Hasira zako Dk. Shein, ni hasara kwako

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein

Jabir Idrissa

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ni dhahiri amepandwa na hasira. Naona tayari “watu wake” wamemlisha fitna. Inawezekana kweli amechukizwa kubaini kundi kubwa la wananchi wa Zanzibar limepata hamasa ya namna ya kuja kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Katiba ya Tanzania au kuikwepa wasiione. Wapambe watakuwa wamempa taarifa sizo. Na desturi inaonyesha mtu alopewa taarifa za uongo na kuziamini kwa kuwa waliompa ni “watu wake” anaowaamini, hujenga hasira. Sasa rais amepandwa na hasira. Nimethibitisha kwa matamshi yake alipokuwa kwenye hafla ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) – katika kijiji cha Koani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Wakati nilipokuwa naandaa makala hii, pembeni yangu alikuwepo jamaa yangu mmoja kutoka Fuoni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, aliyekuja kunisalimia ofisini, akanihoji, “Mbona unasema hafla ya chama chake wakati taarifa nilizosoma zimeonyesha rais alikuwa katika ziara ya kiserikali akizuru mikoa yote ya Zanzibar na alianzia kisiwani Pemba.”
Sasa niseme sina hakika ziara yake ni ya kiserikali au ya kichama. Sikupata mtu wake ili kuthibitisha jambo hili. Angalau katika moja ya picha nilizoziona kupitia vituo vya televisheni vya Dar es Salaam, nimeona wanaokuwa chini yake ni wakuu wa mikoa zaidi ya ilivyo wenyeviti wa CCM wa mikoa anamopita.
Lakini hiyo si mada leo. Akili yangu imenielekeza katika kile ninachokiona kama matokeo ya watu wa Dk. Shein kumpotosha rais, na sasa kukuta tunaye rais aliyejaa hasira rohoni.
Tatizo la hasira, ni kwamba mtu mzima anapokasirika hata watoto watagunduwa haraka atakapojitokeza kwao. Wananchi wa Unguja na Pemba, tayari wanajua “baba yao” – Rais Dk. Shein – amekasirika. Sikiliza anachokisema Dk. Shein: “Naelewa fika kuna watu wanaoleta mambo ya ajabu ajabu lengo lao likiwa ni kuvuruga amani tuliyonayo.” “… lakini nasema tena, maana nimeshasema hakuna mwenye ubavu wa kuivunja amani ya Zanzibar na kama mtu kachoka na amani iliyopo, ahame hapa hapamfai; atafute sehemu nyingine akaishi.”
Rais akamalizia, kauli ambayo naifananisha na alichowahi kukisema rais mstaafu mmoja mwaka aliokuwa anatafuta ridhaa ya mara ya pili ya uongozi. Alitaja “mapanga, myundu na mashoka” yaliyotumika kufanikisha mapinduzi.
Dk. Shein yeye hakutaja majina hayo ya silaha makini na za asili, bali alichokisema kinafanana. Amesema hivi: “Hii (Zanzibar) ni nchi ya kimapinduzi.” Anakumbusha yaleyale. Tafsiri yangu kwa matamshi haya, ni kwamba ukurasa mpya wa uongozi wa mabavu (wengine wanaweza kusema ni udikteta) umefunguliwa.
Kweli Zanzibar ilifanya mapinduzi 12 Januari 1964 baada ya Wazanzibari waliokuwa mbele ya harakati za kuondoa utawala wa wageni, kutoridhika na uongozi wa serikali ya uhuru iliyoundwa kufuatia uhuru wa 10 Desemba 1963, kupindua serikali hiyo. Lakini uhuru huu si ushetani kama unavyoonekana na wapinduzi hao. Ikiwa hivyo ndivyo, basi huko ni kufuta historia ya kule nchi hii ya visiwa vikuu viwili na vingine vingi vidogo, ilikotoka.
