Hatutawasaliti wazanzibari- Maalim Seif

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia katika uzinduzi wa kongamano la Muungano na mchakato wa mabadiliko ya katiba huko Eacrotanal Mjini Zanzibar.

Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi wametokana na Wazanzibari wenyewe. Viongozi hao ni Wazanzibari kindaki ndaki, wenye kujawa na kiwango kikubwa cha uzalendo. Wanaipenda Zanzibar kama Mzanzibari mwengine yoyote yule.Viongozi wapo kulinda maslahi ya Zanzibar na watu wake, kama vile viongozi wa Tanganyika walipo kulinda maslahi ya wananchi wenzao wa Tanganyika. Kwamwe viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hawata wasaliti wananchi wa Zanzibar. Tutaheshimu na kutetea maoni yenu wananchi kama mlivyo yatoa kwa Tume ya Jaji Warioba. Muhimu jitokezeni kwa wingi mtoe maoni yenu. 
HOTUBA YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR MHE. MAALIM SEIF SHARIF HAMAD KATIKA UZINDUZI WA KONGAMANO LA MUUNGANO NA MCHAKATO WA MABADILIKO YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 1977 KATIKA UKUMBI WA EACROTANAL, TAREHE 13 JUNI, 201

Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na watendaji mliohudhuria
Mheshimiwa Mwakilishi wa Ford Foundation Ofisi ya Afrika Mashariki
Waheshimiwa Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Serikali na za Kiraia
Waheshimiwa Wageni wote waalikwa nyote Mabibi na Mabwana

ASSALAM ALEYKUM.

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenye wingi wa rehma kwa kutujaalia afya njema na kutukutanisha hapa, kwa ajili ya kujadiliana masuala muhimu ya Muungano wa Tanzania na Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

Aidha, natoa shukurani zangu za dhati kwa Asasi mbili za Kiraia yaani Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na Ford Foundation Ofisi ya Mashariki mwa Afrika yenye Afisi zake mjini Nairobi, Kenya. Nakupongezeni kwa mashirikiano yenu na ubunifu wenu wa kutayarisha mkusanyiko huu ambao umekuja katika wakati muafaka.

Vile vile sina budi kutoa shukurani zangu nyingi kwenu waandalizi wa Kongamano hili, kwa uamuzi wenu wa kunialika mimi kuja kujumuika nanyi. Kwangu mimi binafsi hii naona ni heshima kubwa mliyonipa na ninaithamini sana,  nasema Ahsanteni.

Niruhusuni nichukua nafasi hii kuipongeza Afisi ya Ford Foundation katika Afrika Mashariki kutimiza miaka 50 tokea ilipoanza shughuli zake katika Afrika Mashariki mwaka 1962. Aidha, naiomba Ford Foundation yenye Makao Makuu yake huku New York iendelee kushirikiana na Asasi za kiraia hapa Zanzibar katika sekta mbali mbali.
Tunaishukuru pia Ford Foundation kwa kuisaidia Zanzibar katika maeneo tofauti kwa mfano Tamasha la Filamu; Idara ya Nyaraka, Makumbusho na Mambo ya Kale; Tamasha la Nchi za Jahazi; Chama cha Waandishi wa Habari Zanzibar; na Jumuiya ya Asasi Zisizo za Kiserikali Zanzibar. Huu ni msaada mzito na wenye maana kubwa kwa nchi yetu. Sisi katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tunatambua na kuthamini mchango huu mkubwa kwa nchi yetu.

Kinachodhihirika wazi hapa ni kwamba, malengo ya Asasi mbili hizi yanafanana au tuseme yanashabihiana, na ndio sababu mukaweza kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kafanikisha maandalizi ya Kongamano hili ambalo tunategemea litakuwan na faida na maslahi kwa nchi yetu na wananchi wake. Nashawishika kusema hayo kwa kuzingatia ule msemo wa Waingereza usemao “Ndege wa aina moja huruka pamoja”  yaani “Birds of the same feather fly together”.Kwa kifupi Madhumuni ya Asasi hizi ni kusaidia wanyonge, ili nao wapate haki na kudumisha heshima ya binadamu na Utawala wa Sheria.

