Maaskofu waomba serikali kuingilia kati

Waziri Mohammed Aboud akioneshwa uharibifu uliotokea katika kanisa la Kariakoo baada ya kuwashwa moto na kuteketezwa baadhi ya vifaa vya kanisa hilo pamoja na gari la Askofu Dickson Kaganga

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mohamed Aboud pamoja na viongozi wa dini jana walitembelea maeneo yaliyoshambuliwa katika vurugu zilizotokea visiwani hapa. Ziara hiyo imekuja wakati hali ya amani ikielezwa kurejea visiwani hapa baada ya ghasia zilizoanza Jumamosi usiku na kuendelea hadi juzi.

Wakizungumza baada ya ziara hiyo, viongozi wa makanisa visiwani hapa walitoa malalamiko yao kuhusu vitendo vya uchomaji na uharibifu wa makanisa huku wakiitaka Serikali kutumia nguvu ya ziada kuingilia kati suala hilo wakisema tangu mwaka 2001 hadi sasa jumla ya makanisa 23 yameshachomwa moto Zanzibar.

Katibu wa umoja wa Wachungaji wa Zanzibar Jeremiah Kobero alisema kuwa licha ya makanisa matatu yaliyochomwa na kubomolewa katika vurugu za sasa, kuna matukio 23 ya uchomaji moto makanisa yametokea tangu mwaka 2001.

Aliyataja matukio hayo kuwa ni pamoja na uchomwaji moto wa makanisa ya The Church of God na Sloam yaliyofanyika mwaka 2011, makanisa mawili yaliyoko Masunguni yote mwaka huo huo, Kanisa la EAGT la Fuoni mwaka huo, kanisa la Pefa mwaka 2009, kanisa la Mwera mwaka 2012, kanisa la Redeemed lililiopo Dilikane mwaka 2001 yote ya mkoa wa Mjini Magharibi.

Alitaja pia makanisa yaliyochomwa katika mkoa wa Kaskazini kuwa kanisa la Tunguu, Unguja Ukuu, kanisa la CMF, Chukwani na Manyanya.

Alitaja pia kuwepo kwa tabia hiyo kisiwani Pemba akisema kuwa imekuwa ni tabia kwa wakristo kusumbuliwa.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la TAG Kariakoo Zanzibar Dickson Kaganga aliwataka Viongozi wa serikali kuchukua tahadhari mapema kabla vurugu hazijatokea.

Wakristo tumewafundisha kuvumilia…juzi walipovamia hapa walichoma moto biblia 50, ingekuwaje sisi tungechoma japo kitabu kimoja cha Kurani? Hayo makanisa yote yaliyochomwa, taarifa ziko polisi, lakini ukienda kutoa taarifa unaulizwa, una kibali? Yaani wanakutafutia tena kosa” alisema Askofu Kaganga.

Kaganga ambaye wakati wote alikuwa akibubujikwa na machozi aliwataka Wazanzibar kutambua umuhimu wa muungano kuwa ni pamoja na kuenezwa kwa dini.

Unapoona makanisa yanaenea hapa, ujue na kule bara misikiti inaenezwa na Wapemba ambao ni wajasiri wa biashara. Hiyo ndiyo faida ya muungano ndiyo faida ya kuoleana” alisema.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa askofu wa TAG kitaifa Askofu Magnus Mhiche alihoji kitendo cha wahuni kuvamia makanisa ilihali Serikali ikiwepo madarakani,

Mimi siamini kama ni Waislamu wamefanya haya, ila najiuliza, kama siyo wao basi ni wahuni. Hivi kweli wahuni wanatawala Zanzibar?” alihoji.

Naye Askofu wa kanisa kuu la Anglican Michael Hafidhi aliiomba Serikali kudhibiti mahubiri yanayotukana dini ya kikristo kwa njia ya kaseti akidai kuwa yanachochea vurugu.

Zipo Kaseti zinazotukana ukristo, zinachochea vurugu, tunaomba serikali idhibiti. Hata ile kamati yetu ya ushirikiano wa dinio nayo imekufa inabidi ifufuliwe.

Kwa upande wake mwakilishi wa ofisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Jongo aliwataka Waislamu kuchukuliwana na Wakristo akisema kuwa hata Mtume (SAW) alifanya hivyo wakati akiitetea dini yake.

Hata Mtume wetu alipopata taabu alipokuwa Madina alikimbilia kwa Wakristo. Mpaka uislamu ulipoenea Makka yote. Hata alipotoka Medina na kwenda Mecca aliyempeleka hakuwa muislamu. Nashangaa leo ninaposikia eti Waislam wanachoma makanisa” alisema Jongo na kuongeza,

Hawa ni waislamu gani, mbona wamechoma hata bendera ya CCM, wamechoma bar na kunywa bia. Nini hasa malengo yao?

WAZIRI wa nchi katika Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mohamed Aboud amepiga marufuku mihadhara na maandamano yanayofanywa na vikundi vinavyopinga muungano akisema kuwa watawachukulia hatua kali za kisheria.

