Sheria ya katiba mpya kuwasilishwa kama taarifa

Katibu wa baraza la wawakilishi Zanzibar, Yahya Khamis Hamad

SHERIA ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itawasilishwa kesho katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoanza kujadili bajeti ya mwaka wa fedha serikali ya mwaka wa fedha wa 2012/2013. Katibu wa baraza hilo, Yahya Khamis Hamad aliwaambiwa waandishi wa habari jana katika mkutano uliofanyika ukumbi wa baraza la wawakilishi, kwamba jambo la kwanza kuwasilishwa kwa wajumbe wa baraza ni sheria hiyo ambayo wananchi wanasubiri kuitolea maoni.

“Hii itakuwa ni taarifa kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi ambayo ni kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar kifungu 132 (2) ambayo inahitaji sheria zinazohusu muungano kuwasilishwa katika baraza” alisema Hamad.

Hamad alisema katiba haitoi nafasi ya kujadili sheria hiyo kwani itakuwa ni taarifa kwa wajumbe wa baraza na sio kuijadili, “Hii ni kwa mujibu wa katiba lakini tusibiri litakaloweza kutokea baada ya kuwasilishwa sheria hiyo kwa sasa hatuwezi kujua nini kitatokea”.

Katibu Hamad alisema sheria hiyo inawasilishwa katika baraza la wawakilishi katika kikao cha kesho kwa sababu ndicho kikao cha kwanza tangu bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitisha sheria hiyo.

“Waziri wa katiba na sheria wa Zanzibar Abubakar Khamis Bakari atatoa taarifa kuhusu sheria hiyo” alisema Katibu huyo.

Akijibu suali la waandishi juu ya kuchelewa kwa kuwasilishwa sheria hiyo kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi, Katibu huyo alisema “Bado hatujachelewa kuwapa wajumbe taarifa kwa sababu hiki ndio kikao cha kwanza” aliongeza Hamad.

Tangu kupitishwa na bunge sheria hiyo na kusaniwa na Rais Jakaya Kikwete ilitarajiwa tume ya katiba ingeanza kazi zake ya kukusanya maoni ya katiba mpya mwezi huu, hata hivyo kikwazo kikawa ni kutowasilishwa katika kikao cha baraza la wawakilishi kama gazeti hili lilipoandika hivi karibuni.

Akizungumzia utaratibu wa kikao hicho ambacho ni bajeti ya pili tangu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa. Katibu alisema hakuna mswada mwengine utakaowasilishwa isipokuwa miswada ya kuidhinisha matumizi ya fedha za serikali.

Alisema jumla ya masuali 197 yataulizwa na kupatiwa majibu na mawaziri wahusika ambapo tayari tayari matayarisho ya kikao hicho yameshakamilika ikiwemo wajumbe wote waliopo kisiwani Pemba kuwasili hapa Unguja.

Tokea kuapishwa kwa wajumbe wa tume ya katiba Rais Kikwete wananchi wa Zanzibar wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na suala la kuwasilishwa sheria hiyo ya katiba katika kikao cha baraza la wawakilishi.

Wazanzibari wengi wamekuwa na shauku kubwa wakitaka kujua kitakachotokea katika baraza hilo juu ya sheria ya katiba itakayowasilishwa na waziri wa katiba na sheria.

Advertisements

18 responses to “Sheria ya katiba mpya kuwasilishwa kama taarifa

 1. SH. YAHYA WW NI MSOMI! USITUANGUSHE! HIVI DHARAU HIZI ZITAKWISHA LINI! KWANINI TUSHAURIWE NA WAJUMBE WASIJADILI KWA UNDALI. HUU MUUNGANO HATUUTAKI! TUMECHOKA MISUGUANO!

 2. Pingback: Sheria ya katiba mpya kuwasilishwa kama taarifa·

 3. kwanini wawakilishi wasiijadili hiyo sheria ya mabadiliko ya katiba ili kuuweka umma wa wazanzibari sawa katika wakati huu ambao wananchi wanatataka kujua hatma ya nchi yao ndani ya huu udanganyifu wa muungano?

