Kampuni ya bia yadhamini ligi kuu Zanzibar

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Grand Malt, wametia saini mkataba wa udhamini wa ligi kuu ya Zanzibar kwa msimu wa mwaka 2012/2013 hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Bwawani. Jumla ya Shilingi milioni 140 zitatumika katika udhamini huo wa miaka mitatu. Mgeni rasmi katika sherehe hyo alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk.

BAADA ya kilio cha muda mrefu, hatimaye Ligi Kuu ya Soka Zanzibar imepata mdhamini na sasa itajulikana kama, ‘Zanzibar Grand Malt Premier League’. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa udhamini huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Saidi Ali Mbarouk, alizitaka klabu zinazoshiriki Ligi Kuu Zanzibar, kusimamia na kuweka mbele suala la nidhamu, sambamba na kuepuka malumbano na migogoro isiyo na tija katika soka.

Mbarouk alisema kampuni ya kinywaji baridi kisicho na kilevi cha Grand Malt, imedhamini Ligi Kuu ya Zanzibar , kwa mkataba wa miaka mitatu, kwa gharama ya sh milioni 140, ukijikita katika suala la utoaji huduma katika usafiri, malazi, chakula na zawadi kwa klabu zitakazoshiriki ligi hiyo.

Katika hafla hiyo iliyowashirikisha viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ), Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), na wale wa klabu za soka, Waziri Mbarouk, alisema nidhamu ni nyenzo muhimu katika uendelezaji wa soka, kwa kuzingatia kuwa hakuna mdhamini atakayefurahia kudhamini ligi ambayo daima inakabiliwa na migogoro.

“Njia pekee ya kuwatia moyo wadhamini hawa, pamoja na wengine wenye azma ya kuidhamini ligi hii ni kudumisha nidhamu na kuepuka migogoro,” alisema.

Alisema wizara yake na serikali kwa jumla, itatoa kila aina ya ushirikiano, katika kufanikisha mchakato ulioanza wenye lengo la kulikomboa soka la Zanzibar kufikia katika maendeleo.

Hata hivyo aliiagiza BTMZ kuweka utaratibu madhubuti, kuona fedha zinazotolewa na wadhamini hao zinatumika kama zilivyokusudiwa, jambo ambalo litaepusha migogoro.

Katika hatua nyingine, Mbarouk alisisitiza msimamo wa serikali na wananchi kuwa kwa mujibu wa hulka na utamaduni wa watu wake, vinywaji vyenye kilevi havitaruhusiwa kudhamini michezo hapa nchini.

Alisema kuna kampuni nyingi zilikuwa na hamu kuona zinakuwa wadhamini wa michezo hapa Zanzibar kupitia pombe wanazotengeneza, lakini jambo hilo ni la muhali na haliwezekani kutokana na madili ya Kizanzibari.

Sambamba na hilo, alimpongeza Waziri Jihad (aliekuwa waziri wa wizara hiyo kabla yake), kwa juhudi kubwa aliyoifanya hadi kukamilika kwa mchakato wa kumpata mdhamini huyo.

Naye Msemaji wa ZFA, Munir Zakaria, alifafanua kuwa kati ya hizo sh milioni 140, milioni 34.8 ni za usafiri kwa klabu 12; na sh milioni 64.32 ni malazi na chakula kwa timu zote 12 zitakapokuwa nje ya vituo vyao.

Zakaria alisema, sh milioni 2 ni kwa ajili ya matayarisho ya viwanja, ambavyo ni Amaan Unguja na Gombani, Pemba, wakati sh milioni 18.5 ni kwa ajili ya zawadi, ambapo bingwa atalamba sh milioni 10, mshindi wa pili milioni 5, huku mfungaji bora akipata sh milioni 1 na sh milioni 1.5 zawadi kwa waandishi bora kutoka magazeti, redio na televisheni.

Mchanganuo mwingine ni shilingi milioni 1 kwa timu yenye nidhamu, milioni 20.38 ni za vifaa kwa timu zote, yaani jezi, viatu n.k, ambako bajeti ya ligi ilikuwa ni sh milioni 179 huku Grand Malt wakitoa milioni 140 sawa na asilimia 70 na wamesema milango iko wazi kwa wadhamini wengine wasiokuwa wapinzani wao wa kibiashara kumalizia sehemu iliyobaki, ambayo ni gharama za utawala na waamuzi.

