Amani tunda muhimu

Moja ya moto uliowashwa na vijana siku ya tukio la fujo zilizotokea katika manispaa ya mji wa Zanzibar baada ya jeshi la polisi kumkamata Sheikh Mussa Juma na kusababisha hasira kwa vijana kukusanyika katika eneo la kituo cha polisi cha madema ambapo polisi walilazimika kuwatawanya vijana hao, hasira ambazo zilichangia kuwashwa moto matairi barabarani na kuweka vizuwizi vya magogo barabarani

MOJA ya majukumu muhimu ambayo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein aliahidi kuyasimamia kama kiongozi wa nchi, wakati akizindua baraza la wawakilishi, ni kulinda amani na utulivu wa nchi. Kila mtu alielewa maana ya ahadi hii. Kwamba inatokana na kuzingatia ukweli kuwa bila ya nchi kuwa katika amani na utulivu wa kweli, hakuna maendeleo yatakayopatikana.

Inashangaza kuona kwamba hata nusu ya muda wake wa uongozi ikiwa haijatimia, tayari kuna dalili kuwa uongozi wa Dk. Shein unapotea njia. Watu kadhaa wamejeruhiwa; mali zimeharibiwa; wananchi wamejaa hofu kuhusu usalama wao; na kwa kweli, amani imezorota mitaani. Kisa? Vurugu.

Tunaamini kulikuwa na uzito katika kuchukua msimamo imara kuhusu hali iliyokuwa ikiendelea Zanzibar, tangu ilipopitishwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Inawezekana udhaifu huo umetokana na kuamini kuwa ilikuwa ikitumia busara na hekima katika kuachia wananchi uhuru wa kujieleza. Hili ni sawa.

Isipokuwa, hata pale serikali inaporuhusu wananchi kutumia uhuru wa kujieleza, inapaswa kuangalia pia mwenendo wa vyombo vyake vya kusimamia sheria na kujiridhisha kuwa vinatekeleza wajibu wao kwa umahiri.

Kilichotokea Zanzibar kimethibitisha kuwa vyombo vya ulinzi na usalama visipokuwa makini katika hilo, mambo yanaweza kwenda kombo na hivyo amani ya nchi kuchafuliwa.

Kupitia safu hiihii, tumekuwa tukihimiza serikali kutambua kuwa ina wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa vyombo vyake vya usalama vinatumia vizuri nguvu zake ili kuepusha madhara yasiyo lazima.

Tunakumbusha kwa mara nyingine umuhimu huu. Kwamba isitokee wakati wowote, na katika namna yoyote ile, vyombo hivi vikatenda kosa kushindana na raia.

Kwa asili yake, vyombo hivi vinapaswa kuwa karibu na raia na kushirikiana nao katika kusimamia amani na utulivu.

Pale vitakapowachoka raia na kuamua kuwakejeli au kuazimia kuwakandamiza, viongozi wake wajue watakuwa wanafanya kosa kubwa, ambalo gharama yake yaweza kuwa kubwa isiyomithilika.

Ndicho kilichotokea Zanzibar. Polisi hawakutumia mbinu bora katika kumkamata mtu waliyeamini ni mtuhumiwa.

Hatua hiyo tu ikaibua chuki na kusababisha watu kujenga dhana kuwa wanaweza kufanya watakalo katika kulinda na kutetea haki zao.

Kinachohitajika sasa ni wananchi kukubaliana na wito wa serikali wa kubaki nyumbani kwao. Polisi kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unakuwepo. Amani inalindwa na kuiendeleza.

Zanzibar inahitaji sana amani na utulivu kuliko watu wanavyoweza kufikiria. Ni vizuri wananchi wakaacha desturi ya binadamu kutojali kile alichonacho; mpaka pale kinapomtoka ndipo hushtuka.

Fikra hizo hazifai. Sasa ni vema kila mtu athamini kitu alichoshikilia; achangie amani kudumu maana ndilo tunda muhimu kuliko mengine.

Advertisements

4 responses to “Amani tunda muhimu

 1. Uvunjifu wa amani unasababishwa na viongozi wachache ZANZIBAR kwa ajili ya kujipendekeza kwa watanganyika. Kwn kunatatizo gani kudai mamlaka ya ZANZIBAR tena kisheria. Tunahitaji kura ya MAONI ili 2zidishe aman zaid.

