Ngonjera za CCM na upepo wa mabadiliko

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Pius Msekwa

Na Abdallah Vuai, Zanzibar

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Pius Msekwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Ujerumani wiki iliyopita aliweka bayana msimamo wa Chama chake kubakia na sera ya Serikali mbili katika Muungano. Katika mahojiano na DW Msekwa alisisitiza na kuwakumbusha wanachama wa CCM wakati watakapotoa maoni mbele ya Tume ya Katiba kukumbuka sera ya Chama hicho katika Muungano ni kubakia na Serikali mbili.

Ama kweli Msekwa ameachwa nyuma katika wakati mpya, anaonekana wazi kuwa anashindwa kubaini hisia za Wazanzibari na hata zile za wanachama wake ndani ya CCM kwamba wamechoka na sera zisizowaletea manufaa.

Muundo wa Serikali mbili umeelezwa na watu wengi kwamba ndio kiini cha matatizo mengi ya Muungano,lakini mtu kama Msekwa ambaye ameshiriki kuandika katiba ya mwaka 1977 angeweza kutoa ushauri ambao unaendana na mazingira ya sasa.

Wazanzibari wengi hawautaki Muungano wa kikatiba, wanapendelea kuwepo na muundo mpya wa Muungano usio wa Serikali mbili wenye manufaa kwao.

Sera ya Serikali mbili ni sawa na nyumba kongwe na nguo iliyochakaa, lakini kwenye macho ya CCM bado inaonekana mpya, fikra za watu wengi walitegemea kikao cha NEC kingekuja na mkakati wa ujenzi wa nyumba mpya iwe na haiba mpya na yenye mvuto hata kwa wapiti njia wakatamani nao kuwa na nyumba ya aina hiyo au ramani yake.

Nyumba hiyo iliyojengwa kwa mawe na chokaa Wazanzibari hawaipendi, hata ukiifanyia matengenezo ni yake yale,mbwa kumwita jibwa , ukiacha mawe,chokaa,udongo wake hauwezi tena kushika chokaa na pia haiwezi kuhimili vishindo,ni lazima ijengwe upya katika mtindo mpya na wa kisasa.

Ikiwa CCM itaendelea kupuuza ujenzi wa nyumba mpya ya matofali,saruji,basi ijiandae kukataliwa na wapigakura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwani kwa hali ilivyo Zanzibar Chama chochote cha siasa ambacho kitakumbatia sera ya Serikali mbali au tatu hakitaweza kupata uungwaji mkono na wapigakura.

Ingawa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu Amani Abeid Karume kabla ya kustaafu aliweka misingi imara ya kukihakikishia Chama chake kubakia ndani ya Serikali hata kikishindwa uchaguzi chini ya maridhiano ya kisiasa yaliyosababisha katiba kurekebishwa na kuwepo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa.

Karume amemaliza kazi ya Urais na mwishoni mwa mwaka huu atamaliza kazi ya Umakamu Mwenyekiti wa CCM kwa kujijengea mazingira ambayo hata kikishika nafasi ya pili katika uchaguzi kitakuwepo,lakini hilo halikuwa lengo la Karume,lakini kwa hali ya leo mwendo wa CCM Zanzibar ni mbaya hauridhishi na zaidi tangu kumalizika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Wana CCM wanamtaja pia Naibu Katibu Mkuu mstaafu,Saleh Ramadhan Ferouz kuwa aliweza kukiongoza Chama hicho katika ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2005 na ule uliopita,lakini wanamashaka kama rekodi hiyo inaweza kuendelezwa au la.

Ile Maskani kaka ya muembe kisonge imekuwa daraja na jiko la kutafuta chejio kwa wengine, magari makubwa kwa kunufaika na siasa za kushupaliana, iwapo CCM itashindwa kukabili wimbi la mabadiko kitajikuta kikimbiwa na wanachama kama wenzao Bara wanavyohamia CHADEMA.

CCM Zanzibar inapita katika kipindi kigumu na ikiwa Naibu Katibu Mkuu Vuai Ali Vuai mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za CCM anayefanyia kazi zake Zanzibar asipokuwa makini na kukubali kusoma wakati anaweza kuingia kwenye historia ya Chama chake kuwa mshindi wa pili katika uchaguzi mkuu.

