Watoto zaidi ya 55 walazwa kwa kuharisha

Vijana wa Red Cross Tawi la Muembeshauri Unguja wakifanya usafi kwenye wodi ya Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ikiwa ni moja ya kazi zao kutowa huduma kwa jamii katika huduma mbalimbali mnamo Aprili 2 mwaka huu.

WATOTO wanane wamefariki dunia na zaidi ya watoto 55 wamelazwa katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja kutokana na matumbo ya kuharisha huku chanzo cha ugonjwa huo kikiwa hakijajulikana hadi sasa. Muunguzi dhamamana wa hospitali hiyo Khadija Muombwa Ame alisema amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo tokea mwezi uliopita hadi sasa na kusema kwamba ugonjwa huo bado haujajulikana kama ni maradhi ya mripuko au laa.

“Ni kweli kuna tatizo hilo la watoto kuharisha sana tokea mwezi uliopita tatizo hili limekuwa likijirejea lakini watoto wanakuja hospitali na kurudi vifo sio vingi lakini watoto wanane ndio waliofariki na watoto kama 58 ndio waliokuwa wamelazwa na sasa hivi hivyo hivyo” alisema Muuguzi dhamana.

Kufuatia wagonjwa hao ambao wamekuwa wakiletwa kwa wingi katika hospitali hiyo ya Mnazi Mmoja Muunguzi Dhamana alisema wanalazimika kuwalaza watoto watatu hadi watano katika kitanda kimoja.

Daktari huyo alisema watoto wengi waliolazwa katika hospitali hiyo ni wenye umri kati ya mwezi mmoja hadi miaka mitano ambapo baadhi yao wamekuwa wakiruhusiwa lakini baada ya siku mbili wanarejeshwa tena kutokana na tatizo hilo hilo la kuharisha mfululizo.

Naye mama mzazi ambaye mtoto wake amelazwa katika hospitali hiyo Fatma Juma Omar Mkaazi wa Tomondo Unguja, amesema hajui kilichomsibu mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili lakini amempeleka hospitali ili kupata matibabu.

“Leo ni ya nne mimi nipo na mwanangu hapa hospitali na nashukuru nimepewa dawa ya mtoto lakini naona bado hajasita kuharisha lakini amepunguza sio kama nilivyokuja mwanzo” alisema mama huyo.

Muuguzi huyo alisema madaktari hadi sasa hawajagundua chanzo cha maradhi hayo maana tunawapa dawa na kuwaruhusu lakini baada ya siku mbili naona wanawarejesha tena watoto hospitali wakisema wamerejea tena kuharisha.

“ Kwa kweli bado hatujajua ni chanzo gani cha maradhi haya lakini nadhani ni kuharisha kwa kawaida tu kumeingia lakini sio kipindupindu” alisema Muuguzi huyo.

Aidha Muuguzi huyo alilalamikia wazazi wa wagonjwa hao wanaolazwa katika hospitali hiyo kwa kushindwa kudumisha usafi katika wodi kutokana na kutupa ovyo nguo za watoto wao wanazowavua (Pampare) pamoja na kutupa ovyo vyakula.

“Mama wanaokuja na watoto wao hapa katika hospitali wanatusikitisha sana kwa sababu hawaweki usafi utamkutaa mama anakula juu ya kitanda hali ambayo insababisha kuwepo vijidudu , wakenda chooni wanawacha uchafu na wanawabadilisha watoto wao nguo bas utamuoana mtu anatupa ovyo pampare sasa hali kama hiyo hairidhishi hapa hospitali” alisema Muuguzi huyo.

Hata hivyo aliwaomba akina mama hao kudumisha usafi na kuwapatia chakula na maji safi watoto wao wanapotoka hospitalini kwani chanzo cha kuharisha wakati mwengine kinatokana na uchafu uliopo katika maeneo mbali mbali ya hapo hospitali na maeneo ya kuchezea watoto hao majumbani na sehemu za nje wanapocheza.

Katibu wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Omar Abdallah amesema hospitali ya mnazi mmoja imezidiwa na wingi wa wagonjwa kutokana na baadhi ya wananchi kujenga dhana kwamba ndio hospitali kuu na yenye huduma zote.

Alisema tabia ya wananchi kufanya ndio kimbilio lao katika hospitali hiyo kunasababisha msongamano mkubwa wa wagonjwa na hivyo kusababisha matatizo kwa wagonjwa na madaktari wenye kutoa huduma kwa wagonjwa hao.

“Ipo haja kwa serikali kulitazama suala hili upya kwa sababu matihaji ya wagonjwa yamekuwa kwa kisi kikubwa na licha ya kuwepo na vituo vya afya vya mikoa na wilaya lakini bado wananchi wana imani kubwa na hospitali kuu na dhana hiyo imekuwa ikileta usumbufu mkubwa kwa wahudumu kutokana na msongamano mkubwa wa wagonjwa” alisema katibu huyo.

Katibu huo huyo aliwashauri wananchi kutumia vituo vya afya vya mikoa na wilaya ili kupunguza mgongamano katika hospitali hiyo ya mnazi mmoja ambapo kwa sasa imekuwa na msongamano mkubwa wa wagonjwa.

