Kesi ya wapinga Muungano kusikilizwa Juni 6

Kiongozi wa kikundi kinachopigania kuwepo kura ya maoni kuhusu Muungano, Rashid Salum Adiy akiwatuliwa wafuasi wake ambao hawapo pichani, nyuma ni afisa wa jeshi la polisi akimtaka awatulize wafuasi wake kabla ya kukamatwa mwezi uliopita

KESI inayowakabili watu 12 walioshitakiwa kwa kosa la kubeba mabango ya kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ushahidi wake umekamilika na inatarajiwa kusikilizwa Juni 6 mwaka huu. Mwendesha Mashitaka Said Ahmed Mohammed, aliieleza Mahakama ya Mwanakwerekwe mbele ya hakimu Omar Mcha Hamza jana kuwa upelelezi umekamilika wakati kesi hiyo ilipofikishwa kwa kutajwa mahakamani hapo.
Mwendesha Mashitaka huyo kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP), aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kusikilizwa.

Kwa upande wake Hakimu Omar Mcha Hamza alikubaliana na hoja zilizotolewa na kuiahirisha kesi hiyo hadi Juni 6 mwaka huu kwa kusikilizwa.

Hakimu Hamza aliutaka upande wa mashitaka kuwasilisha mashahidi siku ya kesi hiyo katika mahakama siku ya hiyo ya kesi kusikilizwa.

Kabla ya kuahirisha kwa kesi, watuhumiwa wa kesi hiyo, waliiomba mahakama imtaje mlalamikaji wa kesi hiyo ambaye amepelekea kushitakiwa kwa watu 12 katika mahakama hiyo ya Mwanakwerekwe.

Mbali na ombi hilo la watuhumiwa hao wote kwa pamoja wameiomba mahakama hiyo iwapatie hati ya mashitaka, pamoja na kutoa muda mrefu ili waweze kutafuta Wakili wa kuweza kuwasimamia na kuwatetea katika kesi inayowakabili watuhumiwa hao 12 ambao wamshitakiwa pamoja na Kiongozi wao Rashid Salum Adiy.

Akijibu kuhusiana na ombi la upande wa washitakiwa, Mwendesha Mashtaka alisema pamoja na kuwapatia hati hiyo ya mashitaka, washitakiwa hao wanapaswa kufahamu kwamba makosa yote ya jinai yanalalamikiwa na serikali kupitia Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), ambaye ndiye mwenye maamuzi ya kuyafungulia mashitaka mahakamani kwa mujibu wa sheria za Zanzibar.

Jumla ya watuhumiwa wa kesi hiyo ni 12 walishitakiwa kwa pamoja baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi mwezi uliopota akiwemo kiongozi wa kikundi hicho, Rashid Salum Adiy (48) mkaazi wa Kikwajuni, Khamis Hassan Hamadi (51) mkaazi wa Jang’ombe na Hashim Juma Issa (54) mkaazi wa Mbweni

Wengine ni Ali Omar Omar (54) mkaazi wa Bububu,Masoud Faki Masoud (31) mkaazi wa Kilimahewa, Rammy Mbaraka Ahmed (48) mkaazi wa Michenzani na Salum Masoud Juma (38) mkaazi wa Rahaleo.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mussa Omar Kombo (67) mkaazi wa Mpendae, Omar Kombo Is-hak (21) mkaazi wa Magogoni, Haji Sheha Hamadi (49) mkaazi wa Chumbuni, Rashid Ali Rashid (21) mkaazi wa Mombasa, Suleiman Mustafa Suleiman (31) mkaazi wa Mombasa wote hao ni wakaazi wa Zanzibar.

Washitakiwa hao wote kwa pamoja wameshitakiwa kwa makosa ya kufanya mkusanyiko usio halali, kuendelea kukusanyika baada ya kutangazwa kutawanyika na ofisa wa jeshi la polisi na shitaka la uhuni na uzururaji na kubeba mabango yenye kupinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo, Said Ahmed Mohammed, aliwasilisha mashtaka hayo mbele ya mahakama hiyo ambayo ilijaa watu ndani na nje waliofika kusikiliza kesi hiyo.

Mapema mahakamani hapo, Mwanasheria huyo wa serikali aliwasomea watuhumiwa hao shitaka la kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na vifungu vya 55 (1) (2) (3) na 56 vya kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Katika shitaka hilo aliifahamisha mahakama kwa kudai kuwa, Aprili 20 mwaka huu, majira ya saa 2:30 za asubuhi, huko Mbweni wilaya ya Magharibi Unguja, kwa pamoja na bila ya halali walijikusanya katika barabara ya Baraza la Wawakilishi huko Mbweni Zanzibar.