Ukweli ulio mchungu kwa baadhi ya makada wa CCM hasa wasiopenda mabadiliko ya mfumo na sera za uongozi wa nchi, ni kwamba kama si uhuru huo, hakungekuwa na mapinduzi. Wangempindua nani? Dk. Shein huna haja ya kukasirikia wananchi. Badala yake ni muhimu sana utambue kuwa hata wao wanaipenda nchi yao kama uipendavyo wewe na ujivuniavyo kuiongoza. Wanaipenda sana. Hebu afikirie kwani wananchi wanaposema “hatutaki Muungano huu” unadhani tafsiri ni kutaka uvunjike au uvunjwe? Hapana. Wanataka viongozi wao mtambue maoni yao na kuyafanyia kazi.
Dk. Shein una bahati kuiongoza Zanzibar ndani ya zama za mapambazuko. Hakuna hata moja sasa linaloweza kufichwa lisijadiliwe na wananchi. Usikhofu maoni ya watu bali yazingatie, ndio sauti yao. Zama hizi zinahitaji sana uongozi unaosikiliza kile wanachokisema wananchi. Hawa wananchi wanaosema hawataki “muungano huu” si wajinga.
Wanajua wanachokisema, nawe wapaswa kujiuliza, “Lakini kwanini hawautaki.” Itakuwa ni jambo la hatari iwapo Dk. Shein na serikali unayoiongoza mtapuuza maoni ya; mtayachukulia kama ni kelele za mlango; mkiyachukulia ni kero kwenu. Viongozi mtakuwa mnafanya kosa kubwa ambalo linaweza kuwagharimu.
Siku hizi, kiongozi anayestarehe madarakani ni yule anayefikiria wananchi wake wanachokitaka. Wanasema nini? Wanachokifikiria. Wanawaelewa vipi viongozi wao. Haya ni mambo muhimu viongozi kuyajua. Hivi tuseme Dk. Shein unakosa nini kuwasikiliza wananchi wanaoamini muungano hauwanufaishi bali unawakandamiza? Sasa si ndivyo waonavyo? Kumbe mtu kufikiri hivi anakusumbua rais?
Dk. Shein kama unataka kuongoza vizuri, basi zingatia vilio vya wananchi unaowaongoza. Tena ungeshukuru na kufurahia kuwasikia wanasema au kulalamika hadharani.
Kama hujanielewa ninachokusudia, panda ndege hadi London. Fika pale eneo ambapo serikali ya Uingereza imefunga vinasa sauti na kupandikiza makachero na kuruhusu watu kutoa maoni kuhusu wanavyoiona serikali yao na wanavyomuona kiongozi wao mtukuka Malkia. Kama kupuuza maoni ya watu ni ushujaa, wangeanza viongozi Uingereza. Hawapuuzi bali wanayasikiliza maoni au malalamiko ya Waingereza. Na si hivyo tu, wanayafanyia kazi yanayosemwa.
Kama ni kero viongozi hujitahidi kuziondoa, kama ni uchafu wanausafisha na kama ni vikwazo vya kupatikana kwa maisha bora, wanaviondoa. Sasa Dk. Shein unataka wananchi walale usingizi hata pale unapohutubia? Unataka uongoze mazombi au majuha kalulu? Uongoze watu wasiofikiri siyo, wala kujinafasi pao? Unataka kuongoza watu muflisi?
Itakuwa ni bahati mbaya sana – kuongoza watu majuha kalulu. Kumbuka tayari Wazanzibari kiasili ni watu wenye akili sana, wanafikiri kabla ya kuamua, wanauliza maswali wakitaka majibu. Dk. Shein unajua vizuri kwamba kwa sababu ya ukweli huo, ndio maana Wazanzibari wengi wanafanya kazi kubwakubwa kwingineko Afrika, na hasahasa Marekani, Ulaya na Uarabuni.
Unajua fika mamia kwa mamia ya wale walioondoka nyumbani kukimbia vitimbi vya utawala mbaya baada ya mapinduzi, wamejijenga na kukabidhiwa dhamana zenye hadhi kubwa ughaibuni. Ni muhimu kutambua vipaji/vipawa vyao. Ukitambua hili huwezi kupata shida kuwaongoza. Utakuwa unajua tangu awali unao watu makini ambao ukiwatumia vizuri watakusaidia kuibadilisha nchi iwe kweli ya maziwa na asali badala ya tope na harufu mbaya.
Ila ukiamua kuwapuuza na kuwakandamiza, utabaki kuongoza kwa shida. Huwezi kuwashinda japo una dola, maana wao ndio wenye dhamana ya uongozi. Nakuaidhi punguza hasira maana hujaipata bado sababu ya kukasirikia wananchi wasioridhika na mfumo wa muungano. Hivi hutaki kujisikia raha kwa kuongoza watu ndani ya mfumo wanaoukubali? Nakusihi sasa, hasira zako ni hasara kwako!

