Serikali yatoa tamko kuhusu eneo la bahari kuu

Kutoka kulia ni Mhe. Zakhia Meghji ( Mb), Bw. Sergei Tarassenko ambaye ameshika sehemu ya nyaraka za Andiko la kudai eneo la maili 61,000 za bahari, Mhe. Waziri Anna Tibaijuka ( Mb), Mhe. Ombeni Sefue, Balozi wa Tanzania Katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Abulrahman Hassan Shah (Mb) na Bw. Ayoub Mohamed Mahmoud Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Ardhi, Makazi na Madini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia alimwakilisha Waziri wake katika hafla hiyo.

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU HOJA YA MAOMBI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUONGEZEWA ENEO LA UISHIO WA NCHI BAHAINI (EXTENSION CONTINENTAL SHELF)

Mheshimiwa baada ya kumshukuu Mwenezi Mungu (S.W) nakushukuru na kukupongeza wewe mwenyewe kwa uongozi wako makini wa Baraza letu. Uongozi wako umesaidia kujenga demokrasia umakini ndani ya Baraza ambayo ndiyo iliyopelekea leo nisimame mbele ya baraza hili tukufu kutoa tarifa hii rasmi ya Serikali.

Pili niwashukuru waheshimiwa wajumbe wa baraza lako tukufu kwa michango na maoniyao katika usimamizi sio tu wa chombo chetu hichi lakini pia katika uendeshaji wanchi yetu.

SABABU ZA KULETA TARIFA.

 

Mheshimiwa Spika.

Katika kikao kilichopita cha Baraza, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitoa ahadi mbele ya Baraza hili tukufu ya kulitafakari suala lamaombi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanazania kuongezewa eneo la Uishio wa ardhi baharini (Externsion of Continental Shelf ). Aidha Serikali iliahaidi kwamba baada ya kulitafakai suala hili itoe tarifa mbele ya Baraza hili tukufu.

Mheshimiwa Spika

Pamoja na ahadi hiyo ya Serikali Mheshimiwa Ismail Jusa .alitoa hoja mbele ya Baraza hili tukufu ya kutaka shauri hili lizungumzwe na baraza kwa vile ni jambo muhimu na la dharura. Katika hoja yake hiyo alipendekeza wakati Serikali itakapolizungumza shauri hili, izingatie baadhi ya mambo yaliyoainishwa katika hoja yake hiyo kufuatia hoja hiyo baraza lako tukufu liliamuakamaifuatavyo:

Mheshimiwa Spika ,

aliwahoji waheshimiwa wajumbe.

“Waheshimiwa wajumbe sasa niwahoji wale wanaokubaliana na hoja ya Mhe Ismail Jussa Ladhu, Kwamba masuala hayo yakazingatiwe na Serikali na baadae kutuletea taarifa kama tulivyokubaliana mwanzo, ikichanya pamoja na lile suala la kuiomba serikali isimamie yale maazimia ambayo yalikuwepo kama ni pendekekezo  la ziada wanyanyue mkono (hoja iliamuliwa na kuafikiwa ….uk 74 Hansard.

Mheshimiwa Spika.

Napenda kuliarifu baraza lako tukufu kwamba, Serikali ya Mapinduzi yaZanzibarkupitia kikao cha Baraza la Mapinduzi  cha tarehe 14 Januar 2012 ilitafakari shaurihilopamoja na mazimio ya baraza kufuatia hoja ya Mhe Ismail Jussa kufuatia mazimio hayo Serikali inawasilisha tarifa hiikamailivyoahidiwa.

UFAFANUZI WA DHANA YA SHERIA ZA BAHARINI EEZ NA  UISHIO WA NCHI BAHARINI (CONTINANTAL SHELF)

Mheshimiwa Spika dhana ya ukanda maalum wa kiuchumi bahaini (Exclusive Economic Zone) na dhana uishio wanchi katika bahari (Continental shelf) pamoja na mfumo mzima wa sheria za ndani na za kimataifa inazongoza suala hilo ni dhana za kitaalamu sana na vile vile ni mpya kwa kiasi fulani. Kwa sababu hiyo kwamba naomba nitangulize kwa kutoa ufafanuzi kwa urefu kidogo, kuhusu dhana hizo ili waheshimiwa wajumbe wapate faida ya kufahamu vyema kiini hasa cha shauri hili.

Mhe spika kwa mujibu wa makubaliano ya kitaifa ya sheria za bahari, nchi yenye kupakana na bahari (Coastal state) na haki ya bahari kwa sehemu tatu Kwanza, Sehemu ya maji ya kitaifa ya bahari lenye upana wa maili za bahari (nautical miles ) kumi na mbili (12NM) .

