Watu 30 wafikishwa mahakamani

Zanzibar leo hii imejikuta ikirejea kule ilipotoka baada ya matukio ya uvunjifu wa amani kujitokeza kwa mara nyengine tena ambapo wananchi na jeshi la polisi kwa pamoja wamekuwa wakifanya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Vijana wenye hasira wamechoma moto matairi barabarani na kuharibu mali za watu lakini na Polisi nao wamekuwa wakiwakamatwa vijana hao na kuwapiga kwa marungu na mateke jambo ambalo ni kinyume na haki za binaadamu ambapo Tanzania imeridhia azimio la umoja wa mataifa la kuheshimu haki hizo.

JUMLA ya watu 30 wakiwemo wanaodaiwa kuwa viongozi wawili wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, leo walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashitaka ya uzembe, uzururaji na uvunjifu wa amani.

 

Shitaka jengine walilosomewa mahakamani chini ya Hakimu Mohammed Ali Mohammed Shein hapo ni pamoja na kufanya mkusanyiko usivyo halali ambapo Mbarouk Said Khalfan (45) Mkaazi wa Taveta Meli nne na Mussa Juma Issa (57) Mkaazi wa Makadara wote wakaazi wa Mjini Zanzibar.


Washtakiwa hao ambao walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa aman, walifikishwa mahakamani hapo wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi.

Viongozi hao kwa pamoja walisomewa mashitaka ya kujikusanya na kufanya maandamano kinyume na sheria kifungu 55 (1)(2)(3)  sheria nambari 6 ya mwaka 2004. ambapo Hakimu Shein alisema mahakamani hapo kwamba mnamo Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:30 za  mchana viongozi hao walijikusanya kinyume na sheria za Zanzibar.

 

Hakimu huyo alisema wananchi hao walifanya maandamano ambayo yalianzia katika uwanja wa Lumumba kupitia Msikiti wa Biziredi na kumalizia uwanja wa Lumumba, ambalo ni kosa kwa vile linaweza kuhatarisha amani na utulivu na kuweza kusababisha
uharibifu wa mali za wananchi wa Zanzibar.

Mbali ya viongozi hao wanaodaiwa wa Uamsho wengine walijumuisha katika kesi hiyo ni Mbwana Hamadi Juma (50) Mkaazi wa Nyerere, Masoud Hamadi Mohammed (17) Mkaazi wa Mtoni Kidatu, Mohammed Juma Salum (35) Mkaazi wa Kianga na Abdulrahman Simai Khatib (19) Mkaazi wa Mbweni.

 

Wengine ni Hashim Juma Issa (54) Mkaazi wa Mbweni Matar Fadhil Issa (54) Mkaazi wa Mbweni, walifikishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu Mdhamini Janet Nora Sekihola kujibu shitaka la  uzembe na ukorofi kinyume na kifungu cha 181 (d) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Watuhumiwa wengine walifikishwa katika mahakama ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, ambao walishitakiwa chini ya kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Mashitaka yote hayo yaliwasilishwa kwa nyakati tofauti na waendesha Mashitaka, Wanasheria wa serikali Mohammed Kassim Hassan, Suleiman Haji Hassan pamoja na Ramadhan Abdallah, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP).

Katika mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, Mwendesha Mashitaka Mohammed Kassim alidai kuwa watuhumiwa Mbarouk Said na Mussa Juma, bila ya halali walipatikana wakiandamana kupitia katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya mji wa Zanzibar, kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikana makosa hayo na kupewa dhamana ya masharti ya shilingi 300,000 kila mmoja ambapo walitimiza masharti hayo na wapo nje ya dhamana hadi Juni 16 mwaka huu, kwa kesi hiyo kutajwa.

Awali mahakamani hapo vikosi vya ulinzi na usalama walionekana kujipanga imara na kuhakikisha usalama umedhibitiwa wakati wote wa uendeshaji wa kesi hiyo ambapo maeneo yote ya Mahakama ya Mwanakwerekwe yaliimarishwa ulinzi ndani na nje ya eneo hilo.

 

Mamia ya wananchi walifika katika eneo la mahakama hiyo na kuja kusikiliza kesi hiyo lakini waliishia nje ya mahakama hiyo kutokana na ulinzi uliozunguka katika eneo hilo mwanzo hadi mwisho wa kesi hiyo.

 

Licha ya watu hao 30 kufikishwa mahakamani leo lakini hali ya amani bado haijatengeneza kutokana na baadhi ya maeneo kurushwa mabomu ya machozi na watu kadhaa kutawanywa katika maeneo ya Mwanakwerekwe, Darajabovu, Amani na Mikunguni muda mfupi baada ya wananchi kutoka katika eneo la mahakama hiyo.