  • …hawaijadili kwa sababu katika wabunge waliopitisha sheria hiyo hata wabunge kutoka majimbo yote ya uwakilishi wa Zanzibar walikuwepo…acheni kulalamika iwapo hamuijui sheria…sasa wewe wataka mbunge wa Zanzibar aipitishe halafu tena ije kujadiliwa na wawakilishi?..kama ni hivyo itabidi na Baraza la wawakilishi wa Tanganyika liundwe ili
   nalo kama hilo la Znzbr lijadili suala hilo ili kuweko na usawa

 4. Asaam aleikum,

  Hii si dharau huu ni ujinga wa viongozi wa SMZ yaani CCM wao wako tayari kutuuza ilimradi yao yanakwenda na wanapewa ulinzi majumbani mwao.

  Mimi nadhani hao Wawakilishi wenye uchungu na Zanzibar wasikubali waseme ni lazima hiyo sheria ijadiliwa japo itakuwa vigumu kwa Wawakilishi wa CCM maana Viai Ali Vuai katibuwao kashawafunga midomo lakini wasijali sisi wananchi tuko pamoja nai na watoe jubu kama isijadiliwa haina haja ya kuletwa kwani hapana mtoto mdogo hapa.

  Yenyi wejinga (CCM) wacheni ujinga enendeni kwenye njia ya uongofu.

 5. mm sina imani la BLW ila kama wawakilishi wana uchungu na zanzibar basi watokee njee ya baraza dah ninakuheshimuni wazanzibar wenzangu na daslma lakini aaaaaaaaaaaaaaah inaumaaaa

 6. kwa wawakilishi wote tunaomba msikubali kuyumbishwa , ikiwa hio sheria haitakiwi kujadiliwa na wawakilishi maanake nini? huu ni udikteta ndugu wawakilishi na mkikubali basi hamna tofauti na makhanithi bora mjiuzulu kuliko kwenda kusomewa sheria ambayo hamuwezi kuikataa au kuijadili , Nd kikwete usiwe kama juha unasaini sheria ambazo hazijadiliwi na wengine kwa kufuata ushauri walio juu yako wanakupeleka mchomo kama hujui! , katiba sio sheria za dini kwamba hazitakiwi kujadiliwa , wito kwa wajumbe wote wa baraza la wawakilishi kugomea , na kuwaambia watanganyika tunataka kurejeshewa nchi yetu MUUNGANO BASI!

 7. hii ndio taabu ya kuwa na viongozi wasio na shule , yaani wewe Katibu unazungumza kwa tabasamu hata huoni aibu? unachekelea zanzibar kumezwa , mpumbavu mkubwa !

 8. Nyinyi wazanzibari wezangu, munasema munataka watanganyika waturejeshee nchi yetu, ebo mthhh , waturejeshee kwani tunwapa? tunasema tuchukue nchi yetu, tuseme hatutaki na kuanzia muda huu kwa kushirikiana na uamsho mapambano mbele tutangazemuungano basi tugawe cha muungano kilichopo, kujadlili katiba ndio tunatafuta muungano haupo tenabwana ulikuwa ni wa miaka 10 kwa mujibu wa mkataba, ingawa wa fichwa ,maana ukitolewa tu basi mambo hadharani
  muungano haupoooooooooooooooooooooo

 9. Tatizo ni kua hapa duniani tupo wanaume wengi, lakini Vidume ni wachache sana.! Na bahati mbaya katika hilo BLW zima likakosa Kidume hata mmoja, zaidi ya ujuzi wa kike wa kuongea sana kuliko MP3. Yaani inashangaza hata mwakilishi mmoja hatoweza kujitolea kupasua KuBREAK the ICE kwa ajili ya maslahi ya Umma mzima…..Kweli viongozi hatuna, ila tunasubiri tujionee…..Kesho c mbali Allaah akitujalia kufika na uhai…By Rumhy wa Guerrara. Ukitaka kunijua kamuulize Bahry.

 10. Hivi ww Mh. Abubakar msomi wa kuaminika unaisaliti ZANZIBAR kwa sababu tu ya Uwaziri. Tunakuomba muheshimiwa please uctake kujaribu kumwaga damu za yako. Tunakumbuka uzuri ww kabla ya uwaziri ulikuwa ni mfano kw wanzanzibar. Leo unaipindisha sheria unatuuza wazanzibar. Na waakishi wengine nyny 2mewaeka sisi wananchi ss iweje leo mnatuuza kwny MUUNGANO huku mnajiandaa kuja tena kuomba KURA. Busara hekma imani hofu mbele ndio mising mizuri ya MWANAADAM.Ee jaman eee waakilish msikurupukeeeeeeeeeeee mtasababisha maafaaaaa