Waheshimiwa Waalikwa wa Kongamano
Mada ya Kongamano hili yaani Muungano na Mchakato wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ni mada nyeti ambayo inamgusa kila Mtanzania. Kutokana na ukweli huo, ni matarajio yangu wajumbe wa Kongamano mtatumia ujuzi, uwezo na uzoefu wenu mkubwa kufanya mjadala ulio hai, usiokuwa na jazba, ambao hatimaye utazaa mawazo na fikra zitakazosaidia kupata Katiba iliyo nzuri inayojali maslahi ya Watanzania wote, iwe wa Tanzania Bara au wa Zanzibar.

Mjadala juu ya Muungano wa Tanzania ni mada kongwe, ambayo wasomi, wanasiasa, wananchi mbali mbali na hata wageni wamekuwa wakiijadili mara kwa mara kwa mapana, na kwa mitazamo tafauti tokea Muungano huo ulipoasisiwa mwaka 1964. Wapo miongoni mwao wanao usifu Muungano wetu kuwa ni Muungano mzuri na wa mfano kutokana na kudumu kwake. Hao wana sababu zao, kati ya hizo ni nchi kadhaa za Afrika zilijaribu kuungana lakini baada ya muda mfupi, nchi hizo zilijikuta katika mizozo na migogoro hatimaye zilitengana.

Baadhi ya nchi hizo ni pamoja na Ghana na Guinea zilizoungana mwaka 1958, Muungano wa Senegal na Gambia (Senegambia Confederation) wa Mwaka 1982 hadi 1989, Muungano wa majaribio wa Libya, Tunisia, Mauritania, Morocco na Algeria (Muungano wa Maghreb) wa mwaka 1956, Muungano wa Misri na Syria wa Mwaka 1958 (United Arab Republic) ambao ulivunjika baada ya miaka mitatu hapo mwaka 1961.

Aidha, watu wengi duniani wakiwemo wasomi mashuhuri, wanafalsafa, wanasiasa waliobobea na wachambuzi wa mambo wanajiuliza kuna siri gani hata Muungano wa Tanzania uliotokana na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika umedumu kwa muda wa miaka 48 na bado unaendelea.
Maswali mengine yanayouulizwa ni pamoja na kwamba, Jee Muungano huu ni wa watu wawili? Yaani waliouasisi Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume au Muungano huu ni wa watu wote? Jee, Muungano huu ulikusudiwa uwe wa muda, kutokana na mazingira yaliyokuwepo wakati huo? Jee, Muungano huo unakidhi sheria za Kimataifa? Jee, Muungano huu ni wa kisiasa? Kwanini hakuna manung’uniko mengi kuhusu Muungano huu?

Mimi binafsi naamini sina jukumu la kujibu maswali yote hayo. Bali Watanzania wa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano watapata nafasi ya kutoa mawazo yao mbele ya Tume iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa madhumuni ya kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.

Lakini angalau kuhusu hili swali la mwisho linalouliza kwamba kwanini kuna manung’uniko ndani ya Muungano? Hili liko wazi. Ni kweli kuwa kumekuwa na manung’uniko mengi na ya muda mrefu juu ya Muungano wetu.
Tume mbali mbali ziliundwa kuangalia malalamiko au kama wengine wanavyoziita kero za Muungano, na zote zimethibitisha kuwepo kwa manung’uniko hayo, na hata kupendekeza hatua za kuchukuliwa kutokana na wakati husika.

Katika uhai wa Muungano huu, wengine wanasema wanabanwa, wanafinywa, wanaumizwa, wanabebwa, wanajitutumua na wanajitanua.
Miongoni mwa Tume zilizoundwa ni pamoja na Tume ya Mheshimiwa William Shellukindo juu ya Changamoto za Muungano, Tume ya Jaji Francis Nyalali kuhusu mfumo wa Vyama vya siasa nchini na Kamati ya Jaji Robert Kisanga kuhusu White Paper iliyotolewa na Serikali.

