Viongozi wa dini, wanasiasa, polisi na serikali wakutana

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar, Abubakar khamis Bakari akifafanua jambo katika mkutano na Baadhi ya Masheikh wa Jumuia za mbali mbali Kiislamu za Kiislam kuhusiana na mchakato wa Katiba mpya na Mihadhara inayofanywa sehemu tofauti Unguja na Pemba. Kulia yake ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed na kushoto yake ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji.

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imewataka wanaharakati wanaoendesha mihadhara ya kutoa elimu kwa umma juu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuata taratibu na sheria za nchi.

 

Kauli hiyo imetolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed,katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi ulipo Kikwajuni mjini hapa mara baada ya kumalizika kikao cha makubaliano baina ya serikali na taasisi za kidini.

 

Kikao hicho kimeajumuisha viongozi wa dini ya kiislamu wanaoendesha mihadhara kuzungumzia suala la Muungano, wanasiasa na jeshi la polisi ambapo kwa Aboud alisema serikali ina maelewano mazuri na haina ugomvi wa aina yeyote na taasisi za kidini na kuwashauri kutumia busara na sheria za nchi.

 

Serikali imesema imelazimika kukutana na viongozi hao wa kidini kufuatia siku za hivi karibuni kuwepo kwa makundi mbali mbali yenye mitazamo tofauti na kuzungumzia hisia kali dhidi ya Muungano wa Tanzania, ambapo baadhi ya viongozi hao wa kidini hutumia lugha kali na kuwahamasisha wananchi kuukataa Muungano ulioopo jambo ambalo serikali imesema kusiwepo mawazo ya kuvunja Muungano.

 

Alisema serikali haizuii watu, taasisi ama jumuiya kutoa maoni na mitazamo yao dhidi ya Muungano, lakini ni vyema msingi ya sheria za nchi ikafuatwa kwa lengo la kuwafanya wananchi wa Zanzibar waendelee kufaidi matunda ya amani na utulivu uliopo badala ya kuwashawishi na kuwahamasisha katika kuleta fujo zitakazogharimu maisha ya watu na kuwataka viongozi hao wasiwe sababu ya kuleta vurugu

 

Waziri huyo alivitahadharisha vikundi na jumuiya za kidini kwa kuzieleza kuwa serikali haitokubali na wala kuwafumbia macho watu ama vikundi vya watu vyenye kutumia mwanya wa utoaji maoni yao huku wakivunja sheria za nchi. Kwa kisingizio hicho.

 

Serikali haina tatizo na na kupokea maoni kwani ina nia njema ya kusikiliza maoni ya wananchi na kuyafanyikazi, ila maoni hayo yasikiuke sheria za nchi wakati yanapotolewa”, alisisitiza Aboud.

 

Alisema serikali inafahamu lengo za wanaharakati wa jumuiya za kidini kutafuta maslahi ya Wazanzibari na kuiweka nchi katika hali ya heshima, lakini alisisitiza kuwa hayo yote yataweza kupatikana wakati wa kutoa maoni ya katiba mpya utakapofika.

 

Waziri huyo aliwaeleza wanaharakati hao wa kidini kuwa, wakati umefika wa kuwa na kauli moja, baina yao na serikali hali ambayo haitawaweka wananchi katika mivutano ya kimawazo na kushindwa kufanya maamuzi sahihi.

 

Waziri wa Katiba na Sheria, Abubakari Khamis Bakari, alisema suala la kuwaambia wananchi kuwa waukatae Muungano wa sasa sio muhimu bali lililo muhimu kwa sasa ni kusema wanataka Muungano wa aina gani na kero zilizopo zitatuliwe vipi.

 

Kwa sasa kusema hamtaki Muungano sio ‘issue’, lakini ‘issue’ ni kutoa maoni jinsi gani kero zilizopo zitatuliwe na yale yaliokuwa hayafai yaondolewe katika orodha ya mambo ya Muungano” alisema Bakari.

 

Alisema huu si wakati wa kuvisikiliza vishawishi ambavyo vimekuwa na lengo la kuchafua amani na utulivu iliyopo kwa maslahi yao na pia kukataa kurubuni kwani Zanzibar ni ya wananchi wote.