Advertisements

25 responses to “Hasira zako Dk. Shein, ni hasara kwako

 1. nd sheni ukitaka usitake muungano basi , ni heri ikiwa kwa amani , wewe tunajua umewekwa kama kibaraka na watanganyika, kwa hio huwezi hata siku moj kuwa mtetezi wa znz , jitayarishe kukutana na mola wako ujue nini utamjibu , huwezi kuwa rais halafu unawaambia wazawa wenye uchungu na nchi wahame, nafikiri ikiwa huwezi kututetea basi bora ujiuzulu , hayo majeshi ya mabwana zako hayatutishi wote tutakufa siku moja hakuna ataeishi maisha au milele , aliye mbora ni yule mwenye kufaidisha wengine kuliko wote , na wewe kwa mantiki hayo humo katika hawa , kibaraka mkubwa !

 2. kabla yako walikuwepo wengi wenye nguvu na majeshi kuliko wewe , lakini ilipokuja adhabu ya Mungu hawakufua dafu , huko kujidai kwako na majeshi uliyopewa na watanganyika si chochote mbele ya uwezo wa Mungu , zezeta mkubwa

 3. KAMA DR NI KIONGOZI AMBAE WAZANZIBARI TULIKUCHAGUA MWAKA 2010 BASI SISI NDIO TUNAOKUTUMA UKAWAMBIE WATANGANYIKA KUA HUU MUUNGANO HATUUTAKI TENA. HIVI UNAOGOPA NINI KUWAAMBIA HAYO HAO WATANGANYIKA WAKATI SISI TULIOKUCHAGUA TUKO NYUMA YAKO? KAMA KAZI IMEKUSHINDA BASI NI VYEMA KWA USTAARABU UKAACHIA NGAZI. HAPA INAONYESHA WAZI KUA DR HUKUINGIA IKULU KWA RIDHAA YA WANANCHI BALI KWA RIDHAA YA HAO UNAOWATUMIKIA TANGANYIKA.NA HAPA NDIPO MAISHA ZANZIBAR TUNAPORUDISHWA NYUMA KWA KUEKEWA WATU AMBAO SIO CHAGUO LETU NA MATOKEO YAKE KUTUSALITI KAMA HIVI. DR KUMBUKA KUA ZANZIBAR SIO YA CCM WALA CUF BALI NI YA WAZANZIBARI WOTE AMBAO KATIKA HILI WAKO KITU KIMOJA HAWAUTAKI MUUNGANO. KAMA NDANI YA CHAMA CHENU MNAUTAKA HIO SISI WAZANZIBARI HAITUHUSU NA TUNASEMA MARA HII MUUNGANO MWISHO. UTATUMIA NGUVU, VITISHO NA KILA KITU LAKINI UMMA WA WAZANZIBARI UNASEMA MUUNGANO BASI. KATIKA KIPINDI HIKI TUNASHUKURU MWENYEZI MUNGU ANATUFICHULIA WANAFIKI WASIOITAKIA MEMA ZANZIBAR KWA MASLAHI YA TANGANYIKA KWA SABABU YA KUPEWA CHEO..

 4. DK NAHIS SAIV UMECHOKA KUISHI KWA RAHA ILA 2NAKUAMBIA IV WAZANZIBAR WOTE HATUUTAK MUUNGANO NA SIO KAMA 2NATANIA NA UKI2MIA NGUV BAS SS 2NAJUA KUFA SIKU1 NA KUZALIWA SIKU 1 NA NINAKAPIA WALLWAH UKIWASHA MOTO HUU HAUZIMIKI TANGANYIKA ILE PALE KARIAKOO NDO 2NAPAANZA PATAKUA HAPATOSH NA UJUE UTAKUFA KIFOKIBAYA MAANA HATUKUACH MUSI2LAZIMISHE KI2 TULICHOKUA HATUKITAKI MUUNGANO HATUUTAKI
  TUACHINI TUPUMUEEEEEEEE

 5. haijahusu kumwandikindia makala kama hiyo Dr Shein alichokisema ni sahihi, kuna watu wanapita kushawishi wananchi kuhusu Muungano kwani si kila mtu ân akili zake na hiari yake kuchagua anachokitaka sấi nakuaje vikundi vya watu kupita mitaani kuchochea watu kuandikisha watu kwa nguvu majumbani mwao hadi kuwalazimisha kutia saini kile mnachokiita kupinga muungano. sấsa hapo tena mnamuonea huyu baba ưa watu. Sikushangaa hât kidogo kuona makala hii na hasa muandikaji wenyewe ikiwa ni wewe mana tayari kwenye mabega yako umeshayabeba ya kuyabeba na kichwani kwako tayari una mchwa wanaoutesa ubongo wako kwahiyo endelea tuu, lakini la ukweli lazima lisémwe, mtu na akili zake huna hậ ya kumburuza kwenda kutoa maoni yake lazima iwe hivi au vile na inaonesha wewe mwandishi ndio mwenye hasira na uchungu kwa kauli ya dr Shein na mimi nakwambia imekula kwako na kamati yako

  • @ mtu kwao

   Ndugu yangu unaonekana hata katiba ya Zanzibar ukombali nayo sana tena sana.

