Fungu Mbaraka ni mali ya Zanzibar

Hii ni sehemu moja ya eneo la bahari ya Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kisiwa cha Fungu Mbaraka kipo umbali wa maili kadhaa katika bahari kuu

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba Kisiwa cha Fungu Mbaraka bado ni mali yake licha ya kuwepo kando ya Zanzibar. Kauli hiyo imetolewa jana aktika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Mjini hapa kufuatia suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mwakajuni (CCM) Mbarouk Wadi Mussa Mtando aliyeka akujua kisiwa hicho ni mali ya nani kati ya Zanzibar na Tanzania bara.
Waziri wa Ardhi, Makaazi na Nishati, Ramadhan Abdallah Shaaban aliwambie wajumbe wa baraza hilo kwamba ni kweli kisiwani hicho kipo mbali na Kizimkazi lakini tokea asili ni mali ya Zanzibar.
“Fungu Mbaraka ni mali yetu na Zanzibar mwaka 1992 serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilikwenda kuweka bendera yake hapo na hakuna hata mtu mmoja aliyeuliza kwa nini ikaweka bendera hapo, ingawa watu wanaweza kujitokeza wakasema ni mali ya upande wa pili kwa kuwa kipo mbali na Kizimkazi” alisema Waziri huyo.
Kisiwa cha Fungu Mbaraka kipo katika bahari kuu Mashariki ya Zanzibar ambapo eneo la bahari kuu lote ni miliki ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Awali Mwakilishi huyo alitaka kujua Zanzibar ina visiwa vingapi ukiacha vile vikubwa vya Unguja na Pemba, ambapo Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Haji Mwadini Makame alijibu kuwa kuna visiwa 62 ambavyo ni mali ya Zanzibar na visiwa 28 vinazunguka kisiwa cha Unguja na Visiwa 34 vinazunguka kisiwa cha Pemba.
Aidha akijibu shughuli za visiwa hivyo kama ambavyo Mwakilishi alitaka kujua, Naibu huyo alisema visiwa hivyo vidogo vidogo vinatumika kwa shughuli mbali mbali ikiwemo makaazi akitoa mfano kisiwa cha Tumbatu na Uzi kwa Unguja na Kojani na Kisiwa Panza kwa upande wa Pemba.
Alivitaja visiwa vyengine ambavyo hutumika kwa shughuli nyengine ambazo pamoja na utalii, kilimo, hifadhi ya wanyama kama ndege na wanyama wengine wakiwemo kasa. Makame akivitaja visiwa amabvyo hutumika kwa utalii ni pamoja na Kisiwa cha Chagwe, Bawe Chumbe na Misali kwa Pemba ambacho kina utajiri mkubwa wa ufugaji wa kasa na mambo ya kali pamoja na matumbawe yaaina mbali mbali yenye kuvutia watalii wengi na wanafunzi kutoka nchi mbali mbali kuja kufanya utafiti na kusoma.
Aidha akijibu suali la Mwakilishi wa Nafasi wa Wanawake (CCM) Asha Bakari ni visiwa vingapi vilivyouzwa Naibu huyo alisema serikali haijauza hata kisiwa kimoja kwani sera ya serikali ni kuvikodisha na sio kuviuza.

 

