Mzee Musobi afariki dunia

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) akizungumza na muasisi wa CUF, Mzee Musobi Mageni, nyumbani kwa muasisi huyo Mwanza, wakati Katibu Mkuu alipokuwa kwenye ziara ya kikazi kwenye mkoa wa Mwanza wiki iliyopita. Mzee Musobi aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho taifa wakati wa uhai wake

Chama cha CUF, kwa niaba ya Watendaji, Wanachama, Wafuasi, na Wapenzi wake wote, wakiwamo kutoka Wilaya zote 10 na Majimbo yote 50 ya Uchaguzi, na Matawi 583 ya Zanzibar, wanatoa Salamu zao za Rambi Rambi kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, na Familia yote ya Marehemu Mzee Musobi, na kushikamana nao wakati huu mgumu wa msiba. Marehemu Mzee Musobi, alikiongoza Chama cha CUF, akiwa Mwenyekiti wa Pili, tangu alipochaguliwa rasmi kushika wadhifa huo, mnamo Tarehe 13 Julai, 1995, nafasi aliyoitumikia hadi kustaafu kwake kwa hiari na kwa heshima zote, Disemba, 1999.

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF- Chama Cha Wananchi)

Office of the Secretary General
Party Headquarters, P.O. Box 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail:cufhabari.co.uk Homepage: http://www.cuftz.org

Our Ref: CUF/HQ/ONKM/U/003/2012/14 Date: 31/05/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Chama cha Wananchi, CUF, kinaarifu kwamba kimepokea kwa masikitiko na mshtuko mkubwa, taarifa ya Kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Mzee Musobi Mageni Musobi.

Taarifa hiyo iliyopokelewa na Makao Makuu ya CUF, Mtendeni Zanzibar, imethibitisha kwamba Mzee Musobi, ambaye aliugua kwa muda mrefu, alifariki Siku ya Jumatano tarehe 30 Mei 2012, majira ya Saa 2.00 usiku, Nyumbani kwake, Ngudu, Wilaya ya Kwimba, Mkoa wa Mwanza.

Chama cha CUF, kimepokea kwa huzuni kubwa msiba wa Kiongozi huyo shupavu, ambaye alibeba jukumu la uongozi, wakati mgumu, na kwa moyo wake wote, chini ya Misingi ya Nidhamu, Umoja, Uwazi, Uadilifu, na Demokrasia ya Kweli.

Chama cha CUF, kwa niaba ya Watendaji, Wanachama, Wafuasi, na Wapenzi wake wote, wakiwamo kutoka Wilaya zote 10 na Majimbo yote 50 ya Uchaguzi, na Matawi 583 ya Zanzibar, wanatoa Salamu zao za Rambi Rambi kwa Mwenyekiti wa Chama Taifa, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, na Familia yote ya Marehemu Mzee Musobi, na kushikamana nao wakati huu mgumu wa msiba.

Marehemu Mzee Musobi, alikiongoza Chama cha CUF, akiwa Mwenyekiti wa Pili, tangu alipochaguliwa rasmi kushika wadhifa huo, mnamo Tarehe 13 Julai, 1995, nafasi aliyoitumikia hadi kustaafu kwake kwa hiari na kwa heshima zote, Disemba, 1999.

Pamoja na Wadhifa wa Mwenyekiti wa CUF Taifa, Mzee Musobi katika uhai wake aliwahi kushikilia nafasi mbali mbali za Uongozi, ambazo ni pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba, na Maendeleo ya Miji, ya Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mwaka 1972 – 1975.

Marehemu Mzee Musobi atazikwa Kijijini kwake Ngudu, Wilaya ya Kwimba, Mkoani Mwanza, Jumatatu Terehe 4 Juni 2012.

Marehemu Mzee Musobi, aliyezaliwa Tarehe 1 Aprili,1931, amewacha Vizuka 2, Watoto 15, na Wajukuu kadhaa MUNGU AMLAZE PAHALA PEMA PEPONI-AMIN

HAKI SAWA KWA WOTE
………………………………………………………
Salim A. Bimani
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
Uenezi na Mahusiano na Umma

Advertisements

One response to “Mzee Musobi afariki dunia

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s