Raza asema kila mtu na dini yake

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini zanzibar, Mohamed Raza kwa kupitia mgeni rasmi, Rais Mstaafu wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi jana amekabidhi vifaa vya maji hamani yake sh.milioni 20, sekta ya afya milioni 10, michezo milioni 1 na sh.milioni 11 na laki nne kwaajili ya vikundi 57 vya ushirika katika jimbo hilo.

MFANYABIASHARA Maarufu Zanzibar Mohammed Raza amesema wazanzibari wana haki ya kuabudu wanachokiamini hata kama ni mbuyu kulingana na imani zao. Kauli ya Raza imekuja siku chache baada ya kutokea vurugu zinazoshabihishwa na taasisi za kiislamu ambapo makanisa matatu yalichomwa moto na mali za watu binafsi kuharibiwa na mamilioni ya shilingi kutopotea kutokana na purukushani hizo.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Uzini Manzese wilaya ya kati wakati akikabidhi vifaa mbali mbali kwa wananchi wa jimbo hilo, Raza alisema wazanzibari ni watu wapole na watu wenye kuheshimu dini za wengine na hivyo watumie utamaduni wao wa kuheshimu dini nyengine.

“Kila mtu ana haki ya kuabudu anachokitaka wapo wanaoabudu Mungu lakini wengine wanaabudu miti kwa hivyo hata mtu akiabudu mbuyu aachiwe na huo ni uamuzi wake kwa hivyo tusiingiliane katika imani za dini kila mtu ana dini yake” alisema Raza huku akiungwa mkono wa wananchi wa jimbo hilo.

Raza ambaye ni Mwakilishi wa jimbo la Uzini alisema aliwataka wazanzibari kutulia na kuacha kushabiki mambo ambayo yataleta mgawanyiko kati ya waumini wa dini tofauti ambapo zanzibar licha ya kuwa na asimilia 99 ya waislamu lakini wakristo waliopo wanaheshimika na wameishi kwa miaka kadhaa kwa amani na utulivu.

“Utamaduni wetu bwana ni kuheshimiana katika dini na hatujawahi kugombana kila mtu anaabudu na anafuata dini yake bila ya kubughudhiwa na huo ndio utamaduni wa wazanzibari kila mtu anaabudu Mungu anayemtaka kama wapo mabaniani, kama wapo wanaoabudu miti au wanabudu waungu wengine lakini tuheshimiane katika imani zetu” alisisitiza Raza.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi, amesema vurugu zinazohatarisha uchafuzi wa amani ya Zanzibar ni dalili tosha kuwa kuna watu ambao wameshavimbiwa na amani iliyopo.

Amesema kwamba hivi sasa kumejitokeza vikundi vya watu wachache ambao wanania ya kuharibu amanai ya Zanzibar na kusema kuwa lengo hilo halitofamikiwa kwa vile bado wazanzibari wapo macho.

Mzee Mwinyi amesema kuwa watu kama hao wapo katika kila pembe ya dunia na kuwafananisha na watu waliokolewa na mateso ya Firauni ambao baadae walikuwa wakitoa maneno ya kejeli kwa Nabii Musa (A.S) na wakashindwa kuthamini viti vizuri walivyoshushiwa na wakaanza kuagiza vitu vyengine.

Amesema kwamba watu hao wanaonekana ni waajabu sana kwa vile wamekuwa wakiwasemea watu mambo ambayo hayamo katika mioyo yao na kuwataka wananchi kuwa makini na watu hao.

Mbunge wa jimbo hilo la Uzini, Mohammed Seif Khatib aliwataka wananchi wa Zanzibar na wanachama wa Chama cha Mapinduzi kukaa kimya na kusubiri uwamuzi wa viongozi wao juu ya suala zima la Muungano wa Tananyika na Zanzibar.

Zanzibar mwishoni mwa wiki iliyopita kulitokea vurugu kubwa lililotokana na wafuasi wa Jumuiya ya Uamsho na Maimamu kushindikiza kutolewa kwa sheikh wao Mussa Issa, vurugu ambazo zilipelekea makanisa, vilabu vya pombe na mali ya watu binafsi kuharibiwa.

