Kikwete apangua baraza la mawaziri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanahabari wakati wa kutangaza Baraza la Mawaziri leo April 4, 2012. hafla hiyo ilichuhudiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamo wa Rais, Mohammed Gharib Bilal

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete leo wametangaza barza jipya la mawaziri na kupangua baadhi ya mawaziri kuwatoa katika wizara moja na kuwapeleka wizara nyengine huku wengine wakibakia wizara zao kama kawaida na wengine kuachwa nje bila ya kuteuliwa tena kuwa mawaziri.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI

MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,

Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI

OFISI YA RAIS

HAKUNA NAIBU WAZIRI

6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.,

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
4 Mei, 2012

Tume ya Warioba isije ikawa kama Tume ya Warioba
Toleo la 237
2 May 2012
KATIKA makala ya wiki jana, pamoja na mambo mengine, nilitoa pole kwa tume ya Jaji Warioba iliyopewa majukumu mazito yanayohusiana na ukusanyaji na uratibu wa maoni ya wananchi juu ya Katiba mpya. Nilisema kwamba ningeieleza hiyo pole yangu. Napenda kuirejea.

‘Pole’ yangu kwa Warioba na tume yake inatokana na ukweli wa mambo ninayoyaona na ninayoyakumbuka, ambayo nina uhakika kwamba na watu wengine pia wanayaona na wanayakumbuka. La kwanza ni kwamba, pamoja na kwamba sipendi kuwapamba wanasiasa, Joseph Sinde Warioba, pasi na shaka, ni Mtanzania wa kipekee, mtu makini wa aina yake, muadilifu na mkweli. Ni mtu ambaye kila utawala ulioingia madarakani tangu tupate Uhuru umeona umuhimu wa kumtumia katika nafasi mbalimbali.

Amekuwa Mwanasheria Mkuu, Waziri wa Sheria na Waziri Mkuu, tukiacha nafasi nyingine alizokuwa nazo nchini na nje ya nchi. Anaheshimika sana kote duniani kwa kazi zake, lakini, muhimu zaidi, ni kwamba anaheshimika nchini mwake kwa sababu anaonekana kama kisiwa cha uadilifu katika jangwa lililokaukiwa na uadilifu, kipande cha almasi katikati ya vipande vya mbao vilivyojaza utawala wetu.

Hivi sasa amekuwa ni “mzee wa kijiji”, ambaye mara kwa mara anajitokeza kutoa matamko ya kuonya, kuasa, kutanabahisha na kukemea inapobidi kufanya hivyo. Anasikilizwa kwa sababu anaaminika. Ndiyo maana haishangazi kwamba, mkabala na madai ya Katiba mpya, Rais Jakaya Kikwete alimwona kwamba yeye ndiye mtu anayeweza kujenga imani miongoni mwa wananchi kwamba zoezi hili litafanyika kwa umakini na matarajio ya wengi yatapata kukidhiwa kwa sababu anayelisimamia ni mtu makini.

Wajumbe wengine wa tume hiyo, angalau wachache miongoni mwao ninaowajua binafsi, wanazo sifa za kutosha za kuwawezesha kulitumikia taifa hili katika shughuli kubwa inayokusudiwa kuleta manufaa kwa nchi yetu. Kwa hiyo ninayoyasema hapa, leo na katika siku zijazo, hayahusiani hata chembe na sifa za wajumbe wa tume hiyo, mmoja mmoja au kwa ujumla wao, bali ninachojaribu kufanya ni kutafakari hali halisi ambamo tume hiyo itafanya kazi yake.

Kwanza tukumbushane kwamba hii si tume ya kwanza kuitwa Tume ya Warioba. Angalau binafsi naikumbuka nyingine, ambayo iliundwa na Rais Benjamin Mkapa mwaka 1996 ambayo Rais aliikabidhi jukumu zito la kuchunguza kwa undani janga la rushwa nchini. Hiyo pia iliitwa Tume ya Warioba, na ilifanya kazi kubwa na nzuri ya kuainisha mapana na marefu ya saratani ya rushwa iliyokuwa inaitafuna nchi, na mwisho wake ikatoa mapendekezo kwa Rais aliyeiteua.