   UAMSHO wanahaki kikatiba ya kueleza mawazo yao, kushawishi wengine katika hilo, kushiriki katika kuendesha nchi yao moja kwa moja au kwa namna nyingine la muhimu wanatakiwa kuyafanya haya kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya Zanzibar.

   Ndugu yangu wacha UONGO, hawa Wazee wetu wenye uchungu na nchi hii (UAMSHO) hawamlazimishi mtu, tujuavyo sisi watu wote wamejaza na wanajaza fomu zile kwa hiari zao. Tujuavyo sisi UAMSHO imekuwa ikilaumiwa na kuhimizwa, kwa kutokuwa na copies za kutosha kiasi kwamba watu katika maeneo mengi ya mijini na mashamba wamekuwa wakiziagiza bila mafanikio, mfano mzuri ni rafiki yangu mmoja katika mtaa wa Jang’ombe Jitini ambaye wakina-Mama wamekuwa wakimuagiza mara kadhaa na mpaka hivi leo hawazipata.

   Sasa wewe unasema kalazimishwa mtu, wapi?. Na ni nani huyo?

   Wacha kusema uongo kwa kuwasingizia vipenzi vya Allah (s.w)

   Mbona unaonekana ku-fall katika Moh’d Aboud’s betrayal policy?

   Au ndio cadre (kada) wa chama fulani na kwa mantiki hiyo ndio upo katika kazi zako za kawaida?

   Au ndio mwenzangu na mie mkuu wa wakurupukaji umejikurupukia na kujiropokea kabla hata hujafikiri vizuri?

   Au ndio unakhofu kuwa labda Muungano ukivunjika utarudishwa kwenu Tanganyika? Au wewe siyee? Kama si katika hao basi hebu kuwa constructive.

   Halafu kweli wewe wa zamani. Umeona wapi mambo ya kijamii hususan matatizo yakatatuliwa na individual power kinyume cha collective power?

   Sasa UAMSHO na wengine wote wakiwemo wanasheria wetu wanapozunguka katika nchi hii wanatafuta nguvu ya pamoja (collective power) ili tuvuke kwenye dimbwi hili la ukoloni wa wa-Tanganyika. Wewe unaposema watulie tuuu si utakuwa unakusudie tuharibikiwe zaidi. Na hapa ndio ninapohoji juu ya uzalendo wako kuwa wewe ni mtu wa aina gani? Au ndio nyinyi CCM-maslahi? Nasema hivyo kwa sababu najua kuwa wapo CCM-wazalendo yaani Pro-Zanzibar CCM wanaumia na nchi yao, na CCM hawa ni wazuri na hawana mawazo mgando ya ku-copy na ku-paste kutoka vizazi hadi vizazi.

   Halafu unamsakama mwandishi na kumwambia “kwenye mabega yako umeshayabeba ya kuyabeba na tayari kwenye kichwa chako una mchwa wanaoutesa ubongo wako” .
   Bila shaka mtu mwenye akili timamu ataona wazi kuwa kauli hii ni sahihi dhidi yako kuwa wewe ndiye hasa unaestahiki kuambia maneno haya.
   Na hata kama mwandishi mabegani mwake amebeba ya kuyabeba basi aliyoyabeba yeye ni tafauti na uliyoyabeba wewe, kwa sababu mwandishi na sisi lake ndio la Wazanzibari wote na limo ndani ya bongo zao kuwa “MUUNGANO HATUUTAKI” na ulilobeba wewe ni kutetea vyama tu na sio nchi kwanza halafu vyama baadae. Utauwa shauri yako.

   MUUNGANO HATUUTAKI

   “When peace fails apply force”

   Busara ikishindwa kukuletea haki yako tumia nguvu.

   JAMHURI YA WATU ZANZIBAR KWANZA.

   Nawasilisha.

   SERELLY.

 6. imekula kwako wewe @mtu kwao. unaeishi tanzanzia. na dhiki zilizo jaa, na bado, lenu hasa!!

