Uamsho wasisitiza mhadhara kesho

Abdallah Said Ali akizungumza na DW hivi karibuni kufuatia vurugu lililozuka mjini Unguja wiki iliyopita kufuatia kukamatwa kwa Sheikh Juma Mussa Issa na kuzusha mvutano kati ya jeshi la polisi na jumuiya ya uamsho na taasisi za kidini

(b). Kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Doctor Ali Mohd Sheini kwa waandishi wa habari siku ya tarekhe 31/05/2012 ikulu mjini Zanzibar haikusimama katika kuzuiya Mihadhara, Makongamano wala Mikusanyiko ya aina yoyote bali ilisimama katika kulinda na kudumusha amani, tunampongeza Mh Raisi kwa hilo na hilo kwa kuwa amelitambua wazi ndilo lengo pamoja na dhamira ya Jumuiya yetu.

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR

Afisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mjini/Magharibi,
Sanduku la Posts 237
Zanzibar.

KUH: KUZUILIWA KUFANYA MHADHARA WA AMANI KATIKA VIWANJA VYA LUMUMBA NA JESHI LAKO LA POLISI

Tafadhali rejea barua yako yenye kumb:RPHQ/MJN/58/VOL.V/59 ya tarekh 01, JUNE, 2012 ambayo ina kichwa cha maneno kuhusu Taarifa ya Mhadhara.
Jumuiya yangu imesikitishwa saana na hatua yako pamoja na Jeshi lako la Polisi ya kutuzuilia kufanya mhadhara wa amani ambao kwa mujibu wa Sheria za nchi ni haki yetu na imeonelea ikuandikie barua hii kwa kuwa sababu ulizozitoa za kuzuiya mhadhara huo si za msingi wala si za kisheria.
Baada ya kukaa pamoja na kujadili hoja ulizozitoa na zilizopelekea jeshi lako kutuzuilia kufanya mhadhara huo wa amani tumeonelea kukuomba wewe pamoja na jeshi lako la Polisi kuyazingatia mambo yafuatayo na tunaomba majibu rasmi juu ya hayo-:
(a). Kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari pamoja na magazeti ya ndani ya nchi, aliyetoa amri ya kuzuiya kufanyika mihadhara, makongamano, maandamano pamoja na mikusanyiko ya aina yoyote ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Raisi ndugu Mohammed Aboud ambaye kisheria hana nguvu juu ya hilo.

(b). Kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh Doctor Ali Mohd Sheini kwa waandishi wa habari siku ya tarekhe 31/05/2012 ikulu mjini Zanzibar haikusimama katika kuzuiya Mihadhara, Makongamano wala Mikusanyiko ya aina yoyote bali ilisimama katika kulinda na kudumusha amani, tunampongeza Mh Raisi kwa hilo na hilo kwa kuwa amelitambua wazi ndilo lengo pamoja na dhamira ya Jumuiya yetu.

(c). Barua yako uliyoitowa kwa Jumuiya yangu ya tarekh 01/06/2012 haisimami kunizuiliya kufanya na kuendelea na shughuli zangu za Mihadhara, Makongamano bali imesimama zaidi kunipa taaarifa juu ya Kauli ya Serikali ambayo kama nilivyokuelezea hapo juu imetolewa na mtu ambaye Kisheria hana nguvu za kufanya hivyo.

Kwa mantiki ya hoja nilizokuelezea hapo juu inaonekana wazi kuwa Jeshi lako la Polisi limeazimia kufanya uvunjifu wa amani pamoja na kufanya mauwaji kwa raia wasio na hatia, hii inatokana na kauli ya Jeshi lako katika barua uliyoniandikia ya kuwa jeshi lipo tayari kuzuiya kwa nguvu za aina zote mhadhara huo.

Napenda kukufahamisha kuwa kufanya mihadhara, makongamano pamoja na Maandamano ya Amani katika nchi yoyote ile inayofuata Demokrasia ya kweli ni kutii sheria na sio kuvunja sheria kama haya yanathibitishwa katika Katiba zote, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar, tafadhali rejea ibara ya 18 (a,b,c,d) na pia rejea ibara ya 20(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia ibara ya 18(1) na 20(1).
Kutokana na maelezo hayo hapo juu, Jumuiya yangu bado inayofursa ya kufanya Mihadhara pamoja na shughuli zake kwa kufuata Katiba ya nchi na kufuata katiba ya Jumuiya iliyoitunga, hii ni kwa sababu mpaka sasa haina ushahidi wowote wa Kimaandishi juu ya kuzuiliwa kufanya shughuli zake.