Taarifa ya Tume ya Warioba I ilipowekwa hadharani kwa muhtasari tu, hamasa ilikuwa kubwa nchini kote, nami nilihamasika kiasi cha kupanda ndege kwenda Mtwara ambako kulikuwa na maandamano makubwa yaliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa, Nsa Kaisi kumpongeza Rais Mkapa kwa ubora wa taarifa ya Tume ya Warioba I. Wananchi wakaamini kwamba sasa saratani ya rushwa, ufisadi na uozo ilikuwa imepatiwa dawa mujarrab. Iliyobaki, kama wasemavyo wenzetu, ni historia.

Taarifa ya Tume ya Warioba I hadi sasa inanukuliwa na wasomi katika mataifa mbalimbali duniani na serikali kadhaa zimeifanyia kazi, lakini si Serikali ya Tanzania. Taarifa imeachwa inakusanya vumbi makabatini wakati wakuu serikalini wakiendeleza ufisadi wa kuchefua, hususan katika taratibu za ununuzi (procurement), ambao ndio msingi mkuu wa taarifa hiyo. Hivi majuzi tumeshuhudia tena, bungeni Dodoma jinsi ambavyo ununuzi unafanyika, na kandarasi zinatolewa kama vile hatujawahi kuwa na kitu kama Tume ya Warioba wala taarifa yake.

Majumuisho ya uzoefu tunaoupata kutokana na Tume ya Warioba I ni kwamba ilikuwa ni kazi bure, halafu kazi bure ghali. Tuliingia gharama kubwa, tukawahangaisha watu waliojitokeza kutoa ushuhuda, maoni na mapendekezo, lakini mwisho wake ni makaratasi makabatini, utekelezaji sufuri. Leo najiuliza, hivi mle ndani ya Baraza la Mawaziri kuna mtu anaikumbuka Tume ya Warioba I?

Sasa, wasiwasi wangu ni kwamba, kama vile watawala walivyotaka kumtumia Warioba kujenga imani mwaka 1996 – ili Mr Cleanaonekane Mr Clean kweli — wanataka kufanya vivyo hivyo safari hii tena, kwa kuukamua uadilifu wa Warioba kwa maslahi yao, huku wakijua kwamba kitakachofanywa na tume hiyo hakitakuwa na uwezo wa kubadilisha jambo lolote la msingi. Itagongagonga debe huku na huku, itaondoa aya na kuingiza aya, itafanya mapendekezo ya kiutawala, lakini haitaweza kuweka misingi ya mabadiliko ya kimaendeleo katika muda iliyopewa.

Hofu yangu ni kwamba kwa mara nyingine tena tunaingia katika ubadhirifu wa mapesa chungu nzima kufanya kazi isiyokuwa na tija ya msingi. Mwisho wa siku tutakuwa tumeshuhudia hekaheka na mshikemshike wa mikutano, semina, makongamano, warsha, malumbano, majibizano na mapandishiano, lakini kitakochotoka hatimaye kitakuwa kiduchu. Walatini wa kale walisema, parituriunt montes, nacsetur ridiculus mus. Milima ina uchungu, kitazaliwa kijipanya kiduchu.

Nasema haya kutokana na ushahidi ninaouona, kwamba, pamoja na umuhimu wa kuwa na Katiba mpya, hatuna budi kwanza kupata mwafaka kuhusu masuala ya msingi kabisa, ambayo ni ya kisiasa kuliko jambo jingine lolote. Hatuna budi kuwa na mwafaka wa kisiasa, ambao kwa hivi sasa siuoni.

Nitoe mfano. Kuandika Katiba mpya (kama kweli ndicho tunachotaka kufanya, na si kutia viraka vipya juu ya viraka vya awali) ni sawa sawa na kujenga nyumba mpya (tofauti na kurekebisha au kukarabati nyumba iliyopo). Hii ina maana ya kuanza upya, kukidhi mahitaji mapya na kuangalia pia mahitaji ya ki-mustakabali.

Wanandoa vijana wanaoishi katika nyumba ya chumba kimoja na sebule watataka kuhamia nyumba yenye nafasi kubwa zaidi wanapoanza kupata watoto wawili, watatu, na watajadiliana pamoja aina ya nyumba wanayoitaka kabla ya kumuita msanifu majengo (architect). Watakubaliana juu ya ukubwa wa nyumba hiyo kutokana na watoto wanaokusudia kuwa nao.

Pia watakubaliana juu ya kuweka nafasi ya kutosha kwa watoto kucheza bila kuhatarisha maisha yao, na kadhalika. Nyumba hiyo itabuniwa kwa msingi wa watoto na mahitaji yao. Kama wamekwisha kupata mtoto mwenye ulemavu wa aina fulani, watakubaliana jinsi nyumba yao itakavyomsitiri.

