Tanzania imejaaliwa kuwa na Raslimali

Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Kazi, Uwezeshaji na Ushirika Zanzibar, Asha Abdallah akiwa katika mkutano wa siku mbili huko Visitors Inn Hoteli Bwejuu katikati ni mjumbe wa bodi ya TPST, Peter Kisawiro na Meneja miradi, Sosthenes Sambua

IMEELEZWA kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye utajiri mkubwa wa rasilimali asili na iwapo zitatumiwa ipasavyo zitaweza kuleta manufaa makubwa nchini. Hayo yameelezwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara  ya  Kazi, Uwezeshaji na Ushirika Zanzibar, Asha Abdallah wakati akifungua mkutano wa siku mbili kwa watendaji wa wizara, na idara za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huko Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.

Katika mkutano huo ambao imeshirikisha mamlaka mbali mbali zinasimamia maendeleo ya sekta ya ujasiriamali, Katibu Mkuu huyo alisema Tanzania licha ya kuwa na raslimali nyingi lakini bado hazijatumika kikamilifu kwa faida za kiuchumi kwa taifa.

Akizitaja rasilimali zilizopo nchini, Katibu Mkuu huyo alisema bahari, na ardhi ya kilimo zina uwezo mkubwa wa kuiwezesha  Tanzania kuongoza katika soko la biashara ya ushindani katika bara la Afrika.

“Tanzania ina rasilimali kubwa sana tena ni rasilimali asili mfano bahari na ardhi tulizonazo kama zitatumiwa vyema basi tunaweza kuwa matajiri wakubwa katika bara letu” alisema Katibu Mkuu huyo.

Aidha waliwataka wajumbe wa mkutano huo kuwa makini katika mafunzo wanayopatiwa na kuchukua mafunzo ya kuwa wabunifu kwani tatizo kubwa linaloonekana kwa watanzania ni ukosefu wa ubunifu katika biashara.

“Tatizo letu kubwa sisi watanzania hatuna ubunifu na ndio maana utaona rasilimali tunazo, ardhi tunayo na wataalamu tunao lakini taifa letu lipo nyuma kiuchumi” alisema Bi Asha.
sha alionya kuwa bila kuwajengea wadau wa biashara uwezo wa ubunifu na ushindani katika biashara, Tanzania itaendelea kuwa nje ya ulingo wa maendeleo ya uchumi naopatikana kwa njia ya ushindani katika biashara.

Alisema ili kufikia hatua ya maendeleo ni lazima wataalamu wajipange kikamilifu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwajengea wajasiriamali uwezo wa kujua vigezo  vya biashara ya ushindani hasa katika kuelekea katika soko la Afrika Mashariki.

“Watanzania rasilimali tunazo kilichobaki tujipange ili tuhimili ushindani, hasa kupitia sekta ya viwanda ,… na vyuo vikuu pia vifikirie kuwa na somo la ujasiriamali ili kuwandaa vijana kujiajiri na kuingia katika utendaji wa kufanyakazi kwa ushindani na ubunifu wa kuongeza thamani ya bidhaa, na tuwacheni kufanya kazi kwa mazowea” alisema Bi Asha.

Alisema raslimali  zinazoweza kuipeleka Tanzania katika nafasi ya kuongoza katika biashara barani Afrika ni bahari, shughuli za uvuvi na mazao yake ya baharini, kilimo kama vile cha mazao ya  mwani kwa Zanzibar, na korosho na mkonge kwa upande wa bara na utalii uliopo ambayo fukwe za kuvutia na utulivu uliopo na amani katika nchi hiii.

Hata hivyo alisema rasilimali watu wenye utaalamu mkubwa ni miongoni mwa rasilimali ambazo baadhi ya nchi hawana hivyo aliwataka wajumbe hao kuchukua mafunzo hayo umakini mkubwa.

Akitoa mada katika mafunzo hayo Sostthenes Sambua alisema Tanzania ni nchi pekee ambayo imepata bahati ya kupata mafunzo hayo na kuwataka washiriki wa mkutano huo kuyatumia vyema mafunzo hayo ili waweze kuwasaidia wajasiriamali wenzao katika kufanikisha ubunifu na biashara nchini.

Alisema watanzania wengi wana ari ya kufanya biashara za ujasiriamali lakini kilichokosekana na ubunifu wa kuweza kuendeleza biashara hizo jambo ambalo alisema litasaidia sana katika kuendeleza harakati za kujikomboa kutoka ndani ya umasikini.

