Mhadhara wafanyika kwa amani

Wazanzibari wakiwasikiliza viongozi wa uamsho (hawapo pichani) katika mhadhara uliofanyika leo jioni katika msikiti wa Mbuyuni baada ya jeshi la polisi kupiga marufuku kufanyika mhadhara katika viwanja vya Lumumba ambapo ulinzi mkali uliimarishwa katika viwanja hivyo.

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) jana imefanikiwa kufanya mhadhara wake katika viwanja vya Malindi katika hali ya amani kabisa. Mhadhara huo awali ulipangwa kufanyika katika viwanja vya shule ya Lumumba lakini jeshi la polisi lilipiga marufuku na kutaka wananchi kutoshiriki katika mhadhara huo kutokana na hali ya kiuslama.

Viwanja vyote vya Lumumba jana vilionekana vimezingizwa na ulinzi mkali tokea majira ya saa sita mchana huku magari ya polisi wa kutuliza ghasya FFU wakizunguka zunguka katika maeneo yote ya mji wa Zanzibar.

Mwananchi ilishuhudia vijana mbali mbali wakiwa kando ya uwanja wa Lumumba na wengine kujibanza vipembeni wakisubiri kuingia uwanjani lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarishwa wananchi hao walishindwa kusogea na walikaa umbali mkubwa wa uwanja huo.

“Ulinzi naona sio wa kawaida na inaonesha hawataki watu hata kusogea umbali wa mita mia mbili, si mnaona mabunduki yake yalivyosimamishwa? Kila mmoja amebeba bunduki yake wamefunga kabisa uwanja” alisema kijana mmoja ambaye alikuwa amekaa kusubiri kuingia uwanjani.

Maelefu ya waumini walihudhuria katika viwanja vya Malindi katika manispaa ya mji wa Zanzibar ambapo viongozi wa jumuiya hiyo walikutana na kukaa msikitini na kuanza kwa sala ya alaasiri na baadae kuanza mhadhara ambapo awali baadhi ya watu walikuwa wakiogopa kusogea katika ameneo ya msikiti huo kutokana na ulinzi mkali kuka kando ya barabara zote za darajani, malindi na barabara ya kuendea Bwawani.

Akizungumza kwa njia ya simu Kamishana wa polisi Mussa Ali Musa alisema mhadhara wa Lumumba haukuweza kufanyika kwa kuwa jeshi la polisi lilitekeleza amri ya serikali ya kutoruhusu mihadhara na mikusanyiko katika kipindi hiki.

Lakini alisema kufanyika kwa mhadhara huo katika viwanja vya Malindi wanahesabu kwamba bado hapo ni maeneo ya msikiti na hivyo hawajakataza watu kuendelea na shughuli zao za kidini iwapo watadumisha amani na usalama wa nchi.

Akizungumza katika mhadhara huo Sheikh Farid Hadi Ahmed amesema jumuiya na taasisi za kidini zitaendelea kufanya mihadhara yake na wataendelea kudumisha amani kwa kuwa lengo lao ni kutoa sauti yao ambao wanadai Zanzibar huru yenye mamlaka kamili.

Sheikh Farid alitoa pongezi wa jeshi la polisi na kamishna Mussa kwa kufahamu lengo la jumuiya hizo na kueleweshana namna ya kudumisha amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho wananchi wa Zanzibar wamegawanyika kutokana na misingi yao ya kivyama.

“Sisi bado tunahitaji kupata utulivu, amani na umoja na hivyo tunapaswa kuwa makini na watu ambao wamekusudia kutugawa lakini tuwe macho na watu kama hao” alitahadharisha Sheikh Farid.

Kwa upande wake Kiongozi wa Uamsho Sheikh Mselem Ally alisema wazanzibari wanadai Zanzibar yao na hivyo hakuna kitu ambacho kitawarejesha nyuma katika madai hayo hadi hapo watakapopata haki yao lakini wataendelea kudai mpaka mwisho wa nguvu zao.

“Sisi madai yetu ni kutaka Zanzibar yetu yenye hadhi na mamlaka kamili kwa hivyo haya yanayotokea ni lazima tuwe na busara na tuwe na subira katika kudai haki yetu lakini tutaendelea kudai mpaka mwisho” alisisitiza Sheikh Msellem.