 7. Mimi naungana mkono na Rais na wala hajakosea hao watu wanaofanya kazi ambayo hawajaajiriwa wala kua na mkataba kwa kazi hiyo wana malengo mengine binafsi ambayo wala si kwa maslahi yetu wazanzibar, sote ni watu wazima tunajua zuri na baya so kwa vile tumepewa fursa muda ukifika kila mtu atoe maoni yake ni vipi anapendelea katiba iwe na huyo asotaka muungano atasema muda ukifika,na sio kuanza harakati ambazo hazina msingi wowote zaidi ya kutaka kuturudisha kule nyumba mambo ya kugawana sote tunajua fika kua muungano ni muhimu kwa sote na sote tunajua kua kuna kasoro ndani ya muungano ambazo hizo ndo muhimu kuzisimamia na kuhakikisha kua katiba mpya itakayokuja inazingatia hizo kasoro na zinaondoka na tunakua na Tanzania yetu ambayo haina minongono ya kasoro za nyuma.Kwa ushauri wangu tuache wananchi waamue nini wanataka na tusiwalazimishe kuwachagulia tunayoyataka sisi,muda umepita na sasa ni zama za uwazi na uhuru wa maamuzi,muungano daima na udumu ila turekebishe tofauti tu ili uwe bora na imara kwa manufaayetu sote watanzania.

  • Ndugu yangu suleiman ama kweli wewe bado umelala usingizi wa pono. Kwa ufupi Tanganyika au Tanzania hawako huko uliko kabisa kwani vikao zaidi ya 40 viliundwa kwa kuondoa kero za muungano je zimeondoka?lengo lao baya sana kwa zanzibar si jema na ndio maana haya yanafanya wasije tufikisha huko waliko kusudia itakuwa majuto,majuto,majuto sisi na vizazi vyetu kwani suleiman muungano hauwi hivi nchi moja kumtawala mwenzake na kumuamulia mamboyake ,na kama muungano huu ni mzuri miaka 48 sasa tokea uanzishwe je kuna nchi yeyote ambayo iliyofikiria kujiunga ,angalia muungano wa nchi za ulaya ulianza na nchi chache sana na sasa ziko zaidi ya 30 na bado ziko zinazotaka nafasi ya kujiunga kwa hali na mali hazijapata nafasi bado,angalia Africa mashariki ulianza na nchi 3 na sasa ziko 5 na bado nyengine zinataka nafasin kwa nguvu zote.na mwisho jua kwamba kizuri hakikataliwi kama ungekua mzuri watu wasinge ukataa walianza viongozi waasisi kina karume na jumbe kuukataa kwasababu waliuona mapema kua huu muungano ni wa dhulma na sasa wananchi wa zanzibar wenyewe tunataka kuiondosha tuungane kwa pamoja ZANZIBAR HURU KWANZA UTAIFA WA ZANZIBAR KWANZA AMKA WEWE JUHA UNAPORWA MALI YAKO.

  • @ Suleiman

   nimechoka kukaa katika na muda umeniishia user interface.
   Lakini kesho nitakuja kukujibu na kushauriana na wewe ndugu yangu. Lakini ndugu yangu suleiman tatizo sio kasoro za muungano tu, lakini tatizo KUU ni nia za Watanganyika katika Muungano huu.

   Jamani tujenge utamaduni wa kusoma vitabu ili mawazo haya yatutoke tena, aibu Jamani.

   Suleiman take an assignment usome angalau vitabu hivi:

   1.Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara ,cha Padri Dr. Sivalon.
   2.Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru (2010),
   Cha Dr. Harith Al-Ghassany.

   MUUNGANO HATUUTAKI

   “When peace fails apply force”

   Nawasilisha.

   SERELLY.

 8. Kwa kweli ni maada ya kuvutia sana: Serikali ya Tanganyika na Zanzibar pia wanatakiwa wasome alama za wakati, waache kujiona kuwa wao ni waungu watu, historia inaonesha kuwa unapokuwa mbali na watu automatic utafeli kwenye kuwaomgoza kwani wao ndio wenye mamlaka
  Dr shein umejionesha tuu upande wa pili wa u-Tanganyika wako ila tunakueleza na ukawaeleze watanganyika kuwa hapa hapatokalika mpaka kieleweke nakushaurini tuvunje muungano kwa Amani ili tuwe na ujirani mwema kama Malaysia na Singapore ila iwapo tutavunja muungano kwa nguvu basi mutegemee ujirani kama wa Ethiopia n Eritrea. Sasa ni juu yenu kuchaguwa wala musifikirie kuwa sisi tunakutegemeni nyinyi history inaonesha nyinyi ndio ambao munatutegemea sisi ila mulitufukarihsa na ndio mana sasa inaonekana hatuwezi kuishi bila ya muungano (hofu ya shein). Ila Malaysia waliwambia Singapore maneno kama ambayo munatuambia sasa hivi kuwa hata maji ya kunywa hawana seuze sisi ambao tuna resource za kila aina jee sasa hivi singapore wako wapi???

