Utawala ng’ang’anizi na Muungano tata

 

wazanzibari wakiwa katika mhadhara unaoandaliwa na taasisi za dini kuzungumzia katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Na Jabir Idrissa

MUUNGANO wa Tanzania , zao lililopatikana baada ya kuunganishwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Jamhuri ya Tanganyika , unazidi kutikiswa. Ukiwa umeasisiwa tarehe 26 Aprili, 1964, hivyo leo 25 Aprili, kuwa siku ya mkesha wa maadhimisho yake ya miaka 48, Wazanzibari wanauombea dua “mbaya.”

Ni katika mkusanyiko ulioandaliwa na Jumuiya ya Uamsho, moja ya jumuiya za kiraia zilizo mstari wa mbele kuelimisha raia kuhusu haki zao, ambapo wataongoza sala na dua maalum kwenye uwanja wa wazi.

Waandaaji wanasema dua zilizotajwa zaidi ni dua ya kuombea Zanzibar izidi kuwa nchi ya amani, leo na siku za usoni; na irudi katika kuwa dola inayojitegemea.

Muungano umekuwa katika mjadala mpana Zanzibar tangu pale Rais Jakaya Kikwete alipotangaza nia ya kuanzisha utaratibu wa kupatikana kwa katiba mpya ya kwanza itakayoshirikisha maoni ya Watanzania.

Uamsho wanahamasisha watu watoke na kusema hawapo tayari kuchukuliwa mamlaka ya nchi yao Zanzibar na kwa hivyo hata katiba inayoandaliwa, haiwahusu, bali wanachotaka serikali yao, Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), kwanza iitishe kura ya maoni ili wananchi watamke kama wanataka au hawataki muungano.

Jambo hili limekuwa mtihani mkubwa kwa serikali katika kipindi hichi ambacho tayari tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba imeundwa, wajumbe wameapishwa na inatarajiwa kuanza rasmi kazi tarehe 2 Mei 2012.

Kuthibitisha namna serikali ilivyotishwa na hamasa zinazoenezwa na wahadhiri wa Uamsho dhidi ya muungano, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Balozi Seif Ali Idi, amekemea mwenendo huo.

Akifunga mkutano wa Baraza la Wawakilishi Ijumaa iliyopita, Balozi Seif alisema serikali haikusudii kuzuia mihadhara, bali haitakuwa tayari kuvumilia vikundi vinavyoeneza chuki na kutukana viongozi wa serikali.

Mara zote viongozi wa Uamsho wanajinasibu kuendesha mihadhara kwa mamlaka waliyopewa na Katiba ya Zanzibar yanayowapa haki ya kusema na kushiriki katika shughuli za uendeshaji wa nchi yao .

Ndani ya mitandao ya kijamii inayoongozwa na vijana wasomi wa Kizanzibari, kuna maoni yanayojengwa kwa lugha kali watoa maoni wakitaka muungano upitiwe upya na sasa wakiibua hoja ya kutaka kuwe na muungano wa mkataba badala ya muungano wa kikatiba uliopo sasa.

Kumekuwa na hoja hii Zanzibar kwamba muungano uliundwa kwa usiri mkubwa na hivyo kusababisha kumong’onyoa siku hadi siku mamlaka ya Zanzibar , yale yalikuwepo mara baada ya uhuru wa 10 Desemba 1963 ambapo Zanzibar ilipata kiti chake Umoja wa Mataifa na yalipofanyika mapinduzi 12 Januari 1964.

Wazanzibari walio wengi wamekuwa wakitaka muungano unaojali haki sawa kwa nchi mbili zilizoungana, na Zanzibar iachiwe mamlaka yake ya kufanya mahusiano na nchi za nje pamoja na kupata misaada kule itakako.

Pia wanasema wamechoshwa na mfumo wa muungano wa serikali mbili kwa msimamo kuwa umeinyonga Zanzibar kiasi cha kulazimika kupata idhini ya serikali ya muungano hata kwa yale mambo ambayo kwa asili hayapo chini ya muungano.

