Wazanzibari wakusanya saini ya kutaka kura ya maoni juu ya Muungano

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa kushirikiana na taasisi kadhaa za kiislamu za hapa Zanzibar zimeanza kutoa fomu ya kuitishwa kura ya maoni juu ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. fomu hizo zinapatikana katika maeneo mbali mbali ikiwemo katika ofisi za Jumuiya ya Maimamu na Jumuiya ya Uamsho zilizopo Mkunazini Unguja

JUMUIYA ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar imetoa fomu maalumu ya kuorodheshwa idadi ya yatu wanaotaka kuitishwa kura ya maoni juu ya mustakabali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya katiba mpya. Jumuiya hiyo imeshirikiana na taasisi nyengine za dini ya kiislamu imeanza kusambaza fomu hizo hapo jana na kuzitawanya sehemu mbali mbali Unguja na Pemba na jijini Dar es Salaam.

Lengo la kujaza fomu hizo ni kuchukua majina kamili, saini na namba ya vitambulisho vya wazanzibari au namba ya pasi ya kusafiria kwa wanaotaka kuitishwe kura ya maoni ya kuulizwa wazanzibari iwapo wanautaka au hawautaki Muungano uliopo wa Tanganyika na Zanzibar kabla ya tume iliyoteuliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete kuanza kazi.

“Tunataka kuulizwa kwanza iwapo tunautaka Muungano au hatuutaki halafu tena tume ya rais ianze kazi ya kukusanya maoni ya kuundwa kwa katiba mpya ya Tanzania lakini wakati huo tuwe tumeshaamua tunataka au hatutaki” alisema Kiongozi wa Jumuiya hiyo, Sheikh Azzan Khalid Hamdan.

Hatua hiyo ni muendelezo wa harakati zinazofanyika hapa Zanzibar zinazofanywa na taasisi hizo ambapo kwa zaidi ya mwezi sasa kumekuwepo mikusanyiko na mikutano mbali mbali ya kuelezea faida na hasara za Muungano uliopo lakini pia matatizo na kero ambazo kwa takriban miaka 48 zimeshindwa kutatuliwa na viongozi waliopo madarakani.

Kwa mujibu wa fomu hizo ambazo Mwananchi imepata nakala yake na kuthibitishwa na Sheikh Azzan kuwa taasisi yake ndio iliyoratibu zoezi hilo la kugawa fomu amesema tayari wameshazisambaza kila sehemu Unguja na Pemba na matarajio yao kufika hadi vijijini ili watu wapate fursa ya kujiorodhesha majina yao na kuweka saini zao kama ni ushahidi kabla ya fomu hizo kukabidhiwa Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein kwa hatua za zinazofuata.

“Tumechapisha fomu 25,000, kila fomu watajaza watu 20 na tayari tunazisambaza kote, mjini na vijijni Unguja na Pemba, lengo ni kukusanya saini 400,000,” alisema Sheikh Azzan.

Kuchapishwa kwa fomu hizo ni miongoni mwa harakati za wazanzibari mbali mbali kupitia vikundi na taasisi kadhaa zinazodai kuitishwa kwa kura ya maoni kwanza kabla ya tume ya Rais Kikwete kuanza kazi zake.

Hivi karibuni Kiongozi mmoja wa kikundi cha wanaharakati wa taasisi ya kiraia iitwayo Umoja wa Wazanzibari (ZARFA), Rashid Salum Adiy na wenzake 12 kufikishwa mahakamani hapa Zanzibar wakituhumiwa kwa uhuni, uzururaji na kupinga Muungano baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi.

Watu hao 12 walikamatwa mwezi uliopita mwaka huu  katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, ambako imedaiwa walikwenda kushinikiza baraza hilo kuitisha kura ya maoni ili kujua kama Wazanzibari wanataka au hawataki Muungano huu uliopo wa Tanganyika na Zanzibar ambao umetimiza miaka 48 hivi karibuni.

Suala la kuitishwa kwa kura ya maoni juu ya Muungano limekuwa likizungumzwa na watu mbali mbali Zanzibar na hata Tanzania Bara ambapo hivi karibuni kupitia kipindi cha mazungumzo mbele ya meza ya duara kinachorushwa na idhaa ya kiswahili ya Ujerumani (DW) mwandishi wa Habari Maarufu Tanzania, Jenerali Ulimwengu alisema ipo haja ya kuitishwa mjadala wa wazi na kufanyika kwa kura ya maoni kwanza kabla ya tume kuanza kazi yake ya kukusanya maoni ya katiba mpya.

“Kabla ya kuwa na Katiba mpya, kuwe na mdahalo wa wazi juu ya Muungano, waulizwe watanzania wanautaka Muungano au hawautaki, vinginevyo ni kupoteza fedha nyingi na muda wa watu,” alisema Jenerali Ulimwengu.

Ulimwengu alisema suala la Muungano linapaswa kupewa nafasi muhimu katiba katiba na bila ya kujadiliwa Muungano hakuna katiba mpya kwani huwezi kuzungumzia katiba ya Tanzania bila ya kugusa Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar.

“Zanzibar haina mwenza wake, Tanganyika …. katika hali hiyo hata uwepo wa Zanzibar katika Muungano hauonekani kikatiba,” alisema Ulimwengu.

Ulimwengi ni miongoni mwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliounda kundi lijulikanalo G 55 na kupeleka hoja Bungeni kutaka kufufuliwa kwa serikali ya Tanganyika lakini kwa wakati ule jambo hilo lilizimwa kimya kimya na Mwalimu Nyerere bila mafanikio yaliokusudiwa.