Katika eneo hili nchi husika ina mamlaka yote ya kiutawala sawa na nchi kavu. Pili ni eneo la ukanda malum la kiuchumi (Exclusive Economic Zone) lenye upana usiozidi maili za bahari mia mbili (200NM) Kimsingi hili ni eneo la bahari ya Kimataifa, lakini nchi husika ina haki ya kipekee  ya kuvuna mali na rasilimali zote zilizomo na kuchukua hatua za kiulinzi na za kimatumizi ya rasilimali hizo lakini nchi haina mamlaka yote ya kiutawala sawa na eneo la bahari ya nchi.

Eneo hili pia hutambuliwa kuwa eneo la bahari ya kimataifa lakini watumiaji wake wanatakiwa kuheshimu mamlaka ya nchi husika kuhusiana na uvunaji, ulinzi na uhifadhi wa  rasilimali zilizomo.

Tatu ni eneo la uishio wa ardhi ya nchi baharini (extended Continental shelf) Kitaalamu inaminika kwamba eneo la nchi kavu baada ya ufukwe mara nyingi ardhi ya nchi hiyo haishii kwenye ufukwe wake huzama kwa maili nyingi kuelekea baharini.

Kwa kuwa ardhi hii iliozama na ile iliyobaki kuwa ni nchi kavu ina jiolojia (mfumo wa miamba ) ya aina moja ,ni dhahir kwamba kwa pamoja rasilimali ya ardhi iliozama na iliyobaki kihistoria ni milki ya nchi hiyo moja.

Kwa wastani mwisho huu wa ardhi baharini hukadiriwa kuwa hizo maili mia mbili (200NM) Ndio maana kumekuwa na dhana kwamba EEZ na Mwisho wa  Ardhi Baharini (Continental shelf) ni kitu kimoja .lakini kuna nchi ambazo mwisho wa ardhi yake baharini ni zaidi ya 200NM .

Hapo ndipo nchi hiyo hupewa fursa ya kudai mwisho huo wa adhi yake bahaini kwa maili mia moja na hamsini (150NM) zaidi .

Katika eneo hili nchi ina haki sawa zile zilizonazo ndani ya eneo la ukanda maalum wa kiuchumi (EEZ) isipokuwa nchi nyengine nazo zimepewa haki kubwa zaidi ya matumizi ya eneo hili.Kwa mfano haki ya kuvua na kutandika nyaya za chini ya bahari.

Aidha eneo hili kwa mujibu wa Ibara ya 86 ya Mkataba wa umoja wa Mataifa wa sheia ya baharini wa 1982 ni sehemu  ya bahari kuu (high sea) tofauti na EEZ ambayo  haitambuliwi kuwa ni shemu ya bahari kuu ingawa ni sehemu ya maji ya Kimataifa .

Mheshimiwa Spika.

Ili kufahamu vyema dhana hii ni vyema pia kuelewa taratibu za kupata au kutambuliwa kisheria kwa nchi kuwa mmiliki wa maeneo ya bahari tuliyoyataja.

Kwa upande wa eneo la bahari ya nchi (territorial waters ) ni kwa nchi yenyewe tu kuitambua mipaka yake hiyo kwa kukubaliana na  majirani zake ili kuondoa mzozo wa mipaka, Baadhi ya nchi  hufatisha hatua hiyo kwa kupitisha sheria ya mipaka yake ya bahari (territorial water deli. mitation law)

Kwa upande wa eneo EEZ, nchi husika baada ya kulitambua na kusawazisha masuala ya maingiliano ya mipaka na jirani zake ,hupitisha sheria ya kulitambua na kuanisha mamlaka yake kisheria ndani ya eneo hilo .Kwa upande wa Jamhui ya Muungano wa Tanzania ,utaratibu  huu wa kuitambua na kutangaza mamlaka ulifanyika kupitia sheria ya EEZ ya mwaka 1989.

Mheshimiwa Spika.

Kwa upande wa eneo la uishio wa ardhi baharini, utaratibu wake wa kulipata  ni tofauti kabisa kwani lazma nchi itimize vigezo vya kitaalamu,kama vifuatavyo:

Kwanza lazima sehemu  ya mwambao wa nchi husika iwe imeingia baharini kimaumbile (natural submarine prolongation of the land mass of the coastal state) .pili lazima uwepo uthibitisho wa kitalamu wa mipaka ya eneo hilo ulioambatanishwa na michoro ya maumbile ya miamba .