Hoja kuu kwao ni kwamba haiwezekani muungano ukaendelea kwa miaka yote 48 bila ya wananchi kupewa nafasi ya kuujadili na kuamua kama ungali na manufaa yaliyokusudiwa.

Kwa hivyo basi, nafasi ya muungano katika katiba mpya inayolengwa kupatikana ifikapo 2014, inachukuliwa kama jambo la msingi sana Zanzibar na wataalamu wa sheria wanaamini hilo ndilo jambo lililozaa katiba ya muungano.

Maana yake, wanasema, kulikuja kwanza muungano ndipo ukajumuishwa katika mfumo wa katiba ingawa, wanaeleza, utayarishaji wenyewe wa katiba ya jamhuri haukufuata sheria kulingana na makubaliano ya pande mbili.

Wanasheria, wakiwemo wale waliojumuika pamoja na kuanzisha asasi iitwayo Baraza la Katiba Zanzibar kwa ajili ya kuhamasisha watu Unguja na Pemba kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ndio hasa wanaojenga hoja ya kwamba sasa ni vema kuwe na muungano wa mkataba.

Awadh Ali Said, wakili maarufu Zanzibar , katika waraka aliowasilisha kwenye moja ya mijadala ya wazi hivi karibuni, amesema mkataba wa muungano ulitayarishwa na wanasheria wa Tanganyika kwa usiri mkubwa na katika zoezi lote hadi uliposainiwa, viongozi waandamizi wa serikali ya Zanzibar hawakushirikishwa.

Anasema hata mwanasheria mkuu wa serikali wakati ule, Wolfghang Dourado (amefariki dunia Machi mwaka huu), hakushirikishwa katika hatua yoyote ile.

Awadh ambaye ni mmoja wa wajumbe 15 kutoka Zanzibar walioteuliwa kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba, anasema kulingana na mfumo wa sheria uliofuatwa kuunda muungano, viongozi wakuu wa nchi mbili wana uwezo kisheria kuingia mikataba ya kimataifa.

Hata hivyo, anasema, mfumo huo unashurutisha kwamba mara baada viongozi hao wakuu kusaini mkataba, lazima mkataba huo uridhiwe na bunge la nchi husika na upitishiwe sheria ya ndani ndipo upate nguvu za kisheria.

Anasema, “… hata mkataba wenyewe wa muungano uliweka suala la kuridhia (Ratification) kuwa ni sharti moja la awali la mkataba (condition precedent. Wakati Tanganyika iliridhia mkataba na kutunga sheria rasmi ili kuupa nguvu na uhalali (kupitia Sheria Na. 22/1964), Zanzibar hadi leo hii haikuridhia mkataba.”

Ukweli huu, anasema Awadh, umebainishwa pia na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, rais wa pili wa Zanzibar , na magwiji wa sheria Dourado na Profesa Issa Shivji katika maandiko yao mbalimbali.

Hoja ya kutaka muungano wa usawa na maridhiano, ndiyo iliyosababisha Mwalimu Julius Nyerere, aliyekuwa rais wa jamhuri, amtake Mzee Jumbe ajiuzulu urais wa Zanzibar mwaka 1984 wakiwa vikaoni, mjini Dodoma .

Ipo katika kumbukumbu kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi (SMZ) aliieleza Mahakama Kuu kwamba SMZ haina mkataba halisi wa muungano.

Alitoa maelezo hayo mbele ya mahakama hiyo katika kesi Na. 20/2005 iliyofunguliwa na Rashid Salum Adi na wenzake tisa (G10) wakitaka serikali ioneshe nakala ya mkataba halisi wa muungano.