 

Advertisements

25 responses to “Watu 30 wafikishwa mahakamani

 1. Sasa hiyo picha ni ya jana au ya leo?
  maana sie tuliokuwa nje ya nchi tumesikia kuwa hali ishakuwa salama na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.!

  • Ni ya leo(jana). Mhadhara umeendelea leo kama kawaida Mbuyuni mjini Zanzibar bila ya hofu licha ya malori yaliojaza polisi-kristo kufanya doria ya tisha toto

 2. Pingback: Viongozi wote wawili wa Muamsho na watu 30 wako nje hadi Juni 16,·

 3. Askari kutoka Tanganyika-Wakristo ni magaidi na maharamia wauwaji hatari, leo wamesababisha vurugu kubwa baada ya kuupiga mabomu na kuuharibu Msikiti mpya wa ghorofa (Omar Ibm Khatwab) uliopo Msumbiji upande wa kushoto kama unatoka Kwerekwe kwendea Amani yaani karibu na Skuli ya msingi ya Nyerere, Msikiti huu wameuvunja vioo na milango kwa mabomu tena basi waliukuta umefungwa wakati huo, baada ya uonevu huu vijana wabichi damu ikiwachemka zaidi na zaidi. Dhima za lawama bado zinarudi kwa Uongozi wa Kanisa na CCM na Borafya Mtumwa Borafya na kina Juma Faki kwa kuwakusanya vijana wa CCM usiku na kulichoma Kanisa la Kariakoo ili waonekane UAMSHO ni wabaya na wanaudini lakini bahari haikai uchafu ushahidi Mungu kashaanza kuuweka wazi. Moh’d Aboud usiwe na haraka usiwe na haraka Wazanzibari wenzako watauliwa tu na Watanganyika, Wanawaizraeli n.k madhali ni Waislamu na Mafuta yapo. Lakini kama si hapa duniani basi soon baada ya kufa na nyinyi mtaonja joto ya jiwe. Haya yote waandishi wa habari wa Tanganyika na vibaraka wao ZBC hawajayaona wameliona KANISA tu.

  Pia ndugu zangu kunataarifa za vijana wawili wameuliwa na polisi na kuzikwa kwa kisingizio cha kutaka kuchoma Transformer. Hii vipi Jamani?

  MUUNGANO HATUUTAKI.

  “Whean peace fails apply force”

  SERELLY.

  • Hamtaki Muungano, au hamtaki makanisa? Mbona hamueleweki nyinyi kama mlosomewa halbadiri!!! Makanisa na Muungano wapi na wapi bwana!! Upuuzi uloandika hapa juu wanaweza kuukubali wajinga kama wewe! Jambo ambalo Kikundi cha Uamsho wanapaswa kufahamu ni kwmba, Uislamu hapa Zanzibar dini iliyoletwa kutoka arabuni kama ulivyo Ukristo. Huwezi kuhalalalisha jambo lisilo asili yake kwenye nchi ya ugeni likawa ndio halali haiji.

   • Usibuni jina> Kaleza tunamuelewa na kamwe hawezi kuandika uchafu huo. Kuwa mwanaume wa kweli na jieleze. Hatutaki yote MUUNGANO NA UKIRISTO

  • Wazanzibari wenzangu hebu tusiwalaumu moja kwa moja askari kutoka bara kwa vurugu za juzi,tuanze na Kameshna kwa sababu yeye ndie msaliti nambari moja,ndie mkuu katika tukio la juzi,ingawa kama tukitathmini vyema tutagundua na ikulu imo kwani tumemsikia Mh. waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa raisi .jinsi.aa alivoalivo a

  • KUHUSU NYUMBA YA IMAMU FARID KUVUNYWA MUNA WATU WAUSALA NA ZBC .AU KANISA LIMEVUNYWA NDO MUNA LALAMA KWASANA.

 4. Jamani wazanzibar tushikamaneni wala tusirudi nyuma kwa hii ni haki yt: lazima tuipate tumechoka na maudhi na mateso yao. Ewe mungu wape wazanzibari uwezo,mshikamano na ushindi. Ameen

 5. shekhe kakamatwa msikitini kashtakiwa kwa uzembe na uzururaji,Rashid salum adiy na wenzake wameshtakiwa kwa uzembe na uzururaji inaonekana ukidai haki yako kesi itakayokukabili ni uzembe na uzururaji!halafu hawa viongozi wa suk sijui wana matatizo gani kikundi hiki cha uamsho hawana haja ya kugombania ubunge au uwakilishi wanachotaka na wazanzibari kwa ujumla ni kuulizwa kama kuna haja ya kuendelea na muungano huu uliopo au laa na kama uwepo uwe wa namna gani na kama hawautaki vilevile hii ni haki yao kwa mujibu wa katiba ya zanzibar.hii kuwalazimisha hivi mnavyotaka nyinyi viongozi matunda yake ndio ya juzi,jana na leo na itaendelea kwa sababu mti mmeupanda nyie ili usiendelee kutoa matunda mabaya muukate na kuukata kwenyewe ni kura ya maoni basi.