Wajumbe watakiwa kujenga imani na serikali
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi wametakiwa kujenga imani na serikali yao kwani lengo la serikali ni kutekeeleza ahadi zake zote zilizoahidi kwa wananchi wake.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu, Issa Haji Usi alipokuwa akijibu suali la Nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni (CCM) Mbarouk Wadi Mussa aliyetaka kujua mpaka lini ahadi za serikali zitatekelezwa kikamilifu.
Naibu huyo alisema licha ya upungufu wa fedha za majeti lakini serikali lengo lake ni kutekeleza ahadi zote ambazo wananchi wake wameahidiwa ikiwemo utengenezaji wa miundimbinu ya barabara katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Awali Mwakilishi huyo alisema wizara ilipotaka kuongeza barabara iendayo Nungwi katika eneo linalopakana na uwanja wa mpira wa Banyamulenge katika kijiji cha Potoa, ilikubaliana na wenye kiwanja kwamba waipitishe barabara hiyo huku eneo la uwanja huo lipanuliwe kwa kusafishwa eneo la upande wa pili katika uwanja huo.
Aidha Mwakilishi huyo katika masuala yake ya msingi alitaka kujua lini wizara itafanya kazi ya upanuaji wa eneo la uwanja ili uwanja huo uweze kutumika ipasavyo.
Ambapo Naibu Waziri alijibu kwamba eneo linalotaka kuongezwa huo ni eneo lenye mawe magumu na hivyo kunahitajika zana zenye nguvu na uwezo wa kufanya shughuli hiyo.
Ussi alisema kwa muda mrefu zana ambayo ilitegemewa kuwa ifanye kazi hiyo ilikuwa imeharibika na matengenezo yake yatafanyika katika kipindi cha muda usio mrefu.
Matarajio ya matengenezo hayo Ussi alisema yatakamilika ndani ya mwaka huu wa 2012 ambapo aliwaomba wajumbe wa baraza hilo kusaidiana na wizara katika kufanikisha malengo yake.
Akijibu sababu za msingi zilizochelewesha upanuzi wa kiwanja hicho, Ussi alisema sababu kubwa ni kushindwa kufanyika kwa wakati ni pamoja suala la gharama kutokana na ukweli kwamba gharama hizi zilizoambatanishwa na gharama nyengine za fidia za vipando na miti ya kilimo.
Naibu waziri huyo alikiri kwamba kuchelewa kutokamilika uwanja huo ni kweli kwenda kinyume na azma ya serikali ya kuendeleza masuala ya michezo lakini pia kukuza vipaji vya wanamichezo hao waliopo katika jimbo la Mkwajuni.
Aidha Mwakilishi huyo alitaka kujua ni sababu gani zinazosababisha ucheleweshaji wa ulipaji fidia unaofanywa na serikali kwa wale watu ambao katika maeneo yao kumekuwepo upasuaji wa miamba na kuathiri nyumba zao kwa kupasuka.
Naibu alisema wizara ya miundombinu na mawasilaino haikusiki moja kwa moja na ulipaji wa fidia ya nyumba zilizoathirika katika maeneo ya upasuaji wa miamba.
Ussi aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba serikali kupitia wiraza yake inawaomba na kuwaelekeza wananchi waathirika wa zoezi hilo, kwenda kufikisha malalamiko yao hayo kwa kampuni husika ya MECCO. Ili kupata majibu ya ufafanuzi unaostahiki.
Alisema Wizara ya miundimbinu na mawasiliano inatambua uzito wa suala hilo ambapo aliahidi wizara kuratibu na kufuatilia kwa karibu ili kuona haki inatendeka kwa kuhakikisha yale malipo yanayostahiki kwa wananchi yanafanyika.

 

