Maaskofu waitolea uvivu SMZ

Askofu Mkuu wa Anglican Tanzania, Dk Valontino Mokiwa wa kwanza kulia akizungumzia kuhusiana na matatizo yaliotokezea Zanzibar ya kuchomwa Moto kwa Makanisa mbalimbali huko katika Ukumbi wa Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walipokutana  Maaskofu mbalimbali na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed

JOPO la Maaskofu wa madhehebu mbalimbali nchini jana wameitolea uvivu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu wa makanisa visiwani humo. Akizungumza kwa niaba ya maaskofu hao mbele ya Waziri wa Nchi Katika ofisi ya Makamu wa Pili Mohamed Aboud, Askofu mkuu wa Kanisa la Anglican Dk Valentino Mokiwa, alisema kuwa vitendo hivyo sasa vimekithiri na kwamba hawaoni Serikali hiyo ikichukua hatua madhubuti hivyo Wakristo wamechoka.

“Kanisa sasa limechoka kutokana na vitendo vya kuchumwa kwa makanisa na kuharibiwa kwa mali zake…..Leo tukirejea historia tangu mwaka 2001 kuna makanisa 25 yameshaharibiwa, yaani kuwa mkristo ni maisha ya hofu” alisema Askofu Mokiwa.

Aliongeza kuwa wakristo visiwani humo wamekuwa wakiishi kwa hofu huku wakitishiwa maish yao kwa kuopigwa mawe, huku wakichukuliwa kama daraja la pili na kwamba Serikali haichukui hatua madhubuti.
“Matukio yote hayo haya yameripotiwa polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Tumesikiwa mkisema eti wanaofanya hivyo ni wahuni, sisi tunasema hiyo ni lugha ya kututia ganzi. Wale siyo wahuni, ni wahalifu na kuna taratubu za kuwachukuliwa kisheria. Serikali inakemea lakini haina ‘confidence’.” alisema Askofu Mokiwa.

Mokiwa pia aliitaka Serikali kueleza miakati waliyoichukuwa na kuwataja majina wahalifu waliokamatwa kwa majina ili waamini kama kweli hatua zimechukuliwa.
Aliongeza kuwa Serikali pia inapaswa kuchukua hatua kwa vikundi vya dini vinavyohubiri siasa kinyume na masharti waliopewa.

“Siyo dhambi watu kutaka nchi yao au serikali yao, lakini masuala haya hayana uhusiano wowote na muungano. Basi kuwe na majadilinao na vikundi hivi ili kuleta maridhiano.

Askofu Mokiwa alionya kwamba japo Wakristo ni wapole, wanaweza kuchukua hatua kali ili kujilinda.
“Kuna wakati tuliomba Serikali tuwe tunajilinda wenyewe na bado tunaendelea kuomba hivyo. Wakristo siku zote ni pole lakini ipo siku bubu anaweza kusema kwa mikono…. ukiona ‘yellow’ ina ‘blinc’ ujue hali ni mbaya” alionya na kuongea,
“”Ukichoma biblia kama walivyofanya unatarajia nini? Kweli tumevumilia sana lakini sasa tunaonekana wajinga.”

Mokiwa pia aliwataka viongozi wa dini zote kuhakikisha kuwa wanawaongoza waumini wao katika kutenda haki.

Akijibu malalamiko hayo Waziri Mohamed Aboud alisema kuwa atayafikisha yote kwa Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kupunguza hata nukta.

Alikiri kuwa Serikali imezembea katika matukio hayo lakini akasisitiza umuhimu wa viongozi wa dini kutoeneza lugha za chuki.

“Lazima tuwe na mkakati wa pamoja na kuhakikisha tunapambana na wote wanaoeneza chuki. Uvumulivu wenu mliouonyesha ni mkubwa hivyo tunaomba mwendelee. Hao wanaofanya hayo tutahakikisha tunawafikisha kwenye vyombo vya sheria.”alisema Waziri Aboud.

Akizungumzia uhusiano kati ya Wakristo na Waislamu visiwani humo, Waziri Aboud alisema tangu kanisa la kwanza lilipoanzishwa visiwani humo mwaka 1870, wamekuwa wakiishi kwa kushirikiana bila kubaguana hadi siku za hivi karibuni.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi kuhusu ukimya wa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein tangu machafuko hayo yatokee, Waziri Aboud alihamaki akisema kuwa ameshatoa matamko mengi kwa nyakati tofauti.

“Rais ameshazungumza kwa nyakati tofauti, akiwa hapa na huko Pemba… ameshazungumza sana, lakini ninyi hamwandiki tu. Hata sasa amenituma nizungumze, sisi ndiyo tunaomwakilisha. Lakini ameshazungumza mno.”alijibu Waziri Aboud.

Advertisements

11 responses to “Maaskofu waitolea uvivu SMZ

 1. Dr. Mokiwa hii imekuja kwa sababu ya Waumini wa Kanisa wanaotaka kulitumia kujitajirisha. Baadahi ya Mitume wanatangaza dini mpya si dhani wako serious. Naona Makanisa ya Mkunazini na Minara Miwili yangetosha kama si Ubinafsi. Naamini Dr. Mokiwa hutatataka uone Mitume hii inatangaza dini kwa kutumia dola kwa dini ni ushawishi. Kwa kuwa Mitume hii yote inahimiza kuhimidiwa kwa Bwana basi ni kwanini kusiwe na ratiba tuu ili Makanisa ya Mkunazini, Kwa Alinatu, Minara Miwili, Kariakoo yatumike badala ya kujenga vibanda vya Makuti kila upande na hata waumini hamna !