Sheikh Msellem alisema wazanzibari baada ya kutenganishwa kwa miaka kadhaa sasa wanatakiwa kujua wanachodai ndnai ya muungano na wasikubali kabisa kugaiwa kwa misingi ya kivyama kwani kumekuwepo na kitendo cha makusudi cha kuwagawa waumini wa kiislamu.

Azzan Khalid Hamad ambaye alikuwa nje ya nchi kwa matibabu alisema wazanzibari wamegawanywa kiwa muda mrefu na katika hili ilitokea khitilafu na baadhi na watu kuchukua nafasi ya kutaka kuwagawa tena jambo ambalo alisema wameweza kulirekebisha.

“Wakati wenzetu watanganyika wanaendeleza nchi yao sisi tunagombanishwa lakini tunasema kwa sasa hamtugawi tena na tumeshawafahamu “ alisema na kusisitiza suala la umoja na mshikamano kati ya serikali na taasisi hizo za kidini.

Alisema taasisi hizo zina imani kubwa sana na Rais wao Dk Shein na Rais Kikwete lakini wanaamini kwamba kauli walizotoa wamezitoa kutokana na kupotoshwa na watendaji wao lakini wakaahidi kuwa na mashirikiano mema na viongozi wao kwani nia ni kuweka amani na utulivu katika nchi.

Jeshi la polisi lilionekana likiranda randa katika eneo la darajani, michenzani, na barabara za viwanja vya Malindi ili kudhibiti iwapo kutatokea vurugu lolote, lakini hata hivyo mhadhara umemalizika kwa salama bila ya kutokea fujo na wananchi wameondoka katika viwanja hivyo kwa usalama wakati jeshi hilo likiwa kando mno na wananchi waliokusanyika.

Advertisements

12 responses to “Mhadhara wafanyika kwa amani

 1. Hii ni aibu kubwa kwa kikwete na Shein na hao naadui wengine CCM wanaonesha wazi kuwa wao ndio wanaoazisha fujo walitaka kuua watu lakini M/mungu mkubwa kawalani wameadhirika.

 2. Kiukweli kwamba tvz ichangia sana kug0mbanisha watu,mi nahisi bad0 haijafikia kuitwa shirika la (zbc).Naiitwe vilevile tv kis0nge,kwa maanaip0 kichama zaid.

 3. Tv yetu zanzibar ni bora kusikiliza kelele za MBWA kuliko tv hii. Lkn tatizo ni serikal kw sbb weng wanaofanya kaz kwny shirika hili ni watu wa maskani za CCM na hio ndio sbb ya kupata ajira zao. Hivyo haishangaz kw wao kufanya tv km ni ya maskani KISONGE au KACHORORA. Ila kumbuka ww unayepotosha ukweli kwmb ipo siku ukwli utadhihir cjui utakimbilia wapi. Kuwa mwadilifu acha ujinga ili upendwe na ALLAH

 4. Vyama isiwe sababu za migawanyik saiz zenj mbele vyawa nyuma angalien mfan wenzetu tanzania bara linapotokea suala la kitaifa hakuna chadema wala ccm wote kitu kimoja je vyama hivo vp znji tu. Chengne mbna makund ya kidn yanayofanya mihadhara tz bara yapo na hayakandamizw je kuna nin amken muangalie dunia ktk pande zote msiangalie ktk masafa madogo chengne viongoz msikubal kugombanishwa na ndugu zenu wa kiislam mkagombana huku watu wamepoa nyiny anaamrishwa ouvu.

