Mv. Seagull yazua kizaazaa baharini

ABIRIA waliokuwa katika meli ya Mv. Seagul jana walikuwa katika wakati mgumu baada ya meli hiyo kuzima moto wakati ikitokea Pemba kuelekea Unguja. Hali hiyo iliozusha tafrani na kukumbushia ajali kubwa ya Mv. Spice Islander iliyotokea Septemba mwaka jana na kuuwa zaidi ya watu 200 ilitokea majira ya saa 7:00 mchana eneo la Nungwi.

Juhudi za kuwapata Nahonda wa meli hiyo na viongozi wa shirika la meli la zanzibar hazikuweza kuzaa matunda lakini baadhi ya aribira waliowasiliana na mwananchi walithibitisha hali hiyo kutokea.

Abiria mmoja aliyejitambulisha Nassor Masoud alisema walianza safari yao saa 4:00 asubuhi kutoka badanri ya Mkoani lakini meli ilipokaribia eneo la Nungwi ikaanza kwenda katiak mwendo usio wa kawaida na kupiteza muelekea na kisha kuzima kabisa mashine.

“Kwa kweli tulikuwa katika hali ngumu huku upepo ukivuma na abiria wengi tukiwa na wasiwasi huku wafanyakazi wa meli hiyo wakihangaika kutengeneza meli lakini khofu kubwa ilikuwa kwa akina mama na watoto ambao walikuwa wakipiga kelele” alisema Masoud.

Meneja wa meli hiyo, Said Abdulrahman alipohojiwa alisema kuwa juhudi za kurekebisha tatizo ndani ya njini lilifanikiwa na meli ikawa inaendelea na safari zake.

Awali abiria walisema kuwa katika hekaheka na upepo mkali meli ilipoteza muelekeo na kuelekea upande wa Tanga, kabla ya mafundi kufanikiwa kutengeneza.

Safari ya meli hiyo ilianza baada ya matengenezo yalichukua muda wa zaidi ya masaa mawili majini na kutarajiwa kufika bandari ya zanzibar  ambapo ilitarajiwa ifike saa 10 jioni.

Hadi tunakwenda mitamboni meli hiyo haijafika zanzibar. Na hakuna taarifa zozote kutoka mamlaka zinazohusika kuhusiana na suala hilo licha ya wananchi kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka hizo. wakizungumza na gazeti hili wananchi mbali mbali wamesema bado serikali haijapata funzo kutokana na vifo vilivyotokea katika ajali mbaya iloiyotokea mwaka jana ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.

wamesema ni jambo la kushangaza kwa serikali iliyo makini kushindwa kutafuta usafiri wa uhakika na badala yake kuwaacha wananchi wake wakitumia usafiri usio na uhakika jambo ambalo wananchi wengi wanasafiria boti hizo kutokana na kutokuwa na uwezo wa kupanda ndege.

“Ingekuwa tuna ndege basi tungekuwa tunasafiri kwa ndege maana usafiri wa baharini imeshakuwa ni kifo sasa lakini kwa kuwa sisi ni masikini hatuna budi kucheza bahati nasimu na maisha yetu kwa sababu ndio usafiri wa watu wanyonge tutafanya nini? alihoji Haji Hamadi Mkaazi wa Mwembetanga Unguja.

Hii ni mara ya nne katiak kipindi cha wiki moja kutokea misukosuko kama hiyo inayohusu meli hiyo hiyo ya Seagul na Sea Express ambapo wananchi wamekuwa na khofu ya usafiri wa Unguja na Pemba kutokana na meli nyingi zinzofanya safari za visiwa hivyo kutokuwa na uhakika wa usalama majini.

Advertisements

14 responses to “Mv. Seagull yazua kizaazaa baharini

 1. Hao viongozi hawajali watu. Shughulikieni mambo kama haya mameli mabovu, wanyonge wanashida, roho zinapotea. Munaacha mambo muhimu kuyashughulikia mwashughulikia UAMSHO kwa kudai haki ya Wazanzibar. Sisi hatuutaki muungano. Enyi viongozi shughulikieni wananchi wenu. Musilinde mahitaji yenu tu. Musitake muungano tu sisi hatuutaki. Hebu kuweni na hisia za ubinadamu wapendeni raia zenu inavyonyesha nyinyi viongozi wa nchi hamujali raia munalojali ni utawala tu. Tumechoka na haya. HATUUTAKI MUUNGANO. Shughulikieni kutafuta vyombo vya usafiri musilazimishe watu kutaka muungano na kukataza mihadhara na makongamano tu.

