Muda muafaka kubadili mfumo wa muundo wa Muungano

Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, na Makamu wake wawili, Maalim Seif na Balozi Seif Idd, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Viongozi wateule na wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi. Tume hiyo inatarajia kuanza kazi rasmi Mei 01, mwaka huu

Juma Mohammed

Sasa la mgambo limelia kuna jambo kubwa Tanzania, Katiba mpya inakuja shime Watanzania kujitokeza kwa wingi kutoa maoni katika Tume hiyo huku tukitanguliza uzalendo mbele katika kuhakikisha tunapata katiba yenye tija kwa pande zote mbili za Muungano. Hoja ya Tanzania kuwa na Katiba mpya ni kilio cha muda mrefu,wengine waliokuwa wakipaza sauti kudai hivi sasa hatunao tena, wametangulia mbele ya haki na wengine wapo hivi leo watatembea kifua mbele kuona kuwa jambo walilokuwa wakilipigania sasa limekuwa,nalo ni Tanzania kupata katiba mpya.

Wakati tukijiandaa kutoa maoni katika Tume ya Katiba ni vizuri pia kuzungumzia mustakabali wa mfumo wa muundo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao katika kipindi chote cha uhai wake umekumbana na misukosuko ya kila aina.

Bila shaka wengi tunakubali kuwa muundo wa sasa una kasoro,kasoro ambazo zinahitaji kurekebishwa kwa kuweka mfumo mwengine wa muundo wa Muungano na kwa jinsi upepo unavyovuma wengi wanapendekeza kuwepo na Muungano wa Mkataba kama ilivyo ule wa Umoja wa Ulaya.

Ni jambo lisilokuwa na ubishi kuwa muundo wa Serikali mbili haufai na ndio maana Tume zote mbili zilizoundwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania takriban miongo miwili iliyopita zilikubali na kutoa mapendekezo ya kubadili mfumo wa muundo wake.

Rais wa awamu ya Pili Tanzania,Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliunda Tume mwaka 1991 iliyoongozwa na Jaji Francis Nyalali ambayo ilikuwa na wajumbe 22 kati ya hao kumi kutoka Zanzibar na wengine kumi kutoka Tanzania Bara.

Baada ya Tume kukamilisha kazi yake,Wajumbe nao walitoa maoni yao ambapo kati ya 22, wajumbe 12 walipiga kura ya ndio kukubali mfumo wa muundo wa Muungano uwe wa Serikali tatu sasa huku wengine 7 walikubali uendelee muundo wa Serikali mbili. Katika ripoti ya Tume ya Nyalali utaona wajumbe watatu wao hawakupiga kura kabisa.

Tume ya Jaji Nyalali ilijenga hoja kwamba chini ya muundo wa Serikali mbili kuna mambo ni magumu utekelezaji wake,wakitaja suala la Uraia,milki ya fedha za kigeni,ukusanyaji na mgawanyo wa mapato kutokana na kodi na ushuru wa forodha,tatizo la fomula ya kuchangia gharama za uendeshaji Serikali ya Muungano.

Mwaka 1998,Rais wa awamu ya tatu,Benjamin William Mkapa aliunda Tume iliyoongozwa na Jaji Robert Kisanga,ikapeleka kwa wananchi waraka wa Serikali maarufu Whitepaper , kama ilivyo kwa Tume ya Nyalali, Tume hii nayo ikarudia yale yale kuwa muundo wa Serikali mbili haufai.

Ripoti ya Jaji Kisanga imesema kasoro za Muungano zilizobaki hazirekebishiki. Maana yake ni kwamba kuna hitajika mfumo wa muundo wenye kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye utakaokuwa tiba ya matatizo mbalimbali.

Chini ya muundo wa Serikali mbili matatizo yamezidi kuongezeka licha ya kuwepo kwa kamati za kushughulikia matatizo hayo,lakini bado mambo yameonekana kutokwenda sawia.