Kwa upande wa Zanzibar, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nayo iliwahi kuunda Kamati kadhaa kushughulikia kasoro zilizopo katika Muungano. Kwa mfano, Kamati ya Mheshimiwa Amina Salum Ali mwaka 1992, Kamati ya Baraza la Mapinduzi kuhusu Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 1990 na Kamati kuhusu Marekbisho ya Sera ya Mambo ya Nje mwaka 1999.
Pamoja na Kamati zote hizo na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati hizo, bado kero za Muungano hazikumalizika. Na badala yake mara nyingi matokeo ya Tume yalikuwa chachu ya kuibua mijadala mipya juu ya kero za Muungano.

Waheshimiwa Waalikwa wa Kongamano
Katika zama hizi tulizonazo, ambapo misingi ya demokrasia inapewa nafasi ya kipekee, hatuna budi kuendelea kuyajadili mambo kama haya ambayo yanagusa maisha na maslahi ya wananchi walio wengi kwa uwazi mkubwa.  Vyama vya siasa na baadhi ya jumuiya za Kiraia nchini zimekuwa mstari wa mbele katika kujadili suala la Muungano kwa dhamira moja tu ya kuwa na mfumo au utaratibu utakaoleta haki na kuondoa malalamiko yaliyopo.

Wapo wanaosema dawa ya matatizo haya ya Muungano ni kuwa na serikali moja tu, wapo wanaosema tuendelee kuwa na serikali mbili huku tukitatua kero zinazojitokeza, wapo wanaosema tuwe na serikali tatu. Na nyote ni mashahidi, wapo wanaokuja na mawazo na fikra kwamba Muungano huu tuuvunje kabisa. Au kama wengine wanavyosema ‘tugawane mbao’.

Aidha, hivi sasa kumekuwa na mtazamo mpya ambao ni kufanya marekebisho ya Muundo wa Muungano, ili kuwe na Serikali mbili  ambazo ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye uhuru na mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake, na Serikali ya Tanganyika yenye uhuru na mamlaka kamili ya kujiamulia mambo yake. Kisha Muungano utakaoanzishwa kwa njia ya mkataba, kwa mambo ambayo nchi mbili hizi watakayo kubaliana.

Wenye mawazo ya mfumo huu wanaamini kuwa huo ndio mwarubaini wa matatizo ya Muungano yanayodumu muda mrefu na ambayo yanaendelea kujitokeza. Mfumo wa Muungano wa mkataba si jambo geni na umekuwa maarufu sana hivi sasa Duniani. Hata Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya (European Union) ni mfumo wa aina hii ya Muungano.

Chini ya utaratibu huu kila serikali inakuwa na mamlaka kamili, lakini katika baadhi ya mambo wanayokubaliana yawe ya pamoja nchi husika zinafungana mikataba ya kuyaendesha na kuyasimamia.
Naamini kwa Wazanzibari lililo muhimu zaidi ni Muungano, na si haki kuwazuia Wazanzibari wasitoe maoni yao juu ya Muungano. Na kwa maana hiyo kwetu lililo muhimu zaidi ni hili la Muungano.

Waheshimiwa Waalikwa wenzangu
Mimi ni mmoja miongoni mwa viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Siasa cha CUF. Lakini pia mimi ni Mzanzibari na Mtanzania. Kwa hiyo nitakuwa na haki ya kutoa maoni yangu wakati ukifika. Tuombe Mwenyezi Mungu atujaalie uhai.

Hata hivyo, nachukua nafasi hii kuendelea kuwahimiza na kuwashauri Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla kuzisoma Hati mbali mbali za Muungano, Katiba za Tanganyika, Katiba za Tanzania na Katiba za Zanzibar na maandiko mbali mbali ya wasomi katika vitabu au magazeti.

