Muwaza wataka kesi ya wapinga Muungano ifutwe

Wananchi wakiwa katika mhadhara ulioandaliwa na taasisi za kiislamu katika harakati za kuhamasisha wananchi watoe maoni yao juu ya kuutaka au kuukataa Muungano jambo ambalo linapigwa na serikali na kutakiwa wasubiri kutoa maoni yao katika tume iliyoundwa na Rais Kikwete

MUWAZA inasikitishwa zaidi kuona kuna baadhi ya Viongozi wetu wa juu katika Serikali wakitowa kauli za vitisho kwa Viongozi wa dini na vikundi mbali mbali vinavyo vinawaelimisha Wananchi udhalimu wa huo unaoitwa eti Muungano ambayo ni haki yao kufanya hivyo maana huo unaoitwa Muungano haukutoka mbiguni kwa Mwenyezi Mungu ila umeanzishwa kwa mabavu na watu wawili waliojifungia kwa siri bila ya ridhaa ya Wananchi wa pande mbili ya Tanganyika na Zanzibar ambao tokea awali umeonesha kuwa hauna nia njema wala maslahi ya Wananchi ila una maslahi kwa Viongozi wachache waliopo madarakani.

YAH: UDHALILISHAJI WANAOFANYIWA WANANCHI KWA KISINGIZIO CHA KUULINDA MUUNGANO

Kwa heshima tafadhali husika na mada ya hapo juu.

Itakumbukwa hivi karibuni kumeanzishwa Tume ya kuratibu maoni juu ya katiba mpya ambayo imezinduliwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano ambayo inatarajiwa kufanya kazi zake wakati wowote kuanzia sasa. Kwa upande wa Zanzibar, wapo Wananchi wengi ambao wanaonelea kuwa kwanza ifanyike kura ya maoni kwa kuulizwa kama wanautaka au hawautaki huo unaoitwa eti Muungano na ikiwa kama watakubaliana na hilo ndio ufanyike huo mchakato wa kukusanya maoni juu ya katiba mpya.

Hakuna asiyejuwa ukiwemo na wewe kuwa huo unaoitwa Muungano umeanzishwa kimabavu na Madikteta wawili ambao ni Karume na Nyerere bila ya ridhaa za Wananchi wa pande mbili yaani Tanganyika na Zanzibar na kusababisha kuipora Zanzibar kila kilicho chake kutoka Uraia, Uchumi, Siasa … n.k.

Hivi karibuni tumeshuhudia udhalilishaji mkubwa unaofanywa ma Jeshi la Polisi kwa vikundi mbali mbali ambavyo vimeonesha hisia zao za kupinga UKOLONI WA KITANGANYIKA katika ardhi za Zanzibar kwa kisingizio cha kuwa eti wanaupinga huo unaoitwa Muungano.

MUWAZA inasikitishwa zaidi kuona kuna baadhi ya Viongozi wetu wa juu katika Serikali wakitowa kauli za vitisho kwa Viongozi wa dini na vikundi mbali mbali vinavyo vinawaelimisha Wananchi udhalimu wa huo unaoitwa eti Muungano ambayo ni haki yao kufanya hivyo maana huo unaoitwa Muungano haukutoka mbiguni kwa Mwenyezi Mungu ila umeanzishwa kwa mabavu na watu wawili waliojifungia kwa siri bila ya ridhaa ya Wananchi wa pande mbili ya Tanganyika na Zanzibar ambao tokea awali umeonesha kuwa hauna nia njema wala maslahi ya Wananchi ila una maslahi kwa Viongozi wachache waliopo madarakani.

Kutokana na hayo, Jumuiya ya MUWAZA inakuomba kuliingilia kati suala hili haraka kwa kuwaadhibu Viongozi wako wanaotowa kauli za vitisho kwa Wananchi wa Zanzibar ili tusiweze kuridishwa huko tulikotoka ambapo hatupataki kurudi. Pia, MUWAZA inakuomba kuwa Wananchi wote waliokamatwa kwenye Viwanja vya Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kuonesha hisia zao juu ya huo Muungano wafutiwe kesi zao mara moja kwani tunaamini walilolifanya ni haki yao ya kupinga kitu ambacho kinawadhalilisha kwa miaka mingi.