Badala yake, kilichopo tangu muungano ulipoasisiwa, ni sheria iliyoridhia mkataba ya Tanganyika , ndani yake kukiambatanishwa kinachodaiwa kuwa ndio mkataba ambacho ndicho hadi leo kinatumika kama ndio mkataba wa muungano. Hili linaleta maswali mengi yasiyojibiwa.

Kutojibiwa kwa utata kuhusu uhalali wa muungano, ndiko kulitarajiwa kuzindue viongozi wakuu wa taifa ili wawape Watanzania wa pande zote mbili nafasi ya kujadili na kutoa maamuzi kupitia maoni yao katika katiba inayolengwa kupatikana.

Hili pengine lisitimie kwa kuwa tayari Rais Kikwete “ameshatoa uamuzi” aliposema wananchi wapo huru kujadili namna ya kuimarisha muungano na siyo kujadili kama muungano uwepo au usiwepo.

Inawezekana tamko la Rais likachukuliwa kama ung’ang’anizi wa utawala kutaka muungano uendelee kuhojiwa hata sasa unapokaribia kutimiza robo karne ya uhai wake.

Advertisements

25 responses to “Utawala ng’ang’anizi na Muungano tata

 1. Huu ni utapeli wa kimataifa hata huyo Jk analijua hilo, wanajua kwa yakini leo ipigwe kura ya maoni watakataa muungano ni wengi! Nawatahadharisha wanasiasa uchwara wasiyojua wanayasema. Hebu tutathmini hizi kauli ati moja ya faida za muungano ati tani kwa tani za mbatata zinazokuja. Ni hoja za comedi na hadithi za paukwa pakawa ebu tuwaulize kwani hizo mbatata na bidhaa nyengine wanatupa bure? Cha ajabu mchele wa mbeya bei yake ni sawa na basmat ya bara hindi , vitunguu vya india kg1, ni 1500/= wakati vya tanganyika 3000/=. Hebu jiulize hivi india na tanganyika wapi mbali tafakari!. Wazanzibar tunayofursa ya kupata maendeleo bila tanganyika! Umoja busara na uvumilivu utatuvusha! Kuna bidhaa nyingi za nje znz ni rahisi kuliko tanganyika mfano gari na vifaa vya electronic . Ahsante pamoja tunaweza. Zanzibar yetu kwanza! Muungano uso na tija ni mzigo usio na ujira! Achana nao!

 2. Pingback: Anonymous·

 3. WAZANZIBAR HAKUNA KULALA MPAKA TUPATE UHURU WA ZANZIBAR-2012 KUTOKA MIKONONI MWA MAKAFIRI WEUSI WATANGANYIKA WAACHENI VIBARAKA WA TANGANYIKA WAUE NA WAWAFUNGE JELA WAZALENDO WA ZANZIBAR WALE WATAKAO BAKI WATASONGA MBELE KUDAI UHURU MPAKA TONE LA MWISHO LA DAMU. Vibaraka watahama wenyewe zanzibar.

  • hahahaaa wewe ndio umethibitisha kabisa kuwa wewe ni mwarabu mbaguzi kabisa ndio maana mnataka kurudi kuwatawala weusi wa zanzibar, yaani tusi la mwarabu ni rangi kenge wewe wa jangwani,

  • mzee hata km maneno alotumia si mazuri lakini kw swala la wazanzibar tuko bara hatubugudhiwi huo ni uongo wabongo kila siku wanawatukana wazanzibar huku tena live wazanzibar hawana raha wakipanda madaladala cha mwisho zaidi wabongo watuekti cc tunawambia kila mtu huringa kwao wakiwepo zanzibar hatutawaacha na wao tutawatukana km wao wanavotutukana kwao

  • Mbwa wewe shika adabu yako. Unahamu ya kufirwa basi nitakufira. Nchi yetu muitawale halafu muletee jeuri. WATANGANYIKA WOTE KIMA PUNJU. WAZANZIBAR TUNATAKA UHURU WETU MIKUNDU MEUSI YA TANGANYIKA NI LAZIMA WALIJUE HILI.

