Hizbu Ut Tahrir walaani udhamini wa pombe Zanzibar

Pia, udhamini huu umeleta idhilali na fedheha kubwa itakayowagaeuza vijana wa umma mtukufu wa kiislamu kuwa vibarua kwa gharama duni (thamanu bakhiys) kuitangaza kampuni ya ulevi ili izidi kuendeleza maovu mengi katika jamii ya Kiislamu na wanaadamu kwa jumla. Yametendeka haya ilhali unajuulikana wazi uharamu wa ulevi Kiislamu, ikiwemo kuutengeza, kuuza, kuusafirisha, kuutangaza nk. Na zaidi ya yote Uislamu umeweka bayana kwamba ulevi ndio mama wa maovu yote, na ni kazi ya Shetani. Adui mkubwa anayeshika bendera ya kupotosha Waislamu na wanadamu kwa ujumla.

Kumb: 1433/02 15 Jumadul Than, 1433 06 /05/2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

TUNALAANI UDHAMINI WA KAMPUNI YA ULEVI
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki imeipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya karibuni ya kupatiwa udhamini Kampuni ya Ulevi Tanzania (TBL) kuidhamini Ligi kuu ya mpira wa miguu Zanzibar. Udhamini utakaochukua muda wa miaka mitatu kwa thamani duni ya Shillingi Milioni 140.
Aidha, Hizb inalaani vikali udhamini huo uliofanywa kijanja kwa kisingizio cha kinywaji cha Grand Malt. Udhamini huu ni dalili ya kutojali kwa Serikali na wizara husika msimamo wa raia kupinga udhamini wa kampuni za ulevi. Jambo ambalo ni kinyume na Uislamu, imani ya walio wengi katika raia.
Pia, udhamini huu umeleta idhilali na fedheha kubwa itakayowagaeuza vijana wa umma mtukufu wa kiislamu kuwa vibarua kwa gharama duni (thamanu bakhiys) kuitangaza kampuni ya ulevi ili izidi kuendeleza maovu mengi katika jamii ya Kiislamu na wanaadamu kwa jumla. Yametendeka haya ilhali unajuulikana wazi uharamu wa ulevi Kiislamu, ikiwemo kuutengeza, kuuza, kuusafirisha, kuutangaza nk. Na zaidi ya yote Uislamu umeweka bayana kwamba ulevi ndio mama wa maovu yote, na ni kazi ya Shetani. Adui mkubwa anayeshika bendera ya kupotosha Waislamu na wanadamu kwa ujumla.
إِنَّمَا يُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَنْ يُوقِعَ بَيْنَكُمْ الْعَدَاوَةَ وَالْبَغْضَاءَ فِي الْخَمْرِ وَالْمَيْسِرِ وَيَصُدَّكُمْ عَنْ ذِكْرِ اللَّهِ وَعَنْ الصَّلاَةِ فَهَلْ أَنْتُمْ مُنتَهُونَ
“Hakika shetani anataka kukutilieni uadui na bughdha baina yenu kwa ulevi na kamari, na anataka kukuzuilieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kukuzuilieni kuswali. Basi je mtaacha ?”

Masoud Msellem

Naibu Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut-Tahrir Afrika Mashariki

Advertisements

12 responses to “Hizbu Ut Tahrir walaani udhamini wa pombe Zanzibar

 1. Hii ni kweli lakini ni uroho wa viongozi walafi wasiotosheka na kujaza matumbo yao, hao viongozi wa Zanzibar kwa tamaa zao na kulinda kwao bwana wao Tanganyika hiyo ndio ile faida jinamizi Muungano kama wanavyo twambia kina Seif Iddi na wenzake Muhamed Abudu masharubu.

  Kuwa muungano umeleta faida kubwa basi ndio hiyo ya kukaribisha vilabu vya pombe, haukuna litakalowatosha hao walafi katika ulimwengu huu ila dongo la kaburini Eee Mola wanangamize madui hawa na uwatayarishie adhabu kali iumizao huku wanako kwenda.

 2. “HAWATOACHA MAYAHUDI NA MANASARA MPAKA MFUATE MILA ZAO” hizo ndo njama za makafiri kua siku zote watumie kila khila na njama watopoteze ili tufanane na wao. swala TBL la kutaka kudhamini ligi ya mpira wa miguu ZNZ lilikuja zamani ila walikwama ndio wakattumia ulaghai kudai eti wamekuja na kinywaji kisichona pombe na kwa bahati wakawakuta viongozi waliorafukwa na njaa ambao wako tayari kuiuza akher yao kwa maisha mafupi ya kidunia. M/MUNGU atuhifadhi na fitna zao.