Iwapo wanatarajia kuishi na mmoja au zaidi ya wazazi wao waliozeeka, watakubaliana ni wapi wazee hao wataishi, na jinsi maslahi ya wakongwe hao hayatavuruga maslahi ya wanandoa hao vijana kwa maana ya faragha yao na ukaribu wa kimapenzi. Mzazi aliyetoka shamba anaweza kuwa na tatizo la “kwenda haja” ndani ya nyumba, kwa hiyo hili litawekewa utaratibu ili choo chake kiwe nje kidogo ya nyumba.

Kama wanandoa wamedhamiria kuishi maisha ya ‘Kiswahili,’ wataamua kwamba nyumba yao lazima iwe na uwa, mahali pa akina mama kufanya shughuli zao za upishi, ususi, ufumaji wa vitambaa, na michapo. Watakubaliana juu ya utaratibu usioruhusu baba na binti zake kukutana wakiwa hawajajiweka ‘sawa’. Hii yote ni kusema kwamba nyumba inajengwa vichwani mwa wanandoa kwa maridhiano yao wawili (wakati mwingine na watoto pia, kama wamekua kiasi cha kutosha), kabla ya msanifu kuitwa na kupewa maagizo ya kuwachorea nyumba itakayokidhi mahitaji mahsusi ya familia yao.

Katiba haina tofauti kubwa na nyumba ya familia. Humo ndimo tunataraji kuishi kama taifa, pamoja na watoto wetu wenye mahitaji yanayotofautiana (jinsia, rika, ulemavu); pamoja na wazazi wetu wakongwe (faragha yetu na yao, maliwato waliyoyazoea wakiwa shamba), na kadhalika. Tungekuwa tunatafuta hoteli, tungeweza kupata hoteli yoyote, kwani hoteli moja ni kama nyingine; zinatofautiana ufahari na bei. Nyumba ya familia ni mahsusi kwa familia, mahsusi kwa mahitaji ya familia husika.

Napenda kurejea kile nilichokisema mara kadhaa. Yapo mambo yanayowasumbua wanasiasa, ndani ya chama tawala na ndani ya vyama vya upinzani. Haya ni yale ya kiutawala niliyoyataja hapo juu: tume huru ya uchaguzi; utaratibu wa uchaguzi; viwango vya asilimia katika uchaguzi; utaratibu wa uchaguzi; madaraka ya Rais; madaraka ya Bunge; kuwapo kwa waziri mkuu au la, na madaraka yake; uwakilishi wa uwiano (PR); ukomo wa mihula ya uongozi, na mambo mengine madogo madogo kama hayo.

Haya yote ni muhimu lakini hayana uzito kama ule ninaouona katika maeneo mengine: Kuwapo kwa Muungano na mgawanyo wa mamlaka na rasilimali baina ya Tanganyika na Zanzibar; mamlaka juu ya rasilimali za nchi kwa ujumla (ardhi, madini, maji, misitu); ugatuzi na mamlaka ya serikali za mitaa na mgawanyo wa madaraka baina ya serikali hizi na serikali kuu; mgawanyo wa rasilimali baina ya wakulima na wafugaji; utamaduni na lugha za asili mkabala na Kiswahili na Kiingereza; mfumo wa elimu utakaojenga Utanzania, na kadhalika.

Baadhi ya masuala haya mazito nilikwisha kuyatolea tafakuri, lakini sijachoka kuyarejea. Nitayajadili upya kadri tunavyokwenda.

Narudia kusema kwamba tusifanye mambo kwa haraka kwani hatuna tunakoenda. Tupo hapa, na tunataraji kuwa hapa kwa miaka milioni ijayo, kama si zaidi. Kwa nini tunafanya mambo kama vile tuko mapitoni (transit) tukienda mahali pengine?

CHANZO: RAIA MWEMA

Advertisements

8 responses to “Kikwete apangua baraza la mawaziri

  1. Mukilivunja, mukilikata maahusat! ni baraza la watanganyika! na wasaliti wa zanzibar. hili lililofanywa ni sawa kundoa tandu na kueka ng’e maumivu palepale njaa ile ile rushwa daima mbele! mutafukuza maisha yote kuzuga walipa kodi ambao ndio mafukara! lakin twawambia wazanzibar hatuna haja na mawazir wenu twataka nchi yetu!