Waziri Aboud aliyasema jana hayo baada ya kutembelea kanisa la Assemblies Of God lililopo eneo la Karikoo mjini Zanzibar lililochomwa moto na kubomolewa kutokana na vurugu zilizozuka kufuatia kukamatwa kwa viongozi na wanachama wa kundi la Jumuiya za mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Uamsho).

Katika ziara hiyo ambayo aliongozana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema na Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa, Waziri Aboud alisema baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi yanayosabaisha vurugu.

Baadhi ya viongozi wa dini wanatoa maneno ya uchochezi, yanachochea vurugu zote hizi…. Maneno ni sumu, ndiyo tumeiingiza nchi katika machafuko yote haya” alisema Waziri Aboud na kuongeza,

Sisi kama Serikali tumewaita wenye makundi hayo na kuzungumza. Tumewaambia, kama mtu hataki dini aje kwenye majukwaa ya siasa. Tumekosea kuwaachia watu waanzishe vyama na vimesajiliwa kisheria kwa lengo la kueneza dini, lakini sasa wanaleta uchochezi.

Kuanzia sasa ni marufuku kufanya maandamano na mikusanyiko yoyote ya aina hiyo” alisisitiza Waziri Aboud.

Naye IGP Said Mwema alisema kuwa jeshi hilo limeongeza ulizni katika maeneo maalum yenye usalama mdogo hasa makanisa.

Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kuwa tunadhibiti maeneo maalum ili yasiendelee kuvamiwa. Tunafanya uchunguzi, ili kuhakikisha nani, kwa nini na wako wapi” alisema IGP Mwema.

Alisema jeshi hilo kwa sasa lina kikosi maalum kwaajili ya kuongeza nguvu ya kudhibiti machafuko kisiwani humo na kwamba hadi jana jeshi hilo lilikuwa limekamata watu 46 na kati yao 43 wamefikishwa mahakamani huku wengine watattu wakifanyiwa uchuguzi.

Aidha IGP Mwema alikiri kwamba jeshi hilo limecghelewa kuzuia uhalifu huo na kwamba hatua iliyopo sasa ni kudhibiti usiendelee.

Kuna mifumo mitatu ya ulinzi, kwanza ni kuzuia kabla mambo hayajatokea, kwa hapo sisi tumeshachelewa. Tuko hatua ya kudhibiti yasiendelee na baada ya hapo tutajenga amani iwe endelevu” alisema.

Wakati huo huo Chama Cha Mapinduzi CCM kimesikitishwa na vurugu zilizotokea ambazo wanaamini kuwa zimeandaliwa na Jumuiya za Uamsho na kuitaka serikali kuchukua tahadhari kubwa katika suala hilo kwani kama hatua hizio hazijachukuliwa huenda likaleta maafa makubwa.

Cham cha Mapinduzi kinaalani vitendo hivyo na kuzitaka serikali zote kudhibiti hali ya amani na utulivu tulioizowea na kuwachukulia hatua kali wote waliosababisha vurugu hizi” alisema taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Kwa upande wake chama cha Chadema kimelaani vurugu hizo zilizofanywa kwa makusudi na vijana ambao wanaonekana wameshapata mafunzo maalumu kwa kusaidiwa na chama kimoja cha kisiasa kinachounda serikali ya umoja wa kitaifa.

Chadema tunavitaka vyama vya siasa kuandaa makundi ya vijana ambayo mwisho wake wanakosa kuwapatia kazi na hatima yake kuwa vikundi vya kihalifu nchini” ilisema taaifa hiyo iliyotiwa saini na Hamad Yussuf Naibu Katibu Mkuu.

Chama Cha Wananchi CUF kimelaani vurugu hizo na kusema zimesababishwa na chuki binfasi, ukosefu wa hekima, matumizi ya nguvu za dola na uchochezi wa makusudi kwa wale wasiopendeleaq maridhiano ya kisiasa ya Zanzibar.

Vitendo vya watu wachache na kuharibu mali za watu ni uvunjifu wa sheria na kinyume na utamaduni wa kizanzibari, uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua bila ya uonevu wala upendele” imesema taarifa hiyo iliyotiwa saini na Salim Bimani.

9 responses to “Maaskofu waomba serikali kuingilia kati

  1. ndugu maaskofu , hizi ni mbinu za kina abudu na wanasiasa wenzake kufitinisha kidini , lazima muwe waangalifu kujua nani amesababisha , anaefaidika na vurugu hizi ni wanasiasa wenye kutaka muungano uendelee kwa faida zao kibinafsi , muungano kuvunjika kutaleta faida kwa wote waznz na watanganyika ikiwa watu wanaona mbali.

    • Abudu chunga usije ukawa kina Mwinyi na wewe huu ni wakati wa mpito tu kwa hivyo kauli zako zitakushtaki kesho na usione kuwa Uwaziri au UCCM ndio maisha yako ila fahamu kuwa kesho ni ndio maisha yako ya milele.