 

Naibu Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Sheikh Azzan Khalid Hamdan, akizungumza katika kikao hicho aliishauri serikali iache kuyafanyia kazi mambo ya fununu na wachunguze kwa umakini kinachozungumzwa katika majukwaa na kutafanyia kazi.

 

Mimi naishauri serikali ichunguze kile tunachozungumza katika majukwaa yetu halafu ndio itoe taarifa lakini ikiwa inachukuwa maneno na tetesi hapo mtakuwa hamtutendei haki” alisema Sheikh Azzan.

 

Sheikh Azzan alisema jumuiya yake ni miongoni mwa mwa taasisi zinazofuata sheria za nchi na pia kuheshimu misingi ya demokrasia iliyopo hivyo wanachofanya katika mihadhara yao ni kutimiza haki yao ya kidemokrasia na sio kuchochea wafuasi kufanya fujo na kuchochea uvunjifu wa amani kama inavyodaiwa.

 

Naye Sheikh, Mselem Ali Mselem alisema mihadhara yao yote inalenga kutoa elimu kwa umma na sio kweli kama wanachochea watu kuhatarisha amani iliyopo kama inavyodaiwa na wapotoshaji.

 

Alisema wanachokihubiri katika majukwaa yao ni kuhamasisha umoja na kuzungumzia madhila na ugumu uliopo katika Muungano na kuwataka wananchi kufahamu matatizo yaliyopo jambo ambalo ni haki kwa kila mwananchi kufahamu hilo.

 

Mwanazuoni huyo alisema wao kama raia wana nafasi kubwa kuzungumza matatizo na kuisimamia dini ya kiislamu katika maamrisho yanayotakiwa na lengo lao ni uislamu na sio kuugawa uislamu.

 

Akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema maoni ya wananchi ni lazima yaheshimiwe kwani wananchi wana madai yao ya msingi katika suala zima la Muungano huu ambao umedumu kwa miaka 48 lakini umekuwa na malalamiko ya muda mrefu na hakuna hatua zinazochukuliwa za kumaliza kero hizo.

 

Akizungumza kwa upande wanasiasa, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Ismail Jussa Ladhu tatizo linalowakabili wanasiasa ni kutokuwa na kauli moja juu ya Muungano na hivyo kuomba iwepo kauli hiyo ya serikali ili irahisishe kuwahamasisha wananchi.

 

Jussa ambaye ni Mwakilishi wa Mji Mkongwe alisema Muungano una kasoro nyingi na kutaliwa kwake kumekuwa kukiwapa shida wananchi sana jambo ambalo limekuwa likizungumzwa hadharani na sio siri tena.

 

Jussa alisema kufuatia tatizo hilo wananchi hivi sasa wamepoteza imani na serikali zao kwa kuamini kwamba matatizo yaliyopo hayawezi tena kutatuliwa kwa njia za vikao kwa kuwa kero hizo zipo kwa takriban miaka yote ya 48 ya kuungana nchi hizi mbili hadi leo hakuna lililotatuliwa na kuwaridhisha wananchi wa pande mbili hizo.

 

Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai aliitaka serikali ikutane katika Baraza la Mapinduzi na watoe kauli moja juu ya Muungano.

 

Naibu huyo alisema Muungano umeleta faida kubwa lakini unakabiliwa na kasoro kadhaa, hivyo ni vyema mazungumzo yakafanyika kwani hakuna lisilowezekana.

 

Alisema zipo dhana kwa Wazanzibari wengi kuwa Bara inafaidika na Muungano kwa jiji la Dar es Salaam kuendelea, lakini mikoani na vijijini mambo yamekuwa sana na kusema afadhali ya Zanzibar maisha kuliko baadhi ya mikoa ya Tanzania Bara.

 

12 responses to “Viongozi wa dini, wanasiasa, polisi na serikali wakutana

 1. Uamsho wamealikwa? Tunahitaji zanzibar yetu kwani muungano ni lazima nashangaa watu baada ya kuabudu Mungu wanaabudu muungano au bila muungano hakuna zenjibar?