Kwa kuwa Jumuiya yangu ni Jumuiya yenye lengo la kulkuza na kudumisha amani katika nchi, viongozi wa Jumuiya wapo tayari kukaa chini pamoja na viongozi wakuu wa Jeshi lako la Polisi kulijadili suala hili na kulipatia ufumbuzi kabla ya madhara makubwa ya umwagaji wa damu ambayo yameazimiwa kufanywa na Jeshi lako la Polisi yasije kutokea.
Kumbuka ni wajibu wa Jeshi la Polisi wanatakiwa wafanye kazi zao kama wanavyotakiwa kwa mujibu wa muongozo wa haki za binadamu kwa Polisi unaosema kwamba polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu. Kila mtu anayo haki ya kuwekewa mazingira muafaka ya kitaifa na kimataifa yatakayomuwezesha kupata haki zake za binadamu.

Polisi wana jukumu la kutunza amani na utulivu na jukumu la kutoingilia haki za watu isipokuwa tu kwa minajil ya kulinda haki za wengine.

Polisi na vyombo vingine vya dola wana jukumu la kuheshimu, kulinda na kutetea haki za binadamu kwa watu wote.

WABILLLAH TAWFIQ

Natanguliza Shukrani

…………………………
ABDALLAH SAID ALI.
KATIBU MKUU.
JUMIKI.
Nakala:
MUFTI MKUU ZANZIBAR
IGP – Tanzania
CP – Zanzibar
RPC – Mjini Magharibi
RCO – Mjini Magharibi
OC FFU Mjini Magharibi
RSO – Mjini Magharibi
DC – Mjini Unguja.
DSO – Mjini Unguja.
Balozi mdogo wa Marekani Nchini Zanzibar
Vyombo vyote vya Habari

Advertisements

12 responses to “Uamsho wasisitiza mhadhara kesho

  • Ndugu zangu polisi wameamua kuanzisha tena vurugu ila nawaomba watu wasiogope hivi vyote ni vikwazo vya kutuzuia tusidai haki yetu. Tuwe pamoja kwa uwezo wa Mungu tutashinda. JAMUHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

 1. POLISI WA ZANZIBAR HAWANA TOFAUTI YOYOTE ILE NA MBWA. WAKIAMBIWA SUUU WANAFUKUZA NA KUUUMA. POLISI SIO KUTUMIA MAGUVU TU LAZIMA WAJIFUNZE KUTUMIA SAIKOLOJIA NA HEKIMA. KAMISHNA MUSSA NA HAO ASKARI WAKO MNAKOSA HEKIMA NA MTAIPELEKA NCHI PABAYA. MTAUA NA SERIKALI ILIYOPO KWA KUA INA HISTORIA YA KUUA TOKEA 1964, 2001 NK. ITAKULINDENI LAKINI MJUE MIKONO YENU IKESHROA DAMU HAISAFIKI TENA NA IKO SIKU SHERIA ITAKUANDAMENI TU HATA MLINDWE VIPI. MUANGALIENI MUBARRAK YUKO WAPI SASA? MUSSA, MUSSA NDUGU YANGU USIONE HAO WANAOKUTUMA WANAKULINDA MSALABA UTAUBEBA PEKE YAKO.

  • Minawapongeza uamsho kwa juhudi walioionesha kwa serikali juu y kudai haki ye2 y nchi nakuondokana mila potofu,udhinifu,wizi na maadili maovu ktk kisiwa cha zanzibar pia kudai mali ze2 hazitendewi haki wizi m2pu muungano must broken

 2. Amir Farid na wenzake tayari wameshapoteza heshima ndani ya jamii ya Wazanzibari, ambao hakuwajuwa kuwa watu wavisiwa hivi hawapendi fujo wa ghasia, haya anayoyalazimisha sasa yawe ni kuishiwa na hekma na busara kwani hata dini yetu inayakataza.Mapambano ya kuidai Zanzibar hayakuanza kwake yalianza pale tu yalipofanyika Mapinduzi 1964 na Muungano 26.4.1964 wengi waliopambana walipotezwa, walifungwa,waliuliwa na wengine kwa mamia wakakimbia nje ya Nchi. lakini mapambano hayajasita hatua kwa hatua zimefuatia, wengi walishiriki kwa wingi katika mihadhara yake mijini na mashamba na umma ukimmuelewa vya kutosha jambo ambalo adui likimuumiza kwa kutakaburi kwake sasa ameamuwa kufanya mapambano ya kijinga kabisa ambayo yanaimaliza Zanzibar kwani Maadui sasa wameshashika mpini watatumaliza, wengi washasema nae Farid asiingize Nchi ndani ya vita hasikii ameamuwa kupambana kijinga, matokeo yake sasa waliomakini wameshaanza kumshuku waliokuwa wanamuamini sasa wana mkwepa, waliokuwa wampenda sasa wanamchukia, haya yote ni kwa kichwa ngumu yake, mapambano ni mbinu sio ubabe kazi yote nzuri iliofanywa na jumuia ya uamsho kesha iharibu kwa muda mchache sana na sirahisi tena kwa jumuia ya Uamsho kurejea katika dawa zao kama walivyokuwa wakifanya usiku na mchana leo ni zaidi ya siku 4 vijana wapatao 30 wako ndani na dhamana ziko wazi hakyuna miopango yeyote ya Farid na wenzake kuwatowa wanateseka wanaatilika ni watoto wa kiislamu inasikitisha nae hajali bado analazimisha damu imwagike subhana llah Amir anamfanyia nani kazii hii haijulikani, kwani asie sikia l;a mkuu huvun jika guuuu.

