Viongozi wakutana, hali bado ni tete

Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi na Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania Inspekta Jenerali Said Ali Mwema wakizungumza katika kikao cha pamoja kati yao na viongozi wa dini na serikali, haja ya kurejesha hali ya utulivu Zanzibar

HALI bado ni tete katika visiwa vya Zanzibar kwa baadhi ya maeneo ambayo vitendo vya uvunjifu wa amani vinaendelea licha ya juhudi za kutaka kurejesha hali ya amani nchini. Juhudi za pamoja zimeanza kuchukuliwa katika kurejesha hali ya utulivu Zanzibar baada ya machafuko ya siku mbili zilizopita zilizosababishwa na wafuasi wa Uamsho na jeshi la polisi na kusababisha hasara za mimilioni ya fedha na uharibifu wa mali.

Kikao cha pamoja kilichowashirikisha waziri wa mambo ya ndani Tanzania, Emmanuel Nchimbi, mkuu wa jeshi la polisi Said Mwema na viongozi wa taasisi za kiislamu Zanzibar jana walikubaliana kufanya kazi kwa pamoja ili kurejesha hali ya amani.

Katika mkutano huo uliofanyika katika makao makuu ya polisi ziwani zanzibar na pia kuwashirikisha maafisa wa sekta ya utalii na baadhi ya maafisa wa kibalozi kutoka Marekani, Ungereza na Norway. Waziri Nchimbi alisisitiza kuwa suala la kulinda amani ni la wote na akawataka viongozi wote wa kidini na wanasiasa kuhakikisha Zanzibar inaendelea kuwa na amani.

“Kwa mwaka mmoja na nusu hivi sasa serikali ya umoja wa kitaifa imefanya kazi nzuri na tunawapongeza viongozi wote kwa kazi hiyo, rais Dk Shein, Makamu wake wa kwanza Maalim Seif na makamo wake wa balozi Seif Ali Idd, sasa tusiwavunje moyo” alisema Nchimbi.

Alisema kuendelea kwa vurugu Zanzibar ni kuonesha viongozi hao wameshindwa kazi jambo ambalo sio sahihi na kwamba vurugu zinaweza kusababisha watalii kuondoka kabisa nchini na hasa kwa kuzingatia kipindi hiki cha msimu wa utalii kukaribia.

Kikao hicho ambacho waandishi wa habari walihudhuria, Nchimbi alisema ujio wake Zanzibar ulilenga katika mambo matatu muhimu ambapo aliyataja mambo hayo kuwa ni kuwahakikishia wazanzibari wote kuwa jeshi la polisi ni lao na litaendelea kuwalinda.

Jambo la pili alisema ni kwamba viongozi wote wa dini na siasa wana jukumu kubwa la kusaidia kujenga mazingira ya utulivu na amani Zanzibar.

Aidha Waziri Nchimbi katika mambo ambayo alihimiza ni kuagiza jeshi la polisi kuchukua hatua ili kuhakikisha kwamba watu wote walihusika na vurugu hizo kuchukulia hatua za kisheria.

Mkuu wa Polisi Tanzania Jenerali, Said Mwema aliahidi kushirikiana na viongozi wa taasisi za kidini ili kuendeleza amani na utulivu nchini.

Alisema kwamba majadiliano na mazungumzo ni muhimu katika kuimarisha amani na kutatua migogoro iliyokuwepo na kwamba kwa nafasi yake ataendelea kubali Zanzibar.

“Vurugu hazisaidii kujenga lakini matumizi ya nguvu pia tunajitahidi kuyaepuka, na katika kuhakikisha mashirikiano yanaendelea mimi nitabakia Zanzibar kwa muda ili kujenga mawasiliano na programu maalumu za ulinzi shirikishi” alisema Mwema.

Kwa upande wa taasisi za kidini walishauri jeshi la polisi katika kujenga mashirikiano na kuepuka michafuko kama hiyo yaliyotokea na kutumia busara wakati wanapotekeleza majukumu yao.

Dk Mohammed Hafidh Khalfan ni kiongozi wa Umoja Kiislamu, wa Elimu, Uchumi na Maendeleo (UKUEM) aliwataka jeshi la polisi kuepuka matumizi ya nguvu wanapotekeleza majumu yao.

Alisema kwamba taasisi yake pamoja na taasisi nyengine za kiislamu zitatumia juhudi na busara za kuwafanya waumini waepukane na vitendo vya fujo kwa sababu fujo inatoa fursa kwa wahalifu kufanya vitendo vya uharibu wa mali na wizi.

Katika kikao hicho ambacho Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) hawakushirikishwa ambapo Dk Hafidh alishauri kikao kama hicho sauti zao ni muhimu kusikika kwani baadhi ya mambo wangeweza kuyatolea maelezo.

Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) Muhidin Zubeir Muhidin ambaye alifanya juhudi za kuwasiliana na polisi na taasisi nyengine katika kutafuta suluhu za machaguko yaliotokea hapa Zanzibar aliahidi kuendelea na mashirikiano na wadau wote wa amani nchini.

“Sote tunajukumu la kuhakikisha hali ya amani inarudi Zanzibar na kwamba, Uislamu hautoi nafasi kwa kufanya uharibifu wala kumdhuru mtu” alisema Sheikh Muhidin.

Kwa upande wao Maafisa wa Mabalozi kutoka Marekani, Uongezeza na Norway ambao walialikwa kama wasikilizaji katika mkutano huo walishukuru ushirikiano kati ya taasisi za serikali katika juhudi za kurejesha amani.

