Wanasheria wa Zanzibar wakerwa

Rais wa Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Awadh Ali Said akiongea katika sherehe za kuadhimisha siku ya sheria duniani katika bustani ya Victoria

Wamefanya kitendo hiki kwa lengo la kumuogopesha (intimidate) Wakili Abdulla Juma na labda kuwahadharisha mawakili wengine waache au waogope kuwatetea watuhumiwa wa kesi hizi zinazoendelea na nyenginezo. Mabomu hayo yameathiri sana ofisi na kuifanya kutokalika kwa siku tatu na hadi wakati huu hatujuwi athari za kiafya zilizowakuta mawakili waliokuwemo ndani ya ofisi hiyo. Vitisho na hujma dhidi ya mawakili vina lengo la kudhoofisha ustawi wa utawala wa sheria, haki za binaadamu na utawala bora. Endelea kusoma taarifa hii

ZanzibarLawSociety

P.O.BOX 3319, Zanzibar, Tanzania. Bwawani Hotel – Ground Floor, Suite # 107 Tel/Fax +255 24 2234890 Mobile: +255 773 092511 Email: zls@zanlink.com

Our Ref: ZLS/Council/09/2012 30 Mei, 2012

Kamishna wa Polisi

Makao Makuu ya Polisi

Ziwani, Zanzibar

Kamishna Mussa Ali Mussa,

KUH: MALALAMIKO YA CHAMA CHA WANASHERIA ZANZIBAR KWA KITENDO CHA POLISI KUPIGA MABOMU OFISI YA WAKILI

Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS), kwa masikitiko makubwa, kinaomba kuwasilisha kwako malalamiko yetu kufuatia kitendo cha Polisi kupiga mabomu ofisi ya wakili ya AJM Solicitors iliopo Amani, Zanzibar. Jumatatu tarehe 28 Mei 2012 majira ya asubuhi katika Mahkama ya Mwanakwerekwe iliopo nje kidogo ya Manispaa ya Zanzibar, walifikishwa katika mahkama hizo watuhumiwa kadhaa kwa mashtaka mbalimbali yahusuyo uvunjifu wa amani. Hii ilikuja baada ya Jeshi la Polisi kuamua kumchukuwa kutoka msikitini Sheikh Mussa Juma Issa, Imam wa msikiti wa Kwa Biziredi majira ya saa 1.30 usiku wa Jumamosi 26 Mei 2012. Wafuasi wake walimfuata hadi polisi Madema alipowekwa ndani. Baada ya muda kupita na taarifa kuenea ndipo waumini wa dini ya Kiislam walipoanza kumiminika kituo cha Polisi, Madema wakisubiri kujua khatma ya kiongozi wao.

Watuhumiwa waliokamatwa Jumamosi tarehe 26 Mei na Jumapili tarehe 27 Mei 2012 walifikishwa mahkamani asubuhi ya tarehe 28 Mei 2012. Kama sote tunavyoelewa, ni msingi mkuu wa sheria zetu kwamba mtuhumiwa huwa hana hatia yoyote mpaka pale Mahkama itakapotamka hivyo baada ya kesi kuendeshwa kisheria. Na ni haki ya kikatiba kwa mshtakiwa kupata utetezi wa kisheria kutoka kwa watu wanaotambuliwa na sheria kuwa mawakili. Wakili Abdulla Juma Mohamed wa AJM Solicitors & Advocates Chambers ni wakili wa utetezi katika kesi ya Jinai inayotokana na MAD/PCR/45/2012 ya Mahkama ya Wilaya Mwanakwerekwe (Mhe. Janet Sekihola) na pia kwa kesi nyengine ya Mahkama ya Wilaya Mwanakwerekwe (Mhe. Mohamed Ali) inayotokana na MKD/PCR/05/2012 inayomkabili Mbarouk Said Khalfan na Mussa Juma Issa. Wakati watuhumiwa katika kesi ya kwanza wanashtakiwa kwa uzembe na ukorofi (kif. 181(d) Sheria ya Jinai 6/2004), kesi ya pili ni ya shtaka la mkusanyiko usio halali (kif. 55 na 56 Sheria Nam 6/2004).