  • kwa kuwa hawapendi fujo ndio wasidai haki yao?ulitaka walale majumbani ndio haki wanaoidai itapatikana?uliona wapi katika uso wa dunia hii haki yako ukaletewa kwenye kisahani cha chai?unasema “wengi washasema farid asiingize nchi ndani ya vita”hao wanaosema inaonekana wana matatizo ya kuficha uhalisia wa jambo hivi uliwahi kumsikia amiri wetu shekh faridi kuhubiri vita?wanaopigania haki wanamkubali amiri farid na wanampenda.ni kweli mapambano ni mbinu na ndio wanavyofanya uamsho na sio ubabe wanafanya serikali kwa kupiga watu mabomu na kukamata mashekh kama wanavyo kamata wala unga au jambazi halafu hapohapo anajitokeza kiongozi anaeheshimika kuwa pongeza polisi eti wamefanya kazi kubwa wewe katika fikra zako alivyofanyiwa shekh musa anaweza kufanyiwa askofu yoyote?

 3. Bwana Ali Kiberengo, mbona unajikanganya huku unasema watu wa visiwa hivi hawapendi fuje , baadaye unakuja na maneno haya , ” Mapambano ya kuidai Zanzibar hayakuanza kwake yalianza pale tu yalipofanyika Mapinduzi 1964 na Muungano 26.4.1964″ hivi mapinduzi hayo hayakuwa na fujo???

  Hujaandika chochote kupinga hoja za uamsho zenye kutegemea vifungu vya katiba wala hujasema chochote kupinga hayo Polisi wanayoyafanya ya kutaka kutumia nguvu.Polisi wengi ni hawa watoto wa wakereketwa na janjawidi ambao hawana elimu baada ya kufeli madarasa ya chini wakapatiwa kazi hizo na wazee wao.
  Kwa kweli kunatakiwa changes kubwa humo ndani ya jeshi la Polisi kupata jeshi lenye wataalamu sio la kijanjawidi

 4. Ndugu, hayo ni mawazo yako tu! ambayo yanaonekana wazi kuwa yamefungamana na chuki zako binafsi. Kwanza utambue kuwa hii harakati si ya Amir Farid bali ni ya Taasisi za Kiislamu nchini ambazo kwa pamoja hujadiliana na kufanya maamuzi, ninamaanisha kuwa huo ndio msimamo wa jumuiya sio wa Farid. kwa taarifa yako, Viongozi hao hawajapoteza heshima bali wamejijengea heshima kubwa sana mbele ya Wazanzibari wazalendo wenye kujua heshima na thamani ya nchi yao kwa kuwa twatambua “No gain without pain” na hii si kwa wao tu bali nasi tuko pamoja nao mpaka tujue moja.

  Ndugu, sahau zile siasa za kutia kinyesi kisima na kusingizia vyama vya upinzani, zama za leo vijana tunasoma, tunatambua, tanatathmini na kuchambua. hakuna asiyejua kuwa fujo hizi kwa makusudi zimeanzishwa na polisi na usalama wa taifa kwa lengo la kuipaka matope jumuiya, hii ni kwa sababu mihadhara mingi imefanyika hakuna hata nzi aliyeuliwa seuzi kuchafua amani ya nchi au kuvunja kanisa. Hiyo mbinu ya kuvunja makanisa ili kupotosha jamii ya kimataifa na kuipa harakati sura ya udini ni ‘muflis’ kwa kuwa ulimwengu mzima unatambua madai yetu sisi hatuna ugomvi na kanisa wala wakristo, madai yetu ni kura ya maoni itayeamua mustakbali mpya wa TAIFA LA WATU WA ZANZIBAR.

