Vijana watakiwa kufanya utafiti

Afisa wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (ACTECH) Bwana Saleh Mikidadi akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar balozi Seif Ali Iddi aliyefungua rasmi Ofisi ya Tume hiyo pamoja na ile ya Nguvu za Atomiki iliyopo katika Jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jmauhuri ya Muungano liliopo Tunguu, nyuma ya Afisa Mikidadi ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wa Serikali ya Muungano, Makame Mnyaa Mbarawa

Uongozi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania {costech} umeombwa kushajiisha Wasomi hasa Vijana wa Vyuo Vikuu Nchini kupenda kufanya tafiti mbali mbali zitakazojenga Mazingira ya kumuondoa Mtanzania kwenye matatizo yanayomkabili. 

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa ombi hilo katika Hafla fupi ya uzinduzi wa Ofisi ya Tume hiyo ilyofanyika hapo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja. Balozi Seif alisema Tafiti kama hizo ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na Mwananchi zinaweza kusaidia kupata Maendeleo kwa kasi zaidi katika Kipindi kifupi kijacho.
Alisisitiza kwamba Serikali kwa upande wake iko tayari kwa namna yoyote ile kutumia vyema matokeo ya Tafiti zinazofanywa na Wazomi wazalendo.
Hata hivyo Balozi Seif alieleza kuwa yapo baadhi ya matokeo ya Tafiti hubakia kuwa siri kwa Taifa lakini mengine yanastahiki kutolewa kwa Wananchi ili waelewe kinachoendelea kwenye maisha yao.
Balozi Seif alieleza kwamba wakati umefika kwa Makampuni pamoja na Viwanda vya hapa Nchini kujenga Utamaduni wa kutoa kazi zao za Utafiti kwa Tume hiyo ili ijipatie fedha za kuendesha shughuli zake za utafiti kama Nchi nyengine zilizoendelea.
Alieleza kwamba Tanzania imepania kuleta maendeleo kwa Wananchi wake kutokana na uamuzi wake wa kutenga Jumla ya shilingi za Kitanzania Bilioni Thalathini { 30,000,000,000/-} kwa ajili ya Utafiti na Maendeleo kwenye Bajeti yake ya Mwaka 2010/2012.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Maendeleo bila ya Sayansi na Teknolojia hayapatikani kwani masuala hayo mawili yanakaribiana katika utekelezaji wake.
Akizungumzia Tume ya Taifa ya nguvu za Atomu Balozi Seif alielezea kufarajika kwake kutokana na mipango m,izuri ya Taasisi hiyo kuhudumia Zanzibar katika masuala ya usimamizi wa matumizi salama ya Mionzi. Balozi Seif alisema ushirikiano wa pamoja wa Taasisi hiyo,Wizara ya Afya Zanzibar na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani katika kuanzisha mradi wa Matibabu ya Saratani katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja unafaa kuungwa mkono.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uamuzi wake wa wa kusogeza karibu na Wananchi shughuli za Ofisi ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomu.
Katika Taarifa yake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania Profesa Iddi Suleiman Nyangarika Mkilaha alisema Taasisi yake itaendelea kutoa Elimu sahihi ya matumizi ya Mionzi. Profesa Nyangarika alisema Taaluma hizo kwa sasa itazingatia zaidi katika sekta ya Viwanda pamoja na Vituo vya Afya ambavyo vinatumia Vifaa vyenye mazingira ya Nguvu za Atomiki.
Mkurugenzi huyo wa Tume ya Nguvu za Atomiki alifahamisha kwamba katika kupanua zaidi huduma zake Taasisi hiyo itaendelea kupima Mionzi katika Mimea ili kujua kiwango sahihi cha kulinda Vyakula kwa ajili yamatumizi bora kwa Wanaadamu. Mapema Waziri wa Mawasiliano,Sayansina Teknolojia wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Makame Mnyaa Mbarawa alisema Wizara hiyo itaendelea kushirikiana na Wataalamu wa ndani na nje ili kuona Tafiti zinazofanywa zinatmika kwa walengwa ambao ni Wananchi.
Alisema Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia na ile ya Nguvu za Atomiki zimeanzishwa zikiwa na wajibu wa kusimamia tafiti na nguvu za Atomiki Nchini kwa kushirikiana na Taasisi za Kanda na zile za Kimataifa.

Advertisements

3 responses to “Vijana watakiwa kufanya utafiti

 1. Seif Ally Idd nini bwanaa! Aah, sisi hili letu sisi (MUUNGANO) tafiti nyingi sana zishafanywa na wataalamu mbali mbali mfano Dr. Harith Al-ghassan, Dr. Moh’d Said, Dr. John Sivalon, Bergern, Roland, Dr. Mushi na wengi wengineo na matokeo ya tafiti zao yameoonesha kuwa MUUNGANO huu uko dhidi ya Zanzibar na Uislamu na wala sio kwa ajili ya Zanzibar na Uislamu, unataka utafiti gani wewe punguani wakati hili hujaliweza?.

  Tunakusubirini kesho kwenye sheria no 8.2012 ya mabadiliko ya katiba. Je! Mtaweza kufunua midomo wajane nyie mbele ya wachumba wenu Watanganyika au ndio mtakula makombo? Wajinga Dunia nzima inatucheka masikini kwa mnavyotuaibisha majuha nyinyi. Aah! Jamani inaumaaa Jamani nyie.

  MUUNGANO HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WAZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 2. Tatizo la Balozi Seif Ali Iddi anapenda kusema tu. Sijui kuwa anafahamu kuwa wakati mwengine anayosema ni kichekesho, kuomba Msumbijii iiifundishe Zanzibar kufuga kamba kwa mfano. Ndugu yetu Balozi kwa wakati huu ukiwa unashikilia nafasi kubwa Zanzibar inabidi uzungumze mambo ambayo ni ya msingi kabisa. Tunajua kuwa tafiti ni muhimu. Ukumbuke hatahivyo kuwa hao wanaojidai kuleta taasisi zao hapa wanajitanulia wigo wa ajira wenyewe. Utaona karibu hata watu wa bustani wanatoka kwao, utaona karibu baa eneo la Tunguu zinaimarishwa, utaona karibu biashara ya kujiuuza inaimarika na mambo mengine machafu yasiyokubalika. Taasisi hii kama kweli ni inaukweli kwanini haijiegemezi tu na Vyuo vikuu vya hapa Zanzibar na hivyo kusaidia kujenga uwezo wa kitafiti wa Wanavyuoni waliopo Zanzibar.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s