 5. Ndugu zangu – Zanzibar tatizo lake kwa sasa ni kuwa inapita kwenye kipindi cha mpito, tofauti na kile cha baada ya Mapinduzi lakini. Katika hali hii ilitakiwa iwe na viongozi wanakubali kushauriana na pia kuonesha njia. Mimi kwa maoni yangu viongozi wa aina hii kwa sasa hatuna. Kukosekana kwa viongozi wenye sifa hii katika kipindi hiki cha mpito ndio kumepelekea kutoka haya yafuatayo:

  1. Kuibuka makundi ya kutaka kujaza nafasi iliyoachwa wazi na ombwe la unogozi. Makundi haya yawe ya kidini au ya kijamii au ya kibaguzi yapo kwa kwa kuwa kwenye mtafaruku asemaye kuhusu uokozi ndie huwa Mungu. Watu wa uma wa Firauni walikuwa katika mtafaruku hawakujua Mungu wa kweli ni yupi ndio Firauni akajita Mungu na Wakamkubali. Mnakumbuka hata Mussa alipotumwa akabanisha ukweli hawakuacha mambo yao waliabudu “Kidama” Mussa alipokwenda Sinai. Inachukua muda watu kuacha waliyayazoea. Zanzibar inafanywa na watu ambao hawatofautiani na wale wa uma zilizopita. Kwa sababu hii na ikichangiwa na ombwe hili la unogozi ndio mana Zanzibar ikatika hali hii leo.

  2. Maendeleo kusita huku ubinafsi ukishamiri. Inasemekana kuwa Uchumi wa Zanzibar kama ulivyo kwa nchi za jirani unakuwa. Hata hivyo ukuaji huu haujaonekana katika maisha ya kawaida ya waliowengi. Si juu ya uchambuzi huu kusema kuwa ni kweli uchumi unakua au laa. Vyovyote itakavyo kuwa kinachoonekana ni ubinafsi kushamiri na hivyo kupunguza kasi ya maendeleo ya nchi. Kwa sababu ya ubinafsi kuna watu wanajihisabu kama ni raia ya wa daraja la pili hapa Zanzibar. Dr. Mokiwa alipodai “kuwa ni Wakiristo tuu walio katika daraja hili” alkosea wapo wengine. Angeuliza sana angetajiwa na pengine hata na hao Wakiristo aliowataja kuwa wanaonewa. Hivi sasa wakati SUK inajitahidi kuleta utengemano miongoni mwa watu wabinafsi wanasambaza vipeperushi vya kudai Wapemba waondoke Unguja. Pengine wanafanya hivi labda kwa kuwa Wapemba ni Wageni Unguja na Mgeni Hachomi Pweza Akanuka. Sisemi Wabinafsi ni sahihi au si sahihi kwa uamuzi wao wa kuwafukuza Wapemba. Hata hivyo, naomba waelewe kuwa nchi haijengwi ni jamii ya aina moja. Kuna taasisi moja hapa ya Serikali kwa kuwa inafanywa na watu wa aina moja haishi kufanya madudu. Kwa mfano kuna kipindi walichapisha T- Shirt – na hawa wote na Mukbwa wao walishindwa kujua tofati ya neno FARE na FAIR = Mashati yao yakaja mitaani yakiwa na FREE AND FARE ————————-.

  Hii ilionesha jinsi gani diversity ikikosekana mambo yendavyo mchomo. Hivi karibuni kijana moja alinadika barua akimwakilisha boss wake na nilipoisoma haina kichwa wala miguu. Nilitamani mtoto wangu aje amfunze huyu kijana kiengereza chap Chap ili asiabishe SUK ambayo yaongozwa ni watu wenye elimu na haiba ya juu. Katika hali hii ya Zanzibar kukubali Ubinafsi mambo hayataenda vizuri dumu dawamu!

  Kwa kuwa karibu tunaingia katika Afrika ya Mashariki tusubiri kuwa watumwa tena sasa wa Wajukuu wa John Okelo tuliye mfukuza. Ubinafsi ulisababisha mwana wa mwanzo wa kizazi cha Adam kumua nduguye tena eti kwa Mke tu. Sasa hili halitokei kwa wake tena wazuri wapigiwa Mbwa. Wabinafsi hawa yabidi wajue kuwa Zanzibar imepita kipindi kirefu tena kigumu. Inabidi iachiwe ipumue kwa upana zaidi kuliko Mashekhe waonavyo. Kukiwa na mahitaji mengi kwa wakati moja inakuwa vigumu kushughlikiwa.