Wakati utakapofika Tume ya Katiba itakapokuja wananchi waweze kuchangia huku wakiwa wanajua kwa undani Muungano wetu, ikiwemo faida na kasoro zake na waseme bila ya woga wanachokitaka.
Hii ni fursa adhimu ambayo wengi wamekuwa wakiililia kwa siku nyingi juu ya haja ya Watanzania kupata fursa ya kutoa maoni yetu, juu ya masuala yote yanayohusiana na Muungano.

Wananchi wawe huru kutoa maoni yao kwa uwazi na pawepo na uvumilivu. Hata kama mtu hakubaliani na maoni, hoja zinazotolewa na mwengine, inabidi asikilize kwa uvumilivu. Naye akipata fursa aseme yake kwa uwazi pia.

Waheshimiwa Waalikwa wenzangu
Naomba kutoka nasaha zangu kwamba katika mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi juu ya mabadiliko ya katiba, ni vizuri sote tukatumia busara ya hali ya juu, hekima na uvumilivu, ili mchakato uende kwa salama. Tukumbuke kuwa vurugu na misuguano ya aina yoyote haina faida na isipewe nafasi katika kutoa maoni yetu kuhusu mchakato wa mabadiliko ya katiba.

Na mwisho wa yote hayo, ni lazima tukubaliane kwamba maoni ya wengi yaheshimiwe baada ya wale wachache kupewa haki yao ya kusikilizwa kwa kikamilifu. Naomba kuchukua nafasi hii kuwatoa wasi wasi wananchi na hasa Wazanzibari. Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi wametokana na Wazanzibari wenyewe. Viongozi hao ni Wazanzibari kindaki ndaki, wenye kujawa na kiwango kikubwa cha uzalendo. Wanaipenda Zanzibar kama Mzanzibari mwengine yoyote yule.

Viongozi wapo kulinda maslahi ya Zanzibar na watu wake, kama vile viongozi wa Tanganyika walipo kulinda maslahi ya wananchi wenzao wa Tanganyika. Kwamwe viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hawata wasaliti wananchi wa Zanzibar.
Tutaheshimu na kutetea maoni yenu wananchi kama mlivyo yatoa kwa Tume ya Jaji Warioba. Muhimu jitokezeni kwa wingi mtoe maoni yenu. Maoni ya wengi naamini yataheshimiwa. Naomba nitahadharishe watu wasijefanya kosa la kuto kwenda kutoa maoni yao. Kama mtu hakwenda anaweza kuja kujilaumu, pale ambapo maoni ambayo yeye hayaungi mkono yakaja kuwa ndio maoni ya wengi, kwa sabababu tu yeye na wenziwe wenye maoni kama yake hawakujitokeza kutoa maoni yao.

Baada ya kusema hayo machache nachukua nafasi hii kukushukuruni nyote kwa kunisikiliza kwa makini na sasa natamka kwamba kongamano la Muungano na Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba limefunguliwa rasmi.

Ahsanteni.

Advertisements

25 responses to “Hatutawasaliti wazanzibari- Maalim Seif

 1. MUNGU WAPE MAISHA MAREFU NA AFYA NJEMA VIONGOZI WETU KAMA HAWA (Maalim SEIF). MUNGU IBARIKI ZANZIBAR NA WATU WAKE WOTE!

  TAFADHALI TUTUMIE VIDEO YA MKUTANOOOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!!!

 2. Nimeelewa lakini inanitia wasi wasi wewe Maalim huna nguvu kwenye Serikali na umesema maneno matam lakini wewe sio mtekelezaji watekelezaji ni CCM kwahiyo M/mungu autsaidie hili jinamizi la muungano lituondoke.