Katika kipindi cha miaka 48 ya Muungano wenye muundo wa Serikali mbili,wapo watu Zanzibar wanaeleza bayana kutokuona faida ya kiuchumi huku wakijenga hoja kwamba kwa muda zote malalamiko yamekuwa ni yale yale ambapo sasa wanaona njia pekee ya kumaliza hali hiyo ni kuwa na muundo usiosababisha manung’nuniko kwa kila upande,hawana nia ya kuvunja Muungano.

Muundo wa sasa una mambo ambayo utekelezaji wake unasababisha malalamiko,kwa mfano suala la Zanzibar kujiunga na Jumuiya za Kimataifa nalo linazungumzwa ni tatizo na wanataja kisa maarufu cha OIC.

Mara baada ya Zanzibar kujiunga na OIC, Kamati Kuu ya CCM Agosti 10 mwaka 1993 ilitoa uamuzi wa Zanzibar ijitoe kwenye Jumuiya hiyo,Rais wa Zanzibar,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hasiwe Makamu wa Rais Tanzania, kupinga Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Nyalali.

Wakati CCM ikitoa uamuzi huo, Wabunge 44 wa Majimbo ya Tanzania Bara walijiandikisha kuwasilisha hoja binafsi kutaka Serikali ya Tanganyika na hoja yao ilionekana kuungwa mkono na kundi kubwa la wananchi na hata baadhi ya Mawaziri.

“Nilipokwisha kuhakikishiwa kuwa sasa sera ya Serikali Tatu ndiyo sera rasmi ya Bunge la Muungano na Serikali ya Muungano, niijaribu kupata maelezo kutoka kwa viongozi wetu;lakini sikufanikiwa” anasema Nyerere katika kitabu chake uongozi na hatma ya nchi yetu.

Kikao cha Bunge cha Agosti 14 mwaka 1993 Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Rais Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu John Samwel Malecela walikwenda Bungeni kuzima hoja ya kuanzishwa Serikali ya Tanganyika, Zanzibar kujitoa OIC na kufuta Rais wa Zanzibar kutokuwa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mabadiliko ya 11 ya Katiba ya Muungano ya mwaka 1994 yaliongeza tatizo latika mfumo wa sasa kwa kuwepo kwa mgombea mwenza kwenye Uchaguzi wa Rais mabadiliko ambayo wanasheria wanayataja kuwa yalivunja makubaliano ya Muungano ya 1964 kwa kumuengua Rais wa Zanzibar ambaye ni mshirika sawa kutokuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.

Mfumo wa uchaguzi haufahamiki kama ni wa Westminster yaani wa Kiingereza au ule wa Presidential System wa Marekani wanaokuwa na mgombea mwenza,huku tukiwa na Waziri Mkuu.

Kasoro kubwa katika muundo wa Serikali mbili ni kuwa mfumo huo ulijengeka katika misingi ya Chama kimoja cha siasa, ‘State Party’ ambapo mwaka 1992 mfumo wa Chama Dola ukafa kwa hivyo nguzo za muundo wa Serikali mbili ukawa unakasoro lukuki.

Inaonekana wazi kuwa wakati ule CCM ilikuwa ikiogopo upande mmoja wa Muungano kikishinda Chama cha Upinzani itakuwaje uendeshaji wa Serikali hiyo kwa ushirikiano mzuri ndio maana kwa woga huo ndio yakafanyika marekebisho ya Katiba na kuweka mgombea Mwenza.

Kama ingelikuwa ni nyumba basi imebakia nguzo moja ambayo ni muundo wa Serikali mbili uliokuwa na ufa na kila siku tunaona jinsi nguvu ya nguzo hiyo zinazidi kupungua na kufanya haja ya kuwa na muundo mujarab kwa mazingira ya leo na kesho ya Muungano katika dhana ya kuwa na Muungano wa treaty.