Taarifa za kijiolojia (geodetic date ) na taarifa nyengine muhimu ambao umewasilishwa kwa maandishi kwa mamlaka husika ya umoja wa Mataifa kama ilivyoelezewa na ibara ya 76(9) ya mkataba awa Umoja awa mataifa wa sheria ya bahari. Tatu lazima nchi husika iwasilishe madai rami ya uhalali wake wa eneo hilo kwa chombo mahususi cha umoja wa mataifa kilichopewa dhamana ya kushuhulikia utambuzi wa eneo hilo .

Nne madai hayo lazima yawasilishwe ndani ya muda maalum ulioawekwa kwa nchi zote na muda mahsusi uliowekwa kwa kila anchi hivyo ni dhahri kwamba utaratibu wan chi kudai mwisho wa ardhi baharini kuitwa kuwa ni upanuzi wa eneo la EEZ ni mazoea tu lakini ukweli halisi na wa kitaalamu ni kwamba.

Kinachofanyika ni kudai (To claim)- sio kuomba onezeko la mwisho wa adhi ya nchi husika baharini (Extension of the continental Shelf ) na wala sio kuongeza neo la EEZ kwani hakuna kitukamahicho katika sheria za bahari.

Usimamizi wa masuala ya madai ya Onezeko la mwisho wa Ardhi baharini uko chini yakamisheni ya Ukomo wa mwisho wa Ardhi Baharini(Commision on the limites of the Continental Sheif –CLCS ) iliyo chini ya Divisheni ya masuala ya baharini na sheria ya bahari (Division for Ocean  Affeirs and the low of the sea –Doalos ) kamisheni  hii ndio msimaizi wa utekelezaji wa kifungu namba 76,aya  4-7 ya makubaliano hayo, ambazo ndizo zinazoruhusu madai ya nyongeza za mwisho wa  Ardhi ya nchi baharini kwenye utekelezaji wa zoezi hili, kamisheni hii ilitoa agizo kupitia hati yake namba DOALOS/07-01406 ya tarehe 14 Agst 2007 kuzitaka nchi zote wanachama ambao hazijatangaza nia ya kudai nyongeza ya mwisho wa ardhi zao baharini ziwe zimeiarifu Sekriterieti ya kamisheni azma hiyo si zaidi ya tarehe 30 Novemba 2007 nchi 27 ziliitikia wito huo ikiwemo Jamhuri ya Muunano wa Tanzania.

Kadhalika kwa hati namba SPLOS/INF/20 ya tarehe 16 Januar 200, Kamisheni ikatoa atiba ya muda wa kila nchi kuwasilisha maombi yake kwa mujibu wa ratiba hiyo, Jamhuri ya Muunano wa Tanzania ilitakiwa iwe imewasilisha maombi yake kabla ya Mei 2009 ilifanya hivyo tarehe 5 Mei 2009 ,na ikatakiwa iwasilishe rasmi andiko la madai yake ifikapo taehe 13Mei 2011.

Mhe spika, kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo tishio la uharamia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa barua namba CGA336/358/01/77 ikaomba iongezewe muda hadi Tarehe 13 Novemba 2011 hata tarehe hiyo pia haikuwezekana na hatimae Jamhuri ya Muunano wa Tanzania ikapewa muda wa mwisho wa tarehe 17 Januar 2012.

Miongoni mwa sababu za utaratibu huu ni kuratibu maombi ya nchi zinazozunguka eneo moja na pia kuiwezesha kamisheni kujipangia ratiba ya kukamilisha kabisa madai ya nchi wanachama .miongoni  mwa maombi yaliyopokelewa kuna nchi kadhaa za Muungano wa aina mbali mbali .

Lakini kwa zote hizo, maombi yaliyopelekwa ni kupituia kwa nchi wanachama wa Umoja wa mataifa, si nchi au himaya zilizoungana .Nchi kama Canada (disemba 2003 ) Uingereza (kama United kingdom of Great Britain and Northern Ireland ) na Urusi (2001) ni miongoni mwao.

Mheshimiwa spika maaelezo yaliyotangulia hapo juu yanadhihirisha mambo .

1.   Jamhuri ya Muunano wa Tanzania haiombi kuongeza EEZ ya               bali inadai kuongeza mwishio wa adhi yake baharini.

