Shukran kutoka kwa familia ya Dk Yussuf

Marehemu Dk Yussuf akiwa na familia yake picha hii amepiga akiwa katika hali yake kiafya imedhoofika, Tunamuomba Mwenyeenzi Mungu ampumzishe huko alipo katika mapumziko ya milele ambayo yenye faraja na amuuingize peponi inshallah

Sisi, ahli ya Dr Yussuf Saleh Salim, tunachukua fursa hii kukushukuruni nyote mliotuletea mkono wa pole pamoja na kumuombea dua marehemu mume wangu na baba yetu. Tunajua wengi wenu mtasema kuwa Dr Yussuf alikuwa wenu pia na hatuna haja ya kukushukuruni. Kadhalika tunaelewa jinsi mlivyojawa na huzuni kama tulivyo sisi. Mungu atatupa sote subra. Mauti hayazuiliki na kama Qur’an inavyosema: ‘Kullu nnafs dhaiqatul mawt,’ (Kila nafsi – yaani mtu -lazima atayaonja mauti.). Mungu amlaze pema marehemu na ampe kauli thabit, Amin.
Tunachukua fursa hii pia kukuhakikishieni kuwa siku zote Dr. Yussuf alikuwa akiienzi Zanzibar. Mapenzi yake juu ya nchi yake yalikuwa hayana mfano. Mpaka dakika za mwisho za uhai wake amekuwa akifuatiliya kwa karibu kabisa maendeleo ya matukio yatakayokuwa na athari na mustakabali wa nchi yake aliyoipenda kwa dhati ya moyo wake.

Wakati huo huo alifuzu kuitukuza vile vile aila yake. Sisi wanawe tunamkumbuka baba yetu kwa kutushaijisha katika masomo na kutupatia yale tunayoyahitajia. Mimi mkewe nimeishi na mume wangu kwa mapenzi makubwa kwa muda wa miaka mingi. Tumebarikiwa Nassor, Omar, Antar na Maryam. Nakuleteeni picha hii kama ukumbusho. Wale wanaomjua watamuona jinsi alivyodhoofika katika siku zake za mwisho.

Mungu atubariki sote, atuongoze katika njia ya haki na atupe moyo kama wa Marehemu wa kuipenda, kuienzi na kuipigania nchi yake.

Nadra Nassor
Nassor Yussuf
Omar Yussuf
Antar Yussuf
Maryam Yussuf

 

Advertisements

2 responses to “Shukran kutoka kwa familia ya Dk Yussuf

  1. Allah ampe kawli thabit, na ampe pepo ya juu. Inshallah na nyinyi musiache kumuombea duwa kwani ni katika hazina alizowacha hapa ulimwenguni.
    na sisi sote Allah atupe mwisho mwema (husni-l-khatima)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s