Tanzania Daima

Advertisements

11 responses to “Kampuni ya bia yadhamini ligi kuu Zanzibar

 1. Huo ndio mwanzo na baadae kidogo tu wataambiwa mpaka wanywe ndio wasaidiwe ndi hao wanao jiida waislam wanadhaminiwa wa ulevi ule M/mungu anaoukataa.

 2. mkuu umetumwa uje kuandika maneno machafu na watanganyika chuma hulainishwa na girisi tumia hoja kuliko matusi au ukiwa usalama au mtanganyika uaweza kuvua nguo ukatembea kama ulivyo zaliwa tuwache tupumuwe na matusi yako jenga hoja sio matusi ili watu wakufahamu hata hao ccm zanzibar na sm,z watu wale wanakili na kuzipima hoja zako

 3. Jamani ama kweli ndege mjanja hunaswa na tundu bovu! Huu ndio mwanzo mwa kunyeshwa pombe! Jamani viongozi chonde chonde! Musilewe madaraka! Kampuni ni ya pombe hebu tuelewesheni hiyo grand malt ni nini? Musidanganye umma kampuni ya pombe haiyachi kutengeneza pombe. Hili ni jina kama ilivyo kilimanjaro, tursker, reds, mwisho tutengenezewa spice na viwanda vitajengwa hapa hapa. Ulevi ni haramu, na mapato ya ulevi ni haram vipi leo ZFAmuchukue pesa za wauza pombe? Tahadharini wazanzibar musijetiwa kwenye dema. Znz salama bila pombe inawezekana!

 4. Madhali ni kinywaji kisicho na kilevi kwanini tusikubali udhamini….musiwe munapinga kila kitu na kama tunasema ni company ya ulevi hata hiyo bajeti ya serikali nzima ni pesa kutoka msaada kutoka nchi za magharibi vp tuzikatae?

  • Iwe ni hivyo hivyo wanavyosema kwamba kinywaji hakileweshi, lakini jambo hili kiislamu huingia katika mlango wa ‘shaka’/shubha ambayo tuna wajibu wa kujiepusha na kinywaji hicho na kukitangaza/promote, kwa kuwa kampuni hii asili ya shughuli zake ni ulevi. Pia kumbuka haramu mbili hazifanyi halali, kwa kuwa tunapata misaada ya nchi za magharibi si hoja kama hili ni halali . Hoja ilikuwa iwe jee kwa udhati wa kitendo hiki ni halali au ni haramu? Mwisho kumbuka kwamba, mbali na ligi hii kutangaza kinywaji hicho pia itatangazwa kampuni ya TBL ambayo ni kampuni ya ulevi.
   Allah atuongoze njia iliyonyooka.

 5. UO NI ULEVI TUU NA SAID ALI MBARUK WE NDO MAS ULI KWA HILI KILA WAZIRI ALO KUJA ALIURUKA MTEGO HUO LAKINI WW UMENASA. O UNATAFUTA FADHILA KWA WATU USIFIWE KUA NI MTENDAJI LAKINI ELEWA KUA KUNA ALLAH

 6. Hatua hii ya Zanzibar iliyofika ni kutokana na kukosekana sera bora za uendeshaji mpira wa miguu. Jibu ni kuanza kufikiria kufanya mpira ni ajira na si huduma ya jamii

 7. kama hiyo ni pombe basi bakhresa naye anatengeza pombe mbona hamusemi malta hiyo na malta ya bakhresa ina tofauti gani

 8. tatizo lenu mumefika mahala hadi kufikiri hamuwezi tena kila kitu munapoliticize, kama ni kweli munajifanya wenye dini mungeacha kuchukua pesa za dhulma kwa kusingizia eti nyie ni wasomali!!

 9. hi si nchi ya kidini na katu haiwezi kuwa ni nchi ya kiislamu kwa taarifa zenu munapoteza muda bure kama kule muna uchungu na hii nchi yetu mungerudi basi na kuaachana na ukimbizi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s