2.   Nchi nyingi zinazopakana na bahari,bila ya kujali haliyaoya kiuchumi ,kijamii na kisiasa ,zimeona haja ya kudai nyongeza hii ya mwisho wa ardhi zao Baharini .Hivyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikukosea kufanya hivyo:

3.   Mawasiliano yote ya umoja wa mataifa juu ya maswala haya hufanywa na nchi wanachama wa Umoja wa mataifa walioridhia makubaliano ya Kitaifa ya sheria za baharini na sio himaya au Dola moja moja nje ya Muungano wao.

4.   Muda wa madai ya upanuzi wa mwisho wa ardhi baharini una ukomo na kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumevumilia sana hadi Januari mwaka huu kutoka Mei 2011 ,Haya ni madai ,sio maombi ,na kwa hivyo hayana namna ya kusitishwa utaratibu uliopo hautoi fursa hiyo.

5   Eneo linaloombwa kuongezewa si la nchi yoyote nchi isipokubaliwa au hata ikijitoa ,litaendelea kubaki kuwa ni la mataifa yote:

6,   Kwa nchi zilizoungana mikataba na maridhiano yao  ya ndani juu ya mipaka ya kila mmoja wao haibadilishwi na ongezeko la mwisho wa ardhi baharini .Ongezeko lenyewe ndani ya Muungano wao litatafsiriwa kwa mujibu wa mchango wa kila mmoja kwenye nyongeza hiyo.

Mhe Spika baada ya maelezo ,hatuna budi sasa kuangalia hoja mbili muhimu kama zifuatavyo.

a)   Je maombi hayo ya  Jamhuri ya Muunano wa Tanazania ya kuongezewa ukomo wa uishio wa bahari ni kwenda kinyume na mazimio ya Baraza la wawakilishi ya tarehe 4 April 2009

b)    Ni kwa kiasi gani maazimio ya Baraza la wawakilishi ya tarehe 4 April 2009 yametekelezwa na matokeo ya utekelezaji wake:

HOJA YA OMBI LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWENDA KINYUME NA MAAZIMIO YA BARAZA LA WAWAKILISHI YA TAREHE 4 APRIL 2009.

Mheshimiwa spika ,mazimio ya Braza la wawakilishi ya tarehe 4 April ,2009 yalitokana na hoja ya Tarifa ya SMZ kuhusiana na mapendekezo ya Uendeshaji wa kazi na Uchimbaji wa mafuta na Gesi asilia Zanzibar ambayo ilitolewa  na waziri wa Maj , Ujenzi, Nishati na Ardhi , Mhe Masoor Yusuf  Himidi tarehe 3/4/2009. taarifa hiyo nayo ililetwa mbele ya baraza la Wawakilishi kutokana na maelekezo ya Baraza la Mapinduzi ya  tarehe 27-3-2009 ambayo yalitolewa baada ya kujadili  waraka namba 225/2009 kuhusiana na ripoti ya mwisho ya mshauri mwelekezi juu ya ugawaji wa mapato na gharama za railimali ya mafuta na Gesi asilia ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .

Kikao hichi kilipitisha mamuzi ya kukubali mapendekezo matatu ambayo ndiyo pia yaliyoletwa mbele ya Baraza la Wawakilishi kupitia Hoja ya Mheshimiwa Waziri wa Maji ,Ujenzi Nishati na Ardhi .Mapendekezo hayo ni kama ifuatavyo.

1.   Adhi na bahari ya Zanzibar, maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar sura ya kwanza, kifungu cha 2(1) ni miliki ya Zanzibar. Katika maeneo hayo, usimamizi, udhibiti na uendeshaji wa shughuli zote zinazohusiana na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia uwe wa Zanzibar pekee kama katiba yetu na matakwa ya Wazanzibari yanavyoeleza.

11.  Serikali inashauri nyinyi waheshimiwa kuwa sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo chake cha kusimamia mambo yote yanayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia …

111  Pendekezo la tatu kwa upande wa bahari kuu (EEZ)  Serikali inashauri baraza la Wawakilishi kukubali mashirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa eneo hili pekee (Hansard ya tarehe 3 April,2009 ,ukurasa wa 61-62 ).

Mhe spika baada ya kuwasilisha mapendekezo hayo baraza hili tukufu liliridhia mapendekezo mawili kati ya hayo matatu, Kwa  upande wa pendekezo la tatu baraza halikuafiki na badala yake liliazimia kuwa hata katika eneo la ukanda maalum wa kiuchumi wa bahari kuu (EEZ) suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia  liwe chini ya mikono ya Zanzibar.

