Kukusanyika ni haki yetu- Uamsho

Amiri wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Msellem Bin Ally akihutubia waislamu katika moja ya mihadhara inayofanyika hapa Zanzibar

Kwa maana hiyo Jumuiya baada ya kushauriana na wanasheria itachukua hatua zote za kisheria za kumfikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mahakamani kwa uvunjifu huu wa amani na ukiukwaji wa katiba unaofanywa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzibar na wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma. Inaonesha kuwa kuna ajenda ya siri iliyokabidhiwa kikundi hicho cha watu wachache kilichoanza na Mh. Balozi Seif Ali Iddi ikafuatiwa na Mh. Mohammed Aboud (waziri katika ofisi yake) pamoja na kumuamuru Mh. Fadhil Suleiman Soraga na kumburuza katika uvunjifu huu wa amani. Sasa wameanza kujitokeza wakuu wa Mikoa kwa ajenda ya wazi kabisa ya kuvunja katiba ya Zanzibar na kuhatarisha neema ya amani iliyopo nchini.

JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145- FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR

Ref: JMK/OUT/VOL-12/2012
DATE: 09/05/2012

TAARIFA RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMKO LA JUMUIYA YA UWAMSHO NA MIHADHARA
YA KIISLAMU ZANZIBAR TAREHE 09/05/2012.
DHIDI YA:
– MH: DADI FAKI DADI MKUU WA MKOA WA KASKAZINI PEMBA
– MH: TINDWA MKUU WA MKOA WA KUSINI PEMBA
– WAKUU WA JESHI LA POLISI KUSINI PEMBA (OCD NA RPC)
Kufuatia taarifa kupitia vyombo vya habari tarehe 08/05/2012 katika mkutano uliofanyika Jamuhuri Garden Wete wakati Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mheshimiwa Dadi Faki Dadi akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama, alipiga marufuku mihadhara inayosimamiwa na Jumuiya ya uwamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar pamoja na kuzuia kutizama DVD za mihadhara kupitia masheha kufuatia tukio la Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mheshimiwa Tindwa akishirikiana na OCD na RPC wa Mkoa wa Kusini Pemba kuvunja mihadhara.
Ndugu waandishi wa habari tunapenda ifahamike kwamba Jumuiya ilifuata taratibu zote za kisheria na kufuata katiba ya Zanzibar bila ya kukiuka katika kusimamisha mihadhara hiyo.
Pili Jumuiya inasikitishwa sana kuliona jeshi la polisi likiburuzwa na wakuu wa mikoa hiyo wachache na kushiriki katika uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa katiba. Tunashangaa sana wakati katiba ya Zanzibar imeweka wazi na kubainisha haki na uhuru wa kuabudu na kueneza dini kama ibara ya19 inavyoeleza “kila mtu anastahili kuwa na uhuru wa mawazo, wa imani… kazi ya kutangaza dini kufanya ibada na kueneza dini itakuwa huru… shughuli na uwendeshaji wa jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi”. Kwa mujibu wa ibara hiyo mtu yoyote yuko huru katika suala zima la ibada na kueneza dini seuze Jumuiya iliyosajiliwa rasmi na vyombo vya dola nayo pia ina haki zote za kuitisha mihadhara makonagamano n.k anaeingilia kati shughuli za Jumuiya kuzizuiya huwa tayari amevunja katiba.
Kwa maana hiyo Jumuiya baada ya kushauriana na wanasheria itachukua hatua zote za kisheria za kumfikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mahakamani kwa uvunjifu huu wa amani na ukiukwaji wa katiba unaofanywa na kikundi cha watu wachache wasioitakia mema Zanzibar na wanaotumia madaraka yao vibaya kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
Inaonesha kuwa kuna ajenda ya siri iliyokabidhiwa kikundi hicho cha watu wachache kilichoanza na Mh. Balozi Seif Ali Iddi ikafuatiwa na Mh. Mohammed Aboud (waziri katika ofisi yake) pamoja na kumuamuru Mh. Fadhil Suleiman Soraga na kumburuza katika uvunjifu huu wa amani. Sasa wameanza kujitokeza wakuu wa Mikoa kwa ajenda ya wazi kabisa ya kuvunja katiba ya Zanzibar na kuhatarisha neema ya amani iliyopo nchini.
Ndugu waandishi wa habari,
Jumuya inatamka wazi kuwa itaendelea kutumia uhuru wake wa kuabudu na kueneza dini kupitia mihadhara, makongamano n.k. Kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar inavyoeleza pia inawataka Wazanzibar na Waislamu kwa ujumla wasiyumbishwe na watu wachache kwa taarifa zao binafsi wanazozitoa katika vyombo vya habari kwa maslahi yao binafsi na kutafuta umaarufu.
Pia Jumuiya inachukua fursa hii kuwanasihi viongozi hao kuacha kutumia madaraka vibaya na kuwakumbusha ibara ya 12 ya katiba ya Zanzibar “watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote” hivyo watawajibika kwa utumiaji wowote mbaya wa madaraka yao pia tunawakumbusha maneno ya Mh. Shein aliyoyasema katika jimbo la Koani “…endeleeni kuitunza amani ya Zanzibar aliyechoka na amani basi aondoke ahame kabisa atuachie…” TUPUMUE, huu si wakati wa kuwalazimisha watu muungano kuukubali au kuukataa watu wapewe uhuru wa KURA YA MAONI kila mtu aamue kwa uhuru wake.
Kila Mzanzibar afahamu kuwa anahaki kamili ya kuabudu, kueneza dini, uhuru wa maoni, uhuru wa kujumuika, kupata habari na taarifa pia kuzitoa na kuzieneza, hayo yote yanalindwa na katiba ya Zanzibar, KILICHOBAKIA NI WEWE MWANANCHI KUWA IMARA KUTUMIA HAKI YAKO BILA YA KUTETEREKA. Rejea ibara zifuatazo katika katiba ya Zanzibar:-
Ibara ya 18 “…kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake na kutafuta, kupokea na kutoa habari kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi”
Ibara ya 20 “…hakuna mtu atakaezuiwa kufurahia uhuru wake wa kuchanganyika au kujiunga… na kujihusisha atakavyo na watu wengine…”
Shime Wazanzibar tudumishe amani na tuilinde pia tutetee haki yetu tusirudi nyuma kwa hili.
Jumuiya kwa mnasaba huu inachukuwa fursa hii kuwatangazia Waislamu na Wazanzibari kuwa itafanya dua kisiwani Pemba pamoja na sala ya Ijumaa ya pamoja tarehe 11/05/2012 hapo Chakechake Pemba ikifuatiwa na mihadhara katika wilaya zote za Pemba Insha’allah.
Wabillahi tawfiq.

