Mpanga ubaya mwisho humrudia

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na waandishi wa habari huko kituo cha televisheni cha serikali (ZBC) Zanzibar

Jabir Idrissa

KUNA uhalifu umefanywa Zanzibar. Ni katika matukio mabaya yaliyoanza usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Watu wamechochewa kupambana na dola. Hili halijaelezwa na serikali. Polisi wamevamia nyumba za viongozi wa Uamsho na kuvunja milango huku wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi na familia zao sambamba na kuwatishia maisha. Polisi hawajalieleza hili. Amir (kiongozi) wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), Sheikh Farid Ahmed Hadi anasema usiku wa Jumamosi hiyo, akiwa kwake, alipata taarifa anafuatwa na polisi wa kuzuia fujo (FFU).

Akajiandaa. Mnamo saa 7.30 kweli wakafika. Wakataka mlango ufunguliwe. Hakuna aliyewatii. Wakarusha risasi hewani. Hakuna aliyetoka. Hakuna aliyepiga kelele kutokea ndani. Lakini, baada ya kuona vishindo vimezidi, Sheikh Farid akasema kwa sauti, “Nipo ndani na familia yangu tumepumzika. Kama mpo tayari, fanyeni chochote nje ila, ninaapa kwa jina la Allah, anayekuja ndani, tutakabiliana mimi sina bunduki.”

Polisi hawakujali. Wakafyatua mabomu. Wakavunja mlango na kuvuruga walivyovikuta nje. Wakataka kuingia ndani. Wakakatazana, “hapana. Mnajua nani wamo ndani? Tuondokeni.” Wakaondoka, anasimulia Sheikh Farid. Amepata simulizi kama hizo kwa viongozi wenzake wa Uamsho. Lakini sokomoko kama lililomkuta, lilitokea nyumbani kwa naibu wake, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, wakati mwenyewe akiwa nje ya nchi kwa matibabu.

Sheikh Azzan aliporudi Ijumaa, akapewa taarifa na familia yake kuwa walifika polisi wa FFU na kufanya fujo. Walifyatua risasi nje, wakavunja mlango. Wakapiga mayowe ya kumtukana matusi yeye na familia. Wakaondoka. Hakutulia. Alikwenda kupiga ripoti kituo cha polisi Mfenesini, karibu na anapoishi. Wakuu wakakana kufika kwake. Wakasema askari waliomfuata walitoka Mwembemadema.
Mwembemadema ni makao makuu ya polisi mkoa wa Mjini Magharibi.

Hawa ndio waliotuma makachero Jumamosi ile wakamshike Ustadhi Mussa Juma Issa, mmoja wa wahadhir wakuu wa Uamsho, kipenzi cha wahudhuriaji wa mihadhara ya jumuiya hii inayohamasisha Wazanzibari kuukataa muungano.

Wapo watu wamejitokeza kutoa ushahidi wa walivyoona polisi wanalipua nyumba na mali za vitegauchumi za raia wema, zikiwemo gari zilizoegeshwa Kisiwandui na Michenzani. Mwanamke anayefanya kazi shirika la ndege la Kenya Airways, gari yake iliteketezwa kwa bomu lililorushwa na polisi. Matukio yote hayo katika siku mbili – Jumamosi na Jumapili.

Leo, taarifa zimepatikana za uhalifu wa Polisi uliofanywa Jumatatu, 28 Mei, muda mfupi baada ya watuhumiwa 30 wa fujo, walipoachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mwanakwerekwe, mjini Zanzibar. Kati yao wapo viongozi wawili, akiwemo Ustadhi Mussa, wa Uamsho.

Wakati wakili wao, Abdalla Juma akiwa Mahakama ya Ardhi, Vuga, vijana wa FFU walivamia ofisi zake Amani, yapata kilomita tano kutoka Vuga. Wakapitisha mitutu ya bunduki madirishani na kufyatua risasi na mabomu ya machozi.

Hawakujali wafanyakazi waliokuwa ndani. Ni mchana kweupe. Hapana, ni mchana wa mola muumba mbingu na ardhi siku ya kazi, Jumatatu. Ipo taarifa ya Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS) kulalamikia kitendo hicho. Wamemtumia barua Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, na kumtaka asake wahusika na kuwashitaki.