Mheshimiwa spika maeleazo yaliyotangulia yanadhihirisha yafuatayo.

a)   Kwamba vyombo vyote viwili baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi havijawahi kujadili Hoja ya umiliki au usimamizi wa Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari Kuu na wala havijawahi kupitisha maamuzi yaZanzibar kumiliki au kuendesha ukanda huo. Kilichojadiliwa na vyombo hivyo viwili na hatimae kutolewa azimio na baraza hili tukufu ni matumizi ya ukanda huo kuhusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia kwa upande wa Zanzibar.

b)   Kwa kuzingatia maelezo yaliyotangulia kwamba kinachodaiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuongeza ukubwa wa mwisho wa ardhi baharini (extension of Continental helf) na sio ukanda maalum wa Kiuchumi wa Bahari kuu (EEZ).

c)   Kwa kuzingatia kwamba hata nyongeza hiyo ikipatikana hapo baadaye, haitaathiri madai wala maslahi ya Zanzibarkatika suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia katika ukanda Maalum wa Kiuchumi na pia katika eneo la ziada linaloombwa.

Mhe Spika ni wazi kuwa maombi ya sasa ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya kuongezwa eneo la ziada la uishio wa ardhi ndani ya bahari hayapingani wala kuathiri Azimio lolote la Baraza hili tukufu katika mazimio yaliyopitishwa na baraza tarehe 4 April 2009 kuhusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia.

HOJA YA MAAZIMIO YA UTEKEEZAJI WA MAZIMIO YA BARAZA LA WAWAKILISHI YALIYOTOKANA NA HOJA YA MHESHIMIWA ISMAIL JUSSA LADHU.

Mheshimiwa Spika kama nilivyotanguliza kueleza kwamba, Serikali kupitia Baraza la Mapinduzi ilipojadili hoja ya maombi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuongezewa eneo la ziada la uishio wa nchi baharini, lilitafakari pia mambo yote yaliyoelezwa katika Hoja ya Mheshimiwa Ismail Jussa Ladhu pamoja na Maazimio ya Baraza hili tukufu yaliyofuatia Hoja hiyo.

Mhe Spika ufuatao ni ufafanuzi wa maazimio hayo na maelekezo ya Serikali katika utekelezaji wake.

1    Serikali ya Mapuinduzi ya Zanzibar iliandikie rasmi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitaka isimamishe mchakato wote wa maombi ya kutaka kuongezewa ukanda wa bahari kuu ,yaani (Externaded Continental shelf) kwa zaidi ya maili za baharini ( nautical miles ) 200 za Exclusive Economic Zone (EEZ) hadi hapo suala hilo litakapopatiwa ufumbuzi wakati wa mjadala wa katiba mpya.

Mhe Spika Katika kutafakari hoja na azimio hilo Serikali ilizingatia mambo matatu makubwa .

Kwanza  kama ilivyokwishatanguliwa kuelezewa,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiombi bali inadai nyongeza ya mwishio wa ardhi yake baharini kwa maili za baharini 150 na si maili hizo 200 zilizotajwa kwenye azimio hili Aidha Tanzania haiombi nyongeza ya EEZ kwa vile hakuna utaratibu huo katika sheria za Kimataifa ,ila Inadai kuongezewa mwisho wa Ardhi yake baharini.

Pili tunapaswa kujiuliza kama Jamhuri ya Muungano waTanzaniainaweza kusitisha mchakato huo. Majibu kamatulivyotangulia kueleza katika maelezo ya utangulizi ni kwamba Jamhuri ya Muungano haiwei kufanya hivyo kwa vile mchakato wenyewe unatakiwa ufanyike sio tu katika muda maalum lakini ndani ya muda mahsusi kwa nchi na nchi.

Hivyo iwapo Jamhuri ya Muungano itasitisha mchakato huo itakuwa imeondoa madai yake jambo ambalo litakuwa ni hasara kubwa zaidi kwa Zanzibar ambayo inategemea zaidi bahari kwa uchumi wake wa sasa na baadaye.

Tatu ni vyema tujiulize kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itasitisha mchakato huo Zanzibar itaweza kuja kuomba tena kuongezewa eneo hilo ambalo sasa Jamhuri ya Mungano waTanzania inalidai? Jibu la wazi ni kwamba Zanzibar haitoweza kufanya hivyo kwa vile kwanza haina uwezo huo chini ya sheria za kimataifa .