 3. Sikufikiria kama Mh.hamad anaweza kusema maneno kama haya na wazanzibari hatujui tukufahamu vipi,wazanzibar tulio wengi hatutaki muungano na ikiwa hatutaki muungano iko haja gani kusema japo neno moja kwa tume ya kuratibu katiba
  wakati tayari wapokeaji wa maneno ya kuratibu katiba wameshawekewa kizingiti ni kipi kizungumzwe mbele yao na kipi kisizungumzwe na hicho ambacho kisizungumzwe ndio lengo la wazanzibar,hapo Mh.hamadi unatuambia nini ?unatutaka tuende kuzungumza matakwa yetu na matakwa yetu yameshawekwa wazi kwamba hayatakubaliwa ,huku ni sawa na kutega dema na chambo chake utupa?.
  Au ndio unajikosha mbele ya wazanzibari ambao mtazamo wao kwa sasa ni tofauti na wako na uonekane kama umesema jambo ambalo ni jema kwa walio wachache na tofauti na walio wengi?
  Jee hamuoni kama mnajimaliza ? na kutaraji tuanzishe kama yaliotokea kaskazini mwa afrika?
  Basi kama mnahitaji kuanzishwa kwa hayo ?wazanzibari wapo tayari ikiwa njia hii ya kistaarabu hamtaki,tusije kulaumiana baadae na kutafutwa suluhu na kwa wakati huo haitapatikana abadan.
  Wallahi Billahi Tallahi pande zote mbili zitaathirika na tutakaoshinda ni sisi wazanzibari kwani mbele ya subhana wataala
  tutakuwa mashahid wa kutetea haki zetu sijui nyinyi mnaopinga wazanzibari kupata haki hizo mtakuaje mbele yake subhana
  Yale yaliotokea 2001 hayatatokea tena ila ngoma ikipigwa zanzibar itachezwa maziwa makuu na asieamini atanikumbuka.

  • Nakubaliana na maneno ya Maalim Seif hawa ndio viongoz tunao wataka na vile vile nakupongeza sana da Salma M/Mungu akupe taufik na uwe mzalendo wa nchi yako ya zanzibar ila ombi langu tusaidie kuiona hii video ya hili kongamano la leo

 4. Maelezo na ushaur n mzur jaman tusome kwa undan na tukija kiubuka tuwe na hoja za msing kuhusu hl

 5. Mm nazan MAALIM c kama anajikosha ila lazma umfahamu ktk mtazamo wk anasema kuwa yeye hajatowa mawazo yake badi km utamfahamu anasema tusubr tume ije! Atatoa mawazo yk.. Na amesema ucje ukamlaumu m2 pale 2me inapo kuja hii inamää kama ha2jenda wapo wachache wenye maslah yao wataenda na kutoa mawazo yao.. Na kuwa ndo katba so nazan 2kiwe kwenye hyo 2me ndo tutumie kusema katka KATBA MPYA isinyoshe km kuna taifa La TANZANIA bali n ZANZIBAR HURU na Tanganyka huru.. Na kama umemsoma vZUR MWISHON anasema kuwa kuna wa2 wanasema muundo ubadilike zanzibar na tanganyka iwe na mamlaka kamilik kila moja katka kuamua mambo yao na MUUNGANO UWE WA MKATABA. Bt ndugu zng nazan tunaweza kwenda step to step kufkia hli. Kwan tayar nch za kikafr kubwa wanaitizama vbaya znz.. MWISHO WA siku kupoteza maisha wala hakuna lolote km 2001 iv kuna kiongoz alotiwa hatian.. ZNZ ni visiwa hakuna msitu mkubwa ukivitanda viswa kwenye maeneo ya bahar hatoki m2.. Sasa tukiazsha UASI WAP tutajfcha au kukimbilia ili kupanga mashambuliz.. Tutajikomboa hatua kwa hatua

 6. wazanzibar ni kama changu dowa sisi leo huyu shaeobaro alaleta pumba nyote munaunga mkonoo ss hatutaki muungano yeye huyu na sefu mweusiii