  2. Wakoloni wetu wameshabadilishabadisha BARAZA LA MAWAZIRI. Sasa watakuja kubadisha viongozi wa SMZ ambao wanakataa kufirwa na viongozi wa TANGANYIKA. WENZENU kina SEIF ALI IDD, SHAMHUNA NA MOH’D ABOUD wao wameshazoea kufirwa na viongozi wa TANGANYIKA ndio maana ni VIBARAKA WA TANGANYIKA.

  3. sawasawa muungano hatuutaki hata mkiwaweka mawaziri wote kutoka znz , haisaidii , danganya toto imekwisha Nd Kikwete , tuvunje huu muungano kwa amani na utulivu kwa faida ya wote , halafu tutaangalia maeneo gani tunataka tushirikiane lakini sio kuungana. Tafadhali Nd Kikwete ufanye jambo hili kabla ya kung’atuka 2015 , utakumbukwa na kuheshimika na waznz na watanganyika kwa ujumla, na ulimwengu mzima utakuheshimu kwa kutatua tatizo hili zaidi ya nusu karne sasa , waswahili wamesema lenye mwanzo huwa na mwisho ……………

  4. Rais kikwete je umesahau kama uliwabembeleza wazanzibar kukupa kura ili utatue matatizo yao? Tunakuomba utimize hiyo ahadi uliyoweka kumbuka ahadi ni deni utakuwa mas-uul mbele ya m.mungu. wazanzibar mungano hatuutaki mchakato wa katiba mpya mwisho msasani zanibar huru lazima bi idhnillah.

  5. Nini mawaziri au nani kikwete ndugu zangu bado tu tunategemea ahadi walizotuwekea viongozi wa kibepari? Hatuchoki kudanganywa ni kweli sisi wazanzibar ni watu subra (na hii kwetu ni ibada) lakini wasitugeuze kuwa kama kupe hata ng’ombe akifa ngozi ishawekwa juani yeye anasubiria tu, sisi waislamu bwana tusidhuriwe na madudu haya mara tofauti katika shimo lao hili la ubepari na siasa zao za shirki za “demokrasia” wamefanya zamu za kutudanganya mara kaja huyu mara mwengine.
    Kwani hawasikii tunachokitaka? sisi tunataka kwanza tujadili mustakbali wa huu muungano wao wanatufanya majinga sisi etu wanatuletea maoni ya katiba ambayo suala la muungano halitakiwi kujadiliwa ee ndivyo walivyoambiwa na mabwana zao Amerika hata huyu (maalim Seif) tuliedhania ndio labda angetuonea huruma mara kadhaa katupelekea kuingia shidani kwa chama chake mara tumo jela, mara tupigwe, tuwe wakimbizi hata tumeuliwa kumbe nae ni wao hana labda vyandarua vilivyotoka kwa makafiri ili wawanunue zaidi. Na kupanga mipango ya kujinufaisha wao na matajiri wakubwa kwa kuunda tume ya bei ambayo imekabidhiwa kwa wafanyabiashara wakubwa, leo mchele alioupinga kuuzwa 900 unauzwa 1600 mwisho lini! mimi nikatike mguu nikienda kutoa maoni katika kufru yao hio au kwenda tuna kujiandikisha kupiga kura.

  6. Jenerali Ulimwengu umezungumza sahihi kabisa. Mimi nina wasisi wasi na Katiba hii itakayoandikwa ambayo unadishi wake umekewa terms of reference na muda wa kukamilika kama vile mradi. Katika mwelekeo huu hii si Katiba itakuwa mradi wa Watawala kukubalika kwa wanadai katiba mypa kabla 2015. Sisi ambao tunahitaji mahusiano yetu na watawala yaoneshwe, sisi ambao tunahitaji taasisi za kiutawala zinoeshwe mipaka na majukumu yake, sisi ambao tuanahitaji mihili ya dola ioneshwe mipaka yake, sios ambao tunahitaji mahusiano ya watawala na watawaliwa inoneshwe, sis ambao tunahitaji mambo mengine yanayohusiana na maisha yetu yawekwe wazi tutabaki hatuna chochote katika mchakato huu. Tunasubiri tuone ni vipi TUME hii intakuwe tofauti na nyengine za huko nyuma.

  7. Pingback: Kesi ya wapinga Muungano kusikilizwa Juni 6·

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s