Pili itakuwa imepitwa na wakati tatu ni kazi inayohitaji gharama kubwa na nne ni kazi ambayo inahitaji kushauriana na mataifa mengine ya jirani jambo ambalo ni dhahiri mataifa hayo jirani hayatakuwa tayari kufanya hivyo. Kwa mfano katika mchakato wa kuandaa ombi la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania serikali ya Muungano ilifanya makubaliano na Kenya ,Comoro na Msumbiji ,Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kenya zilitiliana saini makubalianoa mwaka 2009 Aidha kwa mipaka ya Comoro na Msumbiji makubaliano yalituiwa saini tarehe 5 Disemba ,2011 na mkataba na nchi za sheli sheli unatarajiwa kutiwa saini kabla ya Mei mwaka huu ,Kwa ujumla ni wazi waheshimiwa kuwa haitakuwa kwa maslahi ya Zanzibar kufanya hivyo

2. Iwapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano haitachukua hatua za kusimamisha machakato huo basi serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipeleke ujumbe wake na barua rasmi Umoja wa Mataifa kuutaka usimamishe kushughulikia mambo hayo hadi hapo suala la mchakato wa katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakapomalizika na kukubaliana maeneo ya ushirikiano na maeneo ambayo kila upande utayasimamia wenyewe.

Mheshimiwa Spika kwanza ilivyoelezwa hapo awali mchakato huu ulianza tokea mwaka 2007 ambapo Jamhuri ya Muunano wa Tanznia ilitakiwa kutangaza rasmi nia yake ya kuomba eneo la ziada la uishio wa ardhi baharini Tokea wakati huo hatua kadhaa zimechukuliwa kuendeleza mchakato  huu hatua ambazo sio tu zina gharama ya fedha lakini zinahitaji utaalamu wa hali ya juu kama nilivyozieleza hapo juu .

Pili mchakato huu tokea ulipoanza mwaka 2007 uliridhiwa na Serikali ya Mapinduzi yaZanzibarna kwa vile hakuna madhara kwa maslahi yaZanzibarkatika suala hili hakuna sababu wala haja ya kuchelewesha mchakato huu.

Tatu ni dhahir kuwa jamhuri ya Muunano wa Tanzania itakuwa na kutambuliwa kuwa mmiliki wa eneo hilo la ziada ,haizuii kujadili matumizi na hata usimamizi wa eneo hilo wakati wa mchakato wa katiba mpya .

Kamailivyotangulia kuelezwa mchakato huu hauwezi kuisubiri nchi itakapokuwa tayari.

3.   Srikali ya Mpinduzi yaZanzibaritake Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzaniakusitisha shughuli zote ambazo zinahusiana na kutumia rasilimali zilizomo ukanda wa bahari kuu (EEZ) hadi hapo swala hili litakapomalizwa baina ya pande mbili.

Mheshimiwa spika katika kutafakahari kipengele hichi Serikali imeazinatia mambo yafuatayo.:

a)   tunaposema Serikali ya Jamhuri ya Muungano izuie shughuli zote katika eneo hili tunakusudia hata shuhuli za uvuvi na matumizi mengine ya eneo hili.

Na jee zuio hilo litaihusu Zanzibar kama hivyo ni sawa nivyema tutanabahi kuwa eneo hilo linatumika kwa shuhuli nyini ikiwemo uvuvi wa wananchi ,usafiri wa ndani na wa kimataifa ,utandazaji wa nyaya za mawasiliano n.k .Baadhi ya shuhuli hizo ni haki ya jumuiya ya Kimataifa chini ya sheria ya kimataifa ya Bahari lakini pia  hata Zanzibar inalitumia eneo hilo kwa shughuli mbali mbali .

Hivyo haitawezekana kuzuiya shughuli zote katika eneohilokwa sababu ni kinyume na sheria na athari itatokea kwa pande zote mbili.

b)   katika shughuli za uvuvi wa bahari kuu Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano zina makubaliano maalum katika eneo hilo kwa upande wa mapato mgao ni asilimia 40 kwa  Zanzibar na Asilimia 60 kwa Tanzania bara aidha makao makuu ya mamlaka ya uvuvi wa bahari kuu yamejengwa Zanzibar na tayari leseni kadhaa zimeshatolewa kwa hivyo haito wezekana kusitisha shughuli zote katika eneo hilo.

4   Iwapo hatua hazitachukuliwa kuhusiana na mambo hayo basiZanzibarhaitofungika na chochote kitakachoamuliwa kuhusiana na mambo hayo ambayo hayakushughulikiwa naZanzibaryenyewe.