  Ndugu, nashukuru kwa kutambua kuwa kumbe harakati yetu ina maadui ukimaanisha polisi, na baadhi ya viongozi wa serikali ambao wanashurutishwa na kanisa, asante sana kwa kututanabahisha hilo, sisi tulidhani hawa ni wenzetu ambao kazi yao ni kutunza na kudumisha amani pamoja na kusikiliza matakwa yetu kama wananchi wazalendo kumbe ni maadui zetu!

  Sasa tunatambua kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wana interest zao ambazo ni tofauti na zetu, kama hivyo ndivyo, je watamuongoza nani katika hali kama hiyo? na hata hiyo katiba wanayoilazimisha itapataje ridhaa yetu? hivi hawa wanaakili lakini? Muda ukifika wananchi wakisema “NO” huna mbinu wala hila za kuwadanganya ili wakuamini, miaka ya udhalimu na ukandamizaje imekwisha, hii ni harakati ya Wazanzibari wazalendo ambao kwa asili ni waislamu 99.9% wakiongozwa na Maimamu na Mashekhe wao watukufu, sasa je watatuuwa sote?

  Ndugu, ondoa wasiwasi kuwa eti adui ameshika mpini, hizi si zama za kutishana tena! na ondoa ujinga ulonao kichwani mwako kuwa jumuiya inapambana kijinga labda wewe ndio mjinga usietambua wajibu na haki yako. Jumuiya imejipanga kisheria na kila secta kwa kuwa hizi ni zama za freedom, rudia mapambano ya Misri, Libya na kwengineko. mtazamo wangu hawa ni wafamaji hawatoacha kutapatapa, ni lazima waungane nasi! Wakitaka wasitake! Vyenginevyo mbinu zipo nyingi na wakitaka kutumia nguvu visiwa havitokalika kwa upande wetu na wao pia maana tulivyo wazanzibari kama si wa shangazi basi wa mjomba.

  Ndugu, inaonekana umelala usingizi mzito, kwa taarifa yako harakati itaendelea kama kawaida ukizuia njia moja utambue kuwa unafungua nyengine kumi na moja hususan katika ulimwengu huu wa technologia. Tunawaamini viongozi wetu nasi tuko pamoja nao, tukitambua kuwa “haki ni nguvu” nasi tupo katika kutetea haki yetu mpaka kieleweke! Ukoloni basi tena! kama ilivyosemwa” you can full some people for some time but you can’t full all the people for all the time, now you see the light stand up for your right” ZANZIBAR KWANZA.

 5. sisi haturudi nyuma kwakusikia viji maneno vya watu lengo letu ni moja tu insha allah kwa uwezo wa mungu tuta litimiza.

 6. Kosa kubwa bado liko kwa Polisi ndio walioanza fujo na yakatokea yaliotokea kwa amri finyu,elimu duni ,chuki binafsi na njama za makusudi walizo ziandaa wao hatujui kwa faida ya nani, lakini ni kwa faida ya mabwazao wasio upendelea Uislamu kheri.
  Swali ni kuwa jee watafanikiwa kuudidimiza na kuuwa Uislamu Nchini? .
  Kwanza tuangalie chanzo cha mkasa wote, watu waliandamana bila kutokea fujo yoyote na walirudi salama bila kupigwa mtu ,kuharibu mali za watu na hata hao Polisi hawakuepo na walirudi kuwahutubia watu kwa amani kabisa. Kwa hivyo basi tukubali kuwa hayo yote haikuwa fujo kwani hakuna madhara .
  Ni Polsi wasiokuwa na Elimu na ujuzi wa kutosha juu ya kazi zao ndio waliokosa Hekima na Maarifa ,na walichojuwa wao ni kuingia Msikitini na kujifanya kama wakwenda kusali kumbe {ALLAH }anajuwa nia zao na atawalipa kwa hilo Inshaallah .
  Mimi sio Askari na Mola aninusuru ,lakini kama ningelikuwa hivyo basi ningelitumia njia ya kumwita sk, Mussa kituoni kwa maandishi baada ya kuridhika na kuyafanyia uchunguzi yale yalionifanya kum
  uita Kituoni.
  Kuna mambo mengi hufanywa na Polisi kinyume cha Sheria na hakuna hukumu wala hawaulizwi, ni kwasababu hakuna hiyo Sheria . Vipi Polisi uliekula kiapo kulinda Raia na mali zao leo uwe ndio Hakimu unapiga watu ,unauwa watu ,unasingizia watu kesi za Uongo na huulizwi wala hakuna haki ya kukuhoji, mwisho unapandishwa Cheo kwa kazi nzuri ya kutesa na kuuwa.Jamani mnaulizwa siku ya hesabu ndugu zangu na nyinyi Viongozi hilo mlijuwe.