 3. Hawa viongozi hawaoni mbali wanalojali ni vipi watunishe matumbo yao. Laki nyie viongozi mulioko madarakani mukae mukijuwa kuwa umma wa zanzibar uko mikononi mwenu na iko siku mutaulizwa na Muumba wa vyote. Musileweshwe na madaraka mpaka mukauza utu wa raia zenu. Kwani pombe ni haramu na inaleta uharibifu mkubwa katika aridh ya Allah. Kama hapo haitoshi huu nafikiri ni mpango wa makusudi wakutuharibia vizazi vyetu. Mimi naungana na UAMSHO KWA KAULI MOJA TULAANI NA TUPINGE KWA NGUVU ZETU ZOTE TULIZOJAALIWA NA MWENYEENZI MUNGU NA INSHALLAH TUTASHINDA. WAKATI WA KUBURUZWA UMEKWISHA. HATUUTAKI MUUNGANO UNATUHARIBIA MAADILI ya KIZANZIBARI. VIONGOZI KUWENI NA UFAHAMU

 4. TAMKO la Hizbu U-tahariri ni sawa kabisa. Zanzibar ya kipindi baada ya marehemu Karume imeruhusu ulevi na matunda yake yanaonrkana. Leo ukianika baibui hulikuti, leo ukivua viatu msikitini huvikuti, leo ukitembea pasi na tahadhari utaporwa hata nguo za ndani ni walevi, Baya zaidi ni kuwa kizazi chetu kitakachoturithi kitakuwa kibovu kama nguo ilimwagiwa tindi kali. Suala la hadi Ligi ya Zanzibar kughramiwa na Grand Malt ni kwa sababu ya Viongozi wetu kutaka kila kitu kitumikie siasa, Jengine ni kuwa viongozi wanaongoza michezo hasa mpira hawana Vision wapo wapo tuu. Utatizaji pia upo kwa wanapoenda soka kutoamini kuwa mpira si burudani ni ajira, Watu wengi wendao kuangalia mpira wanataka waone mechi bure. Katika hali hakutakuwa na maendeleo. Hii ya Grand malt is to do only patch work. It will not solve the problem. Wakati huu wa kujadiliana kuhusu uhalali na uharamu Grand Malt ni bora tufikirie kupmba Serikali iweke wazi msimamo wake kuhusu mpira. Matajiri wa Kiunguja pia wana sehemu ya kulaumiwa. Kwa nini wanasubiri timu zifunge goli ndio watoe milioni. Ni kwanini hawajiandai kubalisha soka kwa kuwekeza kwenye vilabu kwa mfumo wa share na badala yake wanawekeza kwenye kuuza chupi na sidiria. Kwa nini hawafungui Shule za kuendeleza vipaji vya watoto kimpira kisha wakauza kwa timu kwa pesa nyingi na hivyo kutaunua wigo wa ajira. MM tuna safari ndefu. Zanzibar inahitaji mambo mengi ndugu zangu! Iko nyanga nyanga!

 5. Wanafiki wakubwa. Malta nimiona ikuzwa chini ya msikiti mtakatifu wa Mecca. Kinywaji hiki kinauzwa na nchi zote za Kiislamu.
  Enyi Hizbu lwatan Raia wa Sultan msituyumbishe. Wanachohitaji wanamichezo wetu ni udhamini. Sasa toeni rai nyengine itakayoweza kufuta kiu ya wanamichezo, sio kulaumu tuuuu.

  Hata huo uislamu umesimama Kutokana na walevi. Huo ni ukeli usiofichika. Masahaba karibu wote waliopigana vita vya Badr kuusimamia UISLAMU walikuwa WALEVI WAKUBWA. Ndio maana hata hiyo Quran kuna aya tatu tofauti zinazozungumzia Ulevi.
  Tumia hekima, lete vitega uchumi, fadhili ndugu zako na katu hutawaona wakitamani kuisikia harufu ya Pombe. Lakini Mahizbu mmekaa huku mkinywa kahawa na zabibu na kula kila raha bila kuwajali hao mnaowasemea, halafu mnakuja na chokochoko zisizo na kichwa wala mkia.