 2. Pingback: Viongozi wa dini, wanasiasa, polisi na serikali wakutana·

 3. haya tenaa aboubakr unasemajeee sasa ikwa wazanzibar wanataka waseme mfumo gani wanautaka semeni na myuowe muongozoo bilal ful nyiee wazanzibar hatutaki muunganoo

  • Nadhani kila kitu kinataka hekma, jazba haziwezi kujenga. Inabidi unapopigania kitu chochote utathmini probabilitie na pia ukipima jee mbele kutakuwaje. Tuache kufikiria vitu kijuujuu tuu. Na hasa sisi ni waislamu katika vitu ambavyo Allah amevisisitiza ni strategy (mipango). Hebu tuangalieni Sulhu ya hudaibia then tutaweza kujifunza mengi sana. Kwa mfano Omar (Ra) alikuwa anaangalia pale alipo tuu ila Mtume (SAW) alikuwa anaangalia mbele zaidi.
   Sasa na sisi wazanzibari inabidi pia tuangalie mbele zaidi. Tunatakiwa tuupime huu upepo pando zote.
   1. Kwa mfano jee ni rahisi kama tunavofikiria kuwa tunaweza kuuvunja muungano kirahisi rahisi tuu (Is it feasible).
   2. Jee kwenye mchakato wa katiba mpya tunaweza kupata nini? a) serikali tatu????
   Kama tunaweza kushinikiza tukapata serikali tatu, jee hiyo haiwezi kuwa njia ya huko baadae kuweza kudai (demand) na mengine????
   3. Kama tutashinikiza kuvunja muungano sasa hivi, na tukawakataza watu wasishiriki kwenye kutoa maoni, jee tutapata nini???? bila shaka tutabaki na hali yetu ya saivi au hali mbaya kuliko ya saivi.
   4. Jee hali hii na hali ya kuwa na serikali tatu bora ipi?????

   Mimi simlaumu Abubakar wala maalim seif wala Balozi seif iddi wala Rais shein,
   Strategically, hawatakiwi waoneshe msimamo wao sasa hivi. najuwa wote muungano hawautaki ila they should not show their face currently. kutokana na mfumo wa siasa za Tanzania ambazo maamuzi yote yanatoka Tanganyika. Naomba murudie jinsi tulipokuwa tunataka kupiga kura ya maoni kuhusu GNU, muliwaona watanganyika walivotuandama???
   Ila pia Uamsho na Taasisi nyengine bado wanahitajika kutowa shinikizo (pressure)
   kwa umakini wa hali ya juu, ili viongozi wetu waweze kujitetea kuonesha kweli ZNZ kuna pressure watu wanataka nini!!!
   Wakatabahu: abaazanzibar@hotmail.com

 4. MZANZIBAR ELEWA BILA YA KUVUNJIKA MUUNGANO WA TANZANIA BASI ZANZIBAR HAITAENDELEA MILELE KWANI WATANGANYIKA KUPITIA TRA WANAHAMISHA MALI ZOTE ZA ZANZIBAR NA KUPELEKA BARA. VILE VILE MZANZIBAR TUMIA MALI NA HALI YAKO KUUDAI UHURU WA ZANZIBAR KWA NI MUAKILISHI UNAEMTEGEMEA SIO WEWE ULIEMUEKA MADARAKANI UKWELI NI AMEWEKWA MADARAKANI NA SEREKALI YA TANGANYIKA ILI AWE KIBARAKA WAO WA KUIFANYA ZANZIBAR KOLONI LA TANGANYIKA. KWA HIVYO, MWAKILISHI NA MBUNGE WA ZANZIBAR HAWEZI KUITETEA ZNZ BALI WATAITETEA TANGANYIKA AMBAKO WANAPATA MASLAHI YAO. Bila ya kuuvunja muungano VIBARAKA WA TANGANYIKA wataendelea kuwatesa WAZANZIBAR. Hata tufe wazanzibar sote lakini tuhakikishe kuwa tunapata UHURU WETU.