Mhe spika kwa vile serikali ya Mapinduzi yaZanzibarhaioni haja ya kuiandikia barua serikali ya Jamhuri yaTanzaniakama ilivyopendekezwa katika hoja ya azimiohilo,msingi wa hoja hii bila shaka nao hautokuwepo.

5. Serikali ya Mapinduzi yaZanzibarisimamie mazimio ya utekelezaji wa mazimio ya baraza yaliyopitishwa tarehe 4 April ,2009.

Mheshimiwa Spika wajibu wa Serikali kusimamia utekelezaji wa mazimio ya Baraza kwa kuzingatia katiba na sheria nyengine za nchi Hivyo katika hili serikali imehimiza taasisi zote husika kuchukua hatua muafaka ili kutekeleza mazimio hayo ,miongoni mwa hatua hizo ni kuitishwa kikao cha pamoja baina ya serikali ya Muunano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uenyekiti wa makamo wa rais wa Jamhuri ya Muunano .

Katika kikao hicho masuala yaliyojadiliwa  ni pamoja na suala la kukamilisha taratibu za kikatiba za kulitoa sualahilokatika Muungano pande hizi mbili zimepeana muda malum wa kulishughulikia suala hili.

Mhe Spika mwisho nimalizie kwa maelezo yaliyotolewa na baadhi ya wajumbe kwamba mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati alifanya makosa kwa kutoliarifu baraza la Mapinduzi juu ya mchakato wa maombi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuongezewa eneo la ziada la uishio wan chi  baharini .

Kama niivyotangulia kueleza kwa urefu hapo awali kwamba mchakato huu ulianza rasmi mwaka 2007 ,katika mwaka huo ndipo uamuzi wa kisera ulipotakiwa kufanywa na serikali ya Muungano wa Tanzania

Na Pia Serikalin  ya Mapinduzi Zanzibar kwani ndipo uamuzi wa kuomba na kuomba kwa utaratibu gani ulipotakiwa kufanywa.Serikali imeridhia kwamba kumbukumbu ziliopo zinathibitisha kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar iliarifiwa na kuafiki juu ya ombi hilo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Spika hatua zote zilizofuata baada ya hapo zilikuwa z ni utekelezaji wa mamuzi hayo ya msingi ya kisheria yaliyofanywa mwaka 2007 Hivyo uwasilishaji wa andiko la maombi hayo ya jamhuri ya Muungano waTanzaniayalikuwa ni ya utekelezaji na sio ya kisera ambayo yangehitaji mamuzi au maelekezo ya baraza la Mapinduzi.

Hivyo haikuwa lazima sualahilokujadiliwa na baraza la Mapinduzi kabla ya andikohilokuwasilishwa katika Umoja wa mataifa.

Hata hivyo Seikali imeagiza kwamba tarifa za mambokamahayo muhimu ya kitaifa ziwe zinawasilishwa katika baraza la Mapinduzi ili kuiwezesha Serikali yote nzima kupata tarifa hizo muhimu.

Mheshimiwa spika mwisho napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru kwa dhati waheshimiwa wajumbe wa Baraza hili tukufu kwa imani ,uzalendo na ari waliyoonyesha juu ya kulinda na kutetea maslahi nchi yao ya Zanzibar .Ingawa katika kujadili suala hili  maneno na kauli zilizotumika zilionekana kali na inawezekana ziliwakwaza baadhi ya wahusika katika kujadili suala hili muhimu hata hiyo namini yote yalikuwa kwa nia ya kujenga .

Naamini tarifa hii ambayo imefafanua suala hili kwa kina itatuejesha katika safu ya pamoja ya kusimamia na kutetea maslahi ya nchi yetu na watu wake .

Aidha bila ya shaka tutakuwa tumejifunza kwamba linapotokea jambo lenye shaka , kuitaka serikali ilifanyie kazi na kutoa taarifa mbele ya baraza hili tukufu ni utaratibu wa busara na unaofaa kutumika .

Mheshimiwa spika baada ya maeleazo hayo naomba kuwasilisha .

Advertisements

24 responses to “Serikali yatoa tamko kuhusu eneo la bahari kuu

 1. ichi ya zanzibar ndo ishafirika kwa nini tusubiri mchakato wa katiba wa kuja kujwa nani mmliki wa eneo hilii tanganyika weshajuwa kuna mali wataliwacha hapa sheria msumeno yakata mbele na nyuma

  • Ahsante kwa taarifa bi Salma ! isipokuwa kuna makosa ya kiuandishi madogo madogo ambayo wakati mwengine inabidi yarekebishwe ishallah ili ipate kuleta ladha nzuri ya report muhimu kama hizi!shukran!

