Wapinga Muungano washitakiwa kwa uhuni

Wananchi mbali mbali wakiwa nje ya mahakama ya wilaya ya Mwanakwerekwe wakisubiri ndugu, jamaa na marafiki wasomewe mashtaka yao yanayowakabili

KESI ya watu 12 wanaopinga Muungano jana imesomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar huku baadhi ya watu kadhaa wakiwa wamefurika katika Mahakama hiyo kusikiliza. Kesi hiyo imesikilizwa chini ya hakimu Omar Mcha Hamza na kusomewa mashitaka matatu tofauti ambayo hata hivyo wote kwa pamoja waliyakana makosa hayo.

Waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na kiongozi wao Rashid Salum Ali (48) mkaazi wa Kikwajuni, Khamis Hassan Hamad (51) wa Jang’ombe, Rashid Ali Rashid (21) anayeishi Mombasa, Hashim Juma Issa (54) mkaazi wa Mbweni,

Wengie ni pamoja na Suleiman Mustafa Suleiman (31) anayeishi Mombasa pamoja na Haji Sheha Hamadi (49) anayeishi Chumbuni, Rami Mbaraka Ahmed (48) wa Michenzani na Salum Masoud Juma (38) anayeishi Rahaleo,

Wengine walioyajwa katika kesi hiyo ni Mussa Omar Kombo (67) mkaazi wa Mpendae, Omar Kombo Is-hak (21) wa Magogoni, Ali Omar Omar (54) anayeishi Bububu na Masoud Faki Massoud (31) mkaazi wa Kilimahewa.

Wote hao kwa pamoja wameshitakiwa kwa makosa ya kufanya mkusanyiko usio halali, kuendelea kukusanyika baada ya kutangazwa kutawanyika na Ofisa wa Pilisi pamoja na shitaka la uhuni na uzururaji.

Mashitaka hayo yaliwasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa mahakama hiyo Said Ahmed Mohammed, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP).

Akiendesha kesi hiyo mahakamani hapo, Mwanasheria huyo wa serikali aliwasomea watuhumiwa hao shitaka la kufanya mkusanyiko usio halali kinyume na vifungu vya 55 (1) (2) (3) na 56 vya kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Katika shitaka hilo aliifahamisha mahakama kwa kudai kuwa, April 20 mwaka huu, majira ya saa 2:30 za asubuhi, huko Mbweni wilaya ya Magharibi Unguja, kwa pamoja na bila ya halali watuhumiwa hao walijikusanya katika barabara ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Alidai kuwa, mkusanyiko huo uliwafanya majirani na watu waliokuwa wanakwenda kwenye Baraza kupata khofu, kuwa wangeliweza kusababisha uvunjifu wa amani wakati hawakuwa na sababu za msingi za kukusanyika.

Akielezea shitaka la kuendelea kukusanyika baada ya kutangazwa kutawanyika na Ofisa wa Polisi, Mwanasheria huyo alidai kuwa baada ya mkusanyiko huo walitakiwa kutawanyika kwa amani na Ofisa wa Polisi, lakini waliendelea kukusanyika kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa Mwanasheria huyo, kitendo hicho cha kukataa amri hiyo halali ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 60 cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.

Shitaka la mwisho linalowakabili watuhumiwa hao ni la uhuni na uzururaji, ambapo mahakama ilifahamishwa kuwa siku hiyo walipatikana wakiwa wamejikusanya kwenye barabara hiyo ya Baraza la Wawakilishi, wakiwa na mabango yenye maneno yanayopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Kitendo hicho ambacho ni kosa chini ya kifungu cha 182 (d) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, ambacho walidaiwa kukifanya katika wakati na mazingira yanayoonesha kuwa hawakuwa na madhumuni halali.

Mahakama ilipowapa nafasi watuhumiwa hao kujibu madai hayo ya upande wa mashitaka waliyakana, na Mwanasheria huyo wa serikali kudai kuwa upelelezi wake bado haujakamilika.

Mwanasheria huyo aliiomba mahakama hiyo kuiahirisha kesi hiyo na kuipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa, ili kutoa nafasi ya kuweza kukamilisha upelelezi huo.

Baada ya hoja hizo, watuhumiwa hao waliomba mahakama hiyo iwapatie dhamana ombi ambalo hata hivyo upande huo wa mashitaka haukuwa na pingamizi nalo.

Wahutumiwa hao iwapo watakuwa na wadhamini madhubuti watakaoweza kutekeleza masharti ya dhamana yatakayotolewa na mahakama hiyo.

Kwa kuzingatia hoja za pande mbili hizo, hakimu Omar Mcha Hamza pamoja na kuwapatia watuhumiwa hao masharti ya dhamana lakini alifahamisha kuwa endapo watashindwa kuyatekeleza watalazimika kubakia rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena.