  • Hamuutaki ukweli, mtakimbia ukweli mpaka lini? Ni vigumu kuwa na maoni yenye mawazo ya aina moja, wacha tutoa hisia zetu ili mjuwe hisia za watu wengine zikoje juu ya jambo mnalodanganyana

   • we bwege kwani kura ya maoni inaenda kupigwa na uamsho tu nani alokuwa hataki ukweli sisi au wewe km munataka kila mmoja atoe mawazo si wengekubali kura ya maoni kila moja akasema analotaka kw kupiga kura we umesoma wapi mbona akili yako haifahamu we ni walewale wanung’unika kuhusu kanisa coz ndo nyumba yako ya kuabudu na ww kama unajua haki sawa mbona hujasema hapa makafiri wenzako walochoma misikiti
    kama huna la kuongea tafuta pahali wende ww sio mzanzibar cc ndo tunajua uchungu wa nchi yetu si ww

   • Hisia za nani?Wazandiki? Tafuta blog yako ya Wakiristo wenzako. Lakini kamwe Ukiristo hautositawi Zanzibar. Walishindwa Wareno itakuwa aibu kwa kizazi cha leo kuruhusu wachuna ngozi wakristo wasambaze imani yao potofu

 6. ndugu zangu wakizanzibar na wazee wangu tuwemakini umojaninguvu kutengana ni udhaifu tulipokua tunashida ya helkopota ijekuokoa roho za jamaa zetu ilipozama mv spaice haikupatikana mpaka ikaja ya mtu binafsi leo inatakiwa kuja kutowa roho za wazanzibari imepatikana tena mapema jamani bado hatuja amka? tuamkeni wazanzibari!!!

 7. NAMUOMBA MWENYEZIMUNGU AIJALIE ZANZIBAR IWE HURU KAMA NCHI NYENGINE. WAZANZIBARI WASHACHOSAWA NA MADHILI YA MUUNGANO. WAZANZIBARI HATUUTAKI MUUNGANO TUWACHIWE TUPUMUWE.

  • VIONGOZI WAA ZANZIBAR NA WATANGANYIKA KAMA HAMUKIELEWI TUNACHOTAKA WAZANZIBAR NI KUWA HATUUTAKI MUUNGANO WA MAIGIZO. MUUNGANO WADHULUMA HATUUTAKI.

 8. Inavoonesha baadhi ya viongozi aidha niwavivu wa kusoma maandiko ya historia ya Zanzibar ama wameamua tu kuwaapuuzia Wazanzibari,sis wazanzibari tunaipenda zaidi dini yetu kuliko chochote na yeyote,alielewa madaraka nijuu yake ,kanuni ya dini inatutaka kupambana kuondoa dhulma hadi kufa.kwani kifo nini mpaka kitushtue tusipambane? Nani engependa asimuone Mtume(saw)?Mbona hatuko nae?.Ufalme wa dunia nikitu kidogo sana, hakina zaidi ya kuongeza idadi ya maswali mazito kwa Mungu yasiyojibika.Wewe Kameshna wewe ;umepatwa na nini mpaka ukaw asababu ya kudhoofisha dini ya Mungu?Au ni cheo ?Viongozi tulio kuchagueni JEE HAYA NDIO MALIPO YA IHSANI?,ikulu sio Firdausi jitahidini kuwa waadilifu, Ivi mlichokifanya ndio upeo wenu au mumezidiwa na Tanganyika?UKOWAPI UHURU WA KUTOA MAONI ULIOELEZWA NDANI YA KATIBA?,AU NDIOSIRI YA VIAPO VYENU PALE MNAPOSEMA”MIMI FULANI BIN FULANI,NAAPA YA KWAMBA NITAILINDA NA KUITETEA KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA?”nchi niya wazanzibari wote,wala mlichokifanya sio kanuni ya kutafuta amani.”MCHENI MUNGU ENYI WAJA WA MUNGU NA OGOPENI SIKU MTAYOPELEKWA MBELE YA MOLA WENU “.ZANZIBA YENYE DINI TELE INAWEZEKANA.