 7. Pingback: Hatutawasaliti wazanzibari- Maalim Seif·

 8. Inalilahi Wainalilahi rajiuni, kama ndio hotuba ya Maalim Seif, tumuachieni m/mungu ndie atakayetuhukumia sisi wazanzibar kama ndio viongozi ndio hawo mimi sina la kusema. Ila nauliza hivi kwanza Maalim umeshakuwa mwanamapinduzi,Pili nauliza hivi maailim Seif unazungumza kwa niaba ya Serikali ya umoja au Serikali ya Mapinduzi.Kwasababu kwenye hotuba yako hukusema kuwa wewe ni kiongozi wa Serikali ya umoja,ila umesema kuwa wewe ni kiongozi wa serikali ya mapinduzi wakati wananchi wamepiga kura ya maoni ili kuunda Serikali ya umoja sasa hii ya Serikali ya Mapinduzi imetoka wapi Mh Maalim Seif au ndio umeshafika kwenye Mzinga wa Asali,umeshasahau kuwa ulikuwa unakula shubiri na umeshasahau mseto.Na mwisho napenda kumuliza Maalim Seif je vipi vilio vya wananchi kuhusu kura ya maoni mbona hujaligusiya suala hilo na Maalim unalifikiriaje suala hilo la wananchi kuhusu kura ya maoni?

 9. Baada ya kimya kikubwa, Maalim kaona bora atoe na yeye dukuduku lake….lakini naona kachelewa, au anaona wapenzi wa chama chake wanazidi kukiacha mkono na kuangalia maslahi ya nchi kwanza kuliko maslahi ya chama…
  kwa upande mwengine nampongeza kwa ujasiri wake…
  kazi mara hii haitofanywa na chama fulani mara hii inafanywa na wananchi wenyewe, na hiyo kazi inaanza kwa kuikomboa na kuirudisha JWZ: ALLAH atufanikishe kwa hilo.

 10. Huu ni usanii baada ya kuona chama chake kinaenda mrama, hana la maana hata moja linalomtetea Mzanzibari.

  Maalim ni tapeli mkubwa wa siasa hapa Zanzibar, kama kweli ana nia njema kwanza angemshauri Sheni kuwasikiliza wananchi kabla ya katiba kutungwa. Halafu cc Wazanzibari tushajulikana ni sawasawa na mbuzi kwa kukokotwa ukataka uctake.

  Tena cha kushangaza anasema eti “namushauri mkatoe maoni kwa wingi la sivyo mtakuja juta”!!! yaani totally hapa kafeli, Wazanzibar hatutaki muungano na tayari kuna hadidurejea,

  Chakujiuliza hapa hayo maoni yako si yatatiwa kapuni ? Viongozi wacheni usanii cc tushamjua katu hatutawasikiliza, nyinyi bakieni na hizo nyazifa zenu.

 11. sawa wazanzibari wengi hawataki muungano , na topic hio imezuiliwa kwenye kutoa maoni kwenye kukusanya maoni ya katiba kwa hio unatwambia nini?

  • Hapo Maalim anatudanganya tuuu, kiukweli Waz’bari tuzinduke si CUF, CCM wala Katiba hazitatusaidia ktk kuutafuta uhuru wetu wa Wazanzibar tuungane pamoja chini ya mwamvuli wa MUAMSHO ktk kuutafuta uhuru wetu la sivyo tusubiri vichogo vitumalize.

 12. Wee semaa Watanganyika lao liko pale pale kuimeza Zanzibar, na CCM wote wa pande mbili za Muungano washaweka mkazo serikali mbili kuelekea moja kwenye Katiba mpya. Samuel Sitta na Padre Spika Mstaafu Piusi Msekwa wametamka wazi kuwa suala la serikali 3 bora Muungano ufe, na kufa Muungano wao hawataki kata kata bali wanatakukamilisha ajenda yao dhidi ya Zanzibar.

