Uamsho wabadilisha katika yake

Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) ikiwa katika kikao chake cha kupitia na kubadilisha katiba yake, mkutano huo umefanyika katika ukumbi la Jamat Khan Mjini Unguja

Advertisements

10 responses to “Uamsho wabadilisha katika yake

 1. Tatizo ni kuwa Viongozi wa UAMSHO wana elimu ya akhera pekee. Elimu ya dunia wengi imewapiga chenga. Kwa Mfano msemaji mkuu Shk Msellem alipata disco mwaka wa kwanza Karume Technical College. Akaja kuokotwa na kuajiriwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kama comminication Assitant baada yakupata mafunzo ya awali huko Kigoma. Mpaka leo hajapata au hana uwezo wa kujiendeleza, Unategemea nini?

  Hatiba gani itanungwa na mbumbumbu? Itakuwa sawa na ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar

  Badala ya Kuamxha watu sasa wamelala wao. Hawana visionna sio wabunifu na ndio maana wakawa wanatumiwa na wana siasa bila wao kujijua.

  • Kaka wewe ndie ambae bujaelimika coz, mwenye elimu wa kujadili watu, kama huna cha kuongea bora kaa kimya.

   • kijana roho yako chafu kama hilo jina lako ulilojita hapo mkombe ………………

 2. Tafadhalini someni Msimamo wa jumuiya ya Zanzinet juu ya muundo wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar. Utaelewa kwa nini nilitoa mawazo yangu hapo juu, Msimao ambao ndio tunaoutaka, umejaa hoja madhubuti, kuzisasambua propaganda za wanasiasa waTanganyika na kutetea hoja kisomi. Utapenda kusoma na kujifunza.
  Laiti Jumuiya ya UAMSHO ingelikuwa na uwezo wa alau kuchambua hoja za muungano kama hivi watu wangeelewa wala wasingewapachika vyama.

  Lakini upeo wao kuona mambo na kutoa takwimu zinazoweza kumfanya mtu kubadilisha msimamo hawana. Wao LAANATULLAH LAANATULLAH basi.

  Nendeni Shule kwanza

 3. Assalam aleikum,
  Unajua mtu mzima haambiwi huna adabu kwa kwetu ni matusi, sasa na wewe naona unaaza kuvungia watu heshma habu kama wewe unajiona msomi atazama hayo maneno yako uliyo andika kweli ni yakisomi? kama ni elimu kamaunavyosema huyo munaemsifu kaikomboa Zanzibar kwa kufanya mapinduzi Marehemu Karume anaelimu gani? hebu tizama video zake baada ya mapinduzi si Abdurahman Babu ndie aliyekuwa akimsaidia kuzungumza na waandishi wa habari?

  Sasa kama ni mwenyeelimu tu ndie anaeweza kuongoza na kujibu hoja mbona munamsifu marehemu Karume kwamba kafanya mambo mazuri na yeye alikuwa hana elimu hata hiyo ya ahra?

  Kamaelimu tu ndio msingi wa kuongoza sasa tizama hao unaowasifu wewe watu wa Muungano kama wana elimu tazama walipotufikisha! mdomo ni nyumba ya maneno sasa wewe kama unachukizako na huyo Sheikh Mselam na Uamsho sawa lakini sisi tunawaamini na yote wenayoyasema nikweli hakuna hata kiongozi mmoja wa siasa aliyewehi kusema ukweli kama wanavyousema wao, na hiyo elimu ya dunia unayoithamini wewe kuliko ya ahra yenyewe imatoka kwenye elimu ya ahra.

  Au ni jambo gani unaloliona wewe kama ni jipya ambalo Uislam hauja litaja? inaonyesga mkosefu wa elimu ni wewe laitani kama ungaliusoma Uislam kutoka kwenye Qur-an, Sunna na historiy za maisha ya Maghalifa wa Kiislam usingesema kama kujua elimu ya dini tu ni ukosefu wa elimu.

  Mimi nakunasihi usidharau watu kwanza jitizame mwenyewe halafu rudi kwenye elimu hiyo unayoiita wewe ya ahra uisome uielewe halafu uje useme hayo wanayoyafanya hao unaowaona wewe wanaelimu yamo au hayamo aidha yatakuwa yameruhusiwa au yamekatazwa kwauwa ni dhulma wanayo tufanyia.

  Zanzibar huru pongezi Uamsho.