 4. Nahisi wewe ni sultani khofu. Naomba utafakari hizi kauli zetu! Kuna tofauti baina ya kuvunja muungano na kufukuzwa wa tanganyika. Hapa kinachodaiwa ni mamlaka ya zanzibar katika ulimwengu wa kimataifa! Hatutaki kuamuliwa na wa tanganyika kwani mahitaji yetu ni tofauti , utamaduni wetu haufanani hata silka zetu hazipamoja. Kuhusu biashara wale wazanzibar walipo kenya, msumbiji, angola, malawi, afrika ya kusini, uganda, comoro, somalia ,bara zima la asia pamoja na europa kule ni kwao . Usiwe na hoja mgando! Sisi hata nyinyi wabara mukitufukuza tutaathirika lkn baada ya muda tutakuwa sawa tu kwani hakuna aliyezaliwa nacho! Tafakari zanzibar yetu kwanza!

 5. KUMAMAMAYO MIAKA LAKI 6. Jee unataka kufirwa KAFIRI WA TANGANYIKA WEWE. Tunakwambia na wambie MAKAFIRI WEUSI WENZIO KUWA WAZANZIBAR TUNATAKA UHURU NA TUTAUPATA UHURU WA ZANZIBAR KUTOKA MIKONONI MWA KIMA PUNJU WA TANGANYIKA KWA NJIA YA KUMWAGA DAM TU. Di halali dam ya kafiri kwa muislam mfirwa wewe nitakufira tu kijusi kafiri wewe.

  • Kama leo unasema makafiri weusi. Kesho utasema wazanzibari weusi. Tutakwenda hivyo? mbona mnaanza kututisha? Tutakuja kubaguana kama wanavyobaguana sasa Sudan ya Kusini. Na Zanzibar itakuwa wazanzibari weupe na wazanzibari weusi. Ni balaa.
   Moderator pana haja ya kuhariri baadhi ya maoni yetu tunayotoa

   • Wewe kibaraka watanganyika WAZANZIBAR TUNAHASIRA NYAMAZA TU. Niwatukane watanganyika kwa kuifanya nchi yetu koloni lao. Narudia kusema WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WEUSI WA TANGANYIKA. Kama kama na wewe mtanganyika ujumbe wa juu unakugusa.

 6. mm ninawaomba wazanzibar wenzangu tujenge hoja zaid kuliko kutukanana hapa husoma watu tofauti mama zetu baba zetu hata haoo kina kificho sef aliy idy na viongozi mbali mbali na wao watu wale akikuta hoja ataizingatia na atapunguwa makali na jazba moyoni mwake lakini ukimimina mitusi yako hapa hata hajasoma amesha katika na kupandisha jazba zakee CHUMA HULAINIKA KWA GIRISI SASA TIZAMA WEPESI WA GIRISI ZINGATIA MZANZIBAR

 7. UKOMBOZI HAUWEZI KUFANYWA KWA MATUSI NA LUGHA CHAFU.. NI VYEMA TUKAWA TUNAJENGA HOJA ILI HAWA JIRANI ZETU WAKAELEWA NINI HASA TUNACHOKIDAI. NNA WASIWASI MKUBWA KUA HUMU KUNA WATU WANATUMIWA KULETA HIZI LUGHA ZA MATUSI ILI KUYUMBISHA (DERAIL) MALENGO YETU YA UKOMBOZI NA KUFANYA BARAZA HII IONEKANE YA WAHUNI. TUACHENI LUGHA CHAFU. SISI LENGO LETU NI ZANZIBAR KUA NA SERIKALI YAKE YENYE MAMLAKA KAMILI NA HAKUNA AJENDA AMBAYO WASIOUTAKIA MEMA UKOMBOZI WANAZITOA ZA KUWAFUKUZA WATU WA TANGANYIKA. TUNACHOTAKA NI UHURU WA ZANZIBAR ULIOPORWA NA TANGANYIKA TAREHE 26 APRIL 1964.