Ubebaji wa nyama begani

JUMLA ya watu 187 wakiwemo wachukuaji na wauzaji wa nyama ya ngombe na kuku wamepima afya zao katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Hayo yameelewa na Waziri wa Afya Zanzibar, Juma Duni haji aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi katika kikao kinachoendelea Mbweni Mjini hapa.
Akiuliza suali la msingi Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub alitaka kujua wafanyakazi wa uuaji na uchukuaji nyama wamepima afya mara ngapi na sababu gani zinazowafanya kutovaa sare maalumu katika kazi hiyo.
Akijibu swali hilo Waziri Duni alisema wauzaji wa nyama wanatakiwa kupima afya zao mara moja kwa mwaka na kuhusu uvaaji wa sare yataanza kuchukuliwa hatua wakati kanuni ya nyama itakapotangazwa katika gazeti rasmi la serikali.
Awali Mwakilishi huyo alitaka kujua wizara ya Afya ina mpango gani wa kudhibiti vitendo vya wachukuzi katika soko la Darajani kubeba nyama begani bila ya kuzingatia kanuni za Afya.
Waziri Duni alisema pamoja na kuwa kanuni za nyama bado hazijatoka katika afisi ya mwanasheria mkuu, lakini bodi ya dawa na vipodozi inaendelea kuwapatia elimu ya usafi wachukuzi hao juu ya masuala ya ubora na usalama wa chuakula ikiwemo na nyama.
Akitaja hatua kwa ajili ya wachukuzi wanaobeba nyama bila ya kufuata utaratibu alisema utachukuliwa mara baada tu ya kanuni za kusimamia mambo hayo ya nyama na usafi wake kwa ujumla zitakapotoka kutoka afisi ya mwanasheria mkuu wa serikali.
Wakati huo huo Waziri Duni alisema serikali ina mpango wa kupeleka huduma karibu na jamii chini ya mpango wake wa ‘out rich programme’ ambapo wataalamu wake ni kutoka hospitali kuu ya mnazi mmoja.
Alisema chini ya mpango huo wataalamu hao huweka siku maalumu kwenda kutoa huduma nje ya hospitali hiyo kuwepo katika hospitali nyengine na baadae watu kutangaziwa wafike kupata huduma katika kituo hicho kilichochaguliwa.
Alisema huduma hiyo hutolewa katika kituo cha kitogani na Kivunge kila baada ya wiki mbili ambapo sambamba na hilo pia kwa kushirikiana na umoja wa watu wenye ulemavu kuna siku maalumu inayoandaliwa kwa ajili ya kuwahudumia watu wneye ulemavu.
Awali Mwakilishi wa Nafasi za Wanawake (CCM) Raya Suleiman Hamad aliyetaka kujua iwapo zahanati, kliniki au hospitali zinazotoa huduma na marekebisho kwa watu wenye ulamavu hapa Zanzibar.
Akijibu suali hilo Waziri Duni chini ya sheria Namba 9 ya mwaka 2006 ya watu wenye ulemavu kifungu cha 11 kinaeleza mtu mwenye ulemavu ana haki ana haki ya kupatiwa huduma ya afya na kuchukuliwa hatua za kumkinga na jambo linaloweza kumpa ulemavu ambapo kimsingi alisema anakubalaina na hilo.
Alisema kifungu hicho kipo na ndio maana majengo ya hospitali yote sasa yanayojengwa huwekwa ngazi ambazo zinaweza kupandisha kiti cha magurudumu ambacho kinatumiwa na watu wenye ulemavu ‘Ramp’ kwa ajili yao.
Duni alizitaja hospitali zenye kutoa huduma kwa watu wenye ulemavu kuwa ni Hospitali ya Abdallah Mzee, Chake Chake na Wete.
Alisema katika upande wa kliniki ni kitendo cha uchuwaji ‘Physiotherapy’.

Kitengo cha mafunzo ya kazi kwa vitendo ‘Occupational Theraphy’ na kitengo cha marekebisho ya viungo na mifupa ‘Orthopaedic Therapy’.

 

 

 

 

Advertisements

9 responses to “Fungu Mbaraka ni mali ya Zanzibar

 1. Maneno ya Mheshimiwa kuwa Kisiwa hiki kina bendera ya Zanzibar toka 1992 hayatoshi. Tunahitaji kujiuliza kisiwa hiki kinatumiwa vipi kwa faida ya Zanzibar. Jambo jengine ambalo lingehitaji kuuulizwa ni kama kuna taratibu za kisheria za Zanzibar kujimilkisha. Suala la kuwa toka Enzeli halifai kwani Zanzibar toka enzeli ni ya Wazanzibari lakini leo imeshawatoka na wanaiskia tuu kuwa ni yao.

 2. Ni kweli hapa jawabu la waziri linaonyesha wazi kua kisiwa sio mali ya Zanzibar. Kuchomeka bendera tu sio umiliki sio hasha ukasikia hapo Waume za watu wana hati miliki napo wanakaa kimya subiri yaonekane mafuta hapo utakavyosikia mambo.Waziri atupe uthibitisho ni vipi Zanzibar inamiliki kisiwa hicho.