 4. Nimefuatilia kadri muda ninavyoupata hawa uamsho,wanachokisema asilimia kubwa ni sahihi,labda tatizo lao ni namna ya ushahidi ikiwa kama ni mifano wanayoitoa inagusa moja kwa moja kundi la watu fulani,mfano wanapotoa historia ya zanzibar kwamba zanzibar haikustahiki kuwepo hapa ilipo leo katika nyanja za maendeleo na kiuchumi hata kijamii,inakua ni sumu kwa kundi hilo kwa kuwa muda wote wamekuwa wakihubiri amani pale ukweli unapowekwa bayana ambapo hutumia nguvu za dola katika kutoa vitisho kwa kuamini ndio njia pekee ya kuzima mageuzi ya wananchi kutokana na mabadiliko ya kiutawala dhidi ya watawaliwa.na kwa kweli hali ni wazi sasa muda wa wananchi kujiamulia umewadia hivyo sasa walio madarakani ndio muda muafaka wa kujitathmini na kuweza kutoa kauli ambazo hazito teteresha amani iliyopo hapa nchini.MUNGU IBARIKI ZANZIBAR HURU MUNGU WABARIKI WAZANZIBARI

 5. Chris, Chris ni ishara ya ujinga kiasi cha kuliogopa jina lake mwenyewe. Karume alikuwa mjinga ndani ya wajinga kama ewe. ndio ikawa rahisi kwake kutawala na akakuuzeni kwa Tanganyika kirahisi na nyie mkaridhia. Kwenu ilikuwa Inshaalah, inshaalla na Katoliki Nyerere akautumia udhaifu wenu akakumalizeni. Ni siasa za msomi Alhaj Jumbe ndio alau akakuteteeni lakini bado Nyerere akatumia wajinga wenzenu kina maalim Seif kumsaidia Nyerere na kumuangusha Jumbe.

  Tukitegemea hekaya za Uamsho Zanzibar kamwe haitakua huru. Ndio maana hata kwenye Kamati y kuratibu maoni hakuna mwakilishi kutoka jumuiya hiyo kwa vile wote ni mbumbumbu.

  Acheni umbumbumbu kwenye karne ya SAYANSI NA TEKNOLOJIA MNACHEKWA na kupingwa hata na taasisi za kiislamu wenye elimu ya dunia na akhera.

  Mtume Muhamad (SAW) aliposema watu waifuate elimu hata China , alikuwa anajua china hakuna elimu ya akhera !!!

  Wacha Upumbafu anka au ni mmoja katika wale?

  • Mimi naona wewe ndio mjinga kwani unaonesha ni kipofu na kiziwi Huyo Mtume S.A.W aliyesema watu waifuate elimu mpaka Chini yeye sindie aliye wafundisha wajinga kama wewe elimu? hiyo hadith ya kutafuta elimu mpaka China wewe umeielewa au unarukia tu kwa utashi wako.

   Uislam haufundishi elimu ya ahera tu hiyo unayoiita wewe ni yadunia kwanye Uislam ipo ndio maana nikakuambia nenda kasome wacha upumbavu wako usione aibu kama hujui usitafsiri mambo kwa manufaa yako kama wewe unaona bila ya Muungano huwezi kuishi basi umechelewa kwani kilichokuwa hakina mwisho ni M/mungu peke yake, huyo huyo muungu wenu nyerere yukowapi munaemsifu kila siku kuwa ni mjanja?

 6. Allah [sa]alimpa utume muhammadi[saw] kwa kujua hanaelimu hata chembe je alikua mjinga allah? kwa kuacha watu wenye elimu zao na utukufu. Tfadhali wewe mshenzi mkombe usidharau maulamaa na wanazuwoni ushike adabu yako tena weka akili yako vizuri laana mmoja we.

 7. Ni sera hainitishi. Kwenu nyinyi ni makumbesa mnafuata msiokijua madhali tu kasema fulani. Haina haja yakutukanana ila jiulize wewe wakati wa vita vya Badr alipowataka mateka wa vita kuwasomesha waislamu na atakaefanikisha basi ataku huru.
  Sasa huyu Nd. yangu Amour sijui ananiunga mkono au vipi? La haniungi mkono asingenitukana. Lakini nadhani yumo kwenye kaumu ya mbumbumbu. Hebu soma viuri makala yaote hapo juu.
  Chris anasema sio mimi ” kama ni elimu kama unavyosema huyo munaemsifu kaikomboa Zanzibar kwa kufanya mapinduzi Marehemu Karume anaelimu gani?” na akaendelea kuponda Karume kwa sababu hakusoma, sasa Amour ananiskama mimi.

  Lakini THUMUN BUQMUN UMYUN………… Nawasamehe

  Kwa mtaji huu, Watanganyika hawatuachii ng’o

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s