NAKALA:

MH: RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI.
MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA ZANZIBAR.
MAKAMO WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR.
MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.
WAZIRI WA SHERIA KATIBA NA UTAWALA BORA.
WAKUU WA MIKOA ZANZIBAR.
KAMISHNA WA JESHI LA POLISI ZANZIBAR.
IDARA YA MUFTI ZANZIBAR.

17 responses to “Kukusanyika ni haki yetu- Uamsho

  1. HIVI NDIVYO INAVYOTAKIWA LAZIMA WAHUSIKA WOTE WA UVUNJWAJI WA HAKI HIZI ZA MSINGI ZA KIKATIBA WAFIKISHWE MBELE YA VYOMBO VYA SHERI KUJIBU. INAKUAJE KATIA WAITUNGE WAO HALAFU WANAPOONA KTIBA HIYOHIYO INAWABANA WAIGEUKE UAMSHO NA WAZANZIBARI SASA HAKUNA KURUDI NYUMA WALA KUOGOPA TUDAI HAKI ZETU KWA NAMNA YOYOTE ILE NA KWA UWEZO WA MOLA AMBAE SIKU ZOTE YUPO PAMOJA NA HAKI TUTASHINDA. HONGERA WANA UAMSHO UMMA WA WAZANZIBARI UKO PAMOJA NANYI.