 9. Hivi kweli moderatoe unayapitia maoni kabla kuyapitisha au vipi? Hivi lugha hizi ndio alizozisifu Mwadishi Jabir kuwa una hazin ya wazanzibari wenye akili ughaibuni?
  Toa hoja na mtu avutiw kuisoma . sio matusi na kashfa zisizo na msingi.

  Kwa mtaji huu Watanganyika hawatuachii ng’o

  • Hakika mkombe hujulikani uko wapi huna mbele wala nyuma kama sigara nyota ZANZIBAR HURU KWANZA.

   • Inawezekana sina mbele wal nyuma lakini hapa kati nilipo najiamini, sitetereki na si kibaraka wa mawazo wala matamshi. Nina msimamo na natafakari kwanza kabla sijakurupuka.

    Kwa mtaji huu, Tanganyika hawatuachii mg’o
    .

 10. Huyu nae pia anaonekana ni KIBARAKA wa Watanganyika hata haelewi anachokisema, kwani nani amelazimishwa?? kinachofanyika ni watu kuelezwa ukweli (uhalisia wa mambo yalivyo) chaguo linabaki ni juu yako.

 11. Mimi sitaki kusema yupi yu sahihi kati yenu nyote mliotangulia. Pia sitaki kukubali pia kuwa rais wetu alikuwa sahihi kuwalaumu watu anaodai wanaweza kupelekea kuvunjika kwa amani nahivyo kuwataka wahame kama wamechoshwa na amani iliyopo Zanzibar.

  Tatizo kubwa ni naloliona ni kuwa rais wetu amekuwa jasiri kuwakemea watu ambao matendo yao hata siku moja hayatapelekea kuvunjika amani huku akipuuza kuwachukulia hatua watu wanafuja mali za Serikali, wanaoiba fedha za uma na wanaotumia madaraka yao vibaya.

  Mimi kwa maoni yangu ni hawa wanaotumia madaaka yao vibaya, ni hawa waibao mali za Serikali, ndio ambao Rais wetu angeamua kuwatunishia misuli kwa kuwa wizi wao na ubadhirifu wao unaharibu wezo wa serikali kuwasomesha vizuri watoto, kuwatibu vizuri wananchi na kufanya mambo mengine ya lazima ambayo nchi lazima iwafanyie raia zake.

  Katika kikao cha mwazo cha Barza la Wawakilishi 2010 Mheshiwa moja aliwataja Makatibu Wakuu wa SMZ kuwa ni miongoni mwa watu wanaofuja fedha za Serikali. Rais alipounda Serikali,watu hawa waliotajwa kama wafujaji walirudi tena Serikalini. Ripoti ya Karibuni ya Omar Ali Shehe imewataja tena miongoni mwao wakitumia vibaya madaraka yao, ikiwemo kuajiri watoto wao na kuwalipa stahiki wazizostahiki. Mambo kama haya ndio yaweza kupelekea uvunjifu wa amani na kwahivyo ndio mheshimiwa Dr. angeshaghulikia.

  Rais pia tumeona baadhi ya vingozi wake walivyoshindwa kusimamia maagizo yake na hivyo kufanya aonekane si chochote na waliowengi. Kwa mfano, aliwahi kuagiza kuwa wanyama wasionekane kwenye mji wa Unguja. Hili halikutekelezwa na hadi leo wanyama wanazagaa mjini Unguja utadhani ni zizi lao. Punda hadi darajani leo wapo na wanatembea bila kamba. Suala hili ndio la kulifanyia kazi tena kweli kweli.

  Jambo jengine ambalo ni muhimu sana na Rais wetu angelivalia njuga ni kusafisha uongozi wa hospital ya Mnazi moja. Huu umeshindwa kusimamia kazi ipasavyo na rushwa kwenye vitengo vingi bado ipo. Mfano idara ya maabara kuna watu wanatumia madawa kufanya vipimo kisha wanakusnya pesa bila risiti. Sehemu nyengine iliyooza ni Mapinduzi Kongwe, ambako kuna dada moja anakusanya pesa kwa kupatana. Hatujui kama haya ni maagizo ya wakubwa au ni kwa sababu anaona asikose chochote kutoka kwa wateja. Dr. Shei waliokupa taarifa za wanaotaka kuvunja amani na hili wangekusimulia kwa kuwa ni hatari zaidi ya wanahuburi kukataa Muungano.

