Maadhimisho ya Mei Mosi

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein akiwahutubia wafanyakazi wa sekta mbali mbali huko Bwawani Mjini Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi kulia kwake ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi (ZATUC) Zahran Mohammed Nassor na kushoto yake ni Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi na Ushirika, Haroun Ali Suleiman.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Serikali anayoingoza itaendelea kuimarisha maslahi ya wafanyakazi huku akitoa wito kwa wafanyakazi kutimiza wajibu wao makazini . Dk Shein aliyasema hay oleo  katika hotuba yake aliyoitoa katika kilele cha sherehe za wafanyakazi duniani (Mei Mosi), zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani, mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na wafanyakazi na viongozi mbali mbali kutoka sekta ya umma na sekta binafsi.
Katika hutoba yake hiyo, Dk. Shein alieleza kuwa kuanzia sasa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lifanye jitihada ya  kuwataka wafanyakazi watimize wajibu wao tena kwa umuhimu zaidi wakiwa makazini.
Alieleza kuwa imefika wakati Shirikisho hilo liwashajiishe, liwaelimishe na ikibidi liseme na kuwakemea watumishi wanaochelewa kufika kazini na kuondoka kabla ya wakati kwani huo si utaratibu wa kazi.
Dk. Shein alisema kuwa  Shirikisho lisisitize kwa wananchama wake na wafanyakazi wengine suala la kuzingatia nidhamu kazini na kuzingatia taratibu zilizowekwa kukiwa na lengo la kuwahudumia wananchi kwa ufanisi na kuepukwa matakwa binafsi badala ya matakwa ya umma.
Alieleza kuwa hatua hiyo italeta msukumo katika kuimarisha dhana ya Utumishi Bora inayozingatia kuleta ufanisi na uwajibikaji katika sehemu za kazi sanjari na kuimarisha uhusiano mwema kati ya Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri ikiwemo Serikali anayoiongoza.  “Hii serikali yetu sote na kila mmoja anahitajia maslahi mazuri hata mimi pia”,alisema Dk. Shein.
Aidha, Dk. Shein alisema kuwakatika muundo wa Serikali anayoiongoza alianzisha Wizara mbili muhimu kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa masuala ya kazi, kukuza ajira na kunyanyua hali ya  maisha ya wafanyakazi na wananchi ikiwemo Wizara ya Kazi, uwezeshaji Wananachi Kiuchumi na Ushirika pamoja na Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Alieleza kuwa katika kipindi hichi kifupi wananchi wameshuhudia mageuzi makubwa ya maslahi ya wafanyakazi katika sekta ya umma na sekta binafsi pamoja na mabadiliko ya maslahi ambayo yamefanywa, serikali bado inapokea malalamiko ya watumishi ambao kwa bahati mbaya wanahisi kuna makosa katika marekebisho ya mishahara yao mipya ilioonezwa.
Alisema kuwa kwa kuelewa mchango wa wafanyakazi wa majumbani Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeamua kunyanyua maslahi yao kwa kuweka sheria mpya ya kuwaongezea mshahara wao kutoka kiwango cha zamani cha Shilingi 30,000 hadi Shilingi 60,000 kwa mwezi.
Dk. Shein pia, alisisitiza wajibu wa kuthamini kazi zao na kulinda maslahi  na utu wao kwani inasikitisha kusikia kadhia mbali mbali zinazowakuta wafanyakazi wa majumbani ambazo hazipendezi hata kuzizungumza.
Pia, Dk. Shein alitoa wito kwa wananchi wote kuzipiga vita ajira za watoto kwa lengo  la kuwatakia mema katika maisha yao ya sasa na hapo baadae na kusisitiza kuwa kila mmoja ampende motto wa mwenziwe na aamini kuwa “Mtoto wa mwenzio ni wako”,alisisitiza Dk. Shein.