  Ndugu yangu Mh. Hamza Juma tulimsikia katika kipindi cha MAONI MBELE YA MEZA YA DUARA kinachorushwa na Duetch Velle kila Jumamosi, ambapo alisema “Sisi CCM hatuna akili za mgando, tunaweza kuibadilisha sera yetu ili kwenda na wakati”

  Je! Bwana Hamza Juma kikao cha NEC umekiona kilivyokuziba mdomo na kukuumbua?

  Maalim Seif unaota mchana mzee wewe kwa hilo, kwani wakatoliki hawana fikra hizo.

  MUUNGANO HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”.

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 13. Maalim ukitaka ushauri wangu bora ujiuzulu hu ni wakati muwafak usije uksingiya kwemye shimo la mamba wanakutumiliya wewe wanajuwa wa Zanzibari wanakusikiliza jiti na macho wekw heshima yako amkaaaaaaa TUWACHENI TUPUMUWEEEEEEEEEEEEEEE

 14. Mwanadamu siku zote amejengeka na sifa mbili nazo ni kusikiliza na kuelewa.
  Maalim hajatoa fikra zake ,wala hajamzuia mtu kutoa ya moyoni mwake.
  Alichokisema ni kutupa picha kamili ya tunachotakiwa tufanye sisi wenyewe
  Sasa anae mlaumu Maalim ni kuwa hajamuelewa au Tayari umejitayarisha kupinga lolote litakalo semwa na Maalim. Wewe na mimi tunayo haki kukubali au kukataa ni sawa ni haki yetu sote , lakini tusubiri hapo atakapozungumza nini kifanyike na kama hukuridhika ndio tumpinge bila wasi wasi, Hawekwi mtu ndani hapa
  Kinachotakiwa ni hoja sio matusi kejeli kiburi na hamasa za kishetani.
  Wewe nenda katoe duku duku lako bila woga .

 15. ww issa itakuwa ww ndo hujamuelewa maalim sefu au hufuatilii mambo yalivo na yanavokwenda ila naomba unisikilize mallim sefu anawambia wa2 wende kwenye tume wakatoe maoni yao kw wingi ili wajuulikane nini wanataka ivi hajui kama kura ya maoni ni haki ya wazanzibar nahajui kua kura ya maoni ndo njia pekee yakujua maoni ya wazanzibar yupi anataka muungano yupi hataki
  jengine ivi unajua km tume wameambiwa wachukue maoni kutokana hadidu rejea na tume inatakiwa ipuuze mawazo ya wale wote wanaotaka muungano uvunjike ss sisi wazanzibar muungano hatuutaki sefu atuambia tukatoe maoni. maoni gani anayotaka yeye au ndo tukaukubali muungano ivi sefu haoni kama wazanzibar wadhalilishwa akiwemo yeye kuitwa majuha viongozi wa SUK sheria ya katiba imepitishwa bara zanzibar ili ukubalike lazima ipitishe BLW wallah mm nimeshangaa kua mpaka baraza la wawakilishi linasimamiwa na wabara wanatakiwa kuikubalia sheria bila kuijadili na nilazima wafanye hivo kwani wasipofanya watakuwa wamewaudhi mabwana zao bara
  ifi nikuulize ww issa haya yote maalim hajayaona akayasema anaenda kuwambia wa2 wende wende wakatoe maoni yao kwenye tume ajua si wazo lake wala wazo la wazanzibar halitakubaliwa mana yeye anataka serekali tatu au serekali mbili na muungano wa mkata wakati keshaambiwa wazi serekali tatu wabara wanahiari muungano uvinjike na serekali mbili kw muungano wa mkata aote kwani maisha kawatakubali zanzibar kuwa na madaraka yake kamili
  ivi ww umesoma nini kw maalim sefu kama si mnafiki tena mkubwa na nimsaliti wa wazanzibar kuwambia wakatoe maoni kwenye tume ya katiba. mallim sefu na wenzake wanalili matumbo yao tu na familia zao wote wanafiki mm nawashauri wazanzibar maswala ya vyama tuachaneni nayo kwani yatatupeleka pabaya bila ya mafanikio
  tuwaunge mkono uamsho muungano hatuutaki na hatujadili katiba kama hatujapiga kura ya maoni
  Allah yuko pamoja nasi tusikatike moyo