Harakati za kutaka kura ya maoni na Zanzibar na kutolewa ndani ya mikono ya Muungano zimekuwa zikiendelea kila siku hapa Zanzibar licha ya kukemewa mara kadhaa na viongozi wa ngazi mbali mbali za serikali akiwemo makamu wa pili wa rais na mawaziri wanaohusika na masuala ya katiba.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati akifunga kikao cha baraza la wawakilishi April 20, mwaka huu,  alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haitawavumilia tena wanaharakati wanachochea vurugu badala ya kutoa elimu juu ya masuala mbali mbali ya kijamii, likiwemo la upatikanaji wa Katiba mpya ya Tanzania .

Lakini licha ya onyo hilo harakati hizo zimekuwa zikipamba moto kila kukicha kama kwamba hakuna tahadhari iliyotolewa kuhusiana na jambo hilo na taasisi hizo zimekuwa zikiongezeka zaidi na kuunga mkono jambo hilo ambapo sasa baadhi ya wanataaluma ya kisheria, wasomi, na wanasiasa mbali mbali wamekuwa wakiunga mkono harakati hizo wazi wazi na kusema mustakabali wa Muungano uamuliwe kwanza kabla ya Katiba mpya.

 

16 responses to “Wazanzibari wakusanya saini ya kutaka kura ya maoni juu ya Muungano

 1. maalim hasan mzalendo ninakusikia facebook nimejifuta,mm shime wazanzibar tutimize sahihi milioni moja haraka iwezekanavyoo kwa muda wa wikiii tuu

 2. Inshaallah Waislam na Wazanzibari wote tujitahidi kujiandikisha katika fomu hizo kwa yule mwenye uchungu na nchi yake.

 3. Na sisi tulioko nje tutapataje hizo formu, Tuachiweeeeeeeeeeeeeeeeeeeee Tupumuweeeeeeeeeeeeeeeeeeee

 4. Naskia moja kati ya masharti ya kupata fomu ni kua na kitambulisho cha mzanzibari mkaazi wanaojua ebu watuambie ukweli.

  • @ Medy
   Ni kweli kabisa, na hii ni kwa7bu ZNZID ndio uthibitisho wetu, kuepusha kujiandisha mara zaidi ya moja na pia kuepusha wasioitakia kheri Znzbar kuzua mambo yao ya kipuuzi na mengineo.
   Zaidi wasiliana na Maamiri wetu Farid, Mselem, Azan n.k. kupata uhakika zaidi.

 5. @ Medy
  Ni kweli kabisa, na hii ni kwa7bu ZNZID ndio uthibitisho wetu, kuepusha kujiandisha mara zaidi ya moja na pia kuepusha wasioitakia kheri Znzbar kuzua mambo yao ya kipuuzi na mengineo.
  Zaidi wasiliana na Maamiri wetu Farid, Mselem, Azan n.k. kupata uhakika zaidi.

 6. Jamani tujitahidi kwa sababu ni rahisi tu unakwenda kwa wakala,mkutanoni au ofisi za UAMSHO au JUMUIYA YA MAIMAMU. Chukua Kitambulisho chako cha ukaazi kwa sababu namba ya kitambulisho inarikodiwa ili kuthibitisha kuwa walijitokeza kwenye madai haya ni Wazanzibar halisi kisheria.

  • Tunaomba Bi salma utuwekee soft copy ya hiyo form ili sisi tulioko mbali tudownload, baadae tutajaza halafu pia weka e-mail ya uamsho tutawatumia baada ya kuscan.
   Sisi Vitambulisho vyetu vya uzanzibari tunavyo pia huku.
   Pia tunawashauri uamsho wafunguwe website ili harakati zetu zieleweke ulimwenguni (Globaly)
   Mungu ibariki zanzibar, Mungu wabariki wazalendo wa Zanzibar

   • AHSANTE SANA NDUGU YANGU KATIKA IMAN UMESEMA MAMBO YA MSINGI HICHI NI KIPINDI CHA UTANDAWAZI WEBSITE OR MATUMIZI YA VYOMBO VYA HABAR NI VITU MUHIMU SANA NI LAZIMA UAMSHO WAANZISHE WEBSITE KAMA HAWANA UWEZO WASEME TU TUTAWACHANGIA UWAMSHO NDIO WAWAKILISHI WA WAZANZIBAR.

 7. Nashangazwa sana na viongozi wa serikali zote za znz na jamauhuri ya mungano wa tanzania,kwa kutaka michango,ridhaa na mawazo ya wananch kuhusu katiba ambayo inaendesha nchi 2 huru,zilizoungana kwa muda wa miaka 48 sasa, kwasabab mungano una kero na matatizo tofauti hata ya kimundo,kwamana hakuna ridha za wananch kuhusu kunganisha nchi mbili hizo,kwanini wasijadili na kuitisha kura ya maoni kuhusu mungano kwanza kuliko kutaka ridhaa za mawazo katiba vp iweje,hapa hakuna democrasia ya ukweli, sabab democrasia ni ya wa2,akiwa kiongoz au raia itende haki kote,iweje viongozi walowekwa na raia wawaamuru rai wao wanavyopenda wao ndo wafanye ivoivo, wanavyo taka raia hawasikilizwi, je hii ndio democrasia?

 8. Naunga mkono wazo kuwa na Mtandao. Hii itarahisisha mawasiliano hasa pale mkusanyiko ukipigwa marufuku.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s