Wenye kudai kura ya maoni ya Muungano watiwa mbaroni

Jeshi la Polisi limemtia mbaroni Kiongozi wa wazanzibari wanaodai kuwepo kwa kura ya maoni juu ya Muungano, Rashid Salum Adiy na wenzake 11 walipokuwa katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakitaka kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho

Watu 12 wamekamatwa na Jeshi la Polisi wakidaiwa kufanya maandamano bila ya kibali visiwani Zanzibar Kwa taarifa zaidi bonyeza hapa.

Advertisements

7 responses to “Wenye kudai kura ya maoni ya Muungano watiwa mbaroni

 1. HIVI KUTAKA KUMUONA SPIKA NA KUMUELEZA JUU YA MAONI YAO IMEKUA NI KOSA ZANZIBAR? HUU MNAOFANYA SASA NI UDIKTETA KWANI KATIBA ZOTE MBILI ZINARUHUSU WATU KUTOA MAONI NA KUELEZEA HISIA ZAO. SASA NIMEAMINI KUA WAZANZIBARI KUMBE HATUNA HAKI YA KUUJADILI MUUNGANO HUU MBOVU. NA TUNAPOTAKA KUUJADILI WAKOLONI WATANGANYIKA KWA KUTUMIA VYOMBO NA VIBARAKA WAO WA HAPA ZANZIBAR WANATUKANDAMIZA. EWE BWANA MSA MKUU WA POLISI ELEWA KUA HICHO CHEO KINA MWISHO WAKE LAKINI UZANZIBARI HAUNA MWISHO. WAMEPITA WENGI HAPO NA LEO WAKO WAPI. WAMESHAFUNGWA MFANO WA PIPI, WENGINE HAWAJITAMBUI, HAO WANAPIGANIA MASLAHI YA WAZANZIBARI AMBAO NI ASILIMIA 99 NA WEWE KWA SABABU YA CHEO CHAKO UNAWANYANYASA NA KUWAONEA. MUNGU ATAKULIPENI HAPAHAPA DUNIANI KAMA KOMANDOO.

 2. HAWA NDIO MASHUJAA WA ZANZIBAR VIJANA TUWAUNGE MKONO TUANDAMANENI NA SISI WATUTIE NDANI MPAKA HIZO JELA ZAO ZIJAE KWANI MAWAZO YAO NI YA WAZANZIBARI WENYE UCHUNGU NA ZANZIBAR WOTE. NAOMBA TUANZE KUWACHANGIA HAWA JAMAA ILI TUWEZE KUWASAIDIA KUPAMBANA NA KESI YAO NA PIA FAMILIA ZAO KWA KIPINDI HIKI. TUWASAIDIENI KUPATA LAWYER WA KUWATETEA MAHAKAMANI.

 3. maoni wazanzibari karibu ya wote ni hayo vijana tuwe na moyo kama wenzetu misri na tuandamane kuukataa mungaano moja kamoja muda ndio huu kwa hili tuone watatutia ndani wazanzibari wote

 4. Kama ni mashtaka watushtaki sote tutakusanyika mazizini pale kwa pamoja kuhakisha wenzetu wanakua huru na baada ya hapo mapambano yanaendelea tumechoshwa na hawa sultani vichogo tutakwenda nao sambamba hadi kieleweke hakuna mtu akaeishi maisha dunia hii potelea mbali tufe sote lakini si kuishi na manyanyaso kama haya ndani ya nchi yetu tuipendayo Zanzibar kwanza,malumbano hatutaki.

  • Likes Given:0

   Dk. Slaa: Nilizuia umwagaji damu 2010

   Mwenyekiti wa Chadma Freeman Mbowe akiwashirikisha wanachama akisema Peoples Power katika mkutano huo.

   na Sitta Tumma, Geita

   KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameeleza namna alivyowazuia Watanzania kushiriki maandamano mazito ambayo yangeweza kusababisha umwagaji damu kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2010.
   Akihutubia maelfu ya wakazi wa Geita katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa magereza mkoani hapa, Dk. Slaa alidai kuwa Watanzania wengi walibaini kile alichokiita kitendo cha kuibiwa kura zake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na hivyo walikuwa wakisubiri kauli yake ya kutaka waandamane.
   Huku akishangiliwa na maelefu ya wananchi, Slaa Alisema kuwa Watanzania wengi walimwomba atoe kauli na walikuwa tayari kuingia barabarani hadi Ikulu, lakini alikataa ili kunusuru umwagaji damu.
   Aliishambulia idara ya usalama wa taifa kwa madai kuwa ilijua namna kura zake zilivyoibiwa, na kwamba kama asingetumia busara za hali ya juu, hali ya nchi ingekuwa tete.
   Slaa aliwashambulia wabunge wa CCM kwa kulamba matapishi kwa yale waliyokuwa wakiyakataa yakiwemo ya nchi kuliwa na mafisadi na mambo ya Katiba mpya.
   Alisema kwa sasa wabunge wa chama hicho wameanza kuungana na yale yanayosemwa na viongozi wa CHADEMA, jambo linalodhihirisha kuwa CCM imechoka kuongoza nchi.
   Alisema wabunge wa chama tawala ni sawa na mavuvuzela kwa kushindwa kuiwajibisha serikali, badala yake wamebakia kupiga kelele tu.
   Lema aunguruma
   Kwa upande wake, aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amemtahadharisha Rais Jakaya Kikwete kwamba asipobadilika kiutendaji na serikali yake isipozuia uporaji wa rasilimali yakiwemo madini, Watanzania watalazimika kuchukua hatua.
   Lema alisema uchumi wa nchi umeyumba na rasilimali zinaporwa hovyo na kumtaka Rais achukue hatua za uwajibikaji.
   Diwani mwingine atoka CCM
   Katika mkutano huo, Diwani wa Kata ya Lugata, wilayani Sengerema Adirian Tizeba (CCM) alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CHADEMA.
   Akizungumza katika mkutano huo, Tibeza alisema amechoka kukitumikia chama kilichobobea kuwakumbatia mafisadi.
   “Rais Kikwete alinirubuni Dodoma lakini nimekuja kubaini CCM imekufa na serikali imebaki kulea mafisadi na kuwatelekeza wananchi,” alisema Tizeba.
   Kujiunga kwa Tibeza, kumefanya idadi ya madiwani waliojiondoa CCM kufikia watatu ndani ya wiki moja.

 5. Ewe mungu waangamize MAKAFIRI HAWA wanaotesa WANAHARAKATI WA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR. Vibaraka wa Tanganyika ni lazima kujua kuwa hata wakiwafunga jela wazalendo wa zanzibar 100000 basi wataibuka wengine milion 1. Waislam tumezoea kufungwa na kuteswa na MAKAFIRI WA TZ. WANAHARAKATI HAKUNA KURUDI NYUMA KILA TUKIKATWA NA MAKAFIRI TUZIDISHE KASI YA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR. Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s