Mkurugenzi wa Utalii Zanzibar, Ali Khalil Mirza alisema sekta ya utalii inachangia pato kubwa la taifa kwa zaidi ya asilimia 75 inaweza kutetereka iwapo hali ya utulivu itatoweka nchini na hivyo kushauri mashirikiano zaidi kati ya taasisi zote na wadau ili kuimarisha hali ya utulivu nchini.

Wiki iliyopita baadhi ya watu wanaosaidikiwa kuwa ni wafuasi wa uamsho walikusanyika katika makamo makuu ya polisi ya mjini magharibi kupinga kukamatwa kwa miongoni mwa wanaharakati wa jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar.

Advertisements

7 responses to “Viongozi wakutana, hali bado ni tete

 1. Tunawashukuru viongozi wa jumuiya za kiislamu kwa kutoa ufafanuzi mzuri katika kikao hicho. binafsi niliangalia ZBC (TV) na kuona jinsi gani walivyoweza kusahihisha baadhi ya mambo ambayo polisi na vyombo vya habari walikuwa wakipotosha usahihi wake. kwa mfano mfumo uliotengenezwa kwa siku nyingi wa kuwafanya wananchi waamini kuwa serikali na polisi hawakosei au kufanya makosa. kwa jambo hili lilotokea Jumamosi na Jumapili bila shaka wananchi au Jumuiya wanamakosa lakini ukichunguza kwa undani utagundua kuwa polisi ndio chanzo na mzizi wa fujo zilotokea vyenginevyo walikuwa na uwezo na kuzuiya fujo isitokee. Hili lingewekana kama polisi wangetumia busara kuliko jazba.

 2. Hivi, ..mpaka leo..
  UMEKOSA UTHUBUTU?
  SALAMU zangu za kutoka moyoni ziwafikie kaka na dada zangu ambao kila kukicha mnazidi kuongezeka katika darasa letu kubwa zuri ambalo hufanya shughuli zake kila jumamosi na lengo lake kubwa ni kujifunza mambo ambayo yanahusiana na maisha yetu ya kila siku.Asante kwa kuchagua kusoma ukurasa huu.
  Leo kwa kiasi kikubwa tutaongelea kuhusiana maisha,mwalimu mwalimu wenu katika uchunguzi wangu ambao si rasmi sana nimekuja kugundua kwamba vijana wengi wamekosa uthubutu wa kufanya mambo yao hasa yanayohusiana na maisha ya kila siku.

 3. jamani hii si inaonesha wazi kama wazanzibar tunaamuliwa maamuzi yetu kutoka upande wa pili
  amani ya zanzibar eti wamekuja viongozi kutoka bara kujakuituliza hii inaonesha wazi viongozi wote wa serekali ya zanzibar ni bibaraka kw bwana zao watanganyika
  uamsho juu muungano hatuutaki

 4. Aslaam Aleykum jamiiya. Ama kwa hakika namsifu sana Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Emma Nchimbi kwa uamuzi wa haraka kufika Zbar kwa nia ya kutuliza machafuko kati ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama na wafuasi wa Uamsho na vijana wenye hasira. Tena sifa zimwendee yeye binafsi na washauri wake kwa kuamua kikao cha pamoja kishirikishe hata viongozi wa taasisi za dini. Hata SUK nayo inastahili pongezi kiasi chake kwa kujitahidi kuchukua hatua za kuwezesha kikao hicho cha mashauriano kufanyika. Hata kikao hichi kufanyika, palitumika HEKIMA na BUSARA, nyenzi muhimu zilizokosekana kwa pande zote ambazo kuvutana kwao ndiko chimbuko la kutoweka ghafla kwa amani na utulivu. Yaliyotokea yatupe funzo sote twenye jukumu la kulinda amani na utulivu ktk nchi yetu.

  • Hayo ndio tusioyataka. Nchimbi imemuhusu nini Zanzibar? Nchimbi ni watawala wetu kama watanganyika wengine na inafaa watengwe. Kama hajasikia kuchomwa kwa makanisa asingekuja kabisa Zanzibar.

 5. Acheni ujinga uo nyie mnaotaka kuiharibu znz hamna lolote kz ni ubaguzi wa dini tu ndoo mlionao kama swala la muungano makanisa na magari kuyatia moto maanake nini?? hakuna muungano kuvunjika wala nini wajinga wakubwa, kwa kipi kikubwa mnachowapa tanzania bara au wao wanapata nini kutoka znz, nia yenu iyo znz iwe ya kilsam kitu ambacho hakiwezekani, kwani mnajijua mkifa mtawekwa wapi kwa mungu, au mtapokelewa vp na muumba? acheni kujifanya kama mungu ni wenu pekeenu! haki! haki! kama wewe mwanamme haki anayo mkeo na kama ni mwanamke haki anayo mmeo acheni mambo ya kishetani wapumbavu wakumbwa! Nakwambie izo zambi mlizozitenda zitawarudia ninyi wote ,eti UAMSHOO! mlidai kue na serikali ya kitaifa, serikali imeundwa, na mambo yanakwenda sawa, sasa tena yamezuka kuamshana maana mlikuwa ucngizini mlipotaka serikali ya umoja wa kitaifa?? mwenzenu uyooo anakula kuku kwa mrija chupi zinawabana sasa! mmeamua kuamshana mmechelewa , unavuta shuka wakati kumekucha, YAGUJUUU! Sasa endeleeni na fujo zenu kuna silaha zimekaa mda kdg hazijatumika na yale mabomu yapo tuu kwenye maghala bila matumizi! nafkiri mda wake umefika wa kuyatumia.

 6. Mkombe

  Nchimbi alikuja kwa kuwa sisi wenyewe tilshindwa kuelewana. Mimi naona sasa ni wakati wa kurudi nyuma kunona nini kipi tunatafuta. Ugomvi au kujenga Zanzibar iliyoimara. “A divided house never stands”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s