 7. Ndugu yangu Ali alisema mapambano yalianza zamani. Ni kweli. Pambano kubwa ni lile la Aboud Jumbe Mwinyi. Wakati huo alikuwa rais wa Zanzibar ilikuwa kazi nyepesi kututoa utumwani kwa Tanganyika kuliko sasa wakati kiongozi wa juu ni muumin wa muungano.
  Lakini kilichofanyika na kutumiwa kibaraka wa Kizanzibari. Mhe. Seif Sharif Hamad kumpinga Jumbe na hatimaye kummaliza kisiasa. Nyerere alitamba baade kuwa yeye hakumng’oa Jumbe ila wazanzibari wenzake.
  Hivi sasa hali ni ngumu sana kutoka kwenye makucha haya hasa baada ya kuzidiwa mbinu na watawala wa kuweza kubadilisha agenda na sasa imekuwa ya kuchoma makanisa na fujo za kibaguzi. Hapa wameshinda hasa walipoweza kuwashawishi mataifa makubwa kuhudhuria Zanzibar katika mjadala wa ghasia hizo.

  Nilisema kwenye jukwaa hilihili huko nyuma ni kuwa tatizo kubwa la UAMSHO ni kuwa viongozi wake mbumbumbu hawakusoma elimu ya dunia na hivyo ni rahisi kuzidiwa maarifa na vigumu kuona mbali.

  Nilipingwa na kutukanwa lakini sasa yamejuzu, Kama alivyosema Ali tumewapa fursa watawala wetu kuzidi kutuangamiza . Sasa UAMSHO wamelala wao. Hakuna mihadhara na wametii amri hiyo na ndio muflis.
  Nilisema kwa mtaji huu Tanganyika hawatuchii ng’o.

  TUMEKOSA KUJINASUA 1984 KWA FITINA ZA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD BASI KAMWE HATUTAWEZA SASA WAKATI SEIF AMESHIKA HATAMU

 8. ndugu, inaonekana wazi kuwa unazungumza kiushabiki.
  kwanza unapaswa kuondokana na mawazo ya kuwa hii ni harakati ya Uamsho. harakati hii ni ya jumuiya za kiislamu zanzibar ikiwemo JUMIKI (uamsho). Ndani ya jumuiya hiyo kuna wasomi katika fani mbalimbali ikiwemo Uchumi, siasa na Sheria. Hii ndio kusema mipango na mikakati ya harakati hii inapangwa na wasomi JUMIKI ni watekelezaji tu.

  Ndugu, harakati hii imefanikiwa pakubwa sana na shida ya taasisi za kiislamu sio kufanya mihadhara kwa kuwa mpaka sasa Uamsho wameshazunguka Zanzibar nzima na watu kweli wameamka na kujua katiba na haki yao ya kuwa Wazanzibari na ndio maana sasa wanaidai. hivi nikuulize je, aliyezidiwa mbinu ni Uamsho au watawala ambao mwanzoni walitia vidole vya masikio kama kwamba hakuna kinachodaiwa lakini sasa kwa makusudi wamekaa na wataendelea kukaa kwa ajili ya kujadiliana na wanaharakati kama walivyotakiwa kufanya na mabwana zao? (mataifa)

  ndugu, kweli wamejaribu kubadilisha ajenda lakini haina maada kuwa wamefanikiwa kwa kuwa hayo mataifa makubwa si mbumbumbu kama wewe na kwa kuthibitisha hilo rudia kauli ya balozi wa marekani isemayo “serikali ya umoja wa kitaifa imeingia doa kutokana na fujo zilizotokea” hii ni shutuma dhidi ya viongozi wa serikali na si uamsho.

  ndugu, mihadhara inaendelea na itaendelea kama kawaida mpaka kieleweke kwa kuwa hii ni haki ya kisheria, inaonekana uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo mno, mhadhara ni mhadhara tu popote utakapofanyika suala la kujiuliza je ujumbe unafika?!

  ndugu, mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yaliyotokana na maridhiano ya Jemedari MAALIM SEIF SHARIF na kamanda Mhe. KARUME ndio mkombozi wetu na nakuhahakishia umebaki muda mdogo kazi itakamilika kama harakati itakavyo, KURA YA MAONI KWANZA sio mchakato wa katiba ya muungano usiokuwa na uhalali. ZANZIBAR KWANZA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s