Brigedia Adam Mwakanjuki afariki duani

Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki wakati wa uhai wake akisalimiana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam.

Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Mwakanjuki amefariki duani jana Alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.

Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Marehemu Mwakanjuki aliwahi kuwa waziri wa kilimo na mifugo, waziri wan chi ofisi ya rais katiba na utawala bora, waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za miko na vikosi vya SMZ na mumbe wa baraza la wawakilishi kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa familia ya marehemu wamesema kwamba taarifa ya mazishi itatolewa leo baada ya kukutana wanafamilia hiyo visiwani Zanzibar.

“Ni kweli Mjomba amefariki hivi punde dare s salaam na mipango ya mazishi itapangwa baada ya kikao cha familia yetu” alisema Vicky Mwakanjuki mtoto wa Dada wa Marehemu.

Wakati wa uhai wake Marehemu Mwakanjuki alikuwa waziri mwandamizi katika serikali ya Zanzibar katika wizara mbali mbali pamoja na kuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM (NEC).

Tangu mwaka 2007 Marehemu Mwakanjuki hakuonekana katika harakati za siasa baada ya kupata ajali mbaya akitokea Dodoma kwenda Dar es Salaam katika eneo la Morogoro ambayo ilisababisha kuvunjika sehemu zake za viungo.

Licha ya juhudi za kupatiwa matibabu ndani na nje ya nchi lakini hakuweza kurudi katika hali yake ya kawaida ambapo wakati wa tukio inatokezea alikuwa akiendesha gari lake mwenyewe pamoja na mwanawe.

Mwakanjuki pia alikuwa afisa mwandamizi katika jeshi la wananchi wa Tanzania na kufikia cheo cha Brigedia Jenerali na ameongoza brigedi mbali mbali ikiwemo pia kuwa miongoni mwa waanzilishi wa jeshi la kujenga taifa JKT.

Hadi kufikia mwaka 2010 Marehemu alikuwa waziri wa mawasiliano a uchukuzi Zanzibar pamoja na kuwa mjumbe wa NEC hadi mauti yanamkuta.

 

 

 

Advertisements

13 responses to “Brigedia Adam Mwakanjuki afariki duani

  1. NINAPIGA KIGELEGELE KWA KUFA MKAFIRI HUUUUUYYYYYYUUUUU EHHHEEHHHHH WATANGANYIKA WAKINA OKELE MUNGU ATAWAONDOWA NA UHURU UTAPATIKANAAA ZANZIBAR BILA YA VIBARAAKAA SHENZI MUNGU MUWEKE MOTONII CHIINII HAWA NDIO WALIO KUWA WAKIFANYA UBAGUZI KWA WAZANZIBAR WENYEWE KWA WENYEWEEE MUNGU MPE BP SEIF ALYY IDIYY SHAMUHUNA NA MUHAMED KHATIB NA SHAMUHUNA WAFEE NA KILA ADUWI WA ZANZIBARRRRRRRR HAAAAAAAAHAAAAAAAA MWAKANJUKOIII LIMEKUFA FOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

  2. HEE jamani ni maangamizi tuu? huyu mtu si wetu tena tumuachie mwenyewe kwa yoote aliyo yafanya ni mifano mizzri kwa wale wanao ona kua siku yao haitafika, mungu ampe anacho stahiki eeeeeeemin

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s