Polisi wawakamata watetezi wa kura ya maoni

Hashim na wenzake wakiwa katika gari la Jeshi la Polisi likiwachukua na kuwapeleka Madema, baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni itakayoamua kuwepo au kutokuwepo Muungano

JESHI la Polisi Zanzibar limewatia mbaroni zaidi ya watu 12 wakiwemo viongozi wa kundi la wanaotaka kuitishwe kura ya maoni kuhusu Muungano, baada ya kukataa kutii amri ya jeshi hilo iliyowataka kuondoka katika viwanja vya baraza la wawakilishi jana.Kundi la watu zaidi ya 40 lilifika katika viwanja vya baraza la wawakilishi huko Chukwani wakitaka kuonana na Spika wa baraza hilo, Pandu Ameir Kificho ambapo kabla ya kukutana Spika alimuagiza Katibu wake Yahya Khamis Hamad kuongea na wananchi hao.

Wakizungumza nje ya viwanja hivyo wananchi hao walisema lengo lao ni kuonana na Spika Kificho ili kuwasilisha ombi lao la kutaka kupelekwa hoja binafsi ya kuitishwa kura ya maoni ya kutaka au kukataa Muungano.

Katibu wa baraza hilo alisema sio vibaya wananchi hao kuwasilisha mapendekezo hayo kwa Spika, lakini aliwataka wananchi hao kufuata utaratibu unaokubalika wa majadiliano na sio kurufika katika viwanja hivyo jambo ambalo linatishia usalama wa chombo hicho muhimu ambacho kinaendelea kujadili masuala mbali mbali nchi.

Waheshimiwa pengine mmekuja hapa kwa nia njema kabisa lakini kwa utaratibu huu nimelazimika kuja hapa nje na kukuombeni muondoke ili muache shughuli za baraza ziendelee kwa sababu sipendi kuona mkipambana na jeshi la polisi katika viwanja hivi” alisema Katibu huyo. Na kuongeza.

Hata Spika alisema kwa utaratibu kama huu hataweza kuwaruhusu kuonana naye lakini kama mtafuata utaratibu mzuri ambao umewekwa na tumeuainisha ndani ya barua zenu basi mnaweza kukutana na kuongea naye, lakini kwa hali kama hii haitawezekana kwa sababu shughuli za baraza zinaendelea lakini pia wananchi wanashindwa kupita hapa na kufanya shughuli zao kwa kuwa mmefunga njia, waheshimiwa wanataka kuja hapa lakini wanashindwa kutokana na hali hii” alisema Katibu Hamad.

Mapema wananchi hao wakiongozwa na Rashid Salum Adiy  walifika katika viwanja hivyo kwa wingi wakiwa na mabango yao yenye ujumbe wa kutaka kuitishwa kwa kura ya maoni kuamua mustakabali wa Zanzibar ambapo walitaka kuingia ndani na kuonana na uongozi wa baraza hilo.

Hata hivyo jeshi la polisi lilitoa tahadhari na kuwataka waondoke katika viwanja hivyo na kuelekea nyumbani ili kupisha viongozi wa wajumbe wa baraza la wawakilishi kuwasili katika baraza hilo ili waendelee na shughuli za baraza hilo ambalo jana limeakhirishwa.

Rashid Sulum Adiy ni kiongozi wa kundi hilo la wazanzibari wenye kudai kuitishwa kura ya maoni juu ya mustakabali wa Zanzibar ndani ya Muungano na anataka baraza la wawakilishi liitishe kura ya maoni ya kuwauliza wazanzibari iwapo wanautaka Muungano au hawautaki.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Aziz Juma Mohammed amesema jeshi lake limejipanga vyema na halitavumilia watu ambao wanakwenda kinyume na sheria. Kamanda alisema watu waliokwenda katika viwanja vya baraza hilo hawakufuata taratibu na hivyo jeshi halitavumilia tena vitendo ambavyo vinakwenda kinyume na sheria na litawashughulikia wale wenye kutoa lugha za matusi katika matamshi yao ambao wanaoendesha mikutano katika maeneo mbali mbali ndani ya jamii.