 3. HAPA HAKUNA JAMBO LA MAANA LILILOZUNGUMZIWA.YOTE HAYA NI MANENO YA WATU WANAOPOTEZA WAKATI KATIKA DUNIA, BADALA YA KUZUNGUMZIA MASUALA YA KUIKOMBOA ZANZIBAR KUTOKA KATIKA UKOLONI WA TANGANYIKA WANAZUNGUMZIA KUHUSU VISIWA NI MALI YA ZANZIBAR AU TANGANYIKA. Kwa ufipi visiwa na bahari ya znz ni mali ya TANGANYIKA. Watanganyika wamenunua visiwa hivi kwa SHAMHUNA NA HATI MILIKI ZOTE WANAZO.

 4. WAFIRWA WA BARAZA LA WAWAKILISHI HEBU MUSIZUNGUMZIE KUHUSU MALI ZANZIBAR KWANI ZANZIBAR HAINA MALI HATA MOJA KWANI KILA RAIS NA WAZIRI ANAEKAA MADARAKANI ZNZ HUUZA CHAKE ANACHOKITAKA Dr. SALMIN KAUZA VISIWA, AMANI KAUZA MAJENGO YA SMZ SHAMHUNA KAUZA BAHARI, VIFAA VYA TVZ NA STZ, SHEIN ATAUZA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA NA IKULU ZIWE HOTEL ZA KITALII. Kilichobakia ni kukodishwa kwa MAHAKAMA KUU YA VUGA KUWA DANGURO LA MAKAHABA NA MASHOGA NA BARAZA LA WAWAKILISHI KUFANYWA UKUMBI WA SHEREHE ZA FREE MASON NA KUFUNGISHA NDOA ZA WATU WA JINSIA MOJA. SMZ HAIMILIKI HATA TOILET PAPER LEO HII IWE NA UWEZO WA KUCHIMBA MAFUTA. Ewe mwakilishi muongo 1992 zanzibar haikua na bendera sema UKWELI KUWA MULICHOMEKA BENDERA YA TANZANIA MSENGE MMOJA WEWE. Hadi leo hii hakuna bendera ya zanzibar bali kuna bendera ya wizara ya znz kutokana na bendera ya znz kufanana na bendera za wizara zote za TZ bendera zote za TZ zina kibendera cha muungano ndani yake kinachoashiria wizara za TZ.

 5. Jamani leo hii Zanzibar imefikia watu kuandika matusi namna hii ? Kama hakuna mtu wa kuzuia basi hata Mwenyez Mungu hatumuogopi ?
  Kitu gani kimetusibu jamani ? Elimuimekuwa,?Wasomi wameongezeka ? au tuseme ni Uhuru wa kutoa mawazo ?.
  Jee kama tutaendelea kutukanana namna hii ndio tutapata haki zetu hivi? Kwa nini tumekuwa waovu,washenzi na wajinga kuliko hata wanyama ?.
  Kuna faida gani tunayopata tukiandika matusi na watoto wetu ,pamoja na Wazee wetu wakisoma ,wewe ulioandika unajisikiaje kwa tabia hiyo ?,
  Ushauri wangu ni kuwaomba tuwe wastarabu na tulinde mila na desturi zetu hata kama tumeudhiwa , hakuna lisilokuwa na mwisho , na Haki ni nazi kavu haiwezi kuzama itakuja juu tuu,
  Mkono utakuwa ni shahidi wako ,kwa ulicho kichuma,kuandika na kila kiungo kitakukalia ushahidi basi tujiepushe na shari jamani waislamu.

  • @issa
   wewe mwenyeo umeanza kutukana “washenzi na wajinga kuliko hata wanyama” hebu toa daawa ili vijana wakuelewe unachoongea wacha kurudia matusi ulioyakataza.

 6. Sometimes hawa wajamaa wanatia ghazabu mpaka mtu unakua out of controll ndo maana vijana wanatukana.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s