Hutuba ya Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar

Jaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, Abraham Mwampashi akitoa hutuba katika uzinduzi wa ripoti ya haki za binadamu ya mwaka 2011 iliyofanyika katika ukumbi wa Bwawani Restaurant Mjini Zanzibar tarehe 14-06-2012.

Haitoshi kuona idadi kubwa ya semina za utoaji wa elimu ya haki za binadamu lakini tungelipenda kuona matunda au matokeo ya semina hizo katika jamii. Swali kuu likiwa – Je! jamii yetu inabadilika au tunaendelea na ule mtindo wa “mambo ni kama kawaida” – business as usual. Kwa mfano: Wazazi waliotalikiana wanaendelea kutoa malezi bora kwa watoto wao, kuwatunza vizuri na kuwapatia huduma zote muhimu ikiwemo elimu afya na upendo? Na wazee wasiojiweza wanahudumiwa? Uhuru wa kutoa maoni na kuabudu unaheshimiwa?

HOTUBA YA JAJI WA MAHKAMA KUU ZANZIBAR MHESHIMIWA ABRAHAM MWAMPASHI KATIKA UZINDUZI WA RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU YA MWAKA 2011 ITAKAYOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA BWAWANI RESTAURANT MJINI ZANZIBAR TAREHE 14-06-2012.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Profesa Chris Maina Peter na watendaji wako mliohudhuria,
Waheshimiwa wawakilishi wa Taasisi mbali mbali za kiraia na Serikali mliohudhuria,
Waheshimiwa waalikwa katika shughuli hii,
Mabibi na Mabwana