Mabadiliko ni lazima hakuna atakayeweza kuyazuia kwani wakati umebadilika,ni matarajio kwamba CCM ndio chama kilichoshinda kwa maana ya Chama tawala kiwaongoze Wazanzibari kufikia katika muundo wa Muungano wanaoutaka ambao ni ule wa mkataba sio tena wa kikatiba.

Na iwe itakavyokuwa, hali halisi ya muundo wa Muungano unahitaji mabadiliko ambayo yatakubaliwa na Wazanzibari,lakini hatua yoyote ambayo inawanyima haki hawatakubali kwani nguvu ya umma ambayo imeoneshwa katika mikutano tofauti ya kudai kuwepo kwa mfumo mzuri wa muungano haiwezi kuzuilika kwa ngonjera za CCM.

CCM inapaswa kutumia fursa ya kuandika kwa Katiba mpya kutoa ushawishi wa kubadili mfumo wa muundo wa muungano ambao kilio cha Wazanzibari kwa sasa kama walivyoamua kuvuana magamba basi nawaamuwe kuvua muundo mkongwe wa Serikali mbili, kwani “ukiamua kula Mbwa ule Mbwa wa Kizungu, usile Popi anayeshinda kwenye majaa. ”

Mfano wa Popi isije kutafsiriwa kuwa ndio kitoweo sahihi cha Watanzania ni kujaribu kutoa tofauti ya Mbwa wa Kizungu na Popi wa Tandale kwa tumbo au Chwaka.

Waafrika wengi wana imani kuwa kitu kizuri na chenye thamani hakiwezi kuwa cha Kiswahili, bali lazima kiwe cha Kizungu. Kuna Kuku wa Kizungu,mayai ya kizungu, embe ya kizungu, na Kuku wa Kienyeji!

Katika Muungano ni hivyo hivyo, Miungano ya kizungu imekuwa haina malalamiko,tazama Muungano wa Ulaya, Uingereza, Ubelgiji na hata Marekani,lakini Afrika wapi leo uko wapi Muungano wa Senegal na Gambia,uko wapi Muungano wa Ginneu, Misri na Morocco,Sudan, Ethiopia?

Yawezekana kabisa kusambaratika kwa Muungano wa Mataifa hayo kumetokana na kuwepo kwa mfumo dhaifu wa muundo,hivyo kwa kuwa Tanzania itaandikwa Katiba mpya wakati ndio huu kuweka sawa nyumba yetu.

Kwa wale wote wanaopenda kuiona Zanzibar ikirudia zama zake za kuwa kituo cha kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki hawana budi kuunga mkono kubadili muundo wa muungano kwani ikiwa tutakuwa na muungano wa mkataba Zanzibar inaweza kuwa kituo kikubwa cha biashara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Bandari huru itafanya kazi kama ilivyo katika nchi za Dubai, Emirate, Singapore, Malasyia, Hong Kong, ambapo itachangia kukuza uchumi wa eneo la maziwa makuuu.

Advertisements

11 responses to “Ngonjera za CCM na upepo wa mabadiliko

 1. CCM wanadhani na kuamini ya kuwa upepo hautowafikia uliovuma nchi kama Egypyt, Tunisia au Libya na kuwang’oa madarakani viongozi wasiotakiwa na wananchi. Na pia hawaamini kama umma wa Kizanzibari ukiamua unaweza kuusambaratisha muungano wenyewe.