Katika barua yao walioiwasilisha kwa Spika Kificho ya Aprili 18 mwaka huu inasema “ Sisi ni wananchi 1825 miongoni mwa watu 300,000 sote wazanzibari na ni watu wazima wenye akili timamu kutoka majimbo 50 ya Unguja na Pemba tunakutaka utuwasilishie mbele ya baraza la wawakilishi ombi la hoja yetu binafsi ya kuwepo kwa kura ya maoni juu ya suala la Muungano wa Tanzania” ilisema barua hiyo.

Wakitilia mkazo hoja hiyo katika barua yao walisema baada ya kipindi cha miaka 48 ya Muungano hoja yao hiyo ya kuitisha kura ya maoni ni muhimu sana kwa wazanzibari na vizazi vya baadae.

Hatukubali kama tutapigwa mabomu, marungu au kukamatwa kwa sababu ya hatari inayotukabili mbele yetu. Kwa hivyo kwa heshima na tunaliomba baraza nalo lishirikiane na sisi kwa kutumiza wajibu wake na kulikubali ombi letu la kuwa na kura ya maoni juu ya Muungano” ilisema barua hiyo ambayo MWANANCHI inayo kopi yake.

Barua hiyo imesema Muungano huo umekosa misingi ya kisheria ya kitaifa na kimataifa, na ndio sababu ya kuongezeka kero na kasoro kadhaa, lawama na matatizo mbali mbali yanayoshindikana kutatuliwa kwa pande mbili hizo.

Walisema kwa kuwa Muungano huo unahusu nchi mbili tofauti, za Zanzibar na Tanganyika ni vizuri wananchi wakapewa nafasi ya kuhojiwa iwapo wanautaka uendelee au uvunjike kwani maamuzi ya wananchi ndio yanayotegemea kuendeleza usalama na utulivu uliopo.

Hivi karibuni Rais Kikwete aliteuwa tume ya kukusanya maoni juu ya katiba mpya na tayari wajumbe wa tume hiyo wameshaapishwa na wataanza kazi rasmi mwanzoni mwa mwezi ujao lakini malalamiko juu ya suala hilo yamekuwa yakijichomoza kila siku hapa Zanzibar.

Makundi mbali mbali yamekuwa yakifanya mikutano ya wazi kuelezea suala hilo huku idadi kuwa ya wazanzibari wakiunga mkono hoja ya kuwepo kura ya maoni kwanza kabla ya tume kuanza kufanya kazi zake.

 

 

 

 


Advertisements

18 responses to “Polisi wawakamata watetezi wa kura ya maoni

 1. Pingback: Wanaodai kura ya maoni ya Muungano watiwa mbaroni·

 2. Watu wanadai haki yao kikatiba mnawakamata basi futeni na sheria ya kura ya maoni mana mumeitunga wenyewe hakuna kukata tamaaa Allah anasema kila penye uzito pana wepesi naamini wepes utapatikana amin

 3. Inaonesha ni kweli pale Balozi Seif Idi aliposema CCM ndio itakayotoa katiba mpya na sio wananchi na dalili ndio hizo.

 4. Huu ni mwanzo, sasa tunatoa onyo kwa Watanganyika popote walipo Zanzibar hii waondoke tunatoa muda wa wiki moja
  20/4 – 29/4/2012, tutawasaka na tutawaonyesha ule ukweli hasa kwa kipigo cha mbwa mgeni.

  • nenda zako wewe kumbe nyie ni wabaguzi sasa watanganyika waondoke mbona nyie mnakimbilia nchi za watu kujiripua kama mataifa mengine kudai haki si kudai ubaguzi je na hao wazanzibari na walioko bara na wao waondoshwe?

