ZLS kuzindua huduma za kisheria bure

Rais wa Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) Awadh Ali Said akiongea katika mkutano na waandishi wa habari kulia kwake ni Wakili wa kujitegemea Abdallah Juma na Mshika Fedha wa chama hicho, Mtaib Abdallah

CHAMA Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kimezindua mpango mpya wa utoaji wa huduma ya ushauri wa kisheria kwa watu wasio na uwezo wa kifedha. Mpango huo ni miongoni mwa huduma zinzoztolewa na chama hicho kwa wananchi wasio na uwezo ambao pamoja na mambo mengine pia utapunguza kwa kiasi kikubwa cha mizozo na msongamano wa kesi mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za watu wneye ulemavu Kikwajuni Mjini hapa, Rais wa chama hicho, Awadh Ali Said kwamba lengo la mpango huo ni kuwasaidia wananchi wasio na uwezo kifedha katika kupata ushauri wa kisheria.

Alisema pia utoaji wa huduma hiyo utapunguza kesi zinazokwenda mahakamani ambazo baadhi yao hazina ulazima wa kufikishwa mahakamani lakini kwa kuwa watu wamekosa kupata ushauri wa kisheria inakuwa vigumu kuelekezwa wakati ameshafika mahakamani na kufungua kesi.

Rais huyo ambaye pia ni Wakili Maarufu Zanzibar alisema miongoni mwa malengo yao ni kuwapa wananchi uwezo wa kujua hatua za  awali za kuepukana na matatizo ya kisheria kabla ya kufikisha shauri lao katika mahakama jambo ambalo litasaidia upunguzaji wa kesi ndani ya mahakama.

“Tunaamini kwamba tukiwapa wananchi ufahamu mzuri wa sheria basi jambo la kwanza tutapunguza kesi katika mahakama zetu” alisema Awadh na kuongeza kwamba huduma hiyo itaanza kutolewa wiki hii.

Alisema kupewa ushauri wa kisheria wananchi ni kuwajengea uelewa wa kupata haki za kisheria utakaotolewa bila kulipia gharama za mawakili kwa kuwa wameona ipo haja ya kuanzishwa huduma hiyo Zanzibar kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wananchi kushindwa kupata haki zao kwa kukosa mawakili lakini pia kwa kushindwa kuelewa sheria na hivyo hukosa haki zao.

Awadh alisema chini ya mpango huo watakaonufaika na elimu hiyo ni watu maalumu ambao ni makundi ya watu wote katika jamii wasiokuwa na uwezo wa kulipa gharama wanapohitaji msaada wa kisheria wanapodai haki zao mahakamani.

Aidha Wakili huyo alisema pamoja na watu wasiokuwa na uwezo kiuchumi, lakini watu wenye uwezo wa kifedha pia wanahitaji ushauri kama huo ili kujua hatua za awali za kuepukana na matatizo ya kisheria wanapoingia katika mikataba ambao mwisho wake husababisha migogoro.

“Wapo watu wana uwezo wa kifedha lakini kwa habati mbaya wanaingia katika kusaini mikataba mbali mbali na baadae mikataba hiyo huwa inasababisha migogoro na kufikishana mahakamani lakini kama wangekuwa wanapata ushauri kabla ya kwenda mahakamani basi ingekuwa vizuri sana kwa sababu wakati mwengine suala lako wala halipaswi kufikishwa katika mahakama ni suala la kumalizana huku huku nje lakini kwa kuwa hawajapata ushauri wa kisheria basi wanafikishana mahakamani na haya hapo mengi sana…” alisema Awadh

Alisema mpango huu umeanzishwa baada ya chama cha wanasheria Zanzibar kuridhika kwamba watu wasiokuwa na uwezo wa kulipia gharama za mawakili wakati mwingine wanaingia katika migogoro ya kisheria inayoweza kuepukwa kwa njia ya ushauri wa kitaalamu na hivyo kupunguza msongamano mahakamani.