Alidai kuwa, mkusanyiko huo uliwafanya majirani na watu waliokuwa wanakwenda kwenye Baraza kupata khofu, kuwa wangeliweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati hawakuwa na sababu za msingi za kukusanyika nje ya viwanja hivyo.

Mwanasheria hiyo alidai mahakamani hapo kuwa shitaka jengine ni kuendelea kukusanyika baada ya kutangazwa kutawanyika na ofisa wa polisi, ambapo washitakiwa hao walitakiwa kutawanyika kwa amani baada ya tangazo polisi, lakini waliendelea kukusanyika kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa Mwanasheria huyo, kitendo hicho cha kukataa amri hiyo halali ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 60 cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Aidha aliieleza mahakama hiyo kwamba shitaka la mwisho linalowakabili watuhumiwa hao 12 ni la uhuni na uzururaji, ambapo mahakama ilifahamishwa kuwa siku hiyo walipatikana wakiwa wamejikusanya kwenye barabara hiyo ya Baraza la Wawakilishi, wakiwa na mabango yenye maneno yanayopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Ilielezwa mahakamani hapo kwamba kitendo hicho cha kukusanyika na kukamata mabango ni kosa chini ya kifungu cha 182 (d) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, ambacho walidaiwa kukifanya katika wakati na mazingira yanayoonesha kuwa hawakuwa na madhumuni halali.

Watuhumiwa wote 12 wapo nje kwa dhamana ya fedha taslimu shilingi 500,000 kila mmoja, pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi, na mdhamini mmoja kati ya wadhamini hao wawili awe ni mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Advertisements

19 responses to “Kesi ya wapinga Muungano kusikilizwa Juni 6

 1. Huyu mwanasheria wa serikali ni muhuni na mwendawazimu kama Sefu Iddi na Moh’d Abudi na wahuni wengineo.

 2. huu ni wakati wa wanasiasa walio na ukweli na uchungu na nchi kuunganisha nguvu na wananchi , muungano hautakiwi , tusilazimishane , wananchi tuna haki ya kuvunja muungano wala hatuna haja ya kura ya maoni , ni upotevu wa fedha tu wakati jibu linajulikana ya nini kutunga mtihani?

 3. Kama kudai haki yako ni uhuni wale kina masharubu na yule ala pasa za mayatima wa mv Spice ni majambazi waio kuwa na haya kwa unafiki wao.

 4. Hivyo ndugu zangu polisi mnaotayarisha kesi kwa nini mnachelewa kuwafikisha mahakamani waliotajwa kwenye ripoti ya Omar Ali Shehe ambao makosa yao pia ni kijinai na taathira zake ni kubwa kwa maisha ya waliwengi hapa kwetu. Ivo kina Rashid ambao hawa washi hawa zimi wana kesi gani kubwa ya kujibu. Katika kipindi hiki ni bora kufanya vitu ili historia iwakumbuke mkiondoka. Hawa kina Rashid si chochote kuliko wanambeza Rais na kushindwa kutekeleza aliyoyataka yafanyike. Angalieni mjini leo punda wapo kila mahali hali Dr. Shein alisema waondoke, angalieni mjini vyoo vimegeuzwa ofisi na watu wajisaidia kama wanyama. Angalia nchi hii leo kila sekta inafanyakazi chini ya matarajio. Sisi ambao tunaona mbali tufanyeni mambo ya mambi si ya kuwatumikia watu ambayo hayana maslahi na sisi na watakaotufatia!

 5. hawa mahakimu wa unguja wanapeana tu nafasi kama ccm na uongozi wao wahuni tu wote
  Ila Allah atasimama kwa ajili ya Zanzibar na watu wake Inshaallah maaana hawa ccm wanafanya kama huu muungano ni wao peke yao watu wengine hawana ruhusa ya kulalamika juu ya hili vimeo kweli hawa lakini huu ndio mwisho wa ccm na mnaombwa siku ya ijumaa mkaribie maeneo ya magomeni uwanja wa mzalendo muwaone wazanzibar wana kindakindaki wakihubiri juu ya zanzibar yetu

  • Mimi nashangaa sana watu kama hawa wakaazi wa Zanzibar wenye heshima zao kuambiwa wahuni na wazururaji ama hili linakera sana,Nakumbuka ccm walileta watu kutoka bara kuja kupiga kura walikua wakizurura bila kujua watatoka wapi wanakwenda wapi na hawakuambiwa kama wahuni wala wazururaji,Yana mwisho haya.