MUWAZA inatarajia barua hii utaipa mashirikiano makubwa

Tunakutakia kila la kheri

KATIBU
Jumuiya ya MUWAZA
UK

Nakala: Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – UK
Balozi wa Kenya – UK
Balozi wa Rwanda – UK
Balozi wa Uganda – UK

Advertisements

6 responses to “Muwaza wataka kesi ya wapinga Muungano ifutwe

 1. Pingback: Muwaza wataka kesi ya wapinga Muungano ifutwe·

 2. MUWAZA mnachotakiwa pamoja na hili la kufutwa kesi lakini pia mufanye maandamano ili kutuunga mkono hukohuko mliko hio itasaidia kwa kiasi kiukubwa kupressurise hawa mabeberu wa SMZ na Tanganyika.

  • Hii ni fikra nzuri na inabidi kuangaliwa kwa ushirikiano na jumuia nyengine za Kizanzibari kama vile Zawa kwa Uingereza na zile zilizoko katika sehemu mbali mbali duniani.

 3. AHSANTENI SANA WAZALENDO WA ZANZIBAR. Umoja ni nguvu na utengano ni UDHAIFU. WAZANZIBAR TUZIDISHE KASI YA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR. Ni lazima tujue kua katika kudai UHURU ni lazima kutokee vifo na majeruhi kufungwa jela laki ni watakao bakia wasonge mbele kudai UHURU WA ZANZIBAR. Pia, tusiache kutumia njia za mitandao kusambaza sms zinazohamasisha wazanzibar kuungana kudai UHURU WA ZANZIBAR. Tukilegeza kamba tu ya kudai UHURU basi VIBARAKA WA TANGANYIKA WATAPATA NGUVU.

 4. ORODHA YA WATU WANAO UTAKA MUUNGANO ZANZIBAR-
  Haitimii hata watu mia mbili katika watu milioni mbili na laki tano

 5. Nyinyi Viongozi wetu wapenzi (SMZ) hata mkijipendekeza vipi kwa Watanganyika ukitoa waislamu basi hawakupendeni hata kidogo, na hapa tulipofikishwa ni kwa sababu ya Uislamu wetu mkikubali ni hivyo mkikataa ni hivyo. Itakumbukwa kuwa chama cha AA kisha ni TAA halafu TANU kilianzishwa na Ndugu zenu wa Kiislama mnaoju au si kweli? Tena masikini ktk kipindi kigumu na hatari sana cha ukoloni wakiwemo kina Tewa,Bibi Titi Moh’d, Mzee Bilali Waikela (huyu ingawa alijitahidi sana ktk mapambano dhidi ya ukoloni lakini Nyerere alimfunga jela kutokana msimamo wake katika kuwatetea waislamu na Uislamu wake. Huyu pia aliwahi kumwambia Mzee wetu Karume kuwa “Karume ndugu yangu angalia wanakutumia hao [kina-Nyerere] “Mzee Karume hakufurahi. Lakini masikini Mzee Karume bila ya kujua siri ya ndani, alihudhuria kikao cha mjini Iringa na kutu khotuba kali akiishutu EAMWS-East Africa Muslim Walfare Society, eti ni adui mkubwa ASP na TANU halafu tena Nyerere akifuta na waumiza waislamu leo.),Mzee Mshume Kiate n.k
  Lakini Je nafasi ya Waislamu katika Tanganyika mnaiona leo ilivyo? kila nafasi serikalini imekamatwa na mkatoliki nafasi za elimu wanaonufaika ni wakatoliki tu, sisi hapa kwetu hatukutakeni nyinyi mubaguwe lakini muwajue na mchukue hatua madhubuti maana haya wao ni maradhi yao. Kama hamsadiki basi mtatuangamiza sote na sisi tutadai haki yetu mbele ya Mungu maana nyinyi waislamu halisi. Amkeni viongozi wetu sisi tunakupendeni na tuko nyuma yenu mpaka mtufikishe pahala pazuri maana tumevamiwa. Kwa hamkumuona Mzee Karume alimfokea Nyerere kwenye Arusha Declaration ? Haya kama nyinyi mnabusara kuliko Mzee Karume haya twende, maana sisi tunaona aibu tenaa mambo yalipofika jamaa aah!.

  Serelly.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s