  Hongera Tanzania Brewaries kwa kuikoa michezo Zanzibar

  • Pole sana ndugu yangu Mkombe umechanganyikiwa, hoja hapa ni kampuni ya ulevi ndiyo iliyodhamini na suala sio kinywaji, hata wangedhamini kwa kupitia maji ingekuwa haramu. Sijui uko dunia gani ndugu yangu hizb ut tahrir si hizb -l watan , hebu ulizia uelezewe kuhusu hizb ut tahrir. Yafaa ufahamu kwanza hiyo michezo si wajibu, kwamba usiposhiriki utapata dhambi. Lakini hata watoto wetu wanahitaji wasome jee tunaruhusiwa wazini au wafanye liwati ili wapate fedha za kudhamini masomo yao?
   Uislamu haukusimama kwa kupitia walevi, hi ni kauli ovu sana, na ni ukosefu wa adabu kwa vipenzi wa Allah Taala na Mtume wake SAAW. Kwa kuwa ulevi ulianza kuwa haramu baada ya kuharamishwa, kabla ya kuharamishwa hatuna uhalali wa kuwaita masahaba walevi. Quran imekuja kutaja ulevi kwa lengo la kuuharamisha na sio kuupigia debe kama wewe.
   Kutumia hekma ni huko kusema haki na kukemea batil. Kuwepo vitega uchumi au kutokuwepo si hoja ya kuhalalisha udhamini wa kampuni ya ulevi.
   Mwisho nakupa nasaha lete tena shahada baada ya kuropokwa maneno mabaya
   somaa dini yako !!!

   • hawa akina mkombe wapo wengi wao hudhani kuwa na mdomo ndio ruhusa ya kusema kila jambo namkumbusha yeye na wenzake maneno ya Bwana wetu MUHAMMAD (SAW)
    1.”NIMEWAJILIENI NA HKUMU YA KUWACHINJA (waropokwaji na watukanifu wa uislamu)
    2. Yoyote anaemuamini ALLAH(SW) na aseme maneno ya kheri au anyamaze.

 6. @MLAANIFU MKOMBE
  INNA LILAHIHI WA INNA ILAIHI RAJUUN Nakuapia mbele ya ALLAH (Mkombe) kama ungeliyasema maneno haya mbele yangu basi kicha chako halali yangu niko tayari kufungwa jela kwa kukuwa mlaanifu wewe huwezi kuutukana uislam dini ya Allah (sw)na waislam wote kwa jumla tafadhali waombe radhi waisla kabla hatujakushtaki kwa M.mungu mtukufu mwingi wa darja.

 7. Aya ya kwanza ya Quran iliwatetea walevi. Aya ya pili iliwatetea walevi kinamna kwa kuwambia kuwa Makruh na wsisogelee
  sala wakiwa wamelewa na ya tatu ndio ilioharamishwa. Ukweli unabaki masahaba waliopigana vita vya Badr walikuwa walevi na naendelea na msimamo huo kwa sababu ndio ukweli.
  Bado hujajibu hoja, sawa kama hiyo kampuni haifai toeni rai ya kuwasaidia ndugu zenu. Sio kulalama tu. Michezo ni muhimu kwa faida ya afya yabinaadamu na hata hizo nchi zinzoitwa za kiislamu Kamavile Iran Na Saudia zina timu za mipira mpaka za wanawake..Mimi nitakuwa na heshima kuwa nikisimamia ukweli na si unfiki. Kul Haq walau kana mura.

  Nasaha ya kusema maneno matamu ya kukufaurahisha na kuufidikiza ukweli hilo jambo katu haliwezekani.
  Lakini hata hivyo umeshindwa kuuelezea maana ya Hizb au hizibu na mtazamo kwa wazanzibari

  Hongera Tanzania Breweries kwa kuikoa michezo Zanzibar. Kelele za mlango hazimkeri wala kumzuia mwenye nyumba kulala. Sisi wa zanzibari wa ndani tuliobaki kuililia Zanzibar yetu ndio tuonao uchungu wa kushuka hadhi kwa takriban kila kitu.