Asalamu Aleykum

Ndugu Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa uongozi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kunialika mimi kuwa mgeni rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2011.
Hii ni mara ya pili kupata nafasi ya kuwa mgeni rasmi katika shughuli za Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.
Shughuli ya kwanza niliyopata bahati kuwa mgeni rasmi katika kazi za Kituo ni ile siku tuliokusanyika katika Ukumbi wa Grand Palace pale Malindi kujadili haki za watoto na nafasi ya sheria.
Nilipewa heshima ya kufunga semina ile ya siku mbili iliyowajumuisha Majaji wa Mahkama Kuu Zanzibar, Mahakimu wa Mahkama za Mikoa na Wilaya kutoka Unguja na Pemba na Makadhi kutoka Unguja na Pemba.
Ndugu Mwenyekiti, huu ni uthibitisho kwamba Kituo kinathamini mchango na nafasi ya Mahkama katika jamii na kipo tayari kufanya kazi na Mahkama ikiwa ni miongoni mwa wadau wakuu katika sekta ya Sheria.
Aidha, ninafarijika sana kupokea kila mwaka nakala za Ripoti ya Tanzania ya Haki za Binadamu zinazotolewa kila mwaka na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar (ZLSC) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kilichopo jijini Dar es Salaam.
Vile vile, ninafarijika kupokea nakala za Jarida la Sheria na Haki linalochapishwa na Kituo na kutolewa kila baada ya miezi mitatu.
Ndugu Mwenyekiti, suala la haki za binadamu linaendelea kuchukua nafasi muhimu katika ngazi za vijiji, vitongoji, mijini, taifa na dunia nzima.
Taarifa zinazotolewa na vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi zinaelezea umuhimu wa kuheshimiwa haki za binadamu au namna haki hizo zinavyokiukwa kwa namna moja au nyingine.
Ndugu Mwenyekiti, uchambuzi wa taarifa au ripoti za kitaalamu zinazohusiana na haki za binadamu ni uthibitisho kwamba haki hizi zinakiukwa na watu wenyewe, taasisi au hali ya vita vinavyozuka na kuendelea katika pembe tofauti za dunia.
Naamini ukiukwaji huo unafanywa kwa makusudi ili kufikia malengo maalum hususan malengo ya kisiasa na kupata madaraka yanayowezesha udhibiti wa rasilimali za taifa.
Jambo linalouma na kusikitisha zaidi ni kwamba wakiukaji wa haki za binadamu wanaachiwa kutamba mitaani bila ya kufikishwa katika vyombo vya sheria (impunity).
Kitendo cha wakiukaji wa haki za binadamu kutochukuliwa hatua za kisheria ni matokeo ya udhaifu wa sheria za nchi husika, kulindana au kuogopana.
Ndugu Mwenyekiti, asasi za kiraia zina jukumu kubwa kufanya ushawishi wa kuheshimiwa haki za binadamu na kuchukuliwa hatua dhidi ya wote wanaokiuka haki za binadamu.
Njia za kufanya ushawishi wa kuheshimiwa haki za binadamu au kuchukuliwa hatua wale wanaozivunja zipo nyingi.
Kwa mfano, kazi hii inayofanywa na asasi hizi mbili (ZLSC na LHRC) ya kufanya utafiti, kufanya tathmini, kuchapisha ripoti na hatimaye kuzisambaza ni jambo zuri.
Ndugu Mwenyekiti, ripoti hizi mnazozitoa zitawafichua, zitawaumbua, zitawaamsha wanajamii na zitakuwa kumbukumbu kwa vizazi vijavyo ili kuepuka kasoro zinazofanywa sasa.
Ninaamini taasisi makini ambazo zimeguswa katika ripoti hii kwa njia ya moja kwa moja au njia ya kuzunguka zitashtuka na kujirekebisha.
Aidha, wale ambao wanahisi haki zao zimevunjwa watapata changamoto ya kuzidai kisheria.
Ndugu Mwenyekiti, ninafahamu kwamba ripoti hii imegawika sehemu mbili kuu. Sehemu ya kwanza ya ripoti imejikita zaidi kwa upande wa Tanzania Bara. Na sehemu ya pili ya ripoti inahusu upande wa Zanzibar.
Ninafahamu kupitia vyombo vya habari kwamba Uzinduzi wa Ripoti hii kwa upande wa Tanzania Bara ulifanyika mwishoni mwa mwezi uliopita jijini Dar es Salaam. Sasa ni fursa yetu Zanzibar kuizindua Ripoti hii ya Haki za Binadamu ya mwaka 2011.
Ndugu Mwenyekiti, naomba uniruhusu nichukue muda mdogo nizungumze machache kuhusu haki za binadamu kwa upande wa Zanzibar kabla ya kuizindua Ripoti yenu.
Pamoja na ukweli kwamba haki za binadamu zinaanza pale binadamu anapozaliwa. Haki hizi ni za urithi wala hazitolewi na Katiba au Sheria yeyote. Kazi kubwa ya Sheria ni kuzitambua, kuzilinda na kuzitekeleza tu.
Lakini inaonekana kuwepo pengo kubwa la ufahamu wa haki za binadamu hususan kwa mwananchi wa kawaida. Kwa msingi huu, ningeliishauri taasisi yako na taasisi nyingine zinazosimamia haki za binadamu kusimama kidete kutoa elimu zaidi ya haki za binadamu kwa nguvu zaidi hapa Zanzibar.
Ndugu Mwenyekiti, matendo mengi yanayosababisha makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanaweza kuepukwa ikiwa wananchi watakuwa na elimu ya kutosha ya kuheshimu haki za binadamu.
Nitafurahi sana nitaposoma Ripoti ya Haki za Binadamu ya mwaka 2012 ambayo itatolewa mwakani nikiona hatua zaidi zlizochukuliwa za utowaji elimu ya haki za binadamu zimeelezwa na matokeo (outcome) ya ufanisi katika jamii.
Haitoshi kuona idadi kubwa ya semina za utoaji wa elimu ya haki za binadamu lakini tungelipenda kuona matunda au matokeo ya semina hizo katika jamii. Swali kuu likiwa – Je! jamii yetu inabadilika au tunaendelea na ule mtindo wa “mambo ni kama kawaida” – business as usual.
Kwa mfano: Wazazi waliotalikiana wanaendelea kutoa malezi bora kwa watoto wao, kuwatunza vizuri na kuwapatia huduma zote muhimu ikiwemo elimu afya na upendo? Na wazee wasiojiweza wanahudumiwa? Uhuru wa kutoa maoni na kuabudu unaheshimiwa?
Vile vile, sheria zilizomo katika vitabu vyetu vya sheria ambazo zinaathiri haki za binadamu zingelianishwa na kupigiwa debe (advocacy) kurekebishwa kwa faida ya jamii.
Ndugu Mwenyekiti, baadhi ya sheria hizo zinazoathiri haki za binadamu ni Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Act No 6 ya 2004), Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act No 7 ya 2004), Sheria ya Ushahidi (Evidence Decree, Cap 5) na Sheria ya Walemavu. Sheria zote hizi zinahitaji kuangaliwa vizuri na kurekebishwa.
Jambo la mwisho ningelipenda kulisema hapa ni wananchi kushawishiwa kutumia Mahkama katika kudai haki zao badala ya kulalamika mitaani; kujichukulia sheria mikononi; au kutumia njia zilizo kinyume na sheria.
Ninashawishika kusema kwamba muamko wa watu kutumia Mahkama kudai haki zao hapa Zanzibar bado upo chini.
Ndugu Mwenyekiti, mwisho ninaomba kuchukua nafasi hii kwa mara nyingine tena kuipongeza ZLSC na LHRC kwa juhudi zao nzuri za pamoja za kutayarisha Ripoti ya Tanzania ya Haki za Binadamu ya kila mwaka kuanzia mwaka 2006 bila kukosa na bila kutoa visingizio. Kila mwaka tunasoma Ripoti ya Haki za Binadamu kuhusu Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Ndugu Mwenyekiti, sasa napenda kutamka rasmi kwamba RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU YA MWAKA 2011 IMEZINDULIWA HAPA ZANZIBAR.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.