ZLS wamekiita kitendo hicho cha makusudi kilicholenga kutisha mawakili wasiwe imara katika kazi yao ya kutetea wananchi wanaposhitakiwa. Polisi wanatuhumiwa sasa kushiriki vitendo vya uhalifu katika kipindi kilekile ambacho wao wanatuhumu Uamsho kuzusha ghasia mjini Zanzibar.

Ninayaeleza haya ili kukumbusha historia ya kisiasa Zanzibar inayochefua. Siasa za maridhiano zilizoanza kustawi tangu 2010 mwishoni, zinachafuliwa kwa nguvu. Ni kama zilivyokuwa zikipandikizwa na kustawishwa siku zile za giza, mara tu mfumo wa siasa za vyama vingi, siasa za ushindani, uliporudishwa chini ya sheria ya Tanzania.

Sasa wapo wasiotaka amani Zanzibar idumu. Wapo. Pengine wanampenda Amani Abeid Karume, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ambao walizijenga, bali wanachukia matunda ya maridhiano.

Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Hapana; si peke yao. Kwa jumla, vyombo vya dola, vya dola, vya dola. Dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola. Vyote vilitajwa kupandikiza chuki kwa wananchi, mgongo ukiwa vyama vingi na uimara wa CUF. Visima vikapakwa kinyesi, ofisi za umma zikawashwa kwa viberiti na makanisa yakachomwa kiajizi. Kanisa linawashwa, dakika mbili tu hao walinzi wamefika.

Ushetani ule ukakoma pale wananchi wa Shengejuu, kaskazini Pemba, walipovizia usiku kutafuta nani hasa wakihusika na vitendo vile vya kiharamia. Waliokutwa mpaka leo Polisi hawajawataja.
Ni askari polisi na mashushushu ndani ya Landrover iliyosheheni madumu ya petroli, mapipa ya kinyesi na viberiti vya kuwashia mabomu ya chupa.

Kutaka kuzubaisha umma wa Watanzania na ulimwengu, IGP Omari Mahita akaunda kikosi kuchunguza. Akamteua Robert Manumba, kachero aliyekuwa msaidizi mkuu wa DCI Adadi Rajabu, kukiongoza.

Alitaka wachunguze chimbuko, sababu na wahusika wa milipuko ile ya kishetani pamoja na vitendo haramu vya kupaka kinyesi madarasa na kukimwaga kwenye visima vya maji wanayotumia wananchi.
Tangu wakati ule, karibu miaka kumi sasa, si DCI Manumba ambaye sasa ndiye DCI, si IGP Mahita wala serikali iliyotoa ripoti ya uchunguzi huo. Wananchi waseme nini hapo? Lakini kwa sababu wahusika walijulikana na kufikia kukamatwa Shengejuu, zile fitna kuwa CUF walikuwa wahusika, zilifutika.

Tungalinao wakorofi wasiopenda maridhiano. Wahafidhina ndani ya CCM wameibuka upya wakitaka kuharibu amani na utulivu. Hawawezi kuitaja CUF moja kwa moja maana wanashirikiana nacho kuendesha serikali.

Wametafuta pa kuingilia – Uamsho. Kwa kuwa taasisi hii imechukua jukumu la kupigania haki za wananchi wasioridhishwa na mwenendo wa muungano, wanawapakazia kuwa wanavunja amani.
Kumbe bado kuujadili Muungano wa Tanzania ni uhaini. Pamoja na serikali kuruhusu Watanzania watoe maoni yatakayotumika kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watawala hawapendi watu wafikiri tofauti na wao.

Tunaona kila viongozi wa polisi wanavyojitahidi kupotosha ukweli wa kilichotendeka mjini Zanzibar, ile dhamira yao ya kupotosha inawarudia. Wanatajwa baada ya kuonekana wazi wakivamia na kuharibu mali ikiwemo ofisi za wanasheria.

Mpanga ubaya mwisho humrudia. Hawajajisafisha, wamejiumbua. Na ndiyo matokeo ya polisi nchini kushabikia siasa. Wanasubiriwa watamshika nani mchoma makanisa. Bado watafute ushahidi kuthibitisha kesi ya watu 30, pamoja na wafadhili wa Uamsho.