 9. Yote haya wa kulaumiwa ni Kikwete na Kamishna Mussa. Kama Kikwete hawezi Demokrasia basi avunje hiyo Tume yake na wajifungie ndani watunge Katiba wanayopenda wenyewe. Kama wanataka sisi wananchi tushiriki kwa uhuru na uwazi asianze kutuekea vikwazo juu ya lipi lizungumzwe na lipi lisizungumzwe. Sisi Wazanzibari katika Katiba linalotukera na ambalo hatulipendi ni MUUNGANO. Hata mkisema tusiujadili Muungano ni kazi bure maana sisi Wazanzibari hatuutaki. Ni vyema Kikwete ukatafakari kua kuujadili Muungano ndio njia sahihi ya kuuboresha na kama ruhusa ya kuujadili ingekua wazi haya yote yasingetokea. Ndo maana nasema kua wewe ndio chanzo cha machafuko yote haya lakini kwa kua ” BOSS IS ALWAYS RIGHT” sawa historia itakuja kukusuta kama MKAPA. Aliiba mali za umma, akaua Wazanzibari na sasa historia inaanza kumsuta na karibu itamhukumu japokua serikali yako inajaribu kumlinda. Siku sio nyingi atapanda Kizimbani kwa kosa la Wizi wa mali ya Umma na Mauaji ya Wazanzibari na Waislamu wa Muembe chai.
  Kamishna Mussa wewe kosa lako ni kua mzembe katika kutekeleza na kusimamia majukumu yako. Ukweli ni kua umeshindwa kuwasimamia vyema askari wako na hatimae wakasababisha hali hii. Hawakua na sababu yoyote ile ya kumkamata Sheikh siku ile ya tokeo. Kwani kama wangemuacha na kumkamata siku nyengine au kama wangempelekea hati ya wito Polisi ingekosa kitu gani? Mussa ulituma askari wako ukijua fika nini matokeo ya kitendo kile kwa wakati ule yangekua. Umeifanya nchi iingie kwenye mtafaruku, amani ipotee, mali za watu, taasisi na serikali kwa mamilioni ziharibiwe kwa sababu ya aidha uzembe wako au kutokujua wajibu na kazi yako. Kama kuna mtu wa kushtakiwa na kuchukuliwa hatua Kamishna Mussa ulikua uwe nambari moja. Hebu wewe jiulize mbona kabla ya kukamatwa huyo imamu watu waliandamana mji mzima na hakuna tokeo lolote lile baya lililofanyika? Kamishana lazima uwe mstaarabu na katika hili ni vyema ukajiuzulu wewe mwenyewe ukafanyika uchunguzi wa tume huru na kusema nani ashtakiwe na nani achukuliwe hatua. Kwa sasa serikali itakulinda kwa kua umeshawafanyia kile walichokua wanakitaka siku nyingi “KUZUIA MIHADHARA YA UAMSHO” kwani bila ya kisingizio hiki isingekua rahisi kuzuia harakati za uamsho. Shkh Mussa ujue una jukumu kubwa hapa duniani na kesho mbele ya Mungu kwa kila ambae ameathirika na uzembe wako huu. Kuna waliopoteza mali, walioumizwa, walioshtakiwa, walioathirika na moshi wa mabomu, waliokosa kufanya kazi za kujipatia riski zao na familia zao nk.
  Matokeo yote haya yanarekodiwa na iko siku haki itakaposimama kama sasa serikali inakulindeni MTAWAJIBIKA.

 10. Aslaam Aleykum jamiiya. Ama nimesoma kwa masikitiko makubwa maoni ya SERELLY. Yamejaa shutuma, hayatoi suluhisho la tatizo liliopo, lakini kilicho kibaya zaidi ni pale anapotoa madai kuwa vijana wa Kanisa, Borafyia na Juma Faki walipeleka vijana kanisa la Kariakoo na kulitia moto ili wakamatwe vijana wa Kiislamu. Je, SERELLY una uhakika na madai haya, maana ni mazito na yanaweza kusaidia upelelezi. Na mimi binafsi ningependa kupata uthibitisho huu ili tuwaeleze vyombo husika kama waliohujumu kanisa wanafahamika ni fulani na fulani na viongozi wao ni fulani na fulani. Hatuwezi kuachia watu wachache wanatumia fursa ya kutoelewana wakachupia mali za watu. Waliohusika watajwe waziwazi ili vyombo vya kisheria vichukue hatua zifaazo. Nitarudi kwenye ukumbi kuja kuangalia kama SERELLY umetoa maelezo zaidi khs madai yako hayo. Siku zote tuelewe kuwa tunayoyaeleza kwenye foramu kama hizi ni muhimu yawe ni ya ukweli na ukweli usio shaka.