 2. PIUS MSEKWA AMEPITWA NA WAKATI. BADO ANA SIASA ZILEZILE ZA BABA WA TAIFA HAONI KUA SASA TUKO KWENYE MILENIA NYENGINE. KAMAMUUNGANO WA SERIKALI MBILI KUELEKEA MOJA KAMA WANAVYONADI NI MZURI NI KWELI ILA NI MZURI KWA MASLAHI YAO BINAFSI NA SIO KWA WAZANZIBARI WALIO WENGI. NAAMINI HATA WATANGANYIKA WALIO WENGI NAO HAWAONI FAIDA YA MUUNGANO HUU ZAIDI YA SIASA ZA NGONJERA. WAZANZIBARI SASA WAMESHACHOKA NA SIASA ZA KUDANGANYANA MCHANA KWEUPE. NI IMANI YANGU KUA NA NDUGU ZETU WA TANGANYIKA NAO WATAZINDUKA NA KUACHANA NA SIASA HIZI ZILIZOPITWA NA WAKATI NA KUVUJILIA MBALI MUUNGANO HUU AMBAO TIJA YAKE NI KWA VIONGOZI TU NA SIO KWA WANANCHI. KAMA NI MUUNGANO MZURI KAMA WANVYODAI VIONGOZI KWA MIAKA 50 NAAMINI JAPO NCHI MOJA JIRANI INGEKUA IMEOMBA KUJIUNGA NA PIA KUSINGEKUA NA HAJA YA KUUNDA MUUNGANO MWENGINE UNGEENDELEZWA TU HUU ULIOPO. ILA BAADA YA VIONGOZI WA AFRIKA MASHARIKI KUONA KUA HUU SIO MUUNGANO BALI NI UKOLONI AMBAPO TANGANYIKA INAITAWALA KWA MABAVU ZANZIBAR WAKAAMUA KUUNDA MPYA WA MIKATABA. KAMA NI MUHIMU KUBAKIA NA MUUNGANO BASI USIWE HUU ULIOPO SASA NI LAZIMA UWE WA MKATABA. EE MWENYEZI MUNGU UANGAMIZE MUUNGANO HUU UBAKIE HISTORIA TU.

 3. Subhaana Allah, walhamdulillah, wa laa ilaaha illa Allah. Allahu Akbaru. Mambo si madogo, cha kushukuru yako mwisho kabisa tena mwisho. Nilihofia kuwa wangekuja na serikali tatu, ambazo najua wangelazimisha ziwe katika federation na sio katika sura ya confederation. Lakini kama wameganda pale pale watakiona cha mtema kuni.

 4. Ndugu zangu wa-Zanzibari, tuendelee kudai na kudai mfumo wa muungano wa mkataba na kwa njia zozote tuukatae muungano huu wa kikatiba, narejea tena tuukatae muungano tulionao sasa. Zanzibar lazima urudi tena katika umoja wa mataifa UN haraka iwezekanavyo.

 5. sio kweli kina muungano una matatizo , uwe wa kizungu au wakitanganyika, sisi hatutaki muungano wowote ule nd piusi , tuachieni peke yetu muone vipi tunafikia maendeleo katika muda mfupi , na kwanini tunalazimishana nd piusi ?

 6. @ msema

  Unajua ndugu yangu msema, mimi ninawasi wasi na u-CCM wa kina-Msekwa kwa sababu watu kama Samuel Sitta,Pius Msekwa, Dr. Harrison Mwakyembe, Prof. AnnaTibaijuka, Mizengo Kayanza Peter Pinda a.k.a “Zanzibar si Nchi”, Emanuel Nchimbi n.k Hawa bwana hulala CCM na huamkia CHADEMA. Hawa bwana ni mawakala wa Kanisa (CHURCH MOVEMENT AGENTS) panga pangua, lengo lao ndani ya CCM ni kuwasaidia ndugu zao CHADEMA ambao ndio hasa tegemeo la sasa na muda ujao katika kuyalinda maslahi ya Kanisa ili wai-overtake kiulaini CCM. Hii ni kwa sababu Kanisa kwa muda mrefu tangu Nyerere limekuwa likilambishwa asali kupitia CCM, sasa limeamua kuchoka mzinga (Limeunda CHADEMA) kwa kwenda jenyewe Ikulu likakae na hapo Waislamu tutakoma. Na nchi itakapoingia mikononi mwa CHADEMA 2015 hawa wanaujira wao mkubwa tu ndani ya serikali ya CHADEMA kwa sababu kazi itakuwa ni kurejesha cards za CCM hadharani na kuingia CHADEMA huko hawataanza tonge ndogo bali wataanza na tonge kubwa kubwa.

