Maximo ashauri jinsi ya kupata wachezaji bora wa timu ya taifa

Kocha wa zamani wa Taifa Stars Marcio Maximo akisalimiana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete alipokwenda kumsalimia Rais katika hoteli ya Tivoli jijini Sao Paulo.

Vilabu vya soka nchini vimeshauriwa kuwa na timu nzuri kuanzia ngazi ya watoto wenye umri wa miaka nane, vijana na kuendelea ili kupata timu bora ya Taifa. Wito huo umetolewa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Star Marcio Maximo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Sao Paul. Maximo alisema kuwa timu nyingi ambazo ni bora na zinafanya vizuri katika mchezo wa soka zimekuwa zikiwaandaa watoto wenye vipaji vya mchezo huo wangali wadogo ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadaye.
Kocha Maximo pia alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho kikwete, ambapo alimnshukuru sana Rais kwa ushirikiano wa hali ya juu aliompa wakati alipokuwa akiifundisha Taifa Stars miaka takriban mitatu iliyopita. Kwa upande wake Rais Kikwete alimpongeza Kocha Maximo kwa juhudi zake za kuendeleza soka la Tanzania, akimwambia uwepo kwake Tanzania kuliasidia sana kuiweka nchi katika ramani ya mchezo huo.
Rais Kikwete alikubaliana na kocha huyo kwamba ili timu ya Taifa ifanye vyema ni lazima maandalizi yaanzie ngazi za chini, ikiwemo vilabu kuwa na timu za watoto na vijana ambao baadaye watakuwa hazina ya Taifa Stars. Kuhusiana na uvumi ulioenea kuwa anataka kwenda kufundisha timu za Taifa Stars, Azam na Yanga alisema kuwa siyo kweli na wala hajawasiliana na timu hizo na hawezi kwenda kufundisha kwani hivi sasa anamkataba wa kufundisha timu ya Democrata iliyopo nchini humo.
Rais alimshukuru Kocha Maximo kwa kuja kumsalimia na kumpa zawadi ya jezi ya timu ya Democrata anayofundisha, na kumtakia heri na fanaka katika kazi yake hiyo.
“Timu ya Taifa Star ina kocha mzuri ambaye ninamuheshimu na ninaukubali ufundishaji wake hivyo basi kupitia kocha huyo ninaamini watanzania watazidi kuendelea katika soka na kufika mbali zaidi”, alisema.
Maximo alimalizia kwa kusema kuwa anamawasiliano mazuri na watanzania na anawapenda ndiyo maana kila mahali anapopita anajivuna na kusema kuwa Tanzania ni nchi yake ya pili. Hivi sasa Maximo ni kocha wa timu ya Democrata iliyopo nchini humo ambapo wiki ijayo inatarajia kuanza mashindano ya taifa yatakayopelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki mashindano ya kombe la Dunia yanayotarajia kufanyika mwaka 2014 nchini Brazil.

Advertisements

2 responses to “Maximo ashauri jinsi ya kupata wachezaji bora wa timu ya taifa

  1. Aslam aleikum,
    Huyu Jakaya hanampango wowote anakwenda kuonana na Wabrazil anashindwa kuonana na Watanzania! tumempigia simu balozi aache rohombaya kilakiongozi akija hapa anamficha asionane na sisi, mpaka Shamsi Vuai alipokuja na Mizingo pinda kashindwa kuonana na Wazanzibar hawa ndio viongozi wa Mungano.

    Na marahii kaja Jakawa na yule waziri wa Zanzibar walahi wametukimbia atumewafuata hoteli waliyofika tukadai Zanzibar yetu hii ndio faida ya Mungano.

  2. Nimefurahi kuwa Rais Kikwete ameonana na Kocha wa Zamani wa Timu ya Taifa ya Bara. Mheshimiwa Kikwete kubali kuanza kufanya mpira kuwa ajira ili Watanzania wengi wapate ajira. Hii itawasaida sana wasio na Godfathers wa kuangiza Serikalini kwenda kufuja au kuiba mali za Umma. Kuna watoto wengi ambao wana vipaji lakni mfumo wa sasa wa usimazi wa Soka haufai. Na Wapenda Soka wenzangu pia lazima tujue kuwa Mpira ni gharama. Watu wengi leo wanataka maendeleo ya Soka lakini ni wakubwa wa kutaka kuingia mpirani bure! Wakati wa Mashindano ya Kombe la Mapinduzi 2012 nilishangaa kuona watu wanaona mechi kwa Tshs. 3000.00 na hizi wengi hawalipi wanasubiri fungulia mbwa. Katika hali ya kawaida ni bora mtu kuangalia mechi kwenye TV akaruhusu walio na pesa walipe na waaangalie mechi. Mapato makubwa yaliyodhibitia yanaweza kusaidia uwekezeji kwenye maoneo mengine. Sijui kwa nini vilabu vikubwa haviuzwi kwa matajiri na kisha wakauza hisa kwa watu wengine. Mpira wa kadi haupo tena. Watu washabikie lakini walipie kuona mechi!

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s