  Utumiaji vibaya wa mali za Serikali pia ni suala ambalo Rais wetu angepashwa kulikemea. Toka aingie madarakani hatuoni mabadiliko. Bado magari ya Serikali yapo arusini, mazikoni, kwenye dayouts na hata kutumika kubeba mizigo ya watu binafsi. Serikali ambayo ni masikini hata ya kuomba vyandarua haipaswi mali zake kutumia ovyo kama hivi. Kama kuna watu wasiopenda amani basi na hawa ndio lakini sina hakika kuwa wao wahame au wabakie.

  Wizara ya elimu nayo pia ina matatizo. Kuna baadhi ya watu wanadaiwa kuuza hata vitabu vilivyotolewa sadaka ili watoto wajifunzie. Rafiki siku moja alinisimulia juu ya kitabu alichonunua duka la vitabu moja katika mtaa wa Kwahani. Kitabu hiki cha hesabu kimeandikwa hakiuuzwi lakini huyu rafiki yangu alikinunua. Wizara ya elimu pia haijaonekana kuwa makini kusimamia elimu ipasavyo. Tunaona wanajenga skuli tuu. Hii ni sawa lakini mambo ya msingi hayashughulikiwa. Sasa kuna mass failure na siku za mbele Zanzibar itakuwa na vibarua wengi zaidi na watu wasio na kazi na hii itakuwa mbaya zaidi kuliko kelele za kupinga Muungano. Sisemi na hawa wahame kwa kuwa sijui watakwenda wapi kwa kuwa bara baragumu la watu kujisafisha limeshapigwa.

  Ndugu zangu katka wakati wa sasa ni lazima tungalie lipi hasa linataathira za muda mrefu kwa kizazi chetu ambacho naona tukishindwa kukishughlikia basi sisi wazazi ndio siku moja watatuka tuhame wakidai tulichangia kuivuriga amani.

 12. Ndugu akilimalimende umenena. Haya ndio maoni mtu hufurahi kuyasoma sio matusi.
  Serikali kila siku inawaomba taasisi za dini kuwahamasisha wanachi kwa mambo mbalimbali, kamamvile uzazi wa mpango, malaria, sensa, maadili nk. lakini napata kigugumizi kwa nini hili la katiba imekuwanongwa kwa taasisi hizihizi kuzungumzia. Au hawa wamemshika pabaya mtawala?
  Lakini pia sijasikia hata sisimizi kulalamika kuwa mihadhara hii inaashiria shari na uvunjifu wa amani ila kupokelewa kwake na wazanzibari kumewashtua atawala na hasa wale wasiokuwa na majimbo ya kisiasa Zanzibar. Kwao hutegemea kuteuliwa au asili yao ni bara moja kwa moja.

  Mtukwao amejikubalisha kuwa yeye si mzanzibari na hivyo anatetea kwa hali yote maslahi ya kwao Tanganyika. Hongera mtu kwao.
  Ananikumbusha Alhaj Aboud Jumbe alipojenga nyumba yake kule mji mwema Kigamboni aliweka kibango na kusema MTUKWAO. Zanzibar kuja kuchuma tu (maneneno haya ya nyongeza ni yangu)

 13. AKILIMALI MANENO YAKO MAZITO SANA NA YANA MANTIKI. NI KWELI KUA ASILIMIA KUBWA YA VIONGOZI ZANZIBAR WABADHIRIFU LAKINI KWA HILI WAKULAUMIWA NI SHENI NA SIO MWENGINE. WATU WANAJIIBIA TU MALI ZA UMMA WANANCHI TUKISEMA INAKUA NONGWA OH ZA BABA ZENU HIZI? ZETU TUTAFANYA TUNAVYOTAKA. SASA KWELI WANAFANYA WANAVYOTAKA KWANI SHENI MWENYEWE AMESHATOA RUHUSA. NA NDIO MAANA SASA NI MWAKA WA PILI HATUJASIKIA HATA MTU MMOJA KUCHUKULIWA HATUA NA DUNIA NZIMA HATA WATOTO INAWAJUA WIZI WA MALI ZA UMMA ZANZIBAR. HAPA NI MOJA KATIKA MATATU. DR SHENI ANAWAOGOPA KUWACHUKULIA HATUA AU NA YEYE ANAKATIWA KIDOGO KILA KINACHOIBIWA AU HANA UWEZO WA KAZI TULIYOMPA YA URAISI.KUNA WATU WAMEJIUZIA VIWANJA VYA SERIKALI, MAGARI, MAJUMBA NA MENGINEYO TELE NINI AMEKIFANYA? HAKUNA KAMA NI NCHI YA KIDEMOKRASIA ALITAKIWA AWAJIBIKE LAKINI KWA KUA AMEEKWA KWA NGUVU NA TANGANYIKA HAWAJIBIKI LINALOMUWAJIBISHA NI HILI LA MUUNGANO TU NDO MAANA AKATAKA WASIOTAKA MUUNGANO WAHAME.