 5. Na tunawapa onyo kwa wale WATU WA TUME ILITEULIWA MWANAHARAM KIKWETE kutoka Zanzibar kina Ali Salaeh, Awadhi, na wengineo tutahakikisha tutapambana nao hata kama nikupoteza maisha yetu tuko tayari kwa lolote lile kwetu sisi kufa sio tatizo.

 6. Penye nia pana njia hata kama njia itakua ndefu na nyingi vikwazo bali kwa uwezo wa Allah tutafika ISHAALLAH very soon

  • usimuweke Mungu humu wakati ni mbaguzi hata huyo Mungu unaemuabudu amesema La yanhakumullahu anilladhina lam yukatalukum fi diyn – (hamjakatazwa kuka nawema na watu wasiokupigeni vita katika dini) na vile vile wajaalnakum shuuban wakabaila litaarafu- na sio litafaraku nenda kasome uzuri sio kutumia matamshi ya kutokana hapa

 7. Vitisho na Matusi hayajengi ika yanabomoa. Je akija mwendawazimu akaanza kuwasaka wazanzibari huko Tanganyika nani ataumia zaidi?
  Jenga hoja makini na sis wazanzibari tuonekane kama watu werevu na wanaongea wanachokitaka na kueleweka.

  Punguza Jazba.

  • MKUUU wacha woga, kwani wao hawatoi vitisho kwetu? na ikiwa nikujenga hoja, hoja gani tuijenge zaidi ya kura ya maoni au tuandamane tena mpaka UN au tuende Tanganyika, wewe unadhani kwa kuandamana tu watakubali bila ya pressure yoyote, hebu angalia nchi zote zilizopitia issue kama hii walifanya nini ? Halafu na wewe upime !!!
   Wewe mwenyeo ni shahid kilichotokea 2001 mpaka tufika hapa tulipo!!

   Na kama matusi, nadhani hamna tusi lililoletwa hapa ni ukweli mtupu, na pia kuhusu Wazenji huko Tanganyika athari itapatikana kwa wao Tanganyika ikiwa uko na thinking ya kweli, na hakuna Mzenji yoyote alokwenda Tanganyika kuomba au kuuza dawa za kunguni, UPO MKUUU HAPO, WACHA TUSEME.

 8. VITISHO NA MATUSI KWELI HAVIJENGI LAKINI NA UBABE UNAOFANYWA NA SERIKALI ZOTE MBILI NAO HAUJENGI VILEVILE. HAWA WATU WANATUMIA HAKI YAO YA KIDEMOKRASIA KUPINGA MUUNGANO TENA KWA AMANI KABISA POLISI KWA KUWA WANAMFURAHISHA BWANA WANATUMIA NGUVU. HAKUNA SABABU YOYOTE YA KUTUMIA NGUVU WALA KUWASHTAKI WATU HAWA KWANI INAONYESHA WAZI KUA MCHAKATO MZIMA WA KATIBA TANZANIA UNATAKIWA UKUBALI YALE INAYOTAKA SERIKALI NA SIO WANAYOTAKA WANANCHI. KWA MANTIKI HII KIKWETE CHAGUA WATAALAM WAKO UANDIKE KATIBA UNAYOITAKA WEWE NA CHAMA CHAKO CHA CCM NA SIO INAYOTAKIWA NA WANANCHI. WANANCHI WA ZANZIBAR TUMESHASEMA KUA KWANZA TUULIZWE KWA KURA YA MAONI KAMA TUNAUTAKA HUO MUUNGANO AU LA. KIUJUMLA WAZANZIBARI MUUNGANO HATUUTAKI ILA SERIKALI NA CCM MNAULAZIMISHA TU. LAKINI SIKU SIO NYINGI MUUNGANO HUU UTAKUFA KIFO CHA MENDE KWANI WAZANZIBARI SASA TUMESHAAMKA SIO WALE MLIOKUA MKIWABURUZA MIAKAN ILE. TUTADAI HAKI ZETU MPAKA KIELEWEKE.