Alisema hakuna jamii  inayopenda kuwa na mizozo mingi mahakamani, lakini kutokan ana kukosekana huduma kama hii ya bure watu wengine wameshindwa kupata ushauri lakini aliahidi utoaji wa huduma hiyo utakuwa endelevu na sio kwa kipindi fulani ili wananchi wapate kusaidiwa kisheria na kupata haki zao.

Alisema uzuiaji wa mizozo kwa njia ya ushauri ni muhimu kwa sababu wapo watu ndani ya makundi mbali mbali katika jamii, wakiweo wasomi ambao hawaelewi hatua zote za awali za kisheria zinazopaswa kuzingatiwa katika kudai haki zao na zile zinazohusu mikataba.

“Sisi tunaamini kwamba watu wengi na makundi mbali mbali yanahitaji ushauri wa kisheria wakiwemo wataalam wa nyanja mbali mbali mfano elimu, madakatari, wahandisi na hata wakulima na wafanyabiashara wanahitaji ushauri ili waweze kuepukana na matatizo ya kisheria, na hivyo basi tumezindua mpango huu kwa kuanzia ili tuone kama huduma hii watu wataipokea itasaidia katika masuala mengi ya kisheria kutatuliwa” alisema Wakili huyo.

Rais wa chama hicho alisema elimu kwa njia ya ushauri huo itakuwa inatolewa na mtaalam moja katika ofisi ya chama hicho mjini hapa kila Jumamosi kuanzia saa 4 hadi saa 7 mchana huko katika ofisi zao za Hoteli ya Bwawani lakini idadi itaongezeka kwa kadiri ya mahitaji lakini kwa kuanzia wataanza na mawakilsihi wachache.

“Tunavyotaka ni kuwa huduma hii iwe endelevu na kwa kuazia tulisema ni huduma ambayo tutaanzia hapa mjini lakini tunamaini tutapata watu kutoka mashamba kufuata huduma hii lakini tumepanga hata kufika vijijini na Pemba pia kwa siku za baadae” aliahidi.

Utoaji wa huduma hiyo hivi sasa unafanywa na taasisi ya kituo cha huduma za sheria Zanzibar kilcihaonzishwa na Marehemu Professa Haroub Othman ambapo Awadh alikubali kuwa kituo hicho kimefanya kazi kubwa ya kutoa huduma kwa umma katika suala la kisheria na kuwapa wananchi ushauri wa kisheria.

“Wenzetu wamefanya kazi kubwa sana na wamefanikiwa kuanzisha huduma hii kila mkoa, kwa hivyo na sisi tunaunga mkono juhudi hizo na tunaendeleza kwa lengo lile lile la kuwasaidia wananchi wasio na uwezo kupata ushauri wa kisheria katika masuala mbali mbali” aliongeza Wakili Awadh.

Alisema kwa kuwa walengwa ni watu wasio na uwezo idadi ya waelimishaji itaongezeka kwa kuzingatia idadi ya walengwa wataoajitokeza katika kupata ushauri wa masuala mbali mbali ya kisheria na kutoa wito watu kuitumia fursa hiyo ya bure kwani watakapewa huduma hiyo ni wale wasio na uwezo tu.

“Sisi tunawasisitiza wasio na uwezo kuja kujitokeza katika taasisi yetu kwa sababu lengo letu ni kuwaisaidia wasio na uwezo na vigezo ambavyo tutakavyovitumia ni kumtizama mtu mwenyewe ana uwezo au hana ikiwa hana basi tutampa ushauri lakini kama anao uwezo pia tutamshauri aende kwa taasisi zenye kutoa huduma hiyo ya kulipia” alisema.

Advertisements

4 responses to “ZLS kuzindua huduma za kisheria bure

  1. Pingback: ZLS kuzindua huduma za kisheria bure·

  2. mm ninawaomba muape ushauri wale walodhulumiwa ardhi na mashamba yao maana baba yangu anazungushwa miaaka chungu mzima kwa haki yake

  3. Kaka zetu hiyo safi sana, na katika hili tunaomba Wazanzibar wote tuwe tunapitapita kwenye hizi ofisi ili kupata mbinu muafaka za kuuvunja MUUNGANO huu magumashi.HAAAAATUUUUTAAAAAKIIII!.Vingwendu nyiye.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s