Mafunzo hayo yameandaliwa na mfuko wa sekta binafsi Tanzania(TPSF) unaosimamia maendeleo ya sekta ya ujasiriamali kwa mkopo nafuu wa Benki ya ya Dunia na Mfuko wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza (DFID)  kwa Tanzania.

Zaidi ya wajasiriamali 8,3000 wanufaika


UENDESHAJI wa miradi ya uchumi na biashara kupitia Mpango wa Fanikiwa Kibiashara (BGD) umewapa mafunzo zaidi wajasiriamali 8,300 Tanzania Bara na Zanzibar.

Wilaya 120 zimefaidika na mafunzo hayo yenye lengo la kuwaondoshea umasikini na kuwawezesha wawe wabunifu na kumudu ushindani wa kibiashara hasa wakati huu ambapo Tanzania imeingia katika soko la Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Bwejuu katika semina ya siku mbili, Meneja Mipango wa BDG, Sosthenes Sambua, alisema kuwa mbali na mafunzo hayo, wajasiriamali wapatao 6,000 kati  ya hao walipewa mbegu mtaji  kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kilimo.

Semina hiyo ya simu mbili imewapa mafunzo watendaji wa serikali na wakurugenzi wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuwafanya wawe wabunifu na kumudu ushindani wa kibishara ambapo Tanzania ni nchi pekee ambayo hadi sasa inaelezwa kupata wafunzo ya aina hiyo.

 Meneja huyo alisema mafunzo na mtaji huo ni sehemu ya mpango wa miradi yaon mitatu  mikubwa  iitwayo Matching Grants Programme (MGP), Cluster Competitiveness Programme (CCP) na BDG inayolenga kujenga uwezo wa Tanzania kuingia katika ushindani na ubunifu wa biashara kupitia sekta ya ujasiriamali ambapo baada ya mafunzo hayo watendaji hao wa ngazi ya ukurugenzi wataweza kuwafunza wajasiriamali wengine.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi hiyo Sambua alisema inaendelea kutekelezwa kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 25, ikiwa ni mkopo wa Benki ya Dunia kwa Tanzania.

Aliwaambia waandishi wa habari kwamba kwamba miradi yote hiyo mitatu inasimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa Ushindani wa Sekta Binafsi (PSCP).

Aidha Sambua alisema mpango wa BDG umepangwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kinachoishia Agosti mwaka huu kwa msaada  wa fedha millioni 7.6 za Uingereza milioni ambapo alisema fedha hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuwawezesha wajasiriamali wengi kuwajengea uwezo wa kibiashara.

Utekelezaji wa mpango wa  MGP ulianza mwaka 2008 na kukamilika Desemba mwaka jana na CCP unatekelezwa kwa kipindi cha miaka minne kinachomalizika mwezi huu ambapo tayari mafunzo na programu mbali mbali zimeshafanyika katika maeneo mbali mbali nchini bara na visiwani.

Alisema dira ya taifa ya maendeleo ni  kuhakikisha Tanzania inafikia uwezo kamili wa kuhimili ushindani wa kibiashara ifikapo 2025.

pamoja na hilo Alisema mafunzo yanayotolewa kwa watendaji wataalam na wajasiriamali  ni kichocheo cha kufanikisha mipango ya serikali na kuondokana na umasikini nchini.

Mafunzo hayo ya siku mbili yaliandaliwa na mfuko wa sekta binafsi Tanzania (TPSF) na unaosimamia maendeleo ya sekta ya ujasiriamali kwa mkopo nafuu wa Benki ya Dunia (DFID) kwa Tanzania.

Advertisements

4 responses to “Tanzania imejaaliwa kuwa na Raslimali

  1. ZANZIBAR SIO TANZANIA. Na wala wazanzibar si watanzania. WAZANZIBAR NI WAZANZIBAR NA WATANZANIA NI WATANGANYIKA. Wazanzibar hatuutaki muungano na watanganyika.

  2. Dada angu Asha kila mtu anajua kuwa Tanzania ni tajiri. Lisilojulikana ni vipi utajiri huu unatumika.

  3. Muungano unaarudisha nyuma maendeleo hatuutaki muungano. Tanganyika ni kama Tanganyika tu. Tupeni Zanzibar yetu tubuni miundombinu yetu

    • WAZANZIBAR SHIKENI UZI HUO HUO NA SISI YUKO NYUMA YENU TUMECHOKA KUNYANYASWA TUMESHADHALILISHWA SANA NA WABARA TUPEWE ZANZIBAR YETU KUFA KWA JAMAA HARUSI JAMANI EEEEHH

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s