Bei ya umeme sasa ni 85% Zanzibar

Meneja wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) Bw. Hassan Ali Mbarouk

Kwa kusikia taarifa hii kwa sauti tafadhali bonyeza hapa. 

Wakati wananchi katika visiwa vya Zanzibar wanalalamikia kupanda kwa bei za mahitaji muhimu ikiwemo vyakula, serikali katika visiwa hivyo imepandisha bei ya umeme kwa asilimia 85 ambapo wananchi watalazimika kulipia huduma ya umeme kuanzia tarehe mosi mezi ujao. Zanzibar yenye idadi ya watu wanaokisiwa zaidi ya million moja, ina watumiaji wa umeme zaidi ya laki moja na elfu tano.

Kasi ya matumizi ya Umeme Zanzibar imekuwa ukiongezeka kila mara kutokana na matumizi ya nishati hiyo kuongezeka pamoja na kampeni za kutaka wananchi watumie zaidi umeme na kupunguza ukataji miti ili kuepuka uharibifu wa mazingira.

Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Ali Mbarouk akitangaza hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema bei mpya itaanza kutumika Juni 1, mwaka huu.

Alisema shirika limepandisha bei kwa watumiaji wote kwamba bei hiyo mpya imepangwa katika viwango vya makundi matano.

Alisema makundi hayo ni pamoja na huduma ya kiwango cha kiwango cha uwezo mdogo, huduma ya jamii, viwanda vidogo, viwanda vya kati na vikubwa na taa za barabarani.

Mbarouk alisema kuamnzia Juni 1, umeme utauzwa shilingi 66 kwa uniti badala ya shilingi 50, kwa watumiaji wa kiwango cha uwezo mdogo.

Alisema watumiaji wa huduma ya jamii watalipa shilingi 161 kwa uniti badala ya bei ya sasa ya shilingi 120 na  watumiaji wa kiwango cha viwanda wanunua umeme kwa bei mpya ya shilingi 172.00 kwa uniti badala ya shilingi 140.00.

Alisema watumiaji wa kiwango cha viwanda vya kati na vikubwa watalipa shilingi  169.00 badala ya shilingi 140.00 kabla ya bei mpya na kwamba gharama ya umeme wa taa za barabarani umepanda kufikia shilingi 141.00 kwa uniti kutoka bei ya shilingi 105.00.

Mbarouk alisema ongezeko la bei mpya litafanyika katika awamu tatu kabla ya kufikia lengo la kuongeza gharama ya huduma hiyo kwa asilimia 85.

Alisema katika utekelezaji wa awamu ya kwanza umeme utapanda kwa asilimia 40, awamu ya pili bei itaongezeka kwa asilimia 30 na ya tatu pia kwa asilimia 30.

Alipoulizwa sababu za ongezeko hilo, Mbarouk alisema shirika limechukua uamuzi huo kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.

Ni kipindi ambacho sauti za wananchi kulalamikia kupanda ovyo kwa bei imekuwa ikiongozeka, lakini viongozi wa serikali wanasema kwamba hali za bei visiwani bado ni nafuu sana kulinganisha na nchi jirani.

Licha ya maelezo ya viongozi wa serikali, wananchi wanasema kuwa serikali haijaweza kujipanga vizuri ili kudhibiti mfumko wa bei wa bidhaa muhimu, hali ambayo inawaathiri wananchi wengi masikini na sasa kuongezeka bei ya umeme lakini Meneja wa shirika la umeme anasema pamoja na kupanda kwa bei za umeme Zanzibar, wananchi watalipia bei mpya kwa awamu tatu.

Zanzibar inanunuwa umeme wake kutoka Tanzania bara kupitia mkonga (Waya) wa umeme unaopita chini ya bahari hadi katika kisiwa cha Unguja na Pemba.

Hata hivyo waya unaoleta umeme Unguja umechakaa, na serikali kwa msaada wa Dola za Kimarikani milioni 72 kutoka serikali ya Marekani inafanya juhudi za kuweka waya mpya.

Licha ya Zanzibar imo katika juhudi za kutafuta vyanzo vyengine vya umeme mfano matumizi ya nguvu za jua na upepo na wawekezaji kadhaa kutoka nje tayari wamejitokeza. Lakini bado itaendelea kuitegemea Shirika la Tanesco la Tanzania bara.