  • Wakati kama huu si wakati wa kuleta lawama. Tuwaombee dua wasafiri na tuombee chombo kiwe salama kwani chengine hatunacho…

 2. asslaamu aleikum: Bi. Salma, asante kwa kutupa “up to date Info”. wengine tulikuwa tafrani lakini ulitupa moyo sana kwa kutupa habari za upesi upesi. Alhamdulillah. Si haba kuwa abiria wote wako salama.

 3. Viongozi hata wazanzibar wakifa wote kwao ni poa tu ilimradi wao wanatawala hawawezi kuja wao kaziyao ni muungano na muungano na wao lakini M/mungu nao atawangamiza

 4. tatizo hapazungumziwi kuhusu mungano, pangekuwa na panazungumziwa mungano, hasidi seif ali id na mohamed aboud na kina tindwa na dadi wangekwenda, lakini kwa meli wanaona bora wazame kwa roho zao mbaya

 5. ILIVYOKUA SHENI, SEFU IDI , MOHD ABOUD NA FAMILIA ZAO WANAPANDA NDEGE HILI HALITOSHUGHULIKIWA HATA SIKU MOJA. PIA INAONYESHA KUA KILA WAPEMBA WAKIFA KWA VIKOCHA (KWA WINGI) NI FAIDA KUBWA KWAO KWANI KURA ZA UPINZAANI ZINAPUNGUA. HAKIKA WALIPOKUFA WATU ZAIDI YA ELFU MBILI ILIKUA NDANI YA MIOYO YAO NI FURAHA KUBWA. PIA ZAIDI YA ASILIMIA 98 YA WAPEMBA WANAPINGA NA HAWAUTAKI MUUNGANO HIVYO WAKIFA KWA WINGI ITAKUA POA TU. NA HILI LIKITOKEZEA WATU WATAACHA KUZUNGUMZIA KUUPINGA MUUNGANO NA SHUGHULI ZA UAMSHO AMBAZO ZINAUTISHIA MUUNGANO NA VIBARAKA WAKE AMBAO KWA SASA WAZANZIBARI WOTE BILA YA KUWATAJA WANAWAJUA NA BADALA YAKE ITAKUA WANAZUNGUMZIA MSIBA TU. IKIWA HALI KAMA HII WAMESHINDWA KUTOA HATA BOTI MOJA YA KMKM KWENDA ANGALAU KUSIKILIZA KULIKONI. WANAPOTAKA KARAFUU ZETU BOTI ZOTE HUPELEKWA PEMBA KUZUIA MAGENDO SASA KARAFUU BASI BOTI HAZINA MAFUTA. KWELI BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA. NA MISHA YA MLALAHOI ZANZIBAR HAYANA MAANA YOYOTE ILE KWA VIONGOZI.

 6. Jamani mimi bado nalia na Serikali yote kwa ujumla wake jambo kama hili ni jamabo la hatari na ni jamabo la kutia khofu kwa wananchi mnao waongoiza ivi kweli hajuwi kwamba Wanachi wa Zanzibar walio na kipato cha chini wanabahatisha roho zao jamani mara ile tumepoteza nguvu kazi kubwa ya Taifa letu na sasa tunajiandaa kupoteza tena uhai wa wananchi wetu tena walio wengi naiomba Serikati ya Mapinduzi ya Zanzibar kuliangalia suala la kuwapatia usafiri wa uhakika wanachi wa visiwa hivi kani dhiki na idhilali waipatayo sasa imekuwa kama watoto wasio kwao .Tuhurumieni kwa kututafutia meli kubwa na yenye uwezo wa kusafirisha watu bila tabu ivi kweli karafuu ya mwaka huu haiwezi kununua meli ? Hebu oneni huruma na hawa waopoteza maisha au kukosewa kupoteza maisha ndio wapiga kura wenu shaurianeni vyo vyote iwavyo mpate meli kwani Wazanzibari sasa wamechoka.

 7. ZANZIBAR NDIO NCHI PEKEE DUNIANI AMBAYO VIONGOZI WAKE HUFANYA YALE WAYAKAYO WAO BILA YA KUJALI MATAKWA YA WALE WALIOWAPIGIA KURA. SISI TULIOWACHAGUA NDIO MNAPASWA KUTUSIKILIZA NA SIO VYAMA AU WATU WA DODOMA. TUNAWAMBIA HATUTAKI MUUNGANO HUU BATILI ITISHENI KURA YA MAONI MNAJIFANYA VIZIWI. INAKUAJE MNAJITIA KIMBELEMBELE NA KUUKUMBATIA. TUNAWAMBIA VIONGOZI WETU KAMA MNATUTUMIKIA SISI WAPIGA KURA/WANANCHI MUWAMBIE HAO MNAOWAITA VIONGOZI WENU NYINYI ” HATUTAKI MUUNGANO” LA MNATUMIKIA MATUMBO YENU, VYAMA VYENU.