 2. Asaalam aleikum,

  Muandishi nakupa hongera kwa ufundi wako wa kupanga maneno lakini kunakitu nataka ni kukumbushe kwenye dhulma hapana amani na ukilingana kuwa Wazanzibar wengi ni waislam na Uislam unapinga dhulma kwahio haiwezekami kwa Wazanzibar wakaacha kudai haki yao eti kisingizio wanalinda amani.

  Kama ni kulinda amani kwanza ilikuwa hao viongozi na Polisi ndio wa kwanza walinde hiyo amani unayoielezea kwa kuwapa Wazanzibar haki yao wanayo idai.

 3. Umezungumza ukweli lakini wa kulaumiwa kwa yote haya ni SUK kwa kushindwa kwake kuchukua msimamo toka mapema. Vile vile hali hii iliyotokea inawezekana ilitiwa chumvi ili Zanzibar ionekane haikaliki.

  SUK kwa kuendelea kuwabeba watu walioikataa katika kura ya maoni kufeli kwake is inevitable! Itaenda lakini haitafanikiwa kwa wamo ndani yake wanaofanya kampeni ya kuiangusha. Mfano wa hao ni wale wasambazao karatasi za chuki ilihali wakijua kuwa kuna watu wamefanya na wanaendelea kufanya mambo yawakoseshayo watoto wao elimu bora, wake zao better facilities when going to hospital to deliver, wao wenyewe kugombana na jamaa zao kwa kushindwa kukidhi haja due to inflation na mambo mengine mengi.

  Rais wetu amekuwa hazungumzi na akizungumza hutumia lugha ya mafumbo kama mwimbaji wa KIBATI. Hajuai kuwa Serikali ni Taasisi na taassisi ni tofauti na Ukoo kwa unendeshaji wake unakuwa wazi na maelekezo yake huwa clear ili watu wayatekeleze na wakishindwa waeleze kwa nini. Toka SUK ianze tunaona Rais anakutana na Wizara na huku nje tukiona mambo nii yale au ya jana ni bora kuliko ya leo. Wizara hizi zenze watumishi wengi na wengi wao wapiga debe zinatumia budget kubwa kwa kazi za kawaida. Ukienda ofisini unakuta mtu wa kuandika saa unayoingia na kutoka, ukimuacha yeye unakuta mtu wa kukuuliza unakotoka na pengine zaidi ya moja. Nenda kwa mfano Aiport ofisi ya Director, pale kuna Security 2 wanaofanya screening, ukisha kuna wasichana wengine 2 wa kukuuliza wewe ni nani na unakwenda wapi. Ivi mtu na akili yake anaweza kutoka mjini hadi uwanja wa ndege akafata asilolijua? Nenda tena kwa Mtakwimu Mkuu wa Seerikali. Kuna KIbanda nje cha kukuuliza wewe ni nani, ukimaliza kuna kibanda tena cha kukuuliza suali hilo hilo. Nenda taasisi nyengine unakuta mtu hayumo ndani 2 Secretaries wamewasha feni na taa bila ya kujua kuwa hizi ni gharama zinazoweza kuepukwa.

  Sehehemu ya vurugu iliyotokea could also be tributed to SUK failure to deliver. Wakati wa kuanza SUK watu walikuwa na matarajio makubwa. Miaka miwili sasa matarajio haya bado kufikiwa na hawaoni mipango ya kufikiwa huko. Ina wezekana hata hawa Wasambazao karatasi za Chuki nao wanafanya hivyo due to hopelessness. Mtu ukiona anamsakama mwenzie ujue tu ana frustrations na hana pa kuzitolea. Kwa kuwa pengine CHAMA chao kitawaadhibu kuisema Serikali wanaona wawaseme Wapemba kwa kuwa wao ni toilet papers which every needs to cleans his/her shits but always not useful outside the rest room.

  Narudia wito wangu katika muda huu wa majaribu makubwa kwa Zanzibar na Tanzania wa kuamini tuamini kuwa watu sote tunategemeana, kila mtu aheshimiwe kwa kwa kile alichoifanyia nchi si kwa kipi alichokchukua kutoka kwa nchi. Chuki dhidi ya Watu fulani iondoke kwa kuwa hawa waliojenga kwenye vianzio vya maji waliruhusiwa ni waliojenga kwenye maeneo yaliyopimwa. Hawa wajao Unguja hawafati watu wanafata huduma, biashara na mambo mengine muhimu. ingetokea haya yangekuwa Pemba ingekuwa kunyume chake ndugu zangu. Hii ni principle ya kimaumbile

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s