Baada ya kesi tajwa hapo juu kuakhirishwa, Wakili Abdulla Juma aliondoka na kuelekea katika Mahkama ya Ardhi, Vuga Zanzibar. Majira ya saa 6.30 mchana ofisi yake ya uwakili iliopo karibu na Amani Roundabout, ilishambuliwa na Polisi ambao waliingiza mtutu/mitutu ya bunduki ndani ya madirisha na kupiga mabomu ya machozi. Sisi tunaamini kabisa kwamba askari waliofanya hivi wamefanya wakijuwa kabisa kwamba kitendo chao kinakiuka maadili yote ya kazi yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao. Wamefanya kitendo hiki kwa lengo la kumuogopesha (intimidate) Wakili Abdulla Juma na labda kuwahadharisha mawakili wengine waache au waogope kuwatetea watuhumiwa wa kesi hizi zinazoendelea na nyenginezo. Mabomu hayo yameathiri sana ofisi na kuifanya kutokalika kwa siku tatu na hadi wakati huu hatujuwi athari za kiafya zilizowakuta mawakili waliokuwemo ndani ya ofisi hiyo. Vitisho na hujma dhidi ya mawakili vina lengo la kudhoofisha ustawi wa utawala wa sheria, haki za binaadamu na utawala bora.

ZLS inalaani kwa nguvu zote kitendo cha Polisi cha kupiga mabomu ofisi ya wakili. Tunasema kitendo hiki kinalitoa thamani Jeshi la Polisi na kinaondosha imani ya wananchi kwao na pia kuharibu uhusiano wa karibu unaopaswa kujengwa baina ya raia na jeshi la polisi kupitia dhana ya “Polisi Shirikishi”. Sisi kama maofisa wa mahkama tunasikitishwa sana na hali hii na tunakutaka ufanye uchunguzi na watakaobanika kufanya kitendo hiki wachukuliwe hatua zifaazo. Tunaamini kwamba utendaji kazi wa Polisi hauendi kiholela – kila kikundi kinakuwa chini ya udhibiti na uangalizi wa Jeshi la Polisi kama taasisi. Hivyo hakutakuwa na ugumu wowote kumtambua askari aliefanya uhalifu huo. Vyenginevyo utatujengea imani kwamba kitendo hiki kina baraka zote za Jeshi la Polisi.

Wako katika kuheshimu Sheria za Nchi,

………………………….

Awadh Ali Said

Rais, ZLS

Nakala kwa:

1. Mhe. Jaji Mkuu, Zanzibar

2. Mhe. Mwanasheria Mkuu, Zanzibar

3. Mhe. Waziri wa Katiba na Sheria, Zanzibar

4. Mhe. Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais, Zanzibar

5. Mhe. Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Zanzibar

6. Mkurugenzi wa Mashtaka, Zanzibar

7. Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Tanzania

8. Rais, Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS) – Arusha, Tanzania

9. Rais, Chama cha Wanasheria wa Uganda

10. Rais, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika

11. Mwenyekiti, Chama cha Wanasheria wa Kenya

12. Mwenyekiti, Chama cha Wanasheria wa Burundi

13. Mwenyekiti, Chama cha Wanasheria wa Rwanda

Advertisements

12 responses to “Wanasheria wa Zanzibar wakerwa

 1. KAMA NI UCHUNGUZI NI VYEMA UKAFANYWA NA CHOMBO HURU KWANI KATIKA KADHIA HII VYOVYOTE VILE VIWAVO POLISI NDIO CHANZO CHA MZOZO HUU. HAWA UAMSHO NI MBUZI WA SADAKA TU KWA VILE HAWANA MDOMO (VYOMBO VYA HABARI). KAMA SIO KITENDO CHA UZEMBE NA KUKOSA NADHARI NA BUSARA KATIKA KAZI YAO KILICHOFANYWA NA POLISI HAYA YOTE YASINGETOKEA. TUNA KAWAIDA TANZANIA VYOMBO VYA DOLA NA SERIKALI YENYEWE HAIJAWAHI HATA SIKU MOJA KUKUBALI KUA IMEKOSEA. SERIKALI IMEKOSEA SANA KWA KUKATAA HOJA YA UAMSHO YA KURA YA MAONI. KAMA INGEKUBALI HILI KADHIA HII INGEKUA ISINGETOKEA. HIVI SERIKALI INAOGOPA NINI KUWAULIZA WANANCHI KAMA WANAUTAKA MUUNGANO AU HAWAUTAKI? AU MUUNGANO NI LAZIMA KWA WAZANZIBARI WAKITAKA WASITAKE? JEE KAMA TANGANYIKA INGEKUA INAPATA HASARA NA INGETAKA KUJITOA KWENYE MUUNGANO ITAKUA NAMNA HII HII NA WAO KULAZIMISHWA? LAZIMA TUKUBALI UKWELI KUA SASA MUUNGANO NDIO TATIZO NA LAZIMA WANANCHI WAULIZWE KAMA WANAUTAKA AU LA KABLA YA KUENDELEA NA MAREKEBISHO YA KATIBA KWANI TUNAAWEZA KUTUMIA FEDHA NYINGI FOR NOTHING.

