Epukeni udanganyifu katika michezo- Maalim

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ligi ya vijana “Central Taifa” waliofika ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kubadilishana nae mawazo. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na pembeni (kulia) ni mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Sherry Khamis.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar imesema itafanya kila liwezekanalo ili kuiwezesha ligi ya vijana Zanzibar iweze kusonga mbele. Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Said Ali Mbarouk alitoa ahadi hiyo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati kamati ya ligi hiyo Central Taifa ilipokutana na Maalim Seif ofisini kwake Migombani.

Aliahidi kuwa Wizara ya habari itatafuta fedha kwa njia yoyote ili kuhakikisha kuwa fainali za ligi hiyo inayotarajiwa kufikia kilele chake July mwaka huu kwa timu za Juvinail, Junior na Central zinafanikiwa. Alisema ligi hiyo ni muhimu katika kuibua vipaji vya vijana ambavyo vitasaidia kuinua soka la Zanzibar.

Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka viongozi wa ligi hiyo kuwa na dhamira ya kweli katika kuendeleza ligi hiyo, sambamba na kuepukana na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika kuibua vipaji vya wanasoka vijana.

“Sisi serikali tuko very serious na mimi binafsi niko interested kuona hadhi ya michezo inarejea Zanzibar, kwa hiyo na nyinyi viongozi muwe serious kwa hili”, alisistiza Maalim Seif.

Amewatahadharisha viongozi hao kuzitumia fedha wanazopewa kwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa na sio kuzitumia kwa maslahi binafsi. “ Wakati mwengine tunakosa ufadhili kwa kuwa hatuko serious, hao wafadhili nao wanaangalia ni kwa kiasi gani fedha zao zinatumika kwa malengo yanayokusudiwa, vyenginevyo ndio wanaona hakuna haja ya kutoa ufadhili” aliongeza.

Nao viongozi wa chama cha soka Zanzibar ZFA wakiwemo kaimu Rais wa ZFA Haji Ameir na mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Sherry Khamis, wamesifu utendaji wa Waziri mpya wa Wizara hiyo Mhe. Said Ali Mbarouk, na kwamba unawapa changamoto katika utendaji wao.

Wamesema Waziri huyo amedhamiria kweli kufanya kazi aliyotumwa na kamwe hakuna mzaha wala muhali, kama ambavyo mwenyewe amekuwa akieleza mara kwa mara.

Ligi ya vijana kwa ngazi za Juvinail, Junior na Central inazishirikisha timu za mitaani za vijana zilizopata usajili ambazo hushindana hadi ngazi ya Wilaya Unguja na Pemba ambapo hupatikana mshindi mmoja kwa kila Wilaya, na kuanzia hapo ndio kamati ya Central Taifa hushughulikia kwa ajili ya kuandaa fainali ambazo hufanyika Unguja na Pemba.

Advertisements

3 responses to “Epukeni udanganyifu katika michezo- Maalim

  1. maalim naona umesahau majukumu yako , sisi wananchi hatutaki muungano , wewe naona umelewa na masuala ya anasa na starehe , vipi ? utarudi kwa Mungu utamjibu nini? au unafikiri upo milele? nabii sulemani alipomjia malaika Israili ( as) kumtoa roho akalalamika vipi Mungu hakumletea taarifa , akaambiwa aangalie nywele zake na fimbo kuwa uzee ni dalili ya kifo.

  2. Maalim unanganyifu katika michezo ni muendelezo wa falsfa iliyokubalika ya mtu hali hadi adanganye. Sectors zote zilizo chini ya Serikali yako ni danganyifu. Hii haitaji uwe na PhD kuina. Ofisi za Serikali heshima yake haipo watu wanaingia na kutoka kwa muda watakao. Inawezekana kuna sababu nyingi kwanini haya yanatokea.

  3. Hayo ndiyo anayayawezaMaalim Seif pamoja na fitna.
    Kwa mtaji huu watanganyika hawatuachii ng’o

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s