  2. UKIONA KATIKA NCHI YOYOTE ILE DUNIANI VIONGOZI NDIO WANAKUA MSTARI WA MBELE KUVUNJA SHERIA NA KATIBA WALIOZITUNGA WENYEWE, UJUE HAPO KUNA TATIZO KUBWA SANA. HAO NI MAMBUMBUMBU NA WAJINGA HAWAELEWI CHOCHOTE JUU YA DEMOKRASIA WALA HAKI ZA BINADAMU. JAMBO LA KUFANYA NI KUHAKIKISHA KUA YOYOTE ANAEJARIBU KUZUIA HARAKATI HIZI ANABURUZWA MAHAKAMANI JAPOKUA WANADAI KUA MAHAKAMA NI ZAO. PIA WAKATI TUNAFANYA HIVYO TUZIDI KUSAMBAZA KANDA ZA MIDAHALO MIJINI NA VIJIJINI KWANI UJUMBE UNAFIKA VYEMA NA PIA TUTUMIE ILE STAILI YA ZAMANI YA REDIO KIFUA NA KWA WALE WENYE UWEZO FACEBOOK ITUMIKE KUENEZA HABARI HIZI. WASWAHILI WANASEMA UKISIKIA MGONJWA ANALALAMIKA UJUE SINDANO IMEMPATA NDIPO HIVYO DAKTARI HATAKIWI KUICHOMOA. KWA HIVYO NA HAWA HILI LIMEWAPATA NDIPO TUSIRUDI NYUMA.

  3. Lazima kielewekeee biidhni LLAH wataelekea kibla wote hao, tumuombe Allah kwa kila mnafiki apukutishe viungo vya mwili dhahir
    SHNASH

  4. nashangaa dokta shein watendaji wake wamekiuka vifungu vya katiba namba 12,18 na 20 sasa je hawa hawajasababisha uvunjifu wa amaniii? na kama ndio hivo jee hawapaswi kuhamishwaa zanzibar?

  5. HAO WAKUU WAMIKOA YA PEMBA WOTE SI RAIA WA ZANZIBAR KWANI RAIA NI YULE MWENYE UCHUNGU WA NCHI YAKE.HIVYO NAWAOMBA WAJIANDAE NA DUA ZA WAJA WALIOWAZULUMU KWA MUDA MREFU.WAZANZIBARI TUZINDUANE.TUSHIKAMANE.TUUNGANE.TUSHAJIHISHANE KUUPINGA MUUNGANO HARAMU NA KWA UMOJA WETU TUMESHINDA.

  6. Hapo sasa ni sawa kwa sababu wanajiona wako juu ya sheria.kwa kumshtaki huyo iwe funzo kwao wao.insha allah tutafanikiwa.

  7. {يريدون ليطفؤا نور الله بأفواههم والله متم نوره ولو كره اكافرون}
    (سورة الصف)

    (Wanataka kuizima nuru ya Allah {s.w} kwa midomo yao, na Allah {s.w} ni mwenye kuitimiza nuru yake hata kama watachukia makafiri

    ‏{الذين قال لهم الناس إن الناس قد جمعوا لكم فخشوهم فزادهم إيمانا وقالوا حسبناالله ونعم الوكيل}‏‎ ‎‏
    (سورة الأنفال)

    (Ambao {yaani Waislamu-Maswahaba} waliambiwa na watu kuwa hakika watu wamejikusanya dhidi yenu {kimapambano} waogopeni, basi likawazidishia Imani {MSIMAMO} na wakasema “Allah {s.w} anatutosha {kumtegemea dhidi ya maadui na vimbi vyao”