 8. Huu mtindo wa kutajiana eti Muungano ukivunjika wazanzibari wanaofanya biashara Kariakoo watayafanyaje maghorofa yao ?. Wewe kiongozi unasema maneno ya aibu kiasi hiki ! Jamani nani asiyejua kuwa kuna sheria za uhamiaji katika nchi yeyote ile Duniani? Mimi nimewaona Wachina na wasomali wengi tu na hata kufanya biashara nao ya mapazia hapo hapo kariakoo Je! Wale ni Watanganyika ? Hii maana yake ni kwamba wanaishi Tanganyika kwa kufuata sheria za uhamiaji zilizopo Tanganyika, na Muungano (MDUNDANO) ukikatika Wazanzibari watakaotaka kubaki na kuendelea kufanya biashara watafuata sheria hizo za ugenini kama wanavyofanya wageni wenzao. Na kama wakifukuzwa kwa ugeni wao na sisi tutafurahi sana kwani tutapata uhalali wa kuwaondosha wauza uchi,pombe,wala nguruwe na majambazi wanaojipendeza kwenye SMZ kwa vigezo vya uaskofu eti iwatambue lakini wanafikiri na huku watapata (MoU) MEMORANDUM OF UNDERSTANDING ili wapewe pesa za wizi kama bara hapa yagujuu!

  • Hasa nakuunga mkono , umahiri wa kutumia akili , busara, na maarifa! Yatatuvusha! Tuache matusi na jazba! Kuhusu sudan ! Ndugu yangu kumbuka zanzibar si sudan ya kusini! Lakini kwa indhari tu wazanzibar tusibaguane! Zanzibar ni nchi tokea wakati wa nabii suleiman katika jamhur iliyokuwa na nguvu mno ya saba. Wakati huo pemba ikiitwa Qumbalu na Unguja ikiitwa lunjanyu(balad el zenj). Sudan ya kusin ni taifa changa zaid duniani . Zanzibar ni taifa kongwe sana kulikoni tanganyika taifa lilipatikana kwa kinyang’anyiro cha afrika(1884-1885). Watanganyika hawana la kujivunia mbele yetu zanzibar! Labda wizi na utapeli! ZBC muache kututilia khutba za kizushi za mzazibar na wazanzibar ss nyerere si mtume wala hana thamani yeyote kwetu. ALLAH ILINDE ZANZIBAR MAHASADI WATOKE NDANI! Amin

  • Kwa kweli moderator. Tuekee wazi sheria za hapa kwenye blog! Tupo tulio naheshima! Tusipafanye hapa ni sehemu ya matusi! Hii ni hatari mno kuna wengi wanataka kushiriki hapa lakini wanashidwa. Tujirebishe! Sisi ni waislamu! Ahsante!

 9. nguvu na umoja wa wazanzibar ndio itakayotetea nchi yetu kwa hiyo jamani tujitahidini kujenga hoja tusiwe tunatoa matusi hata kam mtu anajazba kwanza azipunguze ili tuweze kueleweka tunataka nini

 10. tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba imeundwa, wajumbe wameapishwa na inatarajiwa kuanza rasmi kazi tarehe 2 Mei 2012. SUALI TUME INA WAJUMBE 34 MIKOWA 32 UKIWACHA MIKOWAYA ZANZIBAR 5 TANZANIA INA WATU MILIYONI 38 AU ZAIDI NIKWELI ITAKUWA ABILIFU KUWAPA WATU HAKI ZAO
  AU NDIYO MSEMO WA KISHWAHLI FUNIKA KAWA MWANA HARAMU APITEEEEEEEEE
  WEWE ULOKULA KIYAPO UTAULIZWA SIKU IKIFIKA
  NA UJUWE KWAMBA IKIWA HAKI HAIKUFANWIKA
  WA ZANZIBAR TUTAHUWA HATUJA SAMEHE
  ELEWA KILA CHE…MWANZO NA MWISHU
  UPOOOOOOOOOOOOOO

 11. vijana wenzangu wazanzibari wenzangu naomba tuacheni matusi najua inatuuma sana lakini matusi hayafai tutakuwa tunabeba dhambi za bure, admin wa Zenjibarza naomba usi approve comment zenye matusi usizi moderate.