 14. Kwa mm fikra yangu hawa uamsho hawajakosea hata kdg kwani wanafuata maamrisho ya dini yetu pale ALLAH aliposema “kumbusha hakika ya ukumbusho unawafaa waloamini.”na hapa hakukutajwa rika wala nn.sote ni wajibu kukumbushwa.kwa hiyo uamsho wanafanya hvy na ni haki yao kufanya hvy kidin na kikatiba.kuwa na akili au kutokuwa na akili hakuzuii kukufanya ww usikumbushwe.ss ww ni shaur yako kukubali au kukataa unalokumbushwa.suala la waznz kudai haki yao ni suala la msingi na ni haki yao.wala hakuna ubaya.ila sishangai ktk haki wakatokeza watu wanaokwenda kinyume na haki yao.kwan hata wkt wa Mitume wanatangaza dini walikuwepo watu km hao.ila wa2 walishika kamba ya ALLAH na sisi tunasema tunashika kamba ya ALLAH na wala hatutorudi nyuma kwani tupo kwa ajili ya ALLAH.na km unahisi tunakosea niko tayar kuweka na ww mjadala wa kufahamishana na sio kutukanana.ww utoe hoja zako na mm nitoe hoja zangu.na kmutashinda bac ktk ukumbi huuu huu nitakuwa wa mwanzo kusema na kuulinda muungano.huu ujumbe ni kwa wale wote wanaopinga suala la uamsho kudai haki na kuwazindua waznz kudai haki yao.funguka akili ndugu yangu.ALLAH Ibariki ZANZIBAR na kizazi chake.

 15. nafikiri dr sheni una wasiwasi kupoteza nafasi yako , lakini kwa mtazamo wangu wewe ni mtumishi wa wananchi , waambie watanganyika watuachie hatutaki muungano , utabaki kuwa rais mpaka uchaguzi mwengine utakapofanyika, kwa muda huo utatumia kukusanya maoni ya waznz kuhusu katiba gani wanaitaka na vitu gani vipewe kipa umbele katika utawala, sidhani kwa nchi kama znz inahitaji vyama vingi, tuweke utaratibu mwenigne , nchi ya watu wasiozidi milioni mbili ya nini vyama vingi? halafu kila mara wanataka ruzuku za kampeni na uchaguzi , tuondoe hilo, kodi za walalahoi zitumike kwenye mashule na hospitali ,

 16. AUPATE WAPI UBAVU WA KUMWAMBIA WALIEMUEKA PAHALA PALE ALIPOPAONA DR SALMIN PATAMU WAKOLONI WA TANGANYIKA. KAFANYWA WAZIRI ASIE NA WIZARA KAKAA KIMYA MBONA MWENZAKE MIAKA KUMI HAKUKUBALI HILO. WATANGANYIKA WAMESHAMJUA KUA NI MTU WA KUFUATA AMRI TU HAWEZI HATA KUJITUTUMUA. DR SALMIN ALIWEZA JAPOKUA ALIZIDIWA NGUVU, AMANI ALIWEZA LAKINI HAPA NAONA HAKUNA SHAURI. HIVI DR SHEIN UNAWATUMIKIA NANI HASA WEWE? WATANGANYIKA WALIOKUPACHIKA HICHO CHEO AU SISI WAZANZIBARI? KAMA UNATUTUMIKIA SISI WAZANZIBARI TUNAKUTUMA UWAAMBIE WATANGANYIKA KUA HATUTAKI MUUNGANO. WEWE KAZI YAKO NI KUSEMA TU YANAYOFUATIA TUACHIE SISI WAZANZIBARI TUTAYASHUGHULIKIA.

 17. @ suleiman.

  Jana nikuahidi kuwa leo nitakujibu ili tujadiliane vizuri ndungu yangu, lakini nimepata mtihani mkubwa.
  Shemeji yangu kapata ajali ya kugongwa na vespa hivyo sorry sitaweza. Naomba Dua zenu.

  MUUNGANO HATUUTAKI

  “When peace fails apply force”

 18. Hi this is kinda of off topic but I was wondering
  if blogs use WYSIWYG editors or if you have to manually code with
  HTML. I’m starting a blog soon but have no coding experience so I wanted to get advice from someone with experience. Any help would be enormously appreciated!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s