  3.Matumizi mambaya ya Madaraka bila ya Checks and Balances – Leo Zanzibar kwa sababu ya kukosa ungozi thabiti watu wanatumia vibaya madaraka huku Mhimili wa kutoa checks ukijengwa na ndoa ya CUF na CCM. Kiongozi moja alionekana shati la Chama chake huku akiendesha gari la Fahari la SMZ. Si hivyo tuu viongozi hawa wanaweza kufanya lolote wakati wowote ule na huku wakicheka. Culture of impunity imewaleswesha kupita kiasi zaidi. Hii inatokea kwa kuwa hakuna kusema akasikika na akachukua hatua. Inafurahisha kuwa Kundi la Wanaokataa Wapemba wanadai Katiba Mpya kwa Zanzibar. Inasikitisha lakini hawazungumzi kuwa Katiiba ijayo ioneshe madaraka ya watu na mipaka ya madaraka yao. Kundi hili halijui kuwa kudai wapemba waondoke pasi na misingi mizuri ya kuongozana kwa wataobaki hali itarudi vile vile na sasa itakuwa vita vya KAE KUU na vitongozi vyengine Ila Akhiri l’aya!

  Zanzibar ya sasa na ya baddae ni lazima iandae si VISION ya Kuomba pesa za Wafadhili kisha zikajengewe Nyumba au kuolea wake na wengine sawa na Wajukuu zetu – Inabidi inaendae Mazingira ya inclusiveness ili kila mtu ajihisi ni sehemu ya Zanzibar ama awe Mbara au Mpemba au Mkae au Mtumbatu nakadhalika. Hawa wote si wanategemeana lakini wameona na wana watoto wengine hawajui hata kwao ni Wapi! Tujenge jamii mpya inayoheshimu taratibu, kusikilizana na kuwa tayari kujima kwa faida ya wote. Ubinafsi haufai, Matumizi mabaya ya madaraka hayafai. Viongozi walikubali kuwa viongozi waoneshhe njia na wawe tayari kuwasubulu wanaharibu kwa njaa zao binafsi

 6. mwenye macho haambiwi tazama.mhadhara umefanyika kwa amani na utulivu,cha kshangaza hamna hamna hata gazeti lililoripoti hii ni kwa sababu ya kuona aibu baada ya kujaribu kuleta uwongo ya kuwa uamsho ndio walioshiriki katika matukio ya uchomaji makanisa ili kupotosha ulimwengu juu ya madai halali na ya msingi.Baada ya kuona uamsho wana amsha watu na watu wanaamka kwa kasi ya ajabu mgunya na wenzake wakatafuta namna ya kuwazuia na vipi watawazuia hali yakuwa mihadhara yote inamalizilika kwa amani na salama.siku walipopata nafasi walitumia kuudanganya ulimwengu kuwa hawa uamsho ni watu wavurugu wanawachukia wakristo ili madai ya wazanzibar yasiwe na nguvu kimataifa. nafikiri umechelewa tena sana.

 7. Bila ya tume ya uchunguzi Raisi Kikwete na Waziri wa Tanzania Dr. Shein mmepata wapi haki ya kuwalaumu na kushutumu waislamu na UAMSHO ?.

  Je! Kama ni makanisa kuchomwa mbona Misahafu imechomwa Tanganyika na Zanzibar hatujakusikieni kusema wala kushutumu Ukristo?

  Je! Mbona Muislamu amepigwa mpaka akauliwa na wakristo Shinyanga kwa kukemea kwake kudhalilishwa Al-qa’abah na hatukukusikieni kusema kitu?

  Je! Mnaushahidi gani kuwa UAMSHO na waislamu ndio waliochoma makanisa na sio CCM wenyewe na Wkristo ili kuwapaka matope Wazanzibari washindwe kudai nchi yao?

  Je! Ni nani kati ya waislamu na WAKRISTO anahistoria ya kufanya propaganda katika nchi hii ili kumchukizisha mwenziwe katika nchi hii na kuvuna huruma ya serikali?

  Je! Hamuoni kuwa mnawapa ujumbe wazanzibari kuwa wawachukie wakristo na wagundue kuwa ni watu wasiokuwa na shukurani ni wala hawasharifiki na hawafai kukaribishwa Zanzibar?

