFUTA NINI KWETU! AMA MWISHO WA MAJI NI TOPE ! WATU KAMA HAWA TUWAPUUZE LKN TUSIACHE KUWACHUNGA! HAWA NI WEHU WASIOJUA WANAYOYATENDA! HAWA WOTE NI KUNGURU KAMWE HAWAWEZI KUA KUKU! MUMELAANIKA MWAPAMBANA NA MAULAMAA? MUSUBIRI KUUMBUKA! MWAWAJUA BOKO HARAM! ALSHABAB NA ALQAIDAH! DUA MBAYA HAICHOMBEZEWI MTOTO! ACHANE ULAFI MUTALISHWA SUMU! ALUTA CANTINUA!

 13. Huyu mmoja jina lake maarufu ni TAPELI. Maana ya Tapeli kila mmoja anajua ni nini. Hivyo sishangai kumsikia akisema maneno haya. Huyo mwengine amelaaniwa tokea kabla hajazaliwa na wazazi wake. Amekua akitumiliwa kila pale ambapo pana muelekeo wa kuleta maslahi kwa Zanzibar. Wakati wa kutaka kuundwa serikali ya umoja wa Kitaifa alikua mpiga kampeni mkubwa kupinga suala hili. Wakati wa kampeni za 2010 na za nyuma walitumika kupaka matope baadhi ya wagombea hivyo wanajulikana wazi wanafanya kazi kwa maslahi ya nani. WASIOITAKIA MEMA ZANZIBAR.

 14. TADEA NI WAPUUZI NA WASHEZI WAKUBWA HAPA ZANZIBAR. KWANINI HAMUKITAJI HICHO CHAMA CHA SIASA KINACHO WAUNGA MKONO MUAMSHO. HALI IKIENDELEA HIVI HIVI 2015 HAKUNA UCHAGUZI. MPAKA ZANZIBAR IPATE UHURU WAKE KUTOKA KWA WATANGANYIKA. TADEA KWANZA NCHI HALAFU NDIO CHAMA CHENU CHA UCHWARA.WANAFIKI WAPO WENGI TU WA ZANZIBAR WAPO WENGISANA. WANACHI WA ZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO.

 15. Mimi nimepata shida kwa kujiita hao ni umoja wa vyama chama ninacho kisimamia mimi hakina habari ya kufanya unafiki wao na wala mimi sina habari na wala hawaja niamabia kwa hivyo walipaswa kutaja vyama vyo tu mimi ninacho kiamaiani ni sawa na wanacho kidai Wazanzibari hii ni nchi yetu na nilazima tusimame kuidai nchi yetu .Watake wasitake tutaendelea kudai uhuru wa nchi yetu .Uwamsho simamieni haki na Mwenyezimungu atakuwa pamoja nanyi hao ni miongioni mwa watu wanaotumika kuwapiga vita nyinyi nawaomba simamieni haki (kwa kuwa wanapenda kuonekana wamesema Mungu atawafumba midomo kwa uwezo wake }

 16. Naona ndugu zngu wengi hamukulewa nia na dhamira ya TADEA,dhamira yetu ni kudai nchi kwa salama na amani na si kwa njia ya vurugu na kuhatarisha usalama kwa wananchi,zanzibar tumeshatoka na siasa za vurugu na hatuhitaji kurudi tena huko,tukumbukeni nchi yetu ni maskini na inategemea UTALII kwa kiasi kikubwa,leo tukifanya vurfugu watalii wataweza kuja?historia haituoneshi kua vuguvugu la mabadiliko haliwezi kuletwa na vikundi/asasi za kidini, ni vizuri tushikamane na kutoa maoni yetu kwenye tume ya katiba kwa ajili ya mustakbali wa nchi yetu,kuwatukana TADEA sio suluhisho,vile vile TADEA haikufananisha uamsho na vikundu vya alqaeda,bokoharamu,alshabaab n.k,isipokua ilitolea mfano juu ya vikundi kama hivyo kua si vizuri kwa ulimwengu wa leo,tukianza kubaguana tunawapa maaduim zetu mwanya,,isomeni makala ya TADEA vizuri na muielewe,kwani ina lengo la kuhamasisha amani na utulivu ndani ya ZANZIBAR yetu,,,,,,,,,,,,,,,TUTII SHERIA BILA YA KUSHURUTISHWA
  MUNGU IBARIKI ZANZiBAR NA WAZANZIBARI WOTE WANAOITAKIA AMANI ZANZIBAR,,,,,,amiyn

 17. sis vijjana wa kizanzibarii tunampongeza TADEA,kwa kauli yao ya amani na utulivu katika nchi ,hatupendi kuona vurugu za uvunjifu wa amani zikitokea katika nchi yetu,jamani lazma tuunge kwa hili………..

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s