 9. MSIWE NA WASIWASI UMMA WA WAZANZIBARI UKO PAMOJA NANYI, NYINYI NDIO MASHUJAA WETU KWANI MMEWEZA VYEMA KUIFIKISHA UJUMBE WA WAZANZIBARI KWA ULIMWENGU MZIMA KUA MUUNGANO HATUUTAKI NA SIO WA WANANCHI BALI NI WA VIONGOZI NA VYOMBO VYA DOLA. KAMA KWELI NI WA WANANCHI WANAOGOPA KITU GANI KUUJADILI NA KUUPIGIA KURA YA MAONI? HUU NI MWANZO MZURI KWANI UKWELI SASA UKO WAZI KUA WAZANZIBARI WANALAZIMISHWA KWENYE MUUNGANO KWA MTUTU WA BUNDUKI.

 10. Pingback: Polisi wawakamata watetezi wa kura ya maoni·

 11. Kama mnaamini kuna Mungu basi dini zote zinahitaji kuwatii viongozi wa nchi Qur-an Inasema,”atiu-Allah wa atio Rassul wa ulul amri minkum”Mtiini MMungu na mtume wake na wale wenye mamlaka” Sasa hao walotumia haki yao ya kimsingi huwenda kweli wameitumia lakni pia hawakufuata ule utaratibu unaowekwa” kuna step by step na sio kulazimisha’

  Pili matusi na ubaguzi M’Mungu amekataza kwani huko Bara pia kuna Wazanzibari na ndio maana Nyerere alisema,mtadai nchi kisha mtachoma moto nyumba za wapemba kisha mtaanza hapa pia kuna wagogo,moja baada nyengine,mara wazaramo mara wamakonde.cha msingi ni makubaliano na kutumia njia za busara.

  Sote tunapenda mabadiliko na kila Mzanzibari anajua nini dhiki-pengine hajui chanzo tu pengine kuna dhiki kubwa zaidi bila huo muungano au pengine kuna faida kubwa zaidi bila ya Muungano cha msingi kwanza ni kuziweka faida zake na hasara zake kisha kupima na kuamua je kuna manufaa au matatizo-kwa kuwa uongo mmoja haufuti ungo mwenngine bali unaongeza uongo,sasa kama kuna tatizo lirekebishwe au litafutiwe ufumbuzi muafaka.

 12. Salaam Waungwana,
  Suala la kutouridhia muugano huu, muungano wa mavamizi ya Zanzibar na kumezwa Dola ya Zanzibar; Wazanzibari tangu sikumosi wameeleza wazi kabsia kutouridhia na sababu za kutouridhia, lakini watawala Dodoma wamekuwa wakipuuza sauti hizi za Wazanzibari. Badala yake wao watawala waliona njia ni kutununua baadhi yetu tuulinde huu muungano haramu. Kwa kufanya hivyo ndivyo wakatokea baadhi yetu kutamka kwamba uruhu wa Zanzibar wa Disemba, 1963 ni uhuru bandia. Pia tukafika kukubali kuunda vyama vya Taifa, yaani vinavyomilikiwa na mvamizi mtawala Tanganyika na kushurutisha kwamba “kuukataa muungano ni uhaini”. Watawala wamefanya hivi, wakisahau kwamba “khiana kuu kwetu sisi ni kuwacha kuwania wattani wetu”. Vilevile watawala hawa hawa wakatuletea ile nyimbo yao, “usitie dini kwenye siyasa/usitie siyasa kwenye dini”. Yaani muhimu ni kututaka tutenganishe baina ya DINI/SIYASA. Kweli lazima idhihiri. Umma umefahamu hakika kwamba Dini ndio Siyasa na Siyasa ndio Dini. Kutokana na hivi; leo Alhamdulliha ukombozi wa Zanzibar urejea palepale – DINI/SIYASA. Inshaallah ukombozi haukombali.

  Watawala Dodoma wamefika katika hali ya mfamaji, kukamata maji, lakini hayo maji sasa hayakamatiki, kwa sababu upepo wa ukombozi kila ukivuma inazidi kuwa maji hayakamatiki.