 8. Tanganyika wakinunua meli mpya na SMZ wanatanunua tu! Kwa sasa ruhusa hawajapata bado kutoka Tanganyika, mfano Kikwete juzi juzi aliwapangua viongozi wa serikali za mitaa, basi Waziri Ally Shein na yeye akaamka na akaruka na kusema “na mimi nitapanguwa kumbe nzuri hii” hii ndio hali kazi kuiga tu kutoka mjini Tanganyika na kuahamishia kijiji ZNZ hizi ni akili za kitumwa. Lakini haya! yanamwisho na wala hauko mbali hata kidogo Inshaa Allah {s.w}

  SORAGA Mbona hujapiga maruku usafiri wa meli hizi mbofu au ndio tufe upande kutusomea khitma ya kitaifa mshitue na shoga yako Tindwa.

  Sisi ndio maana tunasema.

  MUUNGANO HATUUTAKI

  ZANZIBAR KWANZA.

  Nawasilisha

  SERELLY.

 9. Nawashukuru wenzangu kwa kuwakumbusha viongozi wetu.Naomba mujue hao ni sawa na kuku kwa kusahau yote yatendekayo wameshayasahau kwa sababu hakuna hata mmoja katika familia yao wanaopanda meli hizo mbovu.Isitoshe wanafanya hivyo kusudi ili wapate pesa za maafa wanunulie majumba ya ghorofa na magari ya kifahari.Kwa kweli sisi ni sawa na watoto yatima hatuna baba wala mama tujihangaikie kivyetu ili tuweze kuishi.Cha msingi tutumia nguvu zetu zote ili wajue kuwa na sisi ni binaadamu kama wao.

 10. Viongozi acheni ulafi binafsi zingatieni mahitaji ya wananchi. Nyinyi kazi yenu kuwambia wa2 wasingumze muungano haramu huku mahitaji muhimu ya wananchi wanyonge mnayadharau. Hivi nyinyi binaadamu kweli na hata kama kweli nyinyi ni binaadam bac inawezekana ni wale wajuu wa MAKAFIKI waliompiga vita Mtume (s.a.w)

 11. Yote yanayosemwa kuhusu meli za kwenda Pemba Serikali ni yakulaumiwa lakini matajiri nao nao wanastahili laama. Ndugu zangu katika dunia ya leo biashara haiendeshwi na mtu moja. Biashara inaendeshwa na makundi ya Kampuni yaliyokusanya mitaji yao na kushirikiana kufanya biashara hiyo. Mtu hamiliki meli ndugu zangu. Hata hawa kina AZAM bado boti zao zina matatizo hayaonekani tuu kwa kuwa haiendi Pemba. Ni kwani wenye vipato hawaamui kushirikiana na kisha kutaka serikali iwe na Share ikipenda kwenye biashara hiyo! Mimi sioni kama kuna haja kwa Serikali hii pekee kujiingiza kwenye biashara ya Usafiri, yatatokea kama yaliyotokea kwa meli zake hapo nyuma kwa bado haijawa wazi kufanya mambo yake. Wafanya biashara azeni na mtafanikiwa na mitaji yenu itakuwa na mtawekeza kwenye maeneo mengine. Makampuni makubwa mnayoyaona yalianza hivi hivi na kisha yakajitanua kweli kweli. Kudai Serikali inunue Meli hakutatatua tatizo kwa kuwa Serikali hii ina condone corruption na hivyo uwekezaji wake hautafanikiwa. Watu waliokufa na MV Spice tutawathamini zaidi tukiepusha vifo vyengine labda iwe akina ————– wanataka kufanya vifo mtaji wao!

 12. Poleni sana kwa wale wote mlopatwa na ajali kwa ujumla,Suala la Muungano halihusiani kabisa na ajali hiyo isipokuwa serikali yenyewe,vyombo husika na usimamizi wake kushindwa kudhibiti usalama wa meli hizo ndivyo vinavyopaswa kulaumiwa.Ajali inaweza kutokea popote pale sio Zanzibar peke yake nawaombeni mlielewe.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s