Advertisements

8 responses to “Bei ya umeme sasa ni 85% Zanzibar

 1. Mwisho lini tutaacha uvivu na kusimama kw kujitegemea? Nijibu Mh. Wazir
  Hiv nikweli kwmb ZANZIBAR haiwez kusimama na kujitegemea wenyewe?
  Lakin inaonekana hamtaki ukweli lakin uhalisia wa yote haya sababu MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR. Imepelekea wananchi na viongoz wa nyazifa za juu kuhisi kila kitu hawawez kw sbb ya utegemez wa maamuzi. Ewe Mola waonyeshe njia viongoz wetu wanaongangania muungano ili znz isimame kw kujitegemea. Amin amin

 2. ‘Licha ya Zanzibar imo katika juhudi za kutafuta vyanzo vyengine vya umeme mfano matumizi ya nguvu za jua na upepo na wawekezaji kadhaa kutoka nje tayari wamejitokeza. Lakini bado itaendelea kuitegemea Shirika la Tanesco la Tanzania bara.’
  hawawezi ili wapate sababu ya kuutetea muungano

 3. Miongoni mwa hoja alizotoa Mkurugenzi Mkuu wa ZECO kuhalalisha ongozeko la bei ya Umeme ni gharama kubwa za uendeshaji. Katika hizi gharama za uendeshaji zipo ambazo ndugu yangu Mkurugenzi Mkuu zinaepukika. Kwa mfano Shirika kama lina watumishi wengi katika kada ya support staff inatakiwa wapunguzwe na kama haiwezekani basi hizo kazi wafanyazo zibinafasishwe kisha wao wawe wanahisa.

  Jambo jengine ambalo ZECO linaweza kulifanya na kupunguza gharama ni kuingiza approach ya transformation. Hii inakusudiwa kuongeza ufanisi kwa kutumia nyenzo kidogo. Sijui sasa hali ikoje lakini kama ZECO lina kwa mfano magari matatu ni juu yake kuona kuwa magari haya yanatumika kwa shirika lote si kila moja na lake. ZECO kama ina kazi zake inaweza kupanga kwa zile za routine na hivyo gari au madereva wakatumika ipasavyo. ZECO inatakiwa iwe na motorpool ambapo kila mtu atawasilisha ratiba yake ya kazi kwa kutumikiwa. Zile za Emergency zitafanywa kulingana na mahitaji. Taasisi nyingi leo kwa wenzetu zina mfumo huu na zimefanikiwa kupunguza gharama, Haitakiwi kuwe na gari ya Mkurugenzi Mkuu, Mke wake, Watoto wake nakadhalika.

  Suala la ubinafsi pia linachangia kuongeza ghara za Shirika. Inasemekana kuwa ajira hapo zinatolewa kwa misingi ya udugu au uhusiano. Katika hali kama hii uwezo wa taasisi kuzalisha lazima utaathirika na ndio maana Shirika linashindwa kufanyakazi kibiashara. Bila ya utaratibu mzuri ZECO halitafanikiwa na liatendelea kuongeza bei hadi limalize digits mtu anazo zifahamu.

 4. Hata bado. Ni njama tu za kutaka watu watishike na kubadili msimao kuhusu Muungano. Serikali makini haiwezi kuridhia hali hiyo itendeka kwa kuwakandamiza watu wake. Uelewe kuwa katika kipindi cha zaidi ya miaka ishirini Shirika halijabuni njia mbadala wa kutatua kero hii.

  Hivi sasa waya mwengine ndio kwanza utandazwa chini ya bahari. Hivi kweli kama Tanganyika ina nia yakuiachia Zanzibar pamoja na umsikini wake uliokithiri ingekubali mpango wa gharama kubwa wa kuleta umeme Zanzibar?

  YAGUJU, Kwa Mtaji huu, Tanganyika hawatuachii ng’o

 5. inashangaza sana viongozi wa zanzibar badala ya kuondoa kero zinazowakabili wananchi wake ikiwemo kubwa ya muungano na ile ya meli ya uhaakika kwa watu wa Pemba wao ndio wanazizidisha. angalieni sasa kero mpya hii ya umeme wanawabebesha raia masikini kwa kua wao wanalipiwa. Hakuna sababu yoyote ile ya kuongeza bei ya umeme. Hapa cha msingi ni kua mmeshindwa kazi na lililobakia MJIUZULU MSING’ANG’ANIE MADARAKA AMBAYO HAMYAWEZI..

 6. TOBAAA FAIDA YA MUNGANO NDO HII YA UPANDAJI WA BEI YA UMEME WANZANZIBARI AMKENI TUWEZE KUJITEGEMEE WENYEWE. VIONGOZI WOTE TETENI ZNZ YENU

 7. wacheni ujinga huo munataka kutuambia kuwa ingekuwa hakuna muungano mambo yasingekuwa yanapanda, nchi ngapi hazina muungano lakini inflaction ipo kubwa zaidi na kwa taarifa yenu pamoja na ongezeko hilo bado bei ya umeme ni rahisi Zanzibar kuliko bara, pili muungano hauzuii kuwa na chanzo chetu mbadala na ndo mana hivi sasa serikali imeanzisha task force kuangalia njia mbadala

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s