    Ndugu zangu Waislamu Wazanzibari Mashujaa Wanyenyekevu kwa Allah {s.w}, kwa Mtume {s.a.w} na kwa viongozi wa Uislamu na Waislamu katika Ardhi hii yenye heshima na historia tohara iliyonajisiwa mwishoni mwishoni na Watanganyika (Wakatoliki-Nyerere), na enyi wanamliotoka katika damu za waislamu na mishipa madhubuti kama vile Sheikh Hassan Bin Ameir, Sheikh Zaggar, Sheikh Habiyb Ally Kombo (Allah {s.w} ampe maisha marefu), Sheikh Ameir Tajo “Mkubwa”, Sheikh Ameir Tajo “Mdogo”, Sheikh Muhsin Al-Barwan, Sheikh Abdallah Qassim Idous, Sheikh Nassor Bachou, Sheikh Abdallah Swaaleh Al-farsy, Sheikh Thaabit Kombo, Sheiki Msellem Bin Ally, Sheikh Azzan, Sheikh Mussa Omar Makungu, Sheikh Farid Hady na wengine wengi Allah {s.w} awarehemu, sasa haya ndio yale hasa aliyotuahidi Allah {s.w} na Mtume {s.aw} na kweli wamesema kweli wawili hawa kuwa madhalimu hawataiachama dhulma iangamie huku wanaiona bali watasimama kuilinda kiasi kwamba itakapoangamia wataangamia nayo sambamba, na hii ni bora kwetu kwa maisha yajayo. Shime simameni pamoja kuitetea historia hii tukufu “kumbukeni mcheza kwao hutunzwa” na “Mtu kwao”. Hawa wanaoidhalilisha jamii yao kwa uchu wa madaraka hawawezi kupewa ushindi na Allah {s.w} bali nyinyi mnaoitetea heshima ya Allah {s.w} na jamii yenu mna haki na ahadi kwake na wala hatakusalitini abadan.

    Wazee wetu waliotangulia walipambana ana kwa ana na ukoloni halisi na wakoloni halisi hawa tuliowakuta sisi ni makombo na mabaki tu ya ukoloni, Je! Hamuoni kama ni aibu kubwa na fedha kuuachafu huu uendelee ambao ni dhaifu ukilinganisha na ukoloni halisi waliopambana nao wazee wetu?. Mfano mzuri ni Wareno ambao waling’olewa na kuchomoka mbio kutoka Zanzibar kwa silaha na pia waingereza ambao waling’olewa kwa democracy.
    Hivyo ikiwa ndio kama njia pekee ya kuwaenzi wazee hawa ni lazima tushikamane pamoja kupambana na waovu hawa mpaka tuuondoshe uovu huu (MUUNGANO).

    Vitisho, hasira, matusi na maamusi ya kijazba kama haya ndio busara pekee ya watu madhalimu pale wanapokabiliwa na nguvu ya hoja, ambapo jazba hizi daima huashiria upeo wao wa mwisho wa kufikiri ambapo wao hoja wanazosimamishiwa huwapa taswira ya mtu aliyendani ya chupa au kijusi alibanwa na mlango au chatu aliemeza gogo kubwa lenye miba. Huu ni moto wakifuu jamani usitutishe Wazanzibari tufurahi kuuona sasa unaanza kupiga kelele na kuwaka kwa nguvu kwa sababu ni ishara kuu ya kumalizika kwake na hatimae si muda mrefu utafika kikomo na jivu lake litakuwa ndio mbolea safi tutakayoanzia kuliimarifa Bustani (ZANZIBAR) hili lenye matunda matamu kama hayo hapo juu (THE MUSLIM SCHOLARS IN THE MIDDLE AND EAST AFRICA) yaliyowahi kung’ara na kuwavutia wananchi wengi duniani ikawa ni sababu ya kuenea kwa ustaarabu “Civilization” katika maeneo mengi kama vile Burundi, Uganda, Rwanda,Comoro, Congo, Malawi, Msumbiji, Kenya n.k. Kutokana na hali hiyo Nyerere akaja na MUUNGANO haraka haraka na kuharibu mambo yote.