  Ujumbe alipewa Mhishimiwa Sita – Alipokuja Zanzibar Mhishimiwa Sita katika kikao cha Bwawani na Helisalasi alielezwa wazi kabisa kwamba ‘WAZANZIBARI MUUNGANO HUU HATUUTAKI”. Aliombwa Mhishimiwa Sita aufikishe ujumbe huu kwa Mhishimiwa Rais Kikwete. Kwa Wazanzibari, ukombozi wa Zanzibar ni wajibu wa Kidini, hivyo kwa hali yoyote ile – hali na mali – ni lazima waendelee kuwania mpaka ikomboke kwa thamani yoyote ile. Kwa Wanzibari kuridhia kutawaliwa ni muhali.

  حبّ الأوطان من الإيمان وروح الله ينادينا
  إن لم يجمعنا الإستقلال ففي الفردوس تلاقينا

  Busara na kulinda hishima na amani, TUNAIOMBA SIRIKALI ISITUMIE NGUVU, ITUMIE HIKMA NA BUSARA. Nguvu hazitatengeneza, khasara itakuwa kwa nchi. Walimwengu wapenda haqi – bado wapo Alhamdulillah sio wote wouvu – hawatapenda kuona SIRIKALI INATUMIA NGUVU DHIDI YA RAI WANAODAI HAQI YAO YA KIMSINIGI – HAQI YA KUREJEA DOLA YAO.

  NASAHA KWA NDUGU ZETU WAZANZIBARI

  ” وأعدّوا لهم مّا استطعتم مّن قوّة و من رّباط الخيل ترهبون به عدوّ الله ّوعدوّكم وءاخرين من دونهم لا تعلمونهم ، الله يعلمهم ، و ما تنفقوا من شىّء في سبيل الله يوفّ إليكم وأنتم لا تظلمون”. (الأنفال : 60).
  “Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatisha maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu, na wengineo ambao hamwajui, lakini Mwenyezi Mungu anawajua. Na mkitoa chochote katika Njia ya Mwenyezi Mungu mtarudishiwa, na wala nyinyi hamtadhulumiwa”. (Al-anfaali : 60).

  Tudai haqi yetu kwa upole na utaratibu.

  Wa Billahi Tawfiiq

  Farouk
  April, 20, 2012

 13. Jamani nihaki yetu kudai kura ya maoni kwani hiyo ndo itakuwa mkombozi wetu swala tume kuchukua maoni kila pahali na kw kuzingatia hadidu za rejea ni uwazi kua hata hiyo katiba mpya itakayokuja andikwa basi itazidi kumkandamiza mzanzibar na usishangae kuandika kw katiba hii mpya ni azma ya kuimaliza zanzibar moja kw moja na ukweli wa wazi ni pale polisi walipokwenda waondoa watu wanaodai haki yao ya halali kw mujibu wa katiba ya zanzibar ya kuitisha kura ya maoni nje ya baraza la wawakilishi askari walipotoa ilani hawakusema kua wametumwa na serekali ya zanzibar ila walisema kua wametumwa na serekali ya muungano hii inaonesha wazi kua zanzibar hatuna letu na hawa wakiamua kuifuta zanzibar kutambulika km inchi wanaweza kw kila cha zanzibar wao ndo wasimamizi na ndo wanaotoa amri nn kifanyike na nn kisifanyike ndani ya zanzibar
  angalizo: serekali ya zanzibar tuiyambia km haitakuwa makini basi wasifikiri kua watakusalama na wao juu ya hili kwa wao na viongozi na watoto wao tunawaahidi kua km ni kula dongo basi tutakula nao pamoja shame on them

 14. MAKAFIRI WAMEANZA KUWAKAMATA WANAHARAKATI WA KUDAI UHURU WA ZANZIBAR. Lakini tunamwambia mfirwa mkundu seif ali idd kuwa kama anahamu ya kukamata awakamate mabasha wanaowafira baba yake na mama yake awaache wapigania UHURU WA ZANZIBAR.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s