Raza ambaye ni Mwakilishi wa jimbo hilo amewakabidhi wananchi wa jimbo hilo vifaa vinavyogharimu shilingi millioni 61.4 kwa kununuliwa vifaa mbali mbali ikiwemo waya za kusambazia maji, vifaa vya hospitali sita za jimbo hilo, fedha taslim za vikundi 25 vya ushirika wa wanawake (SACCOS) na vifaa vya michezo ikiwemo mipira kwa timu 25 za jimbo hilo.

Raza alisema kuwa kitendo alichokifanya ni moja katika kutekeleza ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa kuomba kura akiwa yeye kama mtumishi wa wananchi anawajibu wa kuwapa yale ambayo aliyowaahidi ikiwa ni moja ya kulipa shukrani zao kwa kumuweka madarakani lakini aliahidi ahadi zote alizozitoa atazitekeleza kwa wakati.

Akikabidhi vifaa hivyo kwa wananchi wa jimbo hilo Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi amewataka wananchi hao kuendelea kuunga mkono juhudi za viongozi wao ambao wamejitolea kwa ajili ya kuleta maendeleo ndani ya majimbo yao na nchi kwa ujumla.

Mzee Mwinyi amesema kuwa kiongozi bora ni yule anaejitolea kwa hali na mali katika kukabiliana na matatizo ya jimbo lake na kuwasiliza na kuyatatua matatizo ndani ya jimbo na kuwataka wananchi hao kuendelea kumuunga mkono mwakilishi wao ili aweze kuwatatulia matatizo ndnai ya jimbo lao kwani kumuunga mkono kwao kutampa nguvu za kuendeleza maendeleo zaidi ya jimbo hilo.

Iidha Mzee Mwinyi amemuusia Mwakilishi huyo kuacha kusikiliza maneno ya watu ambao wanampinga lakini badala yake afanya kazi na wananchi ili kuwanyamazisha wapinzani wake kwa vitendo kwani wanapomuona anajitolea kuleta maendeleo ya jimbo lake wapinzani wake watakuwa wamepata jibu sahihi kwa kuona maendeleo.

“Usisikilize maneno ya watu kwani umeanza kupingwa zamani kabla ya kupata wadhifa huu lakini wewe silaha yako kubwa kushikamana na wananchi wao na wananchi nanyi shirikianeni na muungeni mkono mwakilishi wenu ili mpate maendeleo kwani jibu la wapinzani wako ni maendeleo katika jimbo lako na wale waliokuwa wakisema Raza hawezi watakuwa umeshawajibu kistaarabu wakiona maendeleo yako jimboni” alisema Mzee Mwinyi.

Advertisements

9 responses to “Raza asema kila mtu na dini yake

  1. Mheshimiwa hii nzuri ya kuwapatia watu mipira ya maji. Hatahivyo, itabidi utafute njia bora ili watu hawa wasikutafute usaidie kusiba leakages usambzaji utakapoanza. Wanasiasa kufanya mtaji shida za watu Zanzibar ndio kiini cha watu wa hapa kutojituma ili wajiletee mandeleo yao wenyewe.

  2. we mzee umati wote ule unasemewa na watu wachache?huwajawahi kuwasikia wakisema wenyewe?tafuta cd zao utasikia wakisema tena kwa nguvu hatuutaki muungano.

  3. Hata mimi naamini ni wachache sana ambao hawataki muungano. Sasa tunakiogopa kitu gani kupiga kura ya maoni? Tukifanta hivi tutawafedhehesha hawa.

    Tusiwe waoga tukaendelea kuwakandamiza watu na kuwatawala kimabavu

  4. Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Uzini Manzese

    Hivi nyumbani tayari kuna wilaya za Manzese ??????

  5. huyuu mzeee amefana nisha wazanzibar na kaumu ya musa je nani musa wetu kwa hiyo yeye ni firauni wetu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s