 2. PUMBAF MMESHAUZA NCHI HALAFU MNATULETEA BLABLA ZA KIJINGA KWA VILE MNAFAIDIKA NYINYI NA FAMILIA ZENU. BADO HAPA INAONEKANA KUNA TAARIFA MUHIMU MNATUFICHA NA KUTUDANGANYA. HAIWEZEKANI HATA SIKU MOJA WATANGANYIKA WADAI ENEO HILO BUREBURE HALAFU MTWAMBIE ZANZIBAR NDIO ITAYOCHIMBA MAFUTA. HUU NI UONGO MTUPU LAKINI HISTORIA ITAKUJA KUWASUTA.

 3. Hakika taarifa ni ndefu lakini inatishia yamani ya Wanzanzibari kwa maelezo haya mimi binafsi nimepata khofu kubwa na sasa najiuliza ivi Zanzibar kama nchio inamalizika hivi hivi kwa mujibu wa Taarifa Nchi yetu iliridhi hili na sasa isubiriwe katiba mpya kufanya nini ama kweli mfa maji hawachi kutapa tapa .kwa muelekeo huu nikweli TUMEKWISHA

 4. Imefikia wkati sasa sisi wazanzibari tujue yapi ni mambo ya muungano ambayo si ya muungano je wanzanzibari hawana uwezo wa kusimamia mambo yao wenyewe badala yake kushirikiana kwa kila jambo enye maslahi na zanzbaar tu. mbona kuna madini na maziwa tele tanzania bara wazanzibari wanafaidika nini kuhusiana na hayo.Hii ndoa ya mbwamwitu na kondoo itatupeleka pabaya. waznzibari tuwe makini.

 5. Hii ya kuwa Zanzibar haitaweza kudai kwa kuwa haina sifa kwa mujibu wa sheria za Kimataifa ndio inauma. Ivi mtu akiwa na na ngombe wake anahitaji apate kibali cha mtu kummuza. Rafiki yangu AG wewe nakujua toka tukiwa Skuli ulikuwa mtu wa kusema kwa uwazi. Iweje leo useme kwa mafumbo kama bwana Msa au Shaban Robert. Watu wangapi wanavunja Sheria za Kimataifa leo na hatuoni kunachofanyika kuwaadhibu. Ivo wakati Jeshi la Polisi lilivyotumika kuwauwa watu Pemba Sheria za Kimataifa hazikuvunjwa? Wavunjaji hadi leo wanatanua na wengine hata hupewa kazi za Umoja wa Mataifa. Tulifikiri shida hii kipi ni changu kipi ni chetu ingemalizwa na mchakato huu wa Katiba. Majibu tayari yapo. Shida haitakwisha. Tume iliyoundwa na kujazwa Wanasheria mwisho wake itachukua sura ya Kisiasa, kama ile ya Kisanga, Marehemu Nyalali na nyenginezo. Karl Marx Nyuma alisema kuwa ” It is not the consciouness of men that determines their being, but, on the contrary, their social being that determines their consciousness.” Mambo yanaenda Zanzibar katika ngazi zote inaonyesha ukweli wa matamko ya Marx. Uundaji wa Tume na wajumbe wa Zanzibar tayari unaonesha kufuata mkondo huu wa nadharia ya Marx.

  Wakati wa Kutaja majina Mheshimiwa alisema kuwa “ilikuwa kazi ngumu kupata majina bora kwenye orodha kubwa ya mapendekezo.” Mbona hii si kweli. Kwenye choices kubwa huwezi kuchagua watu wasiojulikana na hata wanaowakilisha au kupata watu wachovu na wanajishughulisha na NGOs za karafuu japo wao si wakulima wa karafuu. Ivi hawa aliwapendekeza nani. Ni kwa nini majina haya hayakupelekwa Barazani kujadiliwa kisha kupitishwa? Ivo hawa ni watu wanaokubalika na kila mzanzibari kua wana sifa za kitaaluma na integrity kiasi cha kuwa wanaweza kusimama mbele za watu kujisifia sifa hizo. AG hii ni changamoto yako kwa siku za mbele!

  Kuhusu Tibajuka na ombi lake sisi wote tunashangaa. Kama mambo yake mliyajua kwa nini Baraza in the very nationalistic tone lilitumia pesa na muda kujadili vitu ambavyo majibu yake yapo. Ivo Wawakilishi waliolishikia bango suala hili hamkuliona? Hii hamjui