 2. “Wakristo siku zote ni pole lakini ipo siku bubu anaweza kusema kwa mikono”

  Embu semeni kwa mikono muone jinsi tutakavyowafanya makafiri nyie! Acheni kututisha. Zanzibar ina 99% waislam. Hii ni nchi ya kiislam, muungano tu ndo unafanya tusiwe! Sasa tumechoka kuona bia na umalaya wa bara unaletwa kwenye jamii yetu ya kistaarabu. Enough is enough!

  SIKU ZINAHESABIKA KWA VIDOLE!

  • sasa mkiambiwa issue sio muungano ni udini mbona mnakataa maanake nini wee alkaida mau kuongea iyo nonsense apo juu nia yako damu imwagike, hata kama mpo aslimia mia mbili znz haijalishi, kuwenu wastarabu mangapi ya laana waislam mnayafanya tena wa kwanza wee mau mbona ulimwingila mkeo kinyume na maumbile, iyo sii laana ya mwenyezi mungu waislam wangapi kula ya paka wako inakushinda nenda katafute muhogo kwa nguru ule acha ujinga mzembe mkubwa!

 3. vyombo vyote vya habari pamoja maaskofu wanawahusisha uamsho na vurugu zilizotokea.hawaelezi chanzo nini?je uamsho wamefanya mikutano mingapi?na je paliwahi kuvunjwa kanisa au kuchoma moto gari au kupigwa mkiiristo yoyote?wakati matembezi ya amani kuna uharibifu wowote ulioripotiwa?hapa moja kwa moja dhana inakuja kuna waliofanya hayo kwa lengo la kuficha kile kinachodaiwa na kudhihirisha kitu ambacho hakipo.nina imani hata hao maoskofu wana jua lililo nyuma ya pazi.

 4. Walitaka kupotosha Umma lakini mwishowe imewagharimu wenyewe maana tayari wameshaitia doa Serikali ya Umoja wa kitaifa kutokana na ubwege wao, ufinyu wa akili na kutaka kulinda maslahi yao. Maskofu, usalama, polisi na baadhi ya viongozi wa SMZ hata wafanye nini kwa sasa wameshachelewa kwa sababu ulimwengu wote unatambua matakwa ya Wazanzibari kuwa wameuchoka muungano kandamizi na ukoloni wa watanganyika.

 5. The proper office of religion is to regulate the heart of men, humanize their conduct, infuse the spirit of temperance, order, and obedience; and as its operation is silent, and only enforces the motives of morality and justice, it is in danger of being overlooked, and confounded with these other motives.

  David Hume
  religion | morality | justice

 6. MH KWELI HUU NI MFUMO KRISTO,YAANI TANGU JUZI HABARI KUU KWENYE VYOMBO VYOTE VYA HABARI NI “KANISA LACHOMWA MOTA ZANZIBAR” MBONA YALE YA KURANI KUCHOMWA, POLISI KUNYANYASA RAIA NA MSIKITI KUARIBIWA NA POLISI JUZI HAYAANDIKWI? MTOTO AKILILIA WEMBE MPE SASA KAMA MNATAKA WAISLAMU TUFANYE HIVO KWELI SUBIRINI TUTAFANYA, IKIWA MASHEKHE WETU WATAHUKUMIWA VIFUNGO KWA MAKOSA YA KUSINGIZIWA BASI KWETU SISI WAZANZIBARI ITAKUWA BORA KUISHI CHINI YA ARDHI KULIKO JUU YA MGONGO WAKE.

 7. mm Naona taabu kukwita wewe docta! mzushi mokiwa hivi wasema kweli ati makanisa 25 yamechomwa moto huu ni upotoshaji mkubwa wa wagalatia! nitatoa mfano unguja ukuu kuna mgalatiya alipewa eneo kulima basi aliita wenzake na kuanza jenga kanisa bila ya kibali! na najis makafir kama hawa kuonana na rais wetu! mokiwa nyinyi muna blanda nyingi mno ikiwemo uwakala wa madawa hapa zanzibar! nyinyi si muliohalalisha kuoana kt ya waume? sikiliza mokiwa nenda kwenu bara ! ukaendelee kuhimiza liwatwi, wizi, ujambaz, ghilba! na kufuru! hii nchi haiwahusu! tuacheni tupumue!

 8. mi nashangazwa mno na hawa viongozi wetu .
  tatizo la zanzibar si vikundi vya dini . tatizo la zanzibar ni muungano, wazanzibar hatutaki muungano. Na hata hayo yalotokea hayakuanza leo c juzi tu hapo watu walichoma vibanda na baar za watanganyika kiwengwa na hali ya kuwa muamsho hawakuwepo!.
  Mi naimani kilichowakuta wakristo wa zanzibar kimesababishwa na viongoz wao kudharau ukweli wa mambo na kutangaza kuridhika na muundo wa muungano ulokuwepo.
  Na siamini kama kuna njia ya maridhiano zaidi ya kura ya maoni ya muungano.

 9. Pingback: Anonymous·

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s