Advertisements

5 responses to “Watoto zaidi ya 55 walazwa kwa kuharisha

 1. sasa wagonjwa kuwaweka kitanda kimoja si kusababisha uambikizi jamani wa mtoto kwa mtoto ? utawaweka vipi watoto wawili kitanda kimoja , wakati hata ugonjwa wenyewe haujajulikana? mnasema vifo sio vingi , hivi mko sirias? yaani kufa mtoto ni kawaida? mjitahidi wasife wote ndio tunavyotaka. Kama kutupa pampers si muweke debe au pipa la kutupia taka humo wodini halafu muone kama watatupa ovyo , hata kuweka pipa mpaka tupate msaada kutoka nje? katika dunia ya sasa hakuna cha bure kila kitu kina namna mfadhili hakupi chake bila kuwa na lengo lake aliloliweka. Ikiwa hapo mnazi mmmoja huduma mbovu unategemea nini huko vituoni si balaa tena ,

 2. au mnazitunga hizi habari ili mulete chanzo za majaribio kujaribia guinea pigs ( watoto wetu) zanzibar , manaake wakati mwengine hawa watu wa afya wakiahidiwa mapesa , hutunga ugonjwa usiokuwepo ili wawashawishi wananchi kutumia chanjo ambazo bado ziko majaribioni ambazo hazijahakikishwa kwa matumizi ya binadamu kwa hio tutaletewa sisi wajaribiwe watoto wetu.

 3. hivi haWA MADAKTARI WETU WANA NINI, IKIWA WAGONJWA WANAPELEKWA HOSPITALI NA TATIZO KAMA HILO Takriban mwezi ss, iweje hawajagundua chanzo cha tatizo nini, hatuoni kwamba hawa watu wapowapo tu, hawajui hata wanachok,ifanya! jamani tutafika kweli!

 4. Inasikitisha kusikia kuwa Hospital haijajua sababu ya ugonjwa ambao upo kwa zaidi ya mwezi sasa. Ivi hawa wanaokufa wangekuwa watoto wa koo za ibni Kinana, Khuzaima au Mudirika Hospital ingesubiri MUngu awateremeshie majibu ya nini kinasababisha Ugonjwa huu. Hiki ni kichekesho jamani. Hospital kazi yake ni kutibu, kuchunguza na kuzuia. Kama kazi hii ya kuchunguza haiwezekani hospital hubaki kama tawi la Chama.

  Muuguzi huyu anaelaumu kina mama kwa kuchafua wodi naye pia astahili kulaumiwa. Watu wa visiwa vya hivi ni wasafi. Wanachafua kwa sababu wodini hawajui watupe wapi taka. Utaambiwa tuu usitupe taka hapa lakni huonyeshwi pa kutupa.

  Muuguzi huyu anaelaumu kina mama kwa kuchafua vyoo naye pia ni wa kulaumiwa. Ivi kweli hospital ambayo ina wafagiaji wengi kuliko madaktari ya shindwaje kufanya usafi wa pampers mbili tatu hadi hii ikawa ni issue ya kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari. Muuguzi huyu jamani hakujua kuwa kulifanya hili kuwa issue anauponza ungozi wake ambao unatumia fungu la kuwalipa wasafishaji mishahara na viinua mgongo. Ningekuwa mimi kiongozi usafi wa wodi ninge ubinafsisha na kelele zingekwisha.

  Katibu huyu wa hospital anaelalamikia watu kwenda Mnazi moja wote na kuacha vituo ivi ni mgeni hapa kwetu. Ivi hajui kuwa hata hapo Mnazi watu wendapo wenda hiyo basi tu. Kwani Katibu huu hajui kuwa vituo vya afya huko pembezoni vipo vipo tuu. Imefika wakati sasa kwa Katibu huyu kufikiria namna gani ataiimarisha Mnazi moja. Kulalamika haitoshi.

  Enyi wataalamu wetu ivi ugonjwa huu usiojulikana sababu yake mbona mnauchukulia kimzaha. Mnataka watu wengi zaidi wafe kisha iundwe Kamati ya Maafa. Ivi kweli mbona kipindi chote hiki hamja omba msaada kuka kwa competent entitiies CDC kwa mfano ili isaidie kutafuta chanzo cha shida hii. Amkeni jamani. Kwa kweli Wizara ya Afya inahitaji mabadiliko ili iendane na mahitajji.

 5. Hapa tutaongelea mengi lakini la msingi ni kuwa hawa viongozi wetu tulionao kuanzia SHEHA mpaku juu kabisa hawajali Raia zao wanachojali ni maslahi yao tu. Hata raia wakaumwa, ikiwa maji safi hayapatikani, hospitalini madawa hakuna wataalamu na vitendea kazi ni kidogo sana wao hawashughuliki. Kwa sababu wanajuwa maslahi yao tu. Leo hii angali wanavyowasakama hawa viongozi wa UAMSHO wanaosimamia haki ya kudai nchi yao huu ni mfano hai kabisa. Lakini sisi tunawambia shughulikieni raia zenu afya ya raia ni muhimu sana kwa faida ya taifa. Musishughulikie UAMSHO NA MUUNGANO TU. Sisi hatuutaki muungano.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s