Muundo wa Serikali mbili kimsingi ulibuniwa kwa haraka haraka wakati ule kama inavyofahamika Zanzibar ndio kwanza Mapinduzi yamefuzu na Jamhuri ya Tanganyika ikiwa na miaka mitatu tangu kupata Uhuru wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1961, hivyo kwa kuwa imepatikana fursa ya Katiba mpya ni muda muafaka kubadili mfumo wa muundo wa Muungano kuwa wa kiuchumi zaidi.

Hilo likitendeka litaufanya Muungano kuwa wenye madhubuti na wenye kuvutia nchi nyengine kujiunga na hatimaye kuwa na nguvu kubwa ya kiuchumi , Kwa mfano dai mojawapo la wapenda mabadiliko ni kuwa Waziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano anaposhughulikia jambo linalozihusu pande zote mbili, kuna uwezekano mkubwa wa Waziri huyo kuipendelea Nchi yake ya asili(Tanganyika)

Lakini pia Wazanzibari wapenda mabadiliko wanahoji hivi inakuwaje kasma za bajeti zinalundikwa pamoja kwa serikali ya Muungano na Tanzania Bara bila ya kutafautishwa?

Ukiacha suala hilo,lakini kuna jambo jengine la kuongezeka na kupungua kwa madaraka ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ukitolewa mfano wa kuunganishwa kwa Afro Shiraz Paty na Tanganyika African Union mwaka 1977.

Kabla ya kuunganishwa vyama,jambo hilo lilikuwa ndani ya uwezo wa Zanzibar,lakini kama tunavyoelewa hilo lilikuwa ni miongoni mwa mambo yaliokuja kuelezwa ni katika kuimarisha Muungano,lakini jambo la kukumbuka ni kwamba vyama vya ASP na TANU havikuwa sehemu ya mambo ya Muungano mwaka 1964.(tazama mapatano ya Muungano).

Wengi wanakumbuka mkasa uliompata Rais wa Pili wa Zanzibar,Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi alipotakiwa kujiuzulu na Chama Dola Chama cha Mapinduzi kule Dodoma mwaka 1984.

Katika hati ya Muungano,CCM haikutajwa kuwa ni mshiriki katika Muungano huo na wala sio Chama cha TANU au ASP vilivyotajwa zaidi ya nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar.

Wataalam wa mambo ya katiba wanasema kwamba kwa sababu hiyo, CCM haina ubavu wa Kikatiba kujiingiza kisheria na kulazimisha haki na wajibu wa Muungano kwa upande wa Tanganyika, Zanzibar au Jamhuri ya Muungano.

Wengi wanahoji vipi CCM ilimuondoa Rais wa nchi aliyechaguliwa kwa mujibu wa sheria ambaye ni mshirika sawa katika Serikali ya Muungano?CCM haikuwa sehemu ya mambo ya Muungano.

Wadadisi wa mambo wanatafsiri hatua ya kumshinikiza Mzee Jumbe ilikuwa sawa kudhalilisha Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 yalioondoa uonevu,dhulma na manyanyaso, kwa kweli kushinikizwa kuachia ngazi kwa Mzee Jumbe ilikuwa ukiukwaji mkubwa wa mkataba wa Muungano na pia kuwadhalilisha Wazanzibari na Kiongozi wao.

CCM kwa kuelewa walikosea walipomwondoa Jumbe madarakani,CCM hiyo hiyo iligeuka na kuunga mkono hoja za Mzee Jumbe kuhusu Serikali tatu na uthibitisho ni kalipio la Mwalimu Nyerere kwa Halmashauri Kuu ya CCM mwaka 1993

Katika Kikao cha NEC kilichofanyika Mjini Dodoma Oktoba 14 mwaka 1993, Mwalimu Nyerere alikemea vikali hoja ya kutaka Serikali tatu ambayo wakati ule ilionekana wazi ikiungwa mkono na kundi kubwa la Wabunge na wanasiasa wengine.