 12. LAINISHA CHUMA KWA GIRISI SIO KWA MCHANGA NDIO UTAFANIKIWA,ILA MUNGU KILA MTU KAMPA AKILI NA KILA NAFSI INAJIISABU SISI TUNAIMANI WALE WOTE WANAOTUKANA HUMU NI USALAMA WA TAIFA ILI KUTAKA KUTOWA WATU NJE YA MADA AU WAHAFIDHINA AU NDI VIBARAKA WENYEWE AU NDIO WATANGANYIKA CHUKI NA HUSDA NDIO ZAO WAZANZIBAR WALE WENYE KUJENGA HOJA MAANA NDIO TUNAO ONEWAA ALIYEKUWA MAMLUKI AU MUHADIM ATUWACHE TUPUMUWE KWA AMANI NA MUSTAREHE TUPUMUWE NA ZANZIBAR YETU PIA NA MATUSI YAKE ATUWACHE TUPUMUWEE

 13. Asalamu Alaykum. Kwanza napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa niaba ya mtandao wangu huu wa zanzibaryetu kwa kutoa maoni yenu mbali mbali na kuchangia katika mtandao huu lakini katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na wachangiaji wamekuwa wakifanya makusudi kuandika lugha za matusi kebeki na dharau dhidi ya wengine na nimechukua jitihada mbali mbali za kuweza kuwasiliana nao kwa njia za kistaarabu na kidiplomasia kwa kuwaandikia pembeni kwamba wanachofanya sio haki, sio ustaarabu na wala sio sahihi kwa sababu mbali ya kwenda kinyume na maadili ya kiislamu ambayo wazanzibari asilimia 99 ni dini yetu tunayoifuata lakini pia sio maadili ya kizanzibari na wala kitanzania kwa hivyo kinachofanyika ni ukosefu wa nidhamu, mtandao huu upo huru kupokea maoni na michango mbali mbali lakini hatuwezi kuvumilia kuona heshima inavyunjwa hali ya kuwa tumenyamaza kwa hivyo ninachoomba kwa mara nyengine tena mtu ambaye anakhisi hawezi kuzuwia jazba zake au hawezi kuchangia mpaka atukane ajizuwia kuchangia katika mtandao huu, nalazimika kusema hivyo kutokana na kuwa siwezi tena kuvumilia matusi na lugha zinazotumika katika mtandao huu ambao unasomwa na watu wenye heshima zao na watu ambao wanahitaji hoja na sio matusi. Natanguliza Shukran. kwa niaba ya zanzibaryetu mimi Salma Said nasema nakuombeni sana maoni na michango iwe kwa kutumia lugha nzuri na sio matusi, kejeli au dharau tafadhalini sana

 14. NNA WASIWASI NA HUYU MALIKI SIO GENUINELY WA KWETU ILA ANATUMILIWA NA WATU WENYE NIA MBAYA NA ZANZIBAR NA HUU MTANDAO ILI KUUONDOLEA HESHIMA NA HADHI YAKE. KAMA KWELI ANA NIA NZURI BAADA YA NASAHA ZOTE ZA ADMINISTRATOR KUA MATUSI YAACHWE BADO ANAENDELEA NA MATUSI. TUWE MACHO NA WATU KAMA HAWA AMBAO WANATAKA KUTUMIA JUKWAA HILI KUTUGAWA KAMA KWAMBA SISI WAZANZIBARI HATUWATAKI NDUGU ZETU WENYE ASILI YA TANGANYIKA JAMBO AMBALO HALIPO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s