Abiria 124 wanusurika kufa baharini

Boti ya Sea Express kutoka Pemba kuja Unguja jana ilipata khitilafu ikiwa baharini boti hiyo iliondoka saa 5:00 asubuhi Pemba na kufika saa 4:30 ndio wamefika katika bandari ya Malindi Unguja abiria wakiwa wamechoka kupita kiasi.

 

WATU 124 wamenusurika kufa maji katika bahari ya hindi baada ya boti ya Sea Express waliokuwa wakisafiria kutoka Pemba kuelekea Unguja jana kupata khitilafu kwenye injini yake na kushindwa kutembea kwa kikawaida. Kwa mujibu wa Kepteni Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar, Makame Hassan alisema boti hiyo ilikuwa maili saba ya bandari ya Pemba ilipoanza kupata khitilafu hiyo na kusababisha mshituko mkubwa kwa abiria waliokuwepo katika chombo hicho.

Kepteni huyo alisema abiria wlaiokuwepo katika boti hiyo walikuwa jumla ni 124 watu wazima 104, watoto 12, na wafanyakazi wanane ambapo ilipata matatizo kutoka bandari ya Mkoani ilipokuwa ikitaka kuondoka bandarini hapo na kusababisha msongamano ndani ya boti hiyo.

Akithibitisha tukio hilo Kepteni wa boti hiyo Ussi Ali Ussi alisema ni kweli walipata khitilafu katika injini kutokana na mashine ya kuchujia mafuta ‘filter’ kundishindwa kufanya kazi kikamilifu na uwezo wa kutembea katika kiwango cha kawaida ulipungua sana kufuatia mafuta kutokuchanganya vizuri kwneye injini hiyo.

Kapteni huyo alisema muda mfupi baada ya kutokea matatizo hayo aliwasiliana na na mamlaka ya bandari  ya Mkoani Kisiwani na Bandari ya Malindi Unguja lakini bahati mbaya hajafanikiwa.

“Baada ya kutokezea khitilafu hiyo tu mimi nilifanya mawasiliano na mamlaka zinazohusika ikiwemo bandari ya Pemba na mamlaka ya bandari ya Unguja lakini bahati mbaya sikufanikiwa” alisema Kepteni huyo.

Alisema boti hiyo ilikuwa umbali mrefu na hivyo kusababisha upatikanaji wa msaada ukawa mdogo sana lakini juhudi mbali mbali alichukua ili kupata msaada wa kuokoa abiria na wafanyakazi waliokuwemo katika chombo hicho.

“Mbali na kuwasiliana na mamlaka zinazohusika lakini pia nilimpigia simu wakala wangu wa boti hii kumjulisha habari hii na khitilafu uliyotokea ili aweze kuchukua hatua na kama tungeweza kupata chombo cha kusaidia” alisema Ussi.

Akivitaja vyombo ambavyo vimetoa msaada katika tukio hilo ni pamoja na Serengeti, Jitihada na boti za vikosi vya KMKM na hatimae boti yake kutengenea na kuaendelea na safari yake hadi Unguja ambapo imefika majira ya saa 4.40 usiku huku abiria wakiwa wamechoka kutokana na kukaa muda mwingi baharini.

 

Akizungumzia tatizo hilo Fundi Mkuu wa boti hiyo, Richard Samuel alisema kwamba baada ya kutokea tatizo hilo alifanya matengenezo kwa kupitisha mpira kutoka katika chujio na kupitisha kwenye tangi la mafuta moja kwa moja na kufanikiwa kutembea taratibu hadi kufika.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti muda mfupi baada ya kuteremka katika boti hiyo abiria hao waliilalamikia serikali kushindwa kutafuta chombo cha uhakika cha kusafiria na badala yake kuwa na vyombo visivyo na usalama.

Abiria waliokuwepo ndani ya chombo hicho walikuwa na khofu kubwa na wengine kupiga kelele na kusababisha baadhi ya wafanyakazi kuhangaika huku na kule ili kuwatuliza abiria hao lakini hali ilikuwa mbaya kiasi ambacho baadhi ya wafanyakazi wengine kuchanganyikiwa kutokana na hali mbaya iliyokuwemo ndani ya boti hiyo.

“Mimi nailaumu serikali kwa sababu mpaka leo wameshindwa kutafuta usafiri wa uhakika mimi nilidhani vifo vilivyotokea ingekuwa funzo wa serikali lakini inasikitisha kuwa mpaka leo wanacheza bahati nasibu na maisha ya watu” alisema kwa masikitiko Bi Moza Said aliyekuwa na watoto watatu akitokea Pemba.

Moza alionesha akiwa amechoka na amebeba mizigo akiteremka katika chombo hicho na kusema “tokea saa tano tupo njiani mpaka sasa hivi hatujala watoto wana

njaa, hakuna vyakula tafrani tupu kwa kweli inasikitisha sana” alisema.

Naye Hamad Omar alisema wamiliki wa vyombo vya usafiri wanapaswa kuhakikisha vyombo vyao viwe salama kabla ya kuwachukua abiria ili abiria wasafiri bila ya khofu na wasiwe na shaka na safari.

“Leo tunapanda tunasafiri lakini khofu tupu unatoa shahada kwanza na ikitokea tatizo kidogo tu watu wanapiga kelele kwa sababu wameshawahi kushuhudia matukio ya ajali mbaya ya hivi karibuni ……serikali hivi haijasoma tu” alihoji Hamad.

 

 

 

 

Advertisements

3 responses to “Abiria 124 wanusurika kufa baharini

  1. hao kmkm wanafanya nini tangu saa 5 hawajatuma boti ya kuokowa watu wakawaingiza abiria boti nyengine hapa serekali iwajibikee au wao kupiga mikwaju wazanzibar tu wewe sheni unafanya nini fukuza watu kazi kwa kukosa uwajibikajii

  2. WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WA TANZANIA. Kama zanzibar ingelipata uhuru kutoka mikononi mwa makafiri weusi wa TANGANYIKA basi znz ingelikua na uwezo wa kununua boti mpya za abiria. MZANZIBAR KATAA MUUNGANO WA TZ, TRA WANAHAMISHA MAPATO YA ZNZ NA KUYAPELEKA BARA HALI AMBAYO INAIPELEKEA SMZ KUWA OMBA OMBA TU.

  3. Hakika kama abiria hawa wangelitoka TANGANYIKA wangaliokolewa kwa boti za JWTZ na KMKM. Mzanzibar shiriki katika harakati za kuuvunja MUUNGANO WA TANZANIA ILI ZANZIBAR IPATE MAENDELEO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s