 6. JAMANI HAWA MUTAENDELEA KUWATESA MPAKA LINI KWANI WAKATI HUU WA UKWELI NA UWAZI KUNA UBAYA GANI MTU KUTOA HISIA ZAKE KAMA JAMABO HILI HALIPENDI ATASEMA WAPI NA HAPA NDIO NCHINI PAKE .NAOMBA MUWAACHIE BURE ILI WAKAKAE NA FAMILIA ZAO NA WAJIPANGE KUJA KUICHANGIA AU KUIKATAA KATIBA MPYA KWA VIGEZO VYAO VITAKAVYO KUWA NA UTULIVU.

 7. Eti “katika wakati na mazingira yanayoonesha kuwa hawakuwa na madhumuni halali…” & “wakati hawakuwa na sababu za msingi za kukusanyika nje ya viwanja hivyo…”.

  Hivi ni kweli Mzanzibari ambaye ameanzia kwenye ngazi ya kufikiri, kuchambua na kutoa maamuzi juu ya nini tufanye sisi wote ili kuyaondoa madhara ya Muungano uliozaliwa na “glandstine movement” (harakati za kisiri siri) za upande mmoja tu {Tanganyika-Kanisa-Nyerere} madhara ambayo ni mengi mno ya kiongozwa na lile la kuiuwa DINI ya Allah (s.w) kwenye ardhi ya waislamu {ya ALLAH (s.w)} ndio kweli hawana sababu za msingi au hawana madhumuni halali ya kukusanyika pahali ambapo inatarajiwa sauti za wanyonge husikilizwa ?

  Au hizi ndio zile Elimu tulizoambiwa ni zenye madhara?

  Je! Mwanasheria wewe kiwete wa kufikiri hujui kama hawa ndugu zetu wamlifuata Mwakilishi wao wa Kikwajuni mara kadhaa na mara zote akawa anawadanganya na kuwakimbia na hivyo kufelisha uwakilishwaji wa maoni yao katika Chombo hicho katika wakati huu muhimu na dharura zaidi katika historia ya nchi ya Zanzibar ?

  Halafu eti unajitia kunukuu vipengele unavyovipenda wewe tu na kuviacha usivyovipenda vinavyoonesha haki ya kila Mzanzibari kushiriki katika uendeshaji wa nchi na katika maamuzi makuu ya nchi kama hili la MUUNGANO ambalo sisi walala hoi ndio waathirika wakuu na badala yake unathibitisha makosa yao kwa kuupinga Muungano ambao hakuna hata raia mmoja wa Zanzibar aliyeshirikishwa au kashawahi kushiriki katika kuutolea ridhaa na wala hakuna hata sheria moja ya Zanzibar inayoonesha “Zanzibari’s retification on the Union” yaani “Ridhaa ya Wazanzibari juu ya Muungano” ridhaa jambo ambalo ni SHARTI la lazima na la kwanza kabisa katika mfumo wa sheria za “Common Law Family” yaani (Yaani sheria za Kiingereza) ambazo ndizo zilizoegemewa katika kuubebea mimba muungano huu na mpaka kuuzaa. Je! Huoni kama kwa hoja hizi hawa ndugu zetu ni “unguilty inocents” (wasiokuwa na hatia hata chembe) wanaofaa moja kwa moja kuachiwa huru na badala yake wale wote walioshiriki katika kuanda kesi hiyo wakafunguliwa mashtaka kwa kuvunja katiba, kupoteza muda wa Mzanzibari huru, kumsingizia raia, kuvunja haki za binaadamu na kumsababishia usumbufu wa kiakili na kisaikolojiwa bila ya sababu raia wa nchi?

  Nakusikitikia sana ndugu yangu mwanasheria wewe ulieumbwa kwa udongo na ukapuliziwa roho ghali usiojua bei yake na ambayo hutapewa mara mbili duniani hapa, kwa kunukuu kwako sheria zilizotungwa na kina Diria, Adam Mwakanjuki n.k na ukaziacha zote zile za Mfadhili wako Mkuu (Allah {sw}) ambazo ni TUKUFU na TOHARA zitokazo mbinguni?

  “When peace fails apply force”
  MUUNGANO HATUUTAKI.

  Nawasilisha
  SERELLY.