  Mawazo haya mtu anaweza akayaona ni ya hapa ukumbini tu na labda hayana ukweli wowote ule, hususan mtu ambaye hajakaa Tanganyika na kujionea mambo yote yanavyokuwa controled na Kanisa legally and ilegally through its well prepared agents kuanzia Kisiasa, Kiuchumi, Utamaduni na hata Kielimu. Kwa ufupi hawa watu wao Ukristo na Bibilia mwanzo au mbele Utaifa na Uzalendo nyuma au mwisho.

  Itakumbukwa kuwa Samuel Sitta amekuwa akishutumiwa mara nyingi kuwa ni CCM-CHADEMA au ukipenda ni DOUBLE FACES yaani ananyuso mbili robo CCM halafu ni CHADEMA kasorobo.

  Hivyo wanapolazimisha policy (sera) ya serikali mbili lengo lao ni kutaka kuendelea kuikandamiza Zanzibar ardhi ambayo ni tatizo kwa maendeleo ya Kanisa na hata hivyo si muhimu kwa ajili yao maana kuna Waislamu wengi na ya Waislamu.

  Vile vile lengo lao la pili ni kutaka kuutumia muamko uliopo ili watu wazidi kuichukia CCM ili CHADEMA itumie mwanya kujiimarisha.

  Ama kuhusu Pius Msekwa naomba muifatilie historia yake ya kiutendaji ili kulibeba Kanisa ndani ya serikali hususan alipokuwa katika NECTA hapo ndio mtapima kwa nini waje na msimamo huu hivi leo ambapo yeye nimakamo mwenyekiti CCM?.

  Issue ni kwa Waziri asiyekuwa na wizara maalum Dr. Ally Moh’d Shein ambaye yeye na timu yake wapo katika kuwaudhi ndugu zao Waislamu Wazanzibari kwa kutegemea rushwa ya uongozi kutoka Dodoma.

  Je! Shein unauhakika na utetezi wa Dodoma kukurudisha tena Ikulu?

  Je! Wazir Dr. Shein huoni kama kuwatetea Wanzibari hivi sasa ndio njia pekee ya kukubakisha madarakani?

  Je! Waziri Dr. Ally Moh’d Shein hujui kama mcheza kwao hutunza na fimbo ya mbali haiui nyoka?

  Sawa kama hujui hayo endelea ila ujue asiyesikia la mkuu huvunjika guu na majuto ni mjukuu. Jikaze wacha kuregea waziri Shein eh! Haya! Langu jicho, wabongo hao!.

  Basi, sikiliza Mheshimiwa Waziri Dr. Ally Moh’d Shein usisubiri mpaka mauti ya uongozi yakuvae ndio uje uanze kutubia kwa Wazanzibari, hutasamehemeka wakati huo maana milango ya toba tutakuwa tushaifunga.

  MUUNGANO HATUUTAKI

  JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA.

  “When peace fails apply force”.

  Nawasilisha.

  SERELLY.

 7. Ujumbe uliopo chini uwafikie wale wote waliotayari kulazimisha mambo yawe vile watakavyo na si kwa mujibu wa kanuni na wakati

  Bartlett’s Familiar Quotations attributes the phrase, “Man is a social animal,” to Baruch Spinoza:

  “Yet it rarely happens that men live in obedience to reason, for things are so ordered among them, that they are generally envious and troublesome one to another. Nevertheless they are scarcely able to lead a solitary life, so that the definition of man as a social animal has met with general assent ; in fact, men do derive from social life much more convenience than injury.”
  -Ethics, IV, proposition 35:note

 8. Pingback: Ngonjera za CCM na upepo wa mabadiliko·

 9. kutokana na umuhimu wa maoni haya ambaye ameyatoa katika mtandao wa email nimeona nitachapishe katika mtandao huu ambao mada hii amechangia Balozi Ali Karume

  From: Amb. Ali Karume

  Date: 2012/5/24

  Subject: CCM imeng’ang’ania ukale wake
  Makala nzuri sana na imefanya utafiti, uchunguzi na ufafanuzi mzuri. Lakini yapo mapungufu hasa kwenye kung’ang’ania maoni ya mtu binafsi yawe ndio sera kabla ya kuruhusu mdahalo. Chama cha kisiasa lazima chende na wakati, na CCM inatambua hilo na imejikita katika kuvua gamba. Ni mategemeo ya wengi kwamba baada ya chaguzi za chama mwaka huu, tutaona sura mpya na damu mpya.