 11. cha muhimu kesho sote tujumuike pale baraza la wawakilishi tusubiri matokeo wakipitisha tuu basi hatoki mtu ndani na hilo jumba ndo mwisho wake kesho litakuwa holi la kufanyiya shuhuli binafsi

 12. Ndugu zangu Zanzibar ni bahati mbaya kuwa Watu Wazuri hawajazaliwa. Hawa ambao walisababisha watu wafe na wateseke wamebadilika kwa posho za vikao. Hii ya wao kukubali kusomewa Sheria kama kisomo cha maiti inaonesha ni kiasi gani wanaweza kufanya chochote kwa maslahi yao binafsi. Ivi akina Maalim Abuu, Jusa ambao mliwahi kuhubiri “People’s Power” hapo nyuma mnaridhika na hali hii. Kwa nini hamkueleza watu hapo nyuma yaliyokatika nyoyo zenu ili wasipoteze muda wao, maisha yao na mali zao kwa ajili yenu. Watu wengi tuliamini kuwa uoni wenu ulikuwa mpana zaidi ya mliowatumia kufikia hapo mlipo ! kumbe sivyo kabisa. Nyinyi leo mmekuwa sawa au chini ya wale mliwatumia. MM !

 13. Laa haula walaa quwwata illa billah.

  Dharauu jamani. Mizengo Pinda kasoro robo apatie. Ni kweli Zanzibar katika ngazi ya uongozi wa serikali SMZ sio nchi, nchi kiuongozi haiwi hivi.

  Ewe Aboubakar Khamis umegeuka Moh’d Seif Khatib?

  Je! Ukifa utakwenda kuishi Serena na sio Kaburini?

  Je CUF mbio zenu zote kumbe hili ndio lililokuwa lengo lenu la mwisho? Yaani ukubwa na kutudhalilisha zaidi bora Allah {s.w} alivyokunyimeni kumbe na nyinyi sio wazuri wala wema.

  UAMSHO bega kwa bega mpaka kieleweke. Allah {s.w} tunusuru tunamalizwa waja wako na wanafiqi.

  MUUNGANO HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 14. WAUNGWANA MIMI SI MTAALAM WASHERIA LAKINI HAPA KIDOGO NAONA KAMA SIPATI PICHA HALISI KUA BUNGE LIJADILI NA KUFIKIA MAAMUZI HALAFU RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO ATIE SAINI KUA SUALA HILO LIMEKUBALIKA SASA HII TAARIFA KWA BARAZA LA WAWAKILISHI INA MAANA GANI NAOMBA UFAFANUZI

 15. ASSALAM ALAYKUM:
  Nadhani hili litakuwa kamajaribio la kutaka kuwazima Wazanzibari, hii ni kwasababu hoja kubwa ya kupinga kushiriki katika mchakato huu ni kukiukwa kwa katiba ya Zanzibar inayotaka sheria yoyote inayotaka kitumika Zanzibar ipitiwe na kujadiliwa na BLW. Kama mtaangalia vizuri majibu ya katibu wa BLW mtagundua kuwa wawakilishi watapokea sheria hiyo kama taarifa na siyo hoja inayohitaji kujadiliwa.

  Kutokana na hali hiyo naona hapa Wazanzibari tujipange upya. Tunaweza kuona madai yetu ya kupinga kushiriki katika mchakato huu yanazimwa kimyakimya.

  Nionavyo mimi wawakilishi wetu hawana ujasiri wa kuipinga SMT.Kama ndio hivyo. Tuanze kwa kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kuwa ile sheria ya mabadiliko ya katiba inakuja lakini bado haina uhalali wa kufanya kazi Zanzibar.

  SOLIDARITY FOREVER.

  HATA MKIJA NA LUGHA GANI, MUUNGANO HATUUTAKI.

  ZANZIBAR HURU KWANZA.

 16. WAAMBIENI HAO WATANGANYIKA KAMA SISI WAZANZIBARI HATUNA HAJANAO HUU MUUNGANO WA BANDIA .
  KAMA BLW HALIWEZI KUJADILI MAMBO YA KATIBA IN AYOHUSU NCHI YETU NI IPI KAZI YAO HAPO ?
  NYINYI TUMEKUCHAGUENI HAPO MTUTUMIKIE SIO MTUUZE KWA MKOLONI MWEUSI ,KWA HIVYO HIO KATIBA YAO IKIWA HAWATAKI MUICHAMBUE AU MUIJADILI BASI ICHANENI AU WAREJESHEENI WENYEWE SISI HATUNA SHIDA NAYOO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s