  Endelea kunya kahawa na kokwa za ende na ungoje lile linoleta heri

  • Mkombe unazungumzia Uislamu lakini huuelewi! Tazama unavyojikanganya katika maelezo yako umesema, lakini huelewi unachokisema, kwamba aya ya tatu ndio ikaharamisha ulevi. Kwa hivyo, mara baada ya kushuka aya hiyo ya kuharamisha, ulevi ndio ukaanza kuwa haramu. Na kwa hivyo, hakuna uhalali wa kusema kwamba waliokuwa wakilewa kabla ya aya ya kuharamisha walikuwa katika dhambi. Na kuanzia hapo ulevi ukawa haramu rasmi kwa kauli ya Allah Taala
   Kwa kuwa mwenye kusema ipi dhambi ni Allah Ta’ala. Sasa labda utueleze baada ya kuharamishwa ulevi kwa hiyo aya ya tatu. jee waliendelea masahaba kulewa?
   Unataka nitoe hoja ilhali umeshakubali kwamba udhamini wa kampuni ya ulevi ni haramu. Unachotaka wewe ni rai, vipi utapatikana udhamini halali.Jibu lake rahisi, dalili ya umma wowote kuanguka kifikra ni kushindwa kuelewa jambo (issue) na jambo nyeti (vital issue).Mpira kama nilivyoeleza si wajibu na tutakuwa daraja ya chini kifikra kama tukajihusisha na mambo yasiyokuwa ya wajibu na tukawacha wajibu. Michezo ni muhimu lakini si wajibu na kufanya michezo iboreshe afya yako hakuna ulazima wa kudhaminiwa na kampuni ya ulevi. Mkombe kusema kauli ya haki si kulalama kama unavyodai. Kwa kuwa kuamrisha mema na kukataza mabaya ni wajibu tuliopewa na dini yetu. Mkombe hakuna ukweli uliofunikwa ni kipi hapa kimefunikwa?
   Kumbe Mkombe, ulivamia kutoa maoni yako ilhali hujui hata hizb ut tahrir ni kitu gani? kwa ufupi hizb ut-Tahrir ni kundi la kulingania Uislamu kiulimwengu na kamwe si hizb ul watan. Hebu zuru mitandao : http://www.hizbut tahrir.org/ hizb ut tahrir .info/ khilafah.com
   Kumbuka Mkombe mada yetu ilikuwa ni kuhusu uharamu wa udhamini wa kampuni ya ulevi na hatujazungumzia suala la uzanzibari. Udhamini huo ni haramu ama ikiwa zanzibar au pengine popote.

 8. Ndugu yangu Amour wacha unafiki. Hata nikiwa nayasema haya mbele yako usingefanya chochote na huu ndio UNAFIKI. Na wewe ni mnafiki, laiti ungekuwa mkweli na mtetezi wa dini yako leo kusingekuwepo uyoga wa makanisa Zanzibar licha ya Pombe unayojifanya kwako kuwa haramu zaidi. Kumbuka kwenye Quran. mwenye enzi mungu alipotuambia nimekuleteeni…….na mitende kwa mtengenezo ya mvinyo> Unalijua hiloooo

  Ungekuwa Muilamu kweli wa kustahiki kuombwa radhi kwa ukweli niliousema, basi itakuwa mja ya dalili ya siku a mwisho

  • @ Mkombe

   Nakuomba ufatilie vizuri maeleza haya kijana wewe:

   {ومن ثمرات النخيل والأعناب تتخذون منه سكرا و رزقا حسنا إن في ذالك لأية لقوم يعقلون}

   Suratul-Nahl {16:}

   (Na kutokana na matunda ya mitende {Tende} na mizabibu {Zabibu} ) mnatengeneza mvinyo {pombe} na mnapata riziki bora. Hakika katika haya kuna dalili kwa wenye kutumia akili)

   Katika aya hii bila shaka ndipo ulimpo mzulia Muumba mbingu na wazazi wako.

   Umejaribu kuudanganya ukumbi huu kwa kuuonesha kuwa Allh {s.w} eti anausifu ulevi unaotokana na mimea hii kuwa ni bora yaani mzuri na kwa hivyo unafaa bila shaka lengo lako kuu hapa ni kutaka (to justify and prove) kuthibitisha ile hoja yako ya kikafiri kuwa hata maswahaba waliousimamisha Uislamu huu walikuwa ni walevi.