“Nilipouliza kwanini hawakupinga hoja ya Serikali tatu kama tulivyokubaliana,majibu ya viongozi wetu wakuu yalikuwa ni ajabu kabisa. Ati wabunge wenye hoja baada ya kuonana na mimi Msasani walikwenda Bungeni wakiwa wakali kama mbogo” anasema Nyerere katika kitabu chake.

Miongoni mwa mashujaa katika uamuzi wa Serikali tatu wakati ule ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ambaye alikubali kusoma alama za nyakati licha ya CCM kupinga,lakini kwa kuwa Muungano sio jambo la CCM Serikali ya Mwinyi ilikubaliana na hoja ya Wabunge wa kundi la 55(G55).

Hatimaye Julai 30 mwaka 1993 Wabunge 55 walitoa taarifa Bungeni kusudio lao la kutaka Serikali tatu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na walijenga hoja ya msingi juu ya kushindwa kwa Serikali mbili. Hoja ya G 55 ni sawa na hii ya sasa ya Wazanzibari wanaotaka Muungano wenye maslahi kwa pande zote ukitilia maanani mabadiliko ya mfumo.

Katika hoje yao walisema “kwa kuendelea mfumo huu wa Muungano usiowaridhisha wananchi wengi wa upande mmoja(Tanganyika) ni kuhatarisha kuendelea na kudumu kwa Muungano na pia kuathiri uelewano kati ya watu wa pande zote mbili”.

Tunawaheshimu waasisi wetu ambao wameunganisha Mataifa huri mawili na kuunda Taifa moja lenye nchi mbili,lakini pia kizazi cha leo kina haki ya kufanya marekebisho katika muundo wa Muungano huo.

Kamwe chini ya muundo wa Serikali mbili kila siku kutazuka malalamiko kwa kuongezeka matatizo,lakini kama ilivyokuwa mazowea kila likizuka jambo litazimwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete atamaliza muda wake huku akiandika historia ya kuwapatia Watanzania katiba mpya

Advertisements

9 responses to “Muda muafaka kubadili mfumo wa muundo wa Muungano

  1. WAZANZIBAR TUWE TAYARI KUMWAGA DAMU ZETU NA DAMU ZA MAKAFIRI WA TANGANYIKA ILI TUPATE UHURU WA ZANZIBAR KWANI TUKITEGEMEA VIONGOZI WA SMZ KUTUPATIA UHURU WA ZANZIBAR BASI TUELEWE KUWA UHURU WA ZANZIBAR HAUTAPATIKANA MILELE KWANI NI UKWELI USIOFICHIKA KUWA VIONGOZI WA SMZ WALIOWENGI HAWAKUCHAGULIWA NA WANANCHI WA ZANZIBAR BALI WAMEIBA KURA. Ni lazima tuyafafanue kwa kina maneno aliyoyasema SHOGA SEIF ALI IDD pale alipowapinga wanaharakati wa kiislam wanaodai UHURU WA ZANZIBAR -2012. Maneno haya hakukurupuka kusema bali haya ndio makubaliano yaliyokwishapitishwa na vibaraka wa tanganyika kuwa ZANZIBAR NI KOLONI LA TANGANYIKA. Lakini wazanzibar lakufanya ni kuhakikisha kuwa tunashirikiana kuutaarifu ulimwengu kwa kutumia njia za mitandao kama vile facebook, marafiki email n’k kila siku juu ya nchi yetu kutawaliwa kuwa KOLONI LA TANGANYIKA KIPINDI AMBACHO UN IMEPIGA MARUFUKU UKOLONI DUNIANI. Hakika vibaraka wa TANGANYIKA watashindwa tu. Ukiona wanasema ujue ujumbe umewafika kuwa WAZANZIBAR HAWAUTAKI MUUNGANO NA MAKAFIRI WEUSI WA TANGANYIKA. Mzanzibar huu ndio muda muafaka wa kushirikiana kudai UHURU WA ZANZIBAR.

