Kifaa cha zima moto kisichohitaji maji chazinduliwa

Kamishna Ali Abadalla kushoto akiangalia kifaa kipya cha kuzimia moto kijulikanacho kama DSPA 5 kutoka kwa askari wa kikosi cha Zima Moto na Uokozi katika hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho hapo Maisara Mjini Zanzibar

KIKOSI Cha Zima Moto na Uokozi Zanzibar jana kimezindua kifaa kipya cha kisasa cha kuzimia moto kisichotumia maji kiitwacho Dry Sprinkler Powder Aerosol (DSPA5). Kifaa hicho ambacho huzima moto ndani ya dakika mbili baada ya ya kutumbuliwa nyuzi zake kwa kwa sekunde nane kina uwezo wa kutumika na kudumu kwa miaka 15 bila kuharibika bada ya kukinunua. Uzinduzi wa kifaa hicho umefanyika Maisara Mjini Zanzibar mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Issa Haji Ussi pamoja na makamanda mbali mbali wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na makamishina kutoka vikosi vyote.

Ussi alisema kupatikana kwa kifaa hicho kutasaidia kwa kisi kikubwa majanga ya moto yanayotokea hapa Zanzibar hasa kwa kuzingatia magari ya zima moto yaliopo ni kidogo na hayakidhi haja kutokana na ukumbwa wa mahitaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ‘Your Solution Tanzania LTD’ ambayo imeshirikiana na AFG Group ya Uholanzi, Damian George akitoa ufafanuzi wa kifaa hicho cha DSPA alisema kuwa lengo hasa la kifaa hicho ni kuwaonesha wazanzibari na watanzania namna ya kukitumia.

Alisema DSPA ni muhimu kutumika pale inapokea janga la moto ambapo hutumika kwa kuzima moto bila ya kutumia maji ya aina yoyote na kinapofunguliwa huzima moto unaowaka.

Akiwatoa wasiwasi watu walifika kushuhudia kifaa hicho na maafisa wa serikali na vikosi vya SMZ, George alisema DSPA ni teknolojia ya kisasa ambayo haina madhara yoyote ya kiafya wakati wa uzimaji moto hata pale mtu atakapokuwa yupo ndani wakati wa uzimaji wa moto huo.

George alisema kifaa hicho kwa nchi za Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwaza kufika ambacho huzima moto kwenye chumba chenye ukubwa wa mita 100 za mraba kwa DSPA 5 moja yenye uzito wa kilo moja ambapo uwezo wake wa kufanya kazi ni mkubwa na huchukua muda wa miaka 15 bila ya kuharibika.

Akitoa shukrani katika uzinduzi huo Kamishina wa kikosi hicho, Ali Abdalla alisema amefurahi sana kuwa kifaa hicho kimekuja wakati muafaka na ni njia mbadala ya kuzimia moto baada ya magari ya kawaida kutumika hapa Zanzibar.

Alisema kutokana na kuwepo kwa matukio mbali mbali ya kuwaka kwa majengo ya Serikali, taasisi za kijamii na hata baadhi ya nyumba za makaazi ya watu binafsi hivyo kifaa hicho kitakuwa muokozi wa maafa hayo iwapo yatatokea kwa sasa.

Amesema Zanzibar ni Taifa linalohitaji mabadiliko ya kidunia ili kwenda sambamba na dhana za kisasa za uokozi pale ambapo pametokea janga la moto na kwamba hakuna budi kupambana nalo bila ya kuleta maafa mengine kwa jamii na nchi.

“Ni matumaini yetu kwamba kifaa hiki kitatumika vizuri, ni kifaa muhimu kwani hakitumii maji kitasaidia kwa kiasi kikubwa nchini kwetu kwani sisi ni sehemu ya dunia” alisema Kameshina Abdalla.

Kamishna huyo alisema Zanzibar ambayo imekubwa na tatizo kubwa la maji na ukosefu wa magari ya kuzimia moto majanga yanapotokea kifaa hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma hiyo ambayo haitahitaji kupatikana kwa maji.

Advertisements

4 responses to “Kifaa cha zima moto kisichohitaji maji chazinduliwa

  1. Pingback: Kifaa cha zima moto kisichohitaji maji chazinduliwa·

  2. Haya sasa naamini majanga ya moto yataweza kudhibitiwa na hakutakua tena na visingizio vya hakuna maji. Isije ikawa kupatikana kwa vifaa hivi sasa sababu ikawa hatuna mafuta.

  3. IKIWA WATANGANYIKA HAWANA KIFAA HICHI BASI LAZIMA WATAKIIBA KIFAA HICHI NA KUKIPELEKA BARA. Wazanzibar hatuutaki muungano na MAKAFIRI WA TANGANYIKA.

  4. Zanzibar hii ndio kawaida yake kuwaonyesha njia Watanganyika-Mfumokristo.
    Mfano ni ya kwanza kuanzisha Baraza la Mitihani na baadae Tanganyika ikaazima wataalamu kutoka Zanzibar ili kuianzishia nayo kijibaraza chake, baraza ambalo kwa muda mrefu limetumika kuirudisha nyuma kielimu ZANZIBAR, wa hili Kigoma Malima kuanzisha matumizi ya namba katika mitihani badala ya majina chanzo chake ni udini (dhidi ya Uislamu) Jee wazanzibari unafikiri nafasi yao ilikuwa ipi kwenye dhulma hii na hata sasa. JUMA FAKI unasikia hapo ?. MUUNGANO WENU Ki-JUMA FAKI hatuuutakiiiii!
    Pia ni ya mwanzo kuanzisha T.V tena ya rangi kabla ya Tanganyika kuanzisha DTV baadae ikaitwa TVT na sasa inaitwa TBC Television, na Afrika asilima takriban 99% ilikuwa bado haina TV. Afrika Mashariki nzima hii ndio T.V pekee iliyokuwa ikitangaza kwa Kiswahili sanifu na fasaha, kwa kulijua na kulihusudu hilo ndio maana (TBC)wakamchukua Kaka yangu Marine Hassan Marine ili wajifunze mengi kutoka kwake likiwemo hili Lugha ambayo Maashaa-Allah Marine ni Mahiri,kama utafatilia hili utagundua wengi miongoni mwa watangazaji wa TBC wanamuiga kila kitu ndugu yetu huyu kwani moja ya sera ya BBC ni ‘use of standardizide English’ na tv zetu zinaiga hapo kila kitu mfano muundo wa majina TBC,ZBC,KBC,UBC n.k, ndio maana kwa sababu kiswahili kwa ni utomvu wa fenesi ndio maana wakamchukua huyu ndugu yetu kama mafuta yatakayo wawezesha kulila fenesi bila ya tabu, jueni mabwana wale wakisha mtumia watamtupa kama ganda la ndizi n.k
    Kiufupi ningeyataja mengi niyafupishe kwa msemo huu “You pipe in Islands (Zanzibar), they dance in the main lakes” yaani “Ukipuliza baragumu Visiwani, hucheza walio katika maziwa makuu”. Hii inamaanisha kuwa ustaarabu (civilization) kihistoria huanzia Zanzibar ndio Watongonyoko nao hukopia, cha kusikitisha wao hujinya ndio ‘before’ wamewaaahi,wajaanja au ndio top kuliko Wazanzibar.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s