 8. Wazanzibari wengi hawautaki huwo muuunganoo bandia, hao watu 12 ni wawakilishaji wa watu walio wengi. HATUUTAKI MUUNGANO. TUNATAKA KURA YA MAONI. MUKASHITAKI. MUKAWAFUNGA. MUKIWAUWA MUKIWANYONGA LAKINI IKO SIKU MUJUWE MUTAULIZWA NA MUTAADHIBIWA KWA DHULMA MUNAYOWAFANYIA UMMA WA WAZANZIBAR. Hatuutaki muungano

  • Yaani mi nashangaa kuona akili za ajabu za hawa tunaowaita eti ni viongozi. Na la kushangaza zaid utakuta anaewaandama hawa wanaoitwa Washtakiwa, jina lake ni Hamza, au Said au Mohammed. Hatumuoni John, Benjamin, Pius wala Julius. Wao wanakaa huko na remote zao wanawaControl hawa tunaowaita et ni viongozi kuwapiga vita ndugu zao, tena basss……ndugu zao wanaowapigania haki na uhuru wao wenyewe.. Wanasahau kua siku hizo za kuhisabika za kumaliza hayo madaraka feki walonayo wataanza nao kua ni wapiga debe vile vile……Halaf wajifanye walikua hawajui. Zindukeni nyi mabupuru… Mtafaham lini nyinyi? Huko Shule mlifaulu vipi hadi kufikia hizo nyadhifa? Au baada kuonekana ni mabupuru ndio mkapewa hizo nafasi ili musukumike kokote kule wanakotaka wao. Hii jamani ni nchi. Msifanye masihara…!! Inabidi muwapongeze hao kina Rashid kwa kuwatetea haki yenu mnayoitaka, na mnayoshindwa kuidai nyinyi, na sio kuwabeza kwa kuwashtaki. Hem kuweni na Ihsan…………Naona cmalizi… Ila mwenye kufaham atafaham, na asiefaham hata ufanye nini……Ni sawa na ckio la kufa…….

 9. hatujitaji kura ya maoni , kwa sababu tunajua kuwa waznz wote hawataki muungano ya nini kutumia mabilioni ya fedha za wananchi kwa kisingizio cha kura, muungano uvunjwe tu bila ya kura ya maoni , tunawaomba wawakilishi wetu waongoze wananchi kwenye uhuru , muda wa kudanganyana umeisha , na kama hawawezi kufanya kazi tunayowatuma , wajiuzulu

 10. Na nyinyi Polisi hebu tuliyeni tusijetukatoa siri zenu nje bure, na nyinyi leo mnajitia kusimamia sheria wakati nyinyi wenyewe zishakushindeni zamani sana?
  Hivi kweli vyeti vya FORM IV muazime kwetu halafu na marungu yenu muelekeze kwetu. Kweli fadhali za Punda mateke. Aaah hiyo itakuwa ngumu wajomba.
  Hivi nani hajui kuwa Traffic Police ndio wala rushwa wakubwa katika nchi hii?
  Nani hajui kuwa wengi wenu mnaendesha vyombo bila ya leseni, roadpass na wala ma-helmet wengi wenu hamyavai?
  Nani hajui kuwa bangi, unga na pombe vinaendelea kuingizwa nchini ama kutengenezwa kwa ushirikiano au ruhusa ya Polisi? Mfano mzuri ni Watanganyika wengi wanaopika gongo maeneo ya Shakani, Machui, Gamba, Miwani, Nyamanzi, Dole, Kiyanga, Kichakapunda na maeneo mengine ambayo Polisi mtatutajia.
  Nani hajui kama askari wengi mnamajina mawili mawili moja la nyumbani na jengine la kazini ? Je! Kwanini mnamajina mawili mawili ? Bila shaka sababu kuu ni vyeti vya kuazima tena vya FORM IV masikini. Kiufupi hamjasoma wakuu wangu, na ushahidi mzuri ni namna mnavyofakazi yaani “MAGUVU THEORY” hufikiri baada ya kutenda na sio kinyume chake. Kazi kupiga watu tuu!
  Kama kazi yenu mmeipata kwa vyeti vya kughushi na kwa hiyo, nafasi mlizokalia hamkustahiki na mmewazuwia wanaostahiki kupata nafasi hizo Je! Mishahara yenu mnayolipwa kwa mujibu wa sifa na sheria za uajiri zilizopangwa vipi halali? Na Swaumu, Zakka, Swala, Hija, Riziki mnazo wapa wake zenu na pia mkala mkapata mbegu za uzazi (Manii) na hatimae mkapata watoto kupitia maslahi yenu kama eti wafanya kazi vipi zinasihi? Haya twende! Akhera kuna mambo langu jicho.
  Kama mambo ndio hayo Je! Ni nani wa kumkamata mwenziwe kati yenu na hawa wazalendo wenye uchungu na nchi na ardhi yao (ya Allah {s.w}) hapa?
  Ama hapa nitanie kidogo. Hivi jamani ukiitiza vizuuri hiyo picha hapo juu ni uso gani ulio na nuru kati ya Brother Rashid na huyu Polisi? Ni nani mwenye “confidence” yaani anaejiamini? Ni nani anayetumia akili yake huru na kutekeleza mawazo yake huru na nani anafuata mawazo ya wengine hata kama yeye hayapendi? Ni nani Bosi na nani ni Mtumwa? Majibu yako hapa bila shaka yata-prove (yatathibitisha) kuwa upolisi kwa serikali hizi (MFUMOKRISTO) si kazi bali ghasi.
  Kiufupi polisi mnamadoa mengi kisheria na hamna haki ya kusimamia sheria maana hamziwezi hususan katika hili la waungwana, wazalendo na wapinga Muungano. Ni wajibu wenu namba moja (no:1) nyinyi polisi kuupinga Muungano haraka sana na sio kukandamiza raia wema wanaofuata sheria katika kujinasua na Muungano hewa na haramu kikatiba. Vinginevyo mtaendelea kuwa watumwa tu amkeni.