Advertisements

5 responses to “Hutuba ya Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar

 1. Labda Mh. Jaji Mkuu unisaidie kitu. Je kupigwa mabomu kwa wananchi wasio na hatia pia ni haki ya binaadamu kama sio ni kw nn askari wa Zanzibar wanaongoza kufanya haya na ww upo na unajua hatukuoni ukisema? Hii ni waz kwmb wavunjifu wa kubwa wa haki za binaadamu ni VIONGOZI hususani wa ngaz za juu kw sbb wao ndio wanaotoa AMRI. Pia Je MAANDAMANO ya Amani si haki ya mwanaadgmu km ni haki Mbona kuna wa2 wameomba kibali cha maandamano hadi leo kimnya? La mwisho Mh. Jaji Je watu wachache hawana haki ya kusikilizwa wanachokihitaji kama wanayo Mbona kuwa Wanzanzibar wanataka NCHI yao hawasikilizwi? Nyny mnataka haki za binaadamu zipi? Acheni uwôngo na fitna haki kwa wote sio kwa wachache na kw haki maalum.

 2. Ndugu jaji nao umetumia muda mwingi kuwasilisha hiyo ripoti wakati ulikuwa unatakiwa utumie second 5 tu kuwaclisha hiyo ripoti?unaona taabu gani kusema ‘z’br hakuna haki za binaadamu?’

 3. kama mkweli nd jaji kwa nini usiseme wananchi wa znz wanataka muungano uvunjike na hio ni haki yao kukubali au kukataa muungano , huna mpya ndugu jaji wewe mwenyewe upo hapo kwa ajili ya muungano umewekwa na serilkali kama shushushu hamna lolote

 4. tena nimesahau nyinyi watu wa sheria mnanuka kuliko usaha kwa rushwa , mnauza haki za watu kwa rushwa , halafu mnakaa mnajiita waheshimiwa , heshima gani mliyo nayo zaidi ya kuchukua rushwa hata aibu hamuoni mkitembea mitaani?

 5. Asalam alykum warahma tul llahi wabarakatu!

  KWANZA KABISA NAPENDA KUMSHUKURU ALLAH (SW) KWA KUMJAALIA BUSARA RAISI WETU MPENDWA Dr. SHEIN ZA KUAMUA KUKUTANA NA VIONGOZI WETU WA DINI (WAPIGANIA HAKI NA MASLAHI YA ZANZIBAR NA WATU WAKE)

  MUNGU MZIDISHIE HEKMA NA BUSARA ZAIDI RAIS WETU, aaamin rabbilaalamina!

  PILI, NAWAOMBA MASHEKHE ZETU, NDUGU ZETU WAPENDWA, (SHEKH FARID, SHEKH MUSSA, SHEKH AZANI, NA WENGINEO WOTE ITIFAKI INAZINGATIWA!)

  TUKUOMBENI KIKAO HIKI CHA KESHO NDIO TURUFU YENU (YETU) YA KUWEZA KUFIKISHA UJUMBE WETU MOJA KWA MOJA MBELE YA Mh. RAIS.

  SIKU ZOTE TULIKUA TUNAONGEA NA WAWAKILISHI WETU(MRs) ILI WATUFIKISHIE UJUMBE WETU KWA RAIS. WAKATI MWINGINE TULIFISHA UJUMBE KWAKE TUKIWA MBALI NAE, YAWEZEKA KABISHA UJUMBE ULIMFIKA ILA ULIMFIKA KATIKA MAZINGIRA GANI? JE NIVILE TULIVYOKUSUDIA UMFIKE? JE KUMEONGEZWA MAJI? JE KUMEPUNGUZWA MAJI? JE KUMETIWA FITNA?

  NADHANI MWENYE UWEZO WA KUYAIBU MASWALI HAYO NI YULE TU ALIEMFIKISHIA UJUMBE WETU Mh. RAIS SI VYENGINEVYO!

  TAUFIQ YA ALLAH IMEMFIKA Mh. RAIS AMEAMUA KESHO J3 KUONGEA NA VIONGOZI WETU WA DINI.

  HAKIKA NIDHAMU YA WOGA HAITA SAIDIA KITU KTK KUKOMBOA ZANZIBAR KTK MAKUCHA YA TANGANYIKA.

  TUNAWAOMBA MASHEKH MUONGEE YOTE TULIKWISHA KUYAONGEA TUKIWA MBALI YA Mh. RAIS, ILI AYASIKIE NA AONE HISIA ZA WAZANZIBARI.

  WALA KIKAO HIKI KISIWE NI CHA KUTAFUTA SULUHU YA KUINGIA KTK MCHAKATO WA KATIBA,( NAFAHAMU MASHEKH HAMLIKUBALI HILI ILA NIMESEMA KAMA TAHADHARI TU!)

  Mh. RAIS ATAKUEPO KUWASIKILIZENI NINI MAWAZO YENU, NINI MNATAKA, NA SISI TUNACHOSUBIRI KUSIKIA KTK MATUNDA YA MKUTANO NI:-

  1)MAKUBALIANO YA KUPANGWA TAREHE YA KURA YA MAONI TUUUU SI CHENGINE.
  2) BAADA YA KIKAO TUPATE TAMKO LA JUMUIYA KUHUSIANA KIKAO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s