    Ndugu zangu Wazanzibari kuna jambo muhimu hapa Allah {s.w} inaonesha anataka kutusomesha, hawa wote wanaosimama na kutetea dhulma hii bila ya kujali tawakuli yetu kwa Allah {s.w} hawatakuwa na mwisho mwema labda watubu haraka sana na waungane na wale wote wanaupigania utetezi kwa vizazi vya Kizanzibari vilivyomo katika idhilali kubwa na ya kutisha (MUUNGANO), laa si hivyo hawa kuangamia kwao hakuko mbali kabisa. Ima wataangamia kutokana na ADHABU itokayo moja kwa moja kwa Allah {s.w} au itakayopitia mikononi mwa {Waislamu} Wazanzibari. Mfano mzuri kuna kiongozi mmoja kule Tanganyika “Augustine Lyatonga Mrema” ambaye aliwanyanyasa sana waislamu wa Tanganyika akiwa waziri wa mambo ya ndani wakamshitakia Allah {s.w}, wakati dua hizi zinaendelea yeye alikuwa akizibeza na kusema “Kila wakiniombea dua wapi! Ndio ninawiri zaidi nipo nadunda tu”. Mara Allah {s.w} akaingia kazini, yule bwana kilichompata ni kikubwa mno mfano ngozi yake hadi leo ni kama ya chatu hutamani kumtizama kwa umakini. Na hawa wetu subirini mtawaona tu kama si leo ni kesho kwa sababu dua ya mwenye kudhulumiwa hairudi hata kama ni kafiri. Warikodini majina yao ili mpate kuwafatilia vizuri na kuzidisha imani zenu kwa Allah {s.w}.

    Masheikh tunajua kuwa mnautembelea ukumbi huu tunaomba mtuongoze dhidi ya hawa walafi na wanafiki waliotumia Qur-an halafi leo wameitupa, mpaka tufikie lengo letu la kuwa huru.

    MUUNGANO HATUUTAKIII!

    “When peace fails apply force”

    JAMHURI YA WATU WA
    ZANZIBAR KWANZA.

    Nawasilisha.
    SERELLY.

  8. MZANZIBAR MWENYE SIFA YA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU EPUKA NA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA WAISLAM MOROGORO – MUM. Chuo hichi kinabagua wazanzibar kwa kuwapa DISCO KWA WINGI mfano mwaka 2012 wanafunzi waliopata DISCO mwaka wa kwanza 198 WAZANZIBAR 150 NA WATANGANYIKA 48. Ulipita msamaha kwa watanganyika 15 ikawa DISCO za watanganyika ni 33. Na wazanzibar 150 ZILE ZILE. Jee ni muungano huu kweli?

  9. Nyinyi UAMSHO ni sawa na Gelileo Galilei alivyopingana na Watawala na Roma kuhusu nadharia yake. Endelleni mwisho ushindi utapatikana. Ingawa si lazima kwa haraka. Ili wachukuwa siku nyingi Muslim Brotherhood kupata unongozi Misri.

  10. WAZANZIBARI MUNAUTAKA AU HAMUUTAKI? NAAMINI HILI HALITAKI TOCHI.HAO WAKUU WA MIKOA NI WASHENZI TU WA TANGANYIKA MBONA ZINAPOKUJA AJIRA ZA JESHI NA POLISHI HUWACHOMEKA WATU WAO TU.WAZANZIBARI TUWENI MACHO .

  11. Maliki on May 10, 2012 at 4:28 pm said:
    MZANZIBAR MWENYE SIFA YA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU EPUKA NA KUJIUNGA NA CHUO KIKUU CHA WAISLAM MOROGORO – MUM. Chuo hichi kinabagua wazanzibar kwa kuwapa DISCO KWA WINGI mfano mwaka 2012 wanafunzi waliopata DISCO mwaka wa kwanza 198 WAZANZIBAR 150 NA WATANGANYIKA 48. Ulipita msamaha kwa watanganyika 15 ikawa DISCO za watanganyika ni 33. Na wazanzibar 150 ZILE ZILE. Jee ni muungano huu kweli?

    Maliki hii ya kusoma viachie vyuo viamue. Wazanzibari wa kizazi chenu si wakweli. Hawasomi ila husubiri mitiihani ivuje. Sisi tulisoma na ilikuwa vyuo vichache na elimu haikuwa biashara na hakukuwa na disco si kwambii leo degree zipatikanapo online. Vyuo vikuu ni biashara na biashara haifukuzi wateja inawavuta.

Leave a reply to Serelly Cancel reply