  Alivyosema Shaaban Robert ni sahihi, na ukisoma vizuri maandishi yake, hakusudii kuyabwaga ya kale na kukumbatia mapya, bali ni kuboresha ufanisi kutokana na kuchanganya mbinu mpya na uzoefu. Abraham Lincoln alikuwa anakemea tabia ya kung’ang’ania Utumwa, ambao aliona kua ni jambo la kale. Kwenye Muungano wa nchi yake, aliridhika kutumia Jeshi, vita na mapambano yalopoteza roho nyingi ili Muungano uwepo. Wakati huo, alikataa mfumo wa muungano wa Confederation ambao Jefferson Davis na wenzake wa Kusini walipendekeza.

  Nikweli kwamba kuanzia 1964 hadi 1977, serikali za Tanzania ziliogozwa kutokana na maadili ya vyama vya TANU na ASP, na serikali ya Muungano ilitiwa shemere na TANU. Lakini viongozi wa TANU na ASP walishauriana kwa ukaribu sana juu ya sera na vikao vingi vya pamoja vilifanyika kwa nia ya mashauriano na maridhiano.

  Baada ya kuzaliwa CCM, madaraka mengi ya uamuzi kisera yalikwenda kwenye chama na serikali zikawa zinapata maagizo na muongozo juu ya utendaji. Tulikumbushwa party “Supremacy” ya CCM.

  Baada ya kuuwawa Mzee Karume, ilikuwa ni jukumu la BLM kuchagua Rais mpya na walimchagua Mzee Jumbe. Mwaka 1980 Mzee Jumbe alikwenda CCM kuomba ridhaa ya chama ili awanie nafasi ya Rais wa Zanzibar. Alipojiuzulu 1984, ilikuwa CCM, na sio BLM, yenye dhamana ya kuteua mgombea mwengine. Madai kwamba BLM ingechagua Rais ni potofu.

  Kila nchi ya kidemokrasia ina mapungufu yake na Churchill alisema “Mfumo wa dimokrasia ni mbaya, lakini mifumo mengine ni alkhasi”. Tumeshuhudia kupindwa kwa Katiba. Katiba ya Zanzibar ya 1984 na ya sasa, inasema kwamba Rais wa Zanzibar awe amezaliwa Zanzibar. Katiba inasema mgombea wa Rais Zanzibar awe ameandikisha kupiga kura na apige kura Zanzibar. Dimokrasia inakwenda sambamba na upigaji kura lakini mgombea mmoja wa urais Zanzibar alipata kura nyingi kuliko wenzake, lakini hakuambua kitu.

  Katika dimokrasia nyingi duniani, kuna tabia(mbaya) ya kupinda na kupotoza Katiba; kupinda na kupotoza sheria, ilimradi watawala wapate walitakalo.

  Mawazo ya kila aina, pamoja na mawazo ya waandishi wa makala hizi, ni lazima yazingatiwe katika kutayarisha Katiba mpya. Sitaki kutisha watu, lakini naamini kwamba siku ile ile katiba mpya inatangazwa, siku hiyo hiyo baadhi ya wenzetu watayaona mapungufu. La muhimu ni kuboresha Katiba yetu, ili hiyo mpya iwe bora kuliko hii tulonayo.

  Balozi Karume

 10. hawa mabalozi wa kupachikwa kama usultani na ufalme wasitubabaishe kusoma hawakusoma hupachikwa degree za heshima ya udaktari angalao waonekane wamesoma kumbe hawana shule , wewe nd karume unataka ukubwa na sifa tu hakuna lolote lile , nyote kina karume mmejaa rushwa mnanuka , hata mkifa makaburi yatakukimbieni, ogopeni kifo , sisi hatutaki katiba yoyote ile zaidi ya kuvunja muungano kawaambie hao waliokutuma kuandika maada hio juu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s