  Je! Wazanzibari wakiamua kuwahujumu wakristo kikweli kweli ili kuwakomesha mtaweza kuwakingia kifua eti kwa bunduki na mabomu? Je! Mnafikiri wazanzibari wanahitaji bunduki na mabomu ili kutekeleza hili au vibiriti, petroli, mafuta ya taa, pilipili, magae ya chupa, upupu n.k vinaweza kubeba jukumu?

  Najua wazanzibari hatuna niya ya hayo lakini dalili zinaonesha kuwa Maraisi nyinyi na serikali zenu mnataka kutupeleka huko, lakini sawa twende.

  Nchi hii si ya mtu yeyote ila ni ya Wazanzibari wenyewe. Dr. Shein hatukuuzia tuongoze tupate nchi yetu.

  MUUNGANO HATUUTAKI.

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 8. Angalia Zanzibar kwa kukosa Uwakilishi inavyogharimika. Wabunge Wetu katika EAC wanakwenda wakirudi tuu. Matangazo kama haya wala hawayajui. Mtume wetu Muhamad alikuwa hajui kusoma wala kuandika. Mungu alipotaka kumpa uongozi alimleta Jibril akamsomesha kwa elimu ni nguzo ya uongozi. Sisi twaongozwa na akina————- ambao watoto wao japo wamesoma wanasherehesha chuki za Unguja na Pemba. Huyu mtoto wa RC SMZ ambaye anasherehesha maandishi ya chuki aulizwe mambo kama ya hapo chini Zanzibar inayoyakosa anayafurahia.

  Home
  SCHOLARSHIP OPPORTUNITIES FOR EAC UNDERGRADUATE STUDENTS 2012
  Submitted by wamai on 24 May 2012 – 11:38am

  Category:
  General
  East African Community (EAC) in cooperation withArcadia University – USA is pleased to announce scholarship opportunities for undergraduate students from EAC Countries interested in Human Rights and Development in Africa.
  The Undergraduate Human Rights Program will be held at the EAC Nyerere Centre for Peace Research in Arusha, Tanzania from 5 June to 14 July 2012. A single course on human rights and capacity-building in East Africa will be taught.
  Interested East Africans should immediately submit their applications, including curriculum vitae, all transcripts (or at least the latest one), a personalized letter of recommendation and an application letter to the EAC Nyerere Centre for Peace Research.
  Please send your application to: adjovir@arcadia.edu with copy to bkaboha@eachq.org.
  Deadline: Not later than 30 May 2012 at 4:00 pm, Arusha time.
  See Attachments for details
  For more information on the EAC Nyerere Centre for Peace Research and the abovementioned program, please visit our website at http://www.eac.int/ncpr. You could also visit the page on the programs from the Arcadia University website:http://www.arcadia.edu.
  Downloads and Essential Attachments:
  Scholarship Opportunities For EAC Undergraduate Students 2012-Acardia University
  Scholarship Opportunities For EAC Undergraduate Students 2012-Acardia University
  Scholarship Opportunities For EAC Undergraduate Students 2012-Acardia University

 9. mimi sina cha kuongeza ila nadhani ujumbe umefika , wazanzibari tunahitaji tupumue , tumegawanywa kimakundi kwa mda mrefu eti wapemba na waunguja tofauti ambayo athari yake ilionekana haikuzaa matunda ,lengo la mgawanyo huu nadhani linajuilikana kwani walengwa wanasema , wagawe uwatawale, na ndio maana tumetawaliwa hatuna uhuru, leo rais wetu mpendwa wa wazanzibari akitoka tu zanzibar hana thamani thamani yake bora waziri mkuu wa Tanganyika, jee hii ni haki ,leo hii zanzibar kama ni nchi haiwezi kupitisha au kusaini mswada wowote wenye maslahi na zanzibar hadi upitie bara jee uhuru uko wapi?,waziri yeyote wa muungano maana yake ni waziri wa zanzibar na tanganyika jee ni waziri gani wa muungano alotetea maendeleo ya zanzibar, jee huu ni muungano wa aina gani ,yakowapi maoni ya wananchi yiliyokusanya kukubali muungano huu au ni makubaliano ya wachache,na walikubaliana mambo mangapi? zanzibar iachiwe ipumue?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s