Akizungumzia suala la kuimarisha amani na utulivu hapa nchini ambayo imeipa sifa kubwa Zanzibar ndani na nje  na kuwataka wafanyakazi kujiepusha na vitendo vinavyoashiria kuivunja amani, lugha ya kejeli kwa serikali na viongozi wake, vitendo vya jazba ambavyo vinachochea hasira na badala yake watumie majadiliano.
Kwa upande wa ajira kwa vijana, Dk. Shein alisema kuwa serikali imo katika juhudi za kulitafutia ufumbuzi huku akiwataka vijana kutosubiri ajira za serikali peke yake na badala yake wawe tayari kujiajiri na kuwataka waajiri kushirikiana pamoja katika kutatua tatizo hilo kwa kuongeza fursa za ajira za heshima kwa vijana nchini.
Pamoja na hayo Dk. Shein alisema kuwa Serikali inatambua kuwa ustawi wa maisha ya wafanyakazi nchini na wananchi wote kwa jumla unaathiriwa sana na mfumko wa bei za bidhaa hususan chakula na kueleza kuwa dawa yake kubwa ni kuzalisha chakula kwa wingi chini ya kauli mbiu ya Mapinduzi ya Kilimo.
Alisisitiza kuwa ni lazima uzalishwaji wa chakula uengezwe zaidi hasa ivyokuwa mahitaji ni makubwa kutokana na idadi ya watu inavyoongezeka na bei za bidhaa ulimwenguni zinapanda.
Dk. Shein alisisitiza suala zima la sensa  linalotarajiwa kuanza Agosti 26 mwaka huu na kutoa wiko kwa  wafanyakazi na wananchi wote kushiriki kikamilifu.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwaeleza wananchi juu ya suala la zoezi la kukusanya maoni juu ya mabadilikoKatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza kuwa wakati bado haujafika na ukifika kila mwananchi atapata fursa ya kutoa maoni yake.
Alisema kuwa wanaotaka kusikilizwa ni wananchi wote na wala sio kikundi Fulani cha watu na wala hakuna mbabe kwa hili kwani Zanzibar inaongozwa na Sheria na Katiba za nchi na kueleza kuwa kamwe Zanzibar haitorejeshwa ilikotoka.
Nao wafanyakazi wa Zanzibar kupitia Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi katika risala yao walipongeza juhudi zinazochukuliwa na serikali chini ya uongozi wa Dk. Shein huku wakieleza wasi wasi wao kwa kujitokeza vikundi vinavyohatarisha amani kwa kukashifu wananchi wenzao na viongozi kwa visingizio vya dini.
Pia, wafanyakazi hao walieleza matarajio yao makubwa kwa viongozi waliomadarakani kuwa watajitahidi kufuata sheria, kutandika miongozo mizuri ya utawala bora na kutimiza ahadi walizoziahidi wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010.
Nae Mkurugenzi wa Jumuiya Waajiri Zanzibar, Salali Salim Salali akieleza ujumbe wa Siku ya Wafanyakazi duniani kwa Zanzibar ni “Mfumko wa Bei, Kodi Kubwa na Mishahara duni ni pigo kwa wafanyakazi”, alisema mishahara popote duniani na sehemu yoyote ya kazi inategemea na uzalishaji, hivyo alisisitiza kufanya kazi kwa bidii ili uzalishaji uongezeke.
Advertisements

2 responses to “Maadhimisho ya Mei Mosi

  1. UMASKI WA ZANZIBAR UNASABABISHWA NA WATANGANYIKA. Wazanzibar hatuutaki muungano na kuma kutoka maji ya kunuka na mikundu iliyooza wa TANGANYIKA

  2. Imefurahisha kuona kila mwaka viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi wanashiriki katika Sherehe za Mei Mosi. Mimi nisichofahamu ni kiasi gani wanawatayarishia watumishi wa SMZ kutoendelea na kuomba omba baada ya kuacha kazi zao rasmi. Wakati huu wa kusherekea Mei Mosi ni jukumu la SMZ kujua kuwa haiwatendei haki wafanyakazi inawaajiri bila ya kai maalumu. Kuna taasisi za Serikali hii Wafanyakazi ni wengi kuliko wahudumiwa. Hii si haki! Watu hawa kama lazima waajiriwe basi bora wangepewa nyezo wakajiajiri wenyewe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s