Advertisements

6 responses to “Mpanga ubaya mwisho humrudia

 1. Binafsi nashkuru kuelewa uhalisia wa mambo yanavyoenda na hufarijik apiakwa umakini wa wazanzibar juu ya myenendo na mbinu za mamluki dhidi ya amani ya wazanzibar KWELI HAWA NI KAMA WAKOLONI hutumia sera ya wagawe na uwatawale ili kuendelea kutunyonya. Ila natamani sana kuelewa juu ya madai yawanao jipachika WAUNGUJA kua wanadai kisiwa chao kama WAISLAMU NA WAZANZIBARI wanaopenda amani tumeliangaliaje hili na uhusiano wa madai ya muungano jee hatuoni kama ni MAMLUKI wamwpandikizwa kulinyamazisha la muungano?

 2. HAYA YOTE NI MAMBO YA USANII WA WALE WASIOPENDA MABADILIKO ZANZIBAR AMBAO KAMA MNAKUMBUKA HISTORIA UNAJIRUDIA TU, NI MBWA MKONGWE KWENYE MSITU MPYA. MIAKA ILE YA ALHAJJ KOMANDOO MAMBO KAMA HAYA YALIKUA YAKIFANYWA KULE PEMBA ILI IPATIKANE SABABU YA KUWAPIGA, KUWATESA NA KUWADHALILISHA KWA KUA WALIKATAA KUIUNGA MKONO CCM WAKATI ULE. VISIMA VILITIWA KINYESI, SHULE NA OFISI ZA SERIKALI NA CCM ZILICHOMWA KIDOGO TU NA BAADAE MKONG’OTO UKAFUATIA. BAADA YA KUGUNDULIKA KUA USALAMA WA TAIFA NDIO WAKIFANYA VILE WAPEMBA WALIPELEKEWA MELODY (FFU) LAKINI HAWAKUBADILI MSIMAMO. KILICHOFUATA WAKATI ULE MH. KIKWETE AKIWA WAZIRI WA NCHI ZA NJE AKATOA BARUA REFU AKILAANI CUF NA KUIHUSICHA NA VITENDO VILE KWA MABALOZI NA MASHIRIKA MBALIMBALI YA KIMATAIFA. SASA USANII ULE UNAJIRUDIA TENA NA WAFANYAJI NI WALEWALE KWANI HAWAFURAHII AMANI ILIOPO. TUNASEMA KUA SIKU ZOTE MUNGU HAMFICHI MNAFIKI KWANI KWA WARAKA WAO WALIOUTOA WANACHOKISEMA NI KUA DR SHEIN HAFAI KUONGOZA ZANZIBAR ARUDI KWAO PEMBA AUZE NYUMBA YA MOMBASA ARUDI PEMBA YULE SEIF WALOMTAJA PALE NI MANENO YA WASWAHILI KIRIOF TU. TUNAVYOFAHAMU SHENI NI MPEMBA NA KAULI ILE IMELENGWA KWAKE NA WATU ANAOAMINI KUA NI WAKE. HAYA NDIO HAYO MANENO YA JABIR UBAYA UNAANZA KUWARUDIA WENYEWE.
  AMA SERIKALI ZA TANZANIA HATA SIKU MOJA HAZIKO TAYARI KUBEBA LAWAMA NA KUKUBALI MAKOSA. ZIMESHAUA SANA PEMBA, ZANZIBA, DAR ES SALAA, ARUSHA NA HIVI KARIBUNI SONGEA LAKINI HATA SIKU MOJA HAIJAWAHI KUKUBALI MAKOSA. KATIKA HILI SERIKALI KUPITIA JESHI LA POLISI LAZIMA IKUBALI KUA ILIKOSEA NA HUO NDIO USTAARABU. MAMBO YALIOFANYWA NA POLISI KATIKA NCHI YA WASTAARABU HAYAKUBALIKI. MAMBO YA KUMTEKA NYARA MTUHUMIWA HUFANYIKA KWENYE NCHI ZA KISHENZI TU. MIMI NILIDHANI HAWA VIONGOZI WOTE ANGALAU MMOJA ATATUMIA AKILI NA MAARIFA NA KUTAKA IUNDWE TUME HURU KUCHUNGUZA SUALA HILI LAKINI WOTE WANAMUELEMEA ALIEANGUKA CHINI MUAMSHO. MANENO YA WASWAHILI AANGUKAE NDIE AELEMEWAE. VYOMBO VYOTE VYA HABARI VYA ZANZIBAR NA VYA TANGANYIKA VINAONEKANA VINA AJENDA YA KUHAKIKISHA WAZANZIBARI WANANYAMAZISHWA WASIDAI HAKI ZAO KWENYE MUUNGANO. YAGUJU HAPA MMECHELEWA KWANI NDIO KWANZA SHUGHULI INATAKA KUANZA. HAMTOTURUDISHA NYUMA KWA USANII WA NAMNA HII TUMESHAUZOEA MIAKA MINGI ILIYOPITA. KOMANDOO SALMINI ALITUPA KOZI YAKE MIAKA ILE. HILI LA KUDAI WABARA WATAHAMISHWA ZANZIBAR LIMETOKEA WAPI? HATA KAMA MTAWAHAMISHA WAZANZIBARI WOTE WALIOPO HUKO SISI HUKU HATUTOMHAMISHA MTU YOYOTE NA HATUTOACHA KUDAI HAKI ZA ZANZIBATR NDANI YA MUUNGANO. WAZANZBARI WAPO KENYA, UGANDA, CONGO, COMORO NA HATA UINGEREZA NA WALA HATUJAUNGANA NA NCHI HIZO. HAYA NI MASUALA YAMELETWA NA MAGAZETI YA TANGANYIKA AMBAYO YANA AJENDA YA KUWANYAMAZISHA WAZANZIBARI WASIDAI HAKI ZAO. TUTADAI MPAKA KIELEWEKE TUKO TAYARI KUACHA KILA KITU CHETU KAMA MTAAMUA HIVYO.