 16. Minawapongeza wazanzibar wasikubali kuchangia katiba bandia kwass mpaka 2ijue hatma y muungano sawa sawaa,alaa kwanini 2fe njaa wakati mali ze2 2nazo

 17. Katika rasimu ibara ya 9 imepiga mafuruku kujadili muungano je mh maalimu sefu tujadili nini.?ikiwa sisi chetu tanganyika ni muungano,pia katika kutowa maoni hunaruhusa ya kutowa maoni ya kuvunja muungano je sisi ambao tulokuwa hatutaki kuboresha muungano tukatowe maoni wapi? Naomba majibu.

 18. VUNJA MUUNGANO SIASA BAADAE. LAZIMA MUUNGANO HUU BANDIA UVUNJIKE KWANZA HALAFU MENGINE YAFUATIE BAADAE

  • ninyi wapemba mnapiga tu porojo udongo uliochanganywa ni unguja na tanganyika wapemba rudini kwenu mtuache waunguja na watanganyika. Na pia wapemba mmejazana bara na kujenga kama kwenu mtarudi kwenu pemba msione wabara tumetulia hatuwanyanyasi ninyi mnatunyanyasia wabara waliopo kwenu tunawasubiri tukisika tu mbara yeyote kaumizwa au kufa nasitutapambana na wapemba waliopo huku bara.

 19. SISI TUTAFURAHI SANA MKIWAFUKUZA HAO HATA HII LEO KABLA YA KUFIKIA HUKO. TUNAJUA KUA SISI NI WATU WA KAZI NA HATA TUKIWAACHIA MALI ZOTE ZA WAPEMBA MTAZINYWEA BIA NA UFUSKA KAMA KAWAIDA YENU NA BAADAE MTAISHI KWENYE UMASIKINI WENU. MLIRITHI MALI NGAPI KUTOKA KWA WAHINDI ALIOWAFUKUZA NYERERE? NA MMERUDIA PALEPALE KWENYE NJAA. WAMBILI HAVAI MOJA NYINYI NI WA MOJA TU. FUKUZENI WAPEMBA WOTE HATUTOACHA KUDAI NCHI YETU. TUACHENI TUPUMUE.

 20. zahor
  Msimamo wetu ni ule ule kudai jamhuri ya watu wa zanzibar ikiwemo hadhi ya rais wetu,mamlaka kamili ya waserikali yetu,tunahitaji mablozi wazanzibar watuwakilishe nchi za nje na sio nyinyi watanganyika ,pia tunahitaji rasilimali zetu kuzitumiya wenyewe bila ya nyinyi na pia tunahitaji serikali tatu yetu ya zanzibar ,ya tanganyika na ya muungano ikishindikana hinyo hatuutaki muungano huu wa kifedhuli na wa danganya toto wa baba na mtoto au mama na baba cici tuntaka wa baba kwa baba na isio watanganyika ndo wenye nguvu.
  HALAFU NYINYI WALEVI WA TANGANYIKA KAMA MNAWAONA WAPEMBA WAZEMBE WAFUKUZENI TU HUKO DAR KAMA HAMTAKUFA KWA NJAA MAANA NYINYI KAZI YENU STAREHE NA CHAPOMBE SANA WAO WATAATHIIRIKA KILE KIPINDI MUTAKCHOWAFUKUZA TU BAADAE WATARIFITI WACHENI UJINGA WENU. HUO. Kama mtu kudi hakki yake ni ugomvi basi wazanzibar kwa sasa wako tayari na KWA SASA KUNA PROGRAM INAITWA ZINDUKA MZANZIBAR AMBAYO INAMUHUSISHA KILA MZANZIBAR.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s