  • Je wewe unauhakika kuwa UAMSHO ndio waliochoma kanisa? Au kwa sababu dola imesema? wewe muandishi kama sikosoi. Ikiwa serikali inaweza kuzua kwa nini mwengine asiwe na uhuru wa kuzua kujenga hoja yake?
   La kuvunda halina ubani

 11. Ila jana juzi usiku nilishtushwa sana nilivomuona Kamishna wa Polisi Zbar, Mussa Ali Mussa. Nimeshituka kukuta akiwa amekasirika mwisho wa uwezo wake wakati akisoma taarifa kwa umma mbele ya waandishi wa habari khs walichokifanya Polisi ktk kadhia iliyotokea. Nilijiuliza Kamishna Mussa alimkasirikia nani ilhali yeye ndiye anayesemekana aliamuru kukamatwa Sheikh Mussa Juma kwa staili ya KIGAIDI na hivyo kuamsha hasira za waumini? Kitu kibaya alichokifanya kingine ni kutosema kuwa Jeshi la Polisi lilianza kuchochea vijana wakasirike na kudai kiongozi wao aachiwe. Kwani askari wangekwenda nyumbani kwa Sheikh Mussa asubuhi Jumapili au hata usiku ule wa Jumamosi, na wakajitambulisha, wangekosa nini? Au alipogundua kuwa kitendo chao cha kumkamata Sheikh Mussa kilichochea vijana kukasirika na kujazana Madema ili kushinikiza kiongozi wao aachiwe, kwanini Kamishna Mussa alishikilia kumshikilia Sheikh Mussa? Ni yeye alishindwa kuwaongoza Polisi kufanya kazi kwa HEKIMA na BUSARA na matokeo yake sasa analazimika kujuta kwa uamuzi wake wa kuzua fadhaa na hatimaye gharika mjini Zanzibar.

 12. Janet mloya: Ndugu zangu waislam wa Zanzibari hao viongozi wenu ndio maadui zenu wakubwa kabisa inakuaje askari au majeshi watoke Tanganyika kuja Zanzibar? eti kwakutuliza amani na wote waliopelekwa Zanzibar takriban wakiristo na tayari wameshabomoa msikiti, kwa hali hii huyu Sheni na Seif na balozi Seif na huyu kamishna Musa,wako wapi? wote wamelewa kwa madaraka lakin mjue hamkuanza nyinyi wapo waliopita na hivi sasa hawajitambui, nini kinachowafanya msiuvunje muungano? na wenyewe wananchi wameshawadhihirishia hawautaki? Viongozi Watanganyika wanawacheka jinsi mnavyogombanishwa wenyewe kwa wenyewe. Hii ni aibu kubwa kwa viongozi kukaa kimya ,Na kama mpo kwa ajili ya wananchi wenu, basi hawautaki muungano uvunjeni, mbona hamjiamini?

 13. Ndugu zangu inabidi tuwe makini tusichanganye mambo. Ni shida sana kwa sasa na hapo badae makanisa kujaa Zanzibar. Mimi siogopi kwa Zanzibarkujaa Makanisa kwaa uislamu hapa si dini tu bali ni mfumo wa watu wa maisha. La kuogopa ni ukikwaji wa taratibu ambao ni adui kwa waislamu na wasiokuwa waislamu. Ukiangalia yaliyopelekea haya kutokea ni mtafaruku wa watu kimaisha ambao wale wenye upeo mdogo huu husisha na Muungano. Mungano inawezekana ukawa ni sehemu ya shida lakini si kwa ujumla wake. Tuangalieni mambo mengine yanayotuchagiza. Vijana wanaodaiwa kushiriki katika vurugu ni sehemu ya mambo hayo. Wazee wengi wanashindwa kwaengage watoto wao katika mambo yatakayo wasaidia. Serikali nayo pia ina sehemu ya kulaumiwa. Katika zama hizi za leo SMZ inatoa elimu duni na hivyo kufanya wahitimu kukosa skills za Maisha. Watoto wengi hawajui si tuu kusoma na kuandika bali hata mazingira yanawazungumza. Kijana wangu amemaliza Form IV akiwa hajui kuwa sabuni in madawa yanaweza kuua mti na huyu hajii mambo mengi si fahamu kwa kuwa sija muuliza. Mimi naona wakati tunadai Zanzibar huru tudai pia ushiriki wa kweli katika uendeshaji wa SEkta ya elimu kwa kuwa hapa ndio roho yetu inaanzia.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s