 2. Hakuna kurudi nyuma hapo hapo ili askari wajue wanachokitenda. Pia wakome ushenzi na dhulma na kuwafanya watu fulani ndio wanastahiki haki na wengine hawastahiki. Naomba astahamiliwe yeyote aliehusika hata kama ni nani ili na wale wengine wanaoburuzwa wakome uhuni huu. Nasisitiza tena asivumiliwe hata hawa wamezoea kuburuzwa.

 3. Poleni wana sheria.
  Poleni kwa kutotambua usemi wa viongozi wa juu wa nchi “TUTAULINDA MUUNGANO KWA HALI YOYOTE ILE” Wanachofanya hawa Polisi ni amri kutoka Amiri jeshi Mkuu wa Tanzania.

  Hata kama uchunguzi utafanyika hakuna kitachoamriwa. Kumbuka Polisi hawahwa walipowauwa wananchi wa Pemba bila ya hatia kimefanyika nini? Labda kuwapandisha vyeo maafande waliofanya udhalimu kuliko wenzake.
  Hakuna cha kufanya, tulie tu. Sasa naamini inawezekana hata kuchoma haya makanisa yamefanywa kwa mipango na ujasusi na jeshi la Polisi.

  Labda itaongeza muamko mbele ya vyombo vya sheria vya nchi jirani kiasi gani watu wazanzibar wanaponyimwa haki mbele ya vyombo vya muungano.

 4. Pingback: Time and tanganyika kufufukaaa·

 5. Haya na hawa wanaolalamika kuchomwa kanisa je hii office ya waliki hawakuiona au ndio wanawatetea wale waliowaweka madarakani?

 6. Mungu ibariki Zanzibar….Mungu zifichue hila zao dhidi ya utu wa wazanzibar wenye nia njema na ardhi na historia ya nchi yao!

 7. Pingback: Wanasheria wa Zanzibar wakerwa·

 8. mm niwambie askari wanaojifanya wao ndo wenye nguvu za kila ki2 kw kushindikizwa na wakubwa wao niwausie kua mukifanya mambo yenu sio kua hatuwajui. tunawajua nyie na familia zenu lakin wazanzibar tumekua watulivu ila siku tutakayosema basi tumechoswa sasa basi mutatujua kua hata sisi tunazo mbinu za kuwafanya na nyie mkalia kama kutalia na mzee wako basi utalia na mke wako salabu kw bolisi vibaraka mara hii tunawaangalia vyema hamutauwa watu halafu tukawaangalia munapandishwa vyeo huku muna cheka tutahakikisha utapandishwa cheo kw kutoa rehani familia yako
  hapo ndo utajua kua cheo nikitamu au kichungu

 9. Awadha

  Shida ni kuwa Mihimili hii mitatu (Executive, Judiciary na Legislature) mipaka yao haijulikani Zanzibar.

 10. Akilimand huyo ni awadh sio awadha! matatizo yote yanasababishwa na nyinyi watanganyika! na tawala zenu. kwani ni dhambi zanzibar kutaka nchi yao! aluta continua!

 11. ss tunawasikiliza viongozi wetu watupe jibu la mandamano mpaka kiweleweke hapa . Napenda kuwambia wapemba walio Dar es salma wacheni chokochoko zezu kama mnataka hili jambo letu tufanikiwe lazima mutuunge mkono huku zanzibar.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s