Masharti hayo kila mtuhumiwa, awasilishe dhamana ya fedha taslimu shilingi 500,000 pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho kikiwemo cha Mzanzibari Mkaazi, na mmoja kati ya wadhamini hao awe ni mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kesi hiyo imeakhirishwa hadi Mei 7 mwaka huu kwa kutajwa tena.

Advertisements

14 responses to “Wapinga Muungano washitakiwa kwa uhuni

 1. Ah ndio nchi yetu hii lakini hakuna lisilo na mwisho. Mimi binafsi ningepata wasiwasi mkubwa na khofu isiyomithilika kama wangeshitakiwa kuwa kudai uhalali wa muungano na kudaiwa kuwa ni kinyume cha sheria (hapa wangetajiwa hivyo vifungu kadhaa wa kadhaa vya sheria).
  Hii ni dalili njema, tunaelekea kwenye uhuru wa kweli na ndio ishara ya mwisho wa huyu subiani aitwae muungano. Allah tupe nguvu na tuwepesishie kwenye mapambano ya kudai nchi yetu.

 2. Huku Zanzibar ina maana wenye pesa tu ndio wenye haki ya kupewa dhamana? Inakuaje hata upande wa mashtaka haukupinga dhamana kutokana na makosa yenyewe kua hayana uzito lakini washtakiwa wanaambiwe waeke laki tano kila mmoja. Au ndo njia ya kuwauzia haki hiyo? Kama ni uhuni Wazanzibari karibu wote ni wahuni maana tunaupinga muungano mtushtaki na sisi. Kwa mtaji huu bado hamjatutisha TUTAENDELEA KUDAI ilivyokua ni haki yetu mpaka kieleweke au MUELEZE WAZI ULIMWENGU kua hii katiba mnayotaka kuiunda ni ya Viongozi na Wana CCM manake sisi wananchi hatuna haki ya kuamua mpaka atuamulie Balozi Sefu Idi.

 3. Hii ni kesi ya kichekesho mno! Hii inaonesha mwisho wa hili Ruhani Muungano kutuondokea. Hebu ni ulize tafsiri wa hizi misamiati hii kwa mujibu wa sheria. Uhuni , uzururaji na amri halali. Hii ni kupotezeana muda! Zanzibar huru yapiga hodi!

 4. WAZANZIBAR TUSHIRIKIANE KWA PAMOJA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR KUTOKA MIKONONI MWA MAKAFIRI WA TANGANYIKA WALIOIFANYA NCHI YETU KOLONI LAO. Wazanzibar tuwepamoja na WAZALENDO WETU WALIOKAMATWA NA MAKAFIRI WA TANGANYIKA. Kwa vyovyote ujumbe umekwisha fika kua wazanzibar hatuutaki MUUNGANO. WAZANZIBAR TUSIWE NA HOFU WAZALENDO WOTE WATATOKA NA HAKUNA ATAKAEFUNGWA WALLAH KUFUNGWA KWA WANAHARAKATI HAWA WA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR, BASI HICHO NDIO CHANZO CHA VIFO VYA MAKAFIRI WA TANGANYIKA WALIOPO ZANZIBAR. Wazanzibar ili tupate uhuru wetu ni lazima TUWAUE MAKAFIRI WA TANGANYIKA WANAOISHI ZANZIBAR.

 5. Hongera rafiki yangu kwa kuzungumza maneno mazuri. Kila siku ya KESI YA WAPIGANIA UHURU WA ZANZIBAR TUHAMASISHANE KWENDA MAHAKAMANI KWA WINGI.

 6. HII KESI WALIOPEWA WAZELENDO WA ZANZIBAR NI KUWATUKANA WAZANZIBAR WOTE KWANI 99% YA WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WA TANGANYIKA. Hivi kwanini tunalazimishwa kukuukubali muungano. MUUNGANO WA TZ HAUNAFAIDA KWA WANANCHI WA ZANZIBAR. Mapambano ya kudai uhuru yatazidi. MFIRWA MKUNDU SEIF ALI IDD KUMAMAMAYO.

 7. jamani mambo haya ya kienyeji tutabaki nayo mpaka lini yani wapigania uhuru wa nchi yao wamekuwa wahuni, wao wanaotuangamiza kwa muungano uliokuwa hauna hata hati, si wa kihuni?

 8. Ndugu zangu,

  Kabla ya kuanza kupinga muungano baina yetu na Tanganyika inatakiwa kwanza tudumishe mshikamano baina yetu, kuondoa chuki baina yetu, kukomesha majungu baina yetu n.k. Pili, ndugu zangu wanaohamasisha wenzao kuendeleza mapambano ya kudai uhuru wa Zanzibar wanatakiwa wafanye vitendo na sio kauli tu. Kama nia zenu ni njema kwa hawa wenzetu waliokamatwa mbona hamjitolei kwenda kuwadhamini mahakamani au hamjitolei kwenda kukusanyika nje ya baraza la wawakilishi kama walivyofanya wao?