  Ukichangia jibu hoja zangu. Usifanye jazba kama wewe kweli bwampolisi.

  MUUNGANO HATUUTAKI
  Wazanzibar tutumie nguvu ya hoja Allah {s.w} atatunusuru tu.

  Nawasilisha
  SERELLY.

 11. Mzanzibar mwenye sifa ya kujiunga na chuo kikuu epuka kujiunga na CHUO KIKUU CHA WAISLAM MOROGORO-MUM chuo hichi kinabagua wazanzibar kwa kuwapa DISCO KWA WINGI mfano wanafunzi waliopata disco mwaka wa 1, 2012 ni 198 wazanzibar 150 na watanganyika 48 ulipita msamaha watanganyika 15 waliondolewa DISCO na kubaki 33 wazanzibar 150 WALIBAKI NA DISCO VILE VILE. Jee huu ni muungano kweli.

 12. ni vyema kwa vibaraka wa tanganyika dr sheni , sefu na mwamedi abudu watambue muungano hautakiwi, wasilazimishe wananchi kwa jambo ambalo halina faida na wananchi , ikiwa wao wanafaidika basi watambue mwisho wao umefika, watasababisha umwagaji damu bila ya msingi, wao wanategemea jeshi na polisi , lakini wajue Mungu ni mkubwa kuliko wote hao , tutaumia sote mara hii sio wananchi tu. VILE VILE NAWAOMBA WANANCHI WAWE NA MSIMAMO KUGOMEA MIKUTANO AU MIKUSANYIKO YOTE AMBAYO VIBARAKA HIVI VITAKUWA VINAHUTUBIA , TUWAGOMEE KTK KILA MKUSANYIKO , HATA WAKIJA KWENYE HARUSI AU MAZIKO BASI WATU WAONDOKE WAWAACHE PEKE YAO , NA WAKIINGIA MISIKITINI WATU WAJITENGE NAO WASWALI JAMAA TOFAUTI NA VINAFIKI HIVI. TUNAKUOMBA BI SALMA UFANYE HIMA MAONI YETU UYACHAPISHE KTK KARATASI UZISAMBAZE KWA WANANCHI WOTE , KWANI WEWE KAMA MWANDISHI PIA UNA JUKUMU KUFIKISHA UJUMBE KWA RAIA.

 13. msema kweli mpeziwa mungu. muungano hatuutakiiiii kwa nini mmetushikilia tuu. ccm hamjui kutawala miaka 50 mkiulizwa chamana mlichokifanya . hamkijui. isipkuwa kuitia tanzania nuksi ya makanisa mengi tu . na kuwafaidisha wa westen na marekani . na kuwaumiza dugu zenu.watu wamepigana kuondoa ukoloni nyinyi mumeurejesha . hawa wanao kutumieni kuwakandaamiza wananchi wenu hawato rizika mpaka . hapa tanzania imwagike damu kama ilivyo mwagika iraki au libya . hapo ndio mtajua kama sisi viongozi wa tanzania ni wapumbavu . moto hauko mbali. zanzibar hatoingiiza kanisani na hizo njama zenu za kizushi .huu moto mujue utaendelea kuwaka mpaka mzanzibar wa mwisho . kama nyinyi mlipata uhuru kwa karatasi hapa watu wame mwaga damu . na tutaendelea kumwaga damu .

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s