   Kwanza kabisa hapa neno‏:‏
   حسنا
   Ni ‘Adjective’ kivumishi cha sifa kinacho sifu neno rizqan ‎رزقا‎ na hivyo kuonesha radhi ya Allah {s.w} katika matunda haya yanapotumika katika namna inayokubalika vile vile ubora wake kiafya na kimweli,
   yaani neno riziqan na hasanan ni na’atun wa manu’utun au swifatun wa mauswufun kiufupi ni sifa na chenye kusifiwa.

   Je! Mkombe Maswahaba watukufu walipo muuliza Mtume {s.a.w} kuhusu pombe aliwajibu vipi Allah {s.a.w}?

   Na Je! Jibu hilo liliwazidisha kunywa pombe?

   Kwa kadiri ya ninavynojua Mimi maswahaba wengi walishituka sana sana wakiwemo baadhi yao wakaacha kuanzia hapo, mfano mzuri ni Saidna Omar.

   Je! Hawa na wewe nani alielewa vizuri aya hiyo?

   Je! Waliwahi kusema kuwa pombe ni nzuri au bora kama ulivyoisingizia aya hiyo hapo juu?

   Kama ni wewe tu peke yako, umeipata wapi hii tafsiri?

   Au wewe ni mlevi?

   Au Sheikh wako alikuwa mlevi?
   Haya ni maswali sikwambii bali nakuuliza.

   Bahati mbaya kwa upungufu wako wa elimu na wingi wa kusema na kuelimisha usiyoyajua umelinasibisha neno hasanan ‎حسنا‎ yaani ‘nzuri/bora’ na neno sakaran ‎سكرا‎ yaai ‘pombe’ na hatimae ukajikuta unaisifu pombe bila ya kutafuna maneno.

   Je, inawezekana Allah {s.w} kuisifu sakaran ‎سكرا‎ yaani ‘pombe’ hapo kwenye aya?

   Ni muhali hilo kutokea kwa sababu Qur-an iko “out of any kind of contradiction in its message and language as well” yaani mgongano wa ujumbe {mafundisho} na hata kilunga kinyume na ilivyo Bible yenu au wewe siye?, kama wewe siye tunaomba ututhibitishie ili tuondoe shaka.

   Kuna maxim moja kutoka katika “Islamic juriprudence principles” yaani usulul-fiqh kwa kiswahili na ‘Misingi ya sheria ya kiislamu’ inasema hivi:

   *كل مسكر حرام و ما أسكر قليله فقليله حرام*

   Tafsiri:
   “Kila chenye kulevya ni haramu, na chenye kulewesha kikiwa kingi basi uchache wake ni haramu pia”

   Kwa hivyo Allah {s.w} aya zake ndani ya Qur-an hufafanuliwa na Mtume {s.a.w} na haya ndio mafunzo aliyoyatoa Mtume {s.a.w} kama ufafanuzi.

   Je! Ndugu yangu MKOMBE unapingana na Mtume {s.a.w} ?

   Je! Ndugu yangu mkombe ulipoibuka na hoja ya Allah {s.w} kusifu pombe ndani ya Qur-an Tukufu ulikuwa unahalalisha pombee au vipi?

   Najua unaweza ukaibuka na hoja yako ya ki-layman kuwa kinywaji hiki cha TBL hakina kilileweshi {intoxicating materials}, lakini hoja yetu ni SMZ kukubali ufadhili wa Kampuni la pombe TBL ambalo vile vile hupata mapato yake kutoka kwenye pombe zake nyengine.

   Je! Huoni kama Kampuni hili baya tutakuwa tunalitangaza ndani ya Ardhi hii tukufu kupitia migongo yetu?

   Je! Hujui kama mbuyu ulianza kama mchicha?

   Je! Huoni kuwa kuwepo kwa watu wenye akili na mitizamo tenge kama yako hapa ZNZ ni hoja tosha ya kuvunja Muungano kabla hamjawa wengi hapa?

   Maana kwa sasa hapa mjini uko peke yako mwenzio mmoja yuko shamba, au kama uko shamba basi utakuwa uko peke yako, maana itakuwa ndio wewewe tu niliyekukuta shamba (kijiji) moja hivi hapa visiwani.

   Babu tahadhari mdo na Dini ya Allah {s.w}. Haya!. Kaa usome shauri yako. Chokchoko mchokoe pweza Mungu hutamuweza.

   MUUNGANO HATUUTAKI

   JAMHURI YA WATU WAZANZIBAR KWANZA
   Keep it up.

   Nawasilisha jibu kwa @MKOMBE

   SERELLY.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s