Mamia wamzika Mwakanjuki

Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Abeid Karume Zanzibar wakitokea Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi

MAMIA ya wananchi wakiongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein jana walishiriki katika mazishi ya aliyekuwa waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Brigedia Jenerali, Adam Clement Mwakanjuki aliyefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu Mwakanjuki uliwasili hapa Zanzibar baada ya kuagwa huko nyumbani na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Mamia na wananchi wakiongozwa na viongozi mbali mbali wa serikali waliupokea mwili wa marehemu Mwakanjuki katika uwanja ndege wa Zanzibar ukitokea jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili Zanzibar mwili huyo ulipelekwa moja kwa moja Kikwajuni kwa Dada yake Bi Teressia Mwakanjuki na kisha kupelekwa katika ukumbi wa baraza la wawakilishi ili kutoa nafasi kwa viongozi wa serikali, ndugu jamaa na marafiki kuuaga mwili huo.
Baada ya kuagwa mwili wake ulipelekwa katika kanisa la Anglikan liliopo Mkunazini na kufanyiwa misa maalumu ya kumuaga na hatimae kupelekwa katika makaburi ya Anglikan huko Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar kwa mazishi ambapo alipigiwa mizinga 11 na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Awali serikali kupitia vyombo vyake vya habari viliwatahadharisha wananchi wanaoishi katika maeneo ya Mwanakwerekwe kutoshituka watakaposikia milio ya mizinga hiyo kwani haina madhara kwa binaadamu bali ni taratibu wa kawaida wa kijeshi.
Viongozi waliohudhuria katika mazishi hayo pamoja na Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais Mstaafu Amani Abeid Karume, Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Ramadhan Makungu na mawaziri, manaibu mawaziri, wabunge, wawakilishi na wananchi mbali mbali.
Marehemu Mwakanjuki amefariki duani juzi wiki iliyopita huko katika hospitali ya jeshi Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza na gazeti hili watu tofauti walisema Brigedia Mwakanjuki katika uhai wake alikuwa ni kiongozi mkali na mwenye ujasiri mkubwa katika utendaji wa kazi zake zaidi alikuwa ni mtetezi mkubwa wa haki za Zanzibar.
Walimtaja marehemu kuwa ni ni mtu ambaye alikuwa akisimamia alichokuwa akikiamini na wakati wote alikuwa ni mtu mcheshi na mwenye matani kwa rika zote.
Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wan chi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ na mumbe wa baraza la wawakilishi kwa muda mrefu.
Wakati wa uhai wake Marehemu Mwakanjuki alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Zanzibar katika wizara mbali mbali pamoja na kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).  Tangu mwaka 2007 Marehemu Mwakanjuki hakuonekana katika harakati za siasa baada ya kupata ajali mbaya akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam katika eneo la Morogoro ambayo ilisababisha kuvunjika sehemu zake za viungo.
Licha ya juhudi za kupatiwa matibabu ndani na nje ya nchi lakini hakuweza kurudi katika hali yake ya kawaida ambapo wakati wa tukio inatokezea alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe pamoja na mwanawe. Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo pia kuwa miongoni mwa waanzilishi wa jeshi la kujenga taifa JKT. Brigedia Jenerali Mwakanjuki ameacha mjane mmoja na watoto watano.

 

Advertisements

4 responses to “Mamia wamzika Mwakanjuki

  1. Marehemu huyu alikuwa miongoni mwa vibaraka wa TANGANYIKA WALIOIFANYA ZANZIBAR KOLONI LA TANGANYIKA PIA, MAREHEMU HUYU ALIKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUUA NA KUWATESA WAISLAM NA WANAHARAKATI WA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR. Yaarab mueke kafiri huyu moto mmoja na FIRAUN.

  2. EWE MUNGU MUINGIZE MAREMU HUYU MAHALA PABAYA MOTONI- AMEEN. Alhamdullillah, wazanzibar tunamshukuru mungu kutuondolea KIBARAKA WA TANGANYIKA HUYU. Yaarab katika nchi yetu kuna makafiri wakubwa zaidi ya huyu makafiri wenyewe ni ALI JUMA SHAMHUNA, SEIF ALI IDD NA MOH’D ABOUD Yaarab WAINGIZE MOTO MMOJA NA FIRAUN VIBARAKA HAWA WA TANGANYIKA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s