 3. Hakuna mwanzo usio na mwisho inshaallah, na mwsho wa hawa jamaa naona unaisha polepole.
  Kwani ni nani alodhani kwamba wananchi watakabiliana na Polisi wahuni namna ile, sasa wanajua kuwa kumbe raia wa Z’bar sio wale wa Miaka ya 1995-2005.
  Mimi naona Waislam tuungane tusiwe wanafiq ili tupate nguvu ya kuupigania uhuru wetu dhidi ya hawa Watanganyika.

  Hakuna POLISI , JESHI wala nguvu yyte ya Serikali yenye kushinda nguvu ya wananchi, kama kufa hakuna atabaki duniani ilimradi tutie nia thabit ya kuwa uislam ndio focus yetu baada ya uhuru wetu Z’bar (hatuwezi kuwa na uongozi wa kiislam ndani ya huu muungano wa kihuni).

  Na wala tusikate tamaa kwa kuwasikia VIBARAKA WA TANGANYKA KINA SEFU IIDI, MOH’D ABUDI, SHAMHUNA, VUAI ALI NA WAHUNI WENGINE (kama Kachorora, TVZ na STZ ambazo tunazijua kuwa ni za watu wa maskani) wakisema muungano hauvunjiki, huu utavunjika na wala tusishughulishwe na upuuzi wao.

 4. Ivi hawa waonao kila kitokeacho ni CUF au Wapemba hawawezi kufikiri vyenginevyo? Unajua ni hatari mtu mzima kutimia generalized approach to tackle the problem. Ndugu zangu Wa Unguja mliosoma wafahamishe hawa msiachie wakatutukanisha tukaoneka Zanzibar yote ina vilaza. !

 5. nawauliza hawa polisi wamesahau hadithi ya mtenda mema? au hile ya mchimba kisima? angalau hile ya mtegoni huingia aliyekuwemo na asiye kuwemo….. salalaaaa mashetani! majini mulopevuka! mwaka huu tuko makini mwasubiri kuumbuka! mwajifunika usoni taa imewamulika! nguo zote ziko chini stara ime waondoka! kama mumekusudia kuwadhalilisha UAMSHO! Tahadharini maji hayachotwi kwa pakacha! polisi pamoja na wapambe wao UV-CCM mwaka wenu wakupazwa umefika Wallahi hamuna njia!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s