  Tatu, msisahau kwamba kuna maelfu ya ndugu zetu wa kipemba na kiunguja waliotajirika kwa kufanya biashara mbali mbali hukoTanganyika. Na wengi wao ndio wanaotoa michango ya hali na mali kwa chama kikuu cha upinzani hapa Zanzibar. Je muungano ukivunjika hatima yao itakuwa wapi?

  Mwisho, Kwa upande wangu, naungana na maalim Sefu pamoja na viongozi wengine wa CUF na CCM wanaodai kuwa muungano tulionao ni lazima urekebishwe (ili kuipa dola yetu ya Zanzibar haki zake zote za msingi) na sio uvunjwe.

  UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU. AL-ITIHAAD QUWWAH.

 9. WAZANZIBAR HATUUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WEUSI WA TANGANYIKA. MUUNGANO WA TZ HAUNA FAIDA YOYOTE KWA ZANZIBAR ISIPOKUA HASARA NYINGI ZILIZOPO. 1- TRA WANACHUKUA MAPATO YA ZNZ 2- WABONGO WANASAMBAZA UKIMWI ZNZ 3-NECTA INAFELISHA WANAFUNZI WA ZNZ. UNIVERSITIES ZA BARA ZINATOA DISCO NYINGI KWA WAZANZIBAR. 4-POLIS NA JWTZ WANAWAFIRA KWA NGUVU NA KUWAUA WAZANZIBAR. 4-RAIS WA ZNZ ANACHAGULIWA DODOMA. 5-NAFASI ZA AJIRA ZA WAZANZIBAR ZINACHUKULIWA NA WATANGANYIKA. Wazanzibar tujitolee kufa ili tupate UHURU.

 10. Uharaka wa Mkurugenzi wa Mashtaka na Polisi kushughulikia kesi hii ni ajabu. Ni kwani DPP hajaanza kuwatengenezea majalada waliotajwa kwenye Ripoti ya Omar Ali Shehe. Au wale si wahalifu. Nini ni tofauti baina ya alieandamana na aliyeuza ardhi?

 11. Poleni sana ndugu zangu Wazanzibari mliokamatwa kwa kugombania haki ya nchi yenu, hio ndio moja ya kupigana jihadi .Ila ningenda kutowa mchango wangu kwa wazanzibar wezangu napenda kuwambiia kuwa sasa ndio umefika wakati mzuri watu kuingia barabarani kudai nchi watu wajitokeze kwa wingi kwenda mahakamani watu watoke mashamba kote kwa magari washuke mjini kwenye mahakama na ndugu zangu wa pemba mje kwa wingi siku ya mahakama sio msubiri mikutano ya CUF NA CCM, ndio mnajitokeza kwa wingi.Tuwe na mapenzi na nchi kushinda vyama vya kisiasa.Sio laziam maalim Seif ndio afanye mkutano ndio watu wajitokeze kwa wingi.Kwahiyo ndugu zangu wazanzibar hu ndio wakati munasab tujitokeze kwa nguvu tuende mahamani na mabango ya kupinga muungano tuone jee watawakamata (wahuni wangapi na wazururaji wangapi) kama wanavyowashitaki hao ndugu zetu. Maana mimi naona kuwa watakamata wengi, na magereza yao yatajaa wazanzibari.Kama tutajitokeza kwa wingi siku ya mahakamani hi ndio fursa jamani tutowe woga tukombowe nchi yetu.ZANZIBAR DAIMA,ZANZIBAR HURU

 12. Na waliokula pesa za michango ya MV Spice Islander nao DPP awatengenezee jalada maana kwa vyovyote vile tutahakikisha wanapanda kizimbani.

 13. “Shitaka la mwisho linalowakabili watuhumiwa hao ni la uhuni na uzururaji, ambapo mahakama ilifahamishwa kuwa siku hiyo walipatikana wakiwa wamejikusanya kwenye barabara hiyo ya Baraza la Wawakilishi, wakiwa na mabango yenye maneno yanayopinga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.”

  Hii inachekesha! ivo mtu mzima na akilli yake aweza kuwa mzururaji

 14. Najua Sheiki Juma Faki na wizi wenziwe(aliiba sana Chuo cha Kiislamu mpaka SMZ Wakalitimulia mbali) wamefurahi sana. Lakini namwambia ha Hussein Mubaarak alidhani hivyo hivyo na lakini mwishowe…ANANYEA NDOONI LEO.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s