  2. HAKIKA ZANZIBAR NI KOLONI LA TANGANYIKA NA VIONGOZI WA SMZ NDIO CHANZO CHA ZANZIBAR KUWA KOLONI LA TANGANYIKA. Kwahivyo, mzanzibar usimpe kura yako kiongozi wa smz aliyeifanya zanzibar kuwa koloni la TANGANYIKA.

  3. HUU SIO MUDA MUAFAKA WA KUBADILI MFUMO WA MUUNGANO WA TANZANIA BALI HUU NDIO MUDA MUAFAKA WA KUUVUNJA MUUNGANO WA TANZANIA. Kwani hata muungano ukirekebishwa lakini bado vibaraka wa Tanganyika wapo katika SMZ kwahivyo, hakutakuwa na mabadiliko yoyote kwa upande wa zanzibar. SULUHISHO NI ZANZIBAR KUPATIWA UHURU TU SIO JENGINE KWANI ZANZIBAR BILA YA KUPATA UHURU HAIWEZI KUENDELEA MILELE. Mzanzibar usimchague kiongozi wa smz ambae ni KIBARAKA WA TANGANYIKA hebu msikilize mwakilishi uliemchagua kwa kumpa kura yako anavyozungumza mambo ya USHOGA katika baraza la wakilishi ” mh. Spika kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 7/USHOGA.USENGE YA BARAZA LA UFIRAJI ZANZIBAR NINATAMKA KUWA WATANGANYIKA WANAHAKI YA KUNUNUA ENEO LA BAHARI YA ZANZIBAR LILILOPAKANA NA MIKUNDU YETU NA PIA, AJIRA ZA UTALII ZA KUTUFIRA WAWAKILISHI ZIWE ZA TANZANIA NA SIO ZA ZANZIBAR NA MAFUTA YA ZANZIBAR YASICHIMBWE MPAKA WAFIRWA WENZETU WA TANGANYIKA WAKUBALI”.

  4. Hata iwe vipi matuamaini ya kufanikisha matakwa ya wazanzibari waliowengi ni madogo. Jambo la kwanza la kufanya iwapo nia na madhumuni ya washika hatamu za serikali ni safi basi wangeingilia kati tatizo kunyimwa vipande vya Zanzibar mkaazi wananchi wa Zanzibar. Likiweza kutatuka suala hilo basi kwa kiasi fulani wazanzibari wangejenga matumaini kwenye zoezi hili vyenginevyo ni sawa na kutuburuza kuelekea kule kunakotakiwa kufikishwa. Allahu Qaadir.

  5. Pingback: Muda muafaka kubadili mfumo wa muundo wa Muungano·

  6. Wacha wawape vipande hao wanaowataka lakini wajue hao vibaraka na mamluki wao hapa hawatopiga kura wakati ukifika. Wametudanganya vya kutosha kwa ajili ya maslahi yao na matumbo yao huku sisi na watoto wetu tukifa njaa na maradhi yanayotibika. Sasa tunawambia basi na tukisema basi tuna maana ya basi. Hao hawatopiga kura hapa na wataondoka wenyewe muda ukifika. Mzanzibari popote pale ulipo unaona ni kiongozi gani anaeiuza Zanzibar na ni chama gani ambacho kinaiuza Zanzibar kwa bei ya rejareja. Sasa kazi kwako ukifika wakati wa Uchaguzi wape kura waimalize KUIUZA Zanzibar au wanyime kura KUINUSURU Zanzibar. Kura zetu ndizo zinazowapa jeuri hii hivyo tuwanyime kura kikwelikweli ili nchi yetu TUITOE KWENYE UKOLONI WA TANGANYIKA.

  7. Tume hii iliyoundwa itafanyakazi kwa sheria batili. Kwanini watu wasiende Mahakamani kudai Mahakama iizuie kufanyakazi Zanzibar. Katiba zote mbili zimekiukwa na Sheria hii namba 8

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s