Professa George Saitoti afariki dunia

Waziri wa Mambo ya ndani nchini Kenya, Professa George Saitoti na Naibu wake,Orwa Ojode wamefariki dunia katika ajali ya ndege

Habari za hivi punde kutoka Jijini Nairobi nchini Kenya zinasema kuwa Helkopta ya Polisi iliyokuwa imembeba Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Profesa George Saitoti, Naibu wake,Orwa Ojode pamoja na maafisa wengine wa ngazi za juu Serikalini imeanguka na kushika moto.

Habari zaidi zinasema maafisa hao wa Serikali ya Kenya wamefariki dunia pamoja na walinzi wao na rubani wa helkopta hiyo. Helkopta hiyo iliyokuwa ikielekea katika eneo la Nthiwa nyumbani kwa Naibu Waziri Ojode imeanguka katika milima ya Ngon’g nje kidogo ya Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi.

Helkopta hiyo ilikuwa na watu saba. Kumbukumbu zinaonesha kwamba nchini Kenya tukio kama hili la kuanguka kwa helkopta lilitokea tarehe kama ya leo Juni 10 mwaka 2008, Waziri wa Barabara, Kipkalya Kones na Naibu Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais Lona Laboso walipoteza maisha.

Polisi wamezingira eneo la ajali hiyo na kamishna wa polisi Mathew Iteere aliyepo katika eneo la ajali anatarajiwa kutoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo. Ajali hiyo ya helikopta imetokea katika siku ambapo Kenya inaadhimisha miaka minne tangu kutokea ajali ya ndege iliyowauwa mawaziri wengine wa serikali, Kipkalya Kones na Lorna Laboso.

Itakumbukwa kuwa Professa Saitoti ni miongoni mwa wanasiasa waandamizi na ni mmoja wa wanasiasa waliojipanga kuwania urais katika uchaguzi ujao nchini Kenya.

Wakati nchini Kenya wakiomboleza vifo hivyo huko Tanzania nako Mwasiasa Mkongwe na Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania,Mohammed Nyanga maarufu kwa jina la Bob Makani amefariki dunia.

Mwasiasa mkongwe na Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania,  Bob Makani amefariki dunia.

mwasiasa mkongwe na Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania,Mohammed Nyanga maarufu kwa jina la Bob Makani amefariki dunia. Mzee Bob Makani amefariki Dunia jioni jana Dar kwenye hospital ya Aghakhan, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeman Mbowe amethibitisha kifo hicho ambapo alisema marehemu  Bob Makani alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kupelekwa hospitali mbalimbali kwa matibabu ikiwemo nje ya nchi,amesema kuwa Mwili wa Marehemu umehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa hifadhi.  Msiba upo nyumbani kwake Mbezi Beach jirani na Rainbow.
Innalillahiwainnailaihirojiun
Advertisements

One response to “Professa George Saitoti afariki dunia

  1. Viongozi wa UAMSHO, Hamza -kwa Mtipura, Jussa -Mji Mkongwe n.k Allah awahifadhi.

    MUUNGANO HATUUTAKI.

    JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

    “When peace fails apply force”

    SERELLY.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s