  • DUNIA HII YA LEO ASIKUA NA NCHII YAKE ATAKA AWE NA NCHI,LAKUSITISHA ZENJ ILIKUWA NI NCHI LEO SI NCHI,NA KWADANGANYA TOTO NI NCHI, VIPI MBONA HAINA
   UBALOZI KOKOTE,BASI HAKUNA NCHI ZENJ KUNA TANZANIA NCHI,SASA HAO NDUGU ZANGU WANAO KUA RAIS, WAZIRI NI WAWAPI ZENJ IPI? WAJI DANGANYA AU WADANGANWA!!!!!!
   WASHUKRA

 5. WAZANZIBAR TUONDOE IMANI ZETU ZOTE KWA VIONGOZI WA SMZ KWANI 99% NI VIBARAKA WA TANGANYIKA PIA, 99% HAWAKUCHAGULIWA NA WAZANZIBAR BALI WAMEWEKWA MADARAKANI NA WATANGANYIKA ILI WAIFANYE ZANZIBAR KOLONI LA TANGANYIKA. Wazanzibar tusiache kutuma sms katika mitandao KUHAMASISHA WAZNZ KUSHIRIKI KATIKA HARAKATI ZA KUDAI UHURU WA ZNZ-2012. Kufa kwa muislam katika kudai haki ni JIHAD.

 6. SABABU YA YOTE HAYA VIONGOZI WETU WA ZANZIBAR MNAONEKANA KUA WASALITI MNAOJALI ZAIDI MASLAHI YA MATUMBO NA FAMILIA ZENU. KAMA MNGEKUA NA MSIMAMO WA PAMOJA NA WANANCHI HAYA YASINGETOKEA. HIVI HAMUONI KUA NDANI YA MUUNGANO HUU MBOVU WATANGANYIKA WANAINYONYA NA KUIDHALILISHA ZANZIBAR? MNAJUA HILO LAKINI KWA KUA MNALIPWA MISHAHARA MIKUBWA NYINYI NA FAMILIA ZENU MNASAHAU DHIKI ZA WANANCHI WANYONGE ZINAZOSABABISHWA NA MUUNGANO. MNATEGEMEA WANANCHI WAFANYE NINI WANAPOONA WAMESALITIWA NA VIONGOZI. HEBU TOENI MSIMAMO WENYE MANUFAA NA WANANCHI MUONE KAMA KUNA MTU ATAKAELETA RABSHA.HUYO MOHD ABOUD TAYARI AMESHATANGAZA HADHARANI KUA YEYE NI KIBARAKA WA TANGANYIKA SASA MNATEGEMEA WANANCHI WATAKUA NA IMANI NAYE TENA? NI VYEMA KWA HESHIMA ZOTE PAMOJA NA KUA NI WAZIRI AEKWE PEMBENI KATIKA HILI NA WAEKWE WATU WENGINE TUMESHAPOTEZA IMANI NAE.

 7. Kama serikali haitofanya khiana kwa raia zake huo ni mwanzo mzuri vikao na Chaguzi nyingi zinafanywa matokeo Yake wakafanya watakavyo wananchi wanasema sasa basi let’s c nini kitakuwa you fool some people some time but you can’t fool us all the time

 8. AMA KWELI ASIEKUJUA HAKUTHAMINI KWANI VIONGOZI WA SMZ HAWAWATHAMINI WAZANZIBAR KUTOKANA NA KUTOWACHAGUA KWA KUWAPIGIA KURA KATIKA UCHAGUZI. Imefikia hatua wawakilishi wa zanzibar hawatatui matatizo ya znz sasa wanatatua matizo ya TANGANYIKA. Wazanzibar kila mtu awe na baraza lake la maamuzi na sio kutegea VIONGOZI WA SMZ

 9. Jamani smz nyinyi mnapenda kula tu na kila mtu anajua mifano iko mingi, sasa hamuoni kama MDUNDANO (MUUNGANO) ukivunjika ndio nafasi nyingi za ajira (mlo) zitapatikana mfano mabalozi,maafisa katika balozi zote za Zanzibar duniani, kukaribisha mabolozi takribani toka nchi zote ?. WABUNGE wa sasa msitutilie kitimbakwiru tutakupeni ubaloziii! jamani, anzeni kujifunza Kiingereza,Kiarabu,Kifaransa,Kijerumani mupo ?maana wengi tunakujueni ni wabofu wa ung’eng’e na chuoni wengi mlikimbia umande. HALAFU NA WEWE MOH’D ABOUD SHIII! HEBU NYAMAZA UTUACHE wakati wa kula ukifika tutakuita na mwenzi SORAGA na dua zake eti “MUNGU washughulikie wasiotaka muungano”.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s