  2. “unapoona makanisa yanaenea hapa ujue na kule bara miskiti inaenezwa na wapemba ambao ni wajasiri wa biashara na hii ndio faida ya muungano na kuoleana”alisema.miskiti yote bara inaenezwa na wapemba na makanisa huku visiwani yanaenezwa na watanganyika. maneno yake yana ukweli kidogo uwongo mwingi,bara uislam ulikuwepo kabla ya muungano na hii kusema miskiti inaenezwa na wapemba ni kutaka kutuonyesha uislam bara ulienea baada ya huu muungano na huu ni uongo ambao umekua ni kawaida katika kueneza propaganda ya kuwa wao ni wenyeji kwa dini yao na waislam ni wageni na hata uhuru wa tanganyika wanaficha majina ya waislam waliojitolea kwa hali na mali na wanamtukuza huyo mwenye heri laanatul llah kana kwamba harakati zote kazifanya yeye wakati kaja kwa waungwana wazee wa dar es salaam wakampokea wakamfundisha ustaarabu kaja na kikaptura kashonewa suruali ili afanane na waugwana.kuhusu kuoleana hii ilikua ikifanyika kabla ya muungano au mnataka kutwambia kabla ya muungano ili kuwa huwezi kuoa au kuolewa?ni kweli kabisa faida ya muungano huu ni kuenea kwa makanisa kupora rasilimali za hawa small brother kuwadhalilisha viongozi wa serikali yao rais awe mjumbe katika baraza la mawaziri chini ya waziri mkuu.

  3. ninavyofahamu me ni kwamba Serikali inavyojisema kwamba haina dini, kwa hiyo isisikilize lolote litakalopelekwa na kanisa ikisiliza tutajua kwamba serikali ina dini na Dini ya ukristo wameipa kipaumbele kuliko dini ya uislam ambapo wazanzibari wote 100% ni waislam, hao makafiri waliopo zanzibar ni wahamiaji tu si wazanzibari

    • so salma, its ok to burn bibles and churches ?? so makanisa yakichomwa wachungaji wasiongee ?? leo ndio serikali haina dini, makafiri ni kina nani ?? tafsiri sahihi ya kafir ni ipi ? na mbona kiongozi wenu ameelezea kuwa mtume alitunzwa na wakristo huko medina, so alikaa na makafir ? jamani acheni udini nyie, na yule mzee waziri brigedia aliyefariki ambaye si muislam na ni mzanzibar mnasemaje juu ya hilo

      • kafiri ni kila anaepinga kile alichokujanacho mtume muhammad saw.kuhusu huyo unaesema ni kiongozi si kila kinachosemwa na kiongozi ni sahihi lazima ujiridhishe kwa kutumia akili kwa kusoma nk.mtume saw kutunzwa na wakiristo hilo ni uwongo na inawezekana alikuwa anawafurahi wale wanaompa shibe.mtume saw kahamia madina na kopokewa na makabila makubwa mawili aus nakhazraj ambayo baadae yalitambulika ansaar.ukitaka kufahamu zaid soma vitabu viko usisikilize ya viongozi.

  4. Wewe Vic unajitia ujuaji! ATI BREGADIA MWAKANJUKI!wafuate hiyo familia yake watakueleza kwao ni wapi? lkn ss wazanzibari hatuna ugomvi wa john! josphina au katrina ! ss tunahaja ya zanzbar yetu! ati wapemba ndio waliopeleka uislamu huko bara maskini uso jijua! hebu hao walimu wenu wawafundishe historia ya uislamu pwani ya afrika mashariki! kazi yenu kufundishwa kukufuru, kwenda uchi, wizi, ujambazi, ulaghai, uongo na umalaya! mumemeza moto mwaka huu zanzibar mutaitema mukataka musitake!

  5. Tena tunawatahadharisha wale wanaowanasabisha watanganyika na ss wazanzibar hizi ni nch 2 tofauti! mbona msikit wa msumbiji umevunjwa vioo mbona hatuja muona yeyote kulani! hawa ndio wanaotudhulumu! hawa sio walotuua! wakatubaka! wakatunajis! na kutupora! mbona hamukulani! juzi walichoma kiwanda cha kuchapishia vitabu vya dini! vya kiislam! mbona hamukuandika! na kulani! alaa anye kuku tu! akinya bata kaharisha!! ss hatuna haja na nyinyi ikiwa mutatuheshimu na kujifahamu nyinyi ni wageni! mwisho nawambia hao watetez wenu hao ndio wanakufanyieni kama mm ni muongo fuatieni! mutapata ukweli ! wanafanya kwa maslah ya kuzuwiya motion za uamsho! lkn wamechelewa! wanakumbuka funga mlango farasi ameshatoroka! zingatia

  6. wazanzibar kukosa elimu kunawasumbua, ni kitu kibaya sana mlichokifanya kudai muungano kwa kuchoma makanisa, nia yenu ni nini??? mnataka kutochangonisha na huku bara kati ya waislam na wakristo? nia yenu haitatimia!!!!

Leave a reply to Abousalah Cancel reply