Wazanzibari watakiwa kuungana kudai haki

Sheikh Mussa Juma Issa akiongea katika mhadhara uliofanyika nje ya msikiti wa Mbuyuni

Wazanzibari wametakiwa kuungana katika kutetea maslahi ya nchi yao wakati wa mchakato wa katiba mpya ikiwa njia mojawapo ya kuhakkikisha madai yao yanakubaliwa. Wakihutubia kwa nyakati tofauti katika muhadhara wa kiislam uliofanyika msikiti wa Mbuyuni Unguja jana,  Sheikh Mussa Juma wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam, ambaye aliwahi kukamatwa na kuzusha sokomoko kubwa nchini, alisema  bila mshikamano hakuna litakalokuwa hivyo amewahimiza Wazanzibari kushirikiana pamoja kupinga dhulma dhidi ya nchi yao pamoja na kuietete Zanzibar.

Sheikh Mussa alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tangu ulipobuniwa umekuwa ni wenye mashaka kwa wazanzibari “Sisi tunataka nchi yetu tumechoka na katika hili tunaomba tusiondolewe kwenye lengo letu maana kuna watu wanataka kuua hoja ya msingi ya dai la Wazanzibari”

Alisema mfumo wa muundo wa Muungano wa sasa haufai na ndio chanzo cha matatizo yote ambayo dawa yake sio kuongeza idadi ya Serikali ni kuweka mfumo mpya utakaowezesha Zanzibar kuwa na Mamlaka yake kama Taifa.

“Muungano huu msingi wake ni mbovu na hilo hatuaanza kulisema sisi watu wa Uamsho, limesemwa siku nyingi tena na wataalam waliobobea,tunaomba Wazanzibari kwa umoja wetu tushirikiane kurejesha nchi yetu katika Mamlaka yake “ Alisema Sheikh Mussa.

Kauli mbiu katika mikutano hiyo ni “Tuachwe Tupumuwe” imekuwa ikipendwa na kupata umaarufu siku hadi siku ambapo sasa vijana wengi wa Kizanzibari wameweka kuwa miito ya simu zao za mkononi.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na watu wengi, Sheikh Mussa ambaye wiki mbili zilizopita alikamatwa kwa madai ya kufanya mkusanyiko usiokuwa halali, aliwasimulia visa na mikasa ya Vyuo vya Mafunzo(Magereza) ambako alishangaa kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wafungwa waliowapa heshima kubwa ndani ya Gereza.

“Jamani  waislamu,tumepelekwa Gerezani, kule tulipoingia tu, tukapokewa kwa furaha na waislamu wenzetu waliokuwa wamefungwa,wakatueleza kuwa pamoja na wao wamo Jela,lakini wanaunga mkono harakati zetu na kututaka tusiogope jambo lolote hadi Zanzibar inakuwa na Mamlaka yake” Alisema Sheikh Mussa.

Kwa upande wake, Naibu Amiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam,Sheikh Azan Khalid alisema shutuma zinazoelekezwa kwa Jumuiya hiyo sio za kweli na zimekuwa zikipikwa kwa nia ya kuipaka matope  zenye lengo la kuwatoa katika dhamira yao.

Sheikh  Azan alisema kamwe mikutano yao haitasita hadi hapo kitakapoeleweka kwa Zanzibar kuwa na Mamlaka yake  kwani Muungano ni jambo la khiyari na sio kulazimishana. Alisema Wazanzibari wakijitegemea wataweza kupiga hatua za maendeleo.

Alisema kwamba vitendo vya uchomaji wa makanisa ni mambo ambayo wanaamini hayafanywi na waislamu bali kuna mpango maalum uliondaliwa kuviza harakati za madai ya wazanzibari katika muungano na kulitaka Jeshi la Polisi kuunda Tume maalum kuchunguza matukio hayo.

Sheikh Azan alisema kwamba Jumuiya yao imekuwa ikiandamwa kipindi kirefu tangu kuanzishwa kwake akitolea mfano mwaka 2004 walipotaka kufanya maandamano Polisi ilikubali kwa kutoa kibali rasmi,lakini siku mbili kabla ya kufanyika kwa maandamano hayo baadhi ya Masheikh wa Jumuiya hiyo walianza kukamatwa kwa visingizio mbalimbali.

“Haya yanayotokea sasa ya sisi kusingiziwa kuwa tumevuruga amani si mageni haya yameandaliwa yalianza siku nyingi ,lakini jambo la kushangaza hapa kulichomwa kuran tukufu hakuna kiongozi aliyekemea,lakini leo yamechomwa makanisa kila kiongozi anasema” Alisema Sheikh Azan.

Alisema sehemu kubwa ya makanisa yaliyochomwa hayakuwa na hati miliki kutoka kwa Mamlaka zinazohusika kwani hapo mwanzo zilikuwa ni makaazi ya kawaida,lakini wakayageuza kuwa makanisa,licha ya kuomba kwa kipindi kirefu,Serikali haikuwa imewapa.

“Nikuchekesheni naambiwa hivi juzi mheshimiwa Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd ameagiza  makanisa yote yasiyokuwa na hati miliki yapewe haraka…naambiwa jana katuma ujumbe kwa watu wa ardhi kwenda kuwahimiza hao ndio viongozi wetu “ Alisema Sheikh Azan.

Advertisements

6 responses to “Wazanzibari watakiwa kuungana kudai haki

 1. Ahahhhhhhh !! Mashekh wetu mnajitahidi kuamsha walolala wengine wemeamka, lakini hawa wengine wamekufa kiakili na kimawazo na hawa wanajua wanasikia lakini majinamizi yamewazibiti kuamka, lakufanya haya majina mizi ni kuyangoa kwanza ili walolala wagubuke toka usingizini na mwaka wa kungoa haya majinamizi ni mwaka 2015 hiyo ni dawa toshaaa! tunakuombeni mashekh msichoke nasi tuko nyuma yenu mpaka kielewekeeee!!!!!!!!!

 2. katu hatutachoka kutafuta haki zetu wazanzibar i tunajua kwamba inaweza hata kutugharimu maisha yetu,La muhimu tusijitazame sisi bali tungalie vizazi vyetu kwani hata masahaba hawakujiangalia wao lakini waliangalia zaidi uislamu na waislamu wa baadaye.inshaallah tupo bega kwa bega na viongozi wetu.

 3. Pingback: Wazanzibari watakiwa kuungana kudai haki·

 4. Kwa yeyote mwenye angalau chembe ya imani ya dini ya kiislam basi atawaunga mkono MUAMSHO.Sisi tunasema kuwa tuko pamoja bega kwa bega mpaka kieleweke inshaallah.Na inshaallah kwa nguvu za Allah tutashinda.

 5. Hilo isiwashughulishe mwenye uwezo wa kuuwa na kufufua ni ALLAH pekeyake. Wako waliohukumiwa vifo na waliotoa amri hiyo ndio waliokufa mwanzo na waliohukumiwa bado tunao akiwemo Mzee Ali Sultan Issa .
  Muislam ni bora kufa kwa kutetea DINI yake na NCHI yake kuliko kufa kwenye Banda kama Mzoga wa Punda.
  Maadui wa Ui slam wako wengi na wanawatumilia waislam waliodhaifu katika Iman ilikuudhoofisha Uislamu na Waislamu,
  Tayari maadui wameshaandika kwenye Magazeti yao wakiwahusisha wanaodai Nchi yao na kurudi tena kwa Jemshid.
  Hebu nyinyi Wajinga wa kufikiri rudidi kwa Mola wenu na murudi kwenye Taarikh ni nani unaemdanganya leo Mzanzibari au ….
  Kauli aliotoa Jemshid mwaka 1972 mpaka leo ni miaka 40 sasa na ni miaka 48 tangu yatokee Mapinduzi . Hawa wanao dai Nchi yao ni Vijana waliodhulumiwa ambao wamechoka kuteswa ,na Umri wao ni kuanzia miaka 35 kuja chini vipi hawa utawahusisha na JEMSHID ? Au kwa sababu wana ndevu basi ? .
  Acheni kauli za kijinga na kutokufikiri kama Mzee Kifimbo aliwaambia mumchukie kila mwenye Nde.Svu basi na hizo picha za Nabii ISSA{A.S}ambae kwenu ni YESU basi ziondoweni makanisani muweke za Paulo.
  Fitna zozote dhidi ya Uislamu na Wazanzibari kwa sasa hivi hazifanikiwi tena .Sisi tunaona fakhari kubwa sana kufa kwa kupigania DINI YETU NA NCHI YETU,kuliko kuishi kama Watumwa wa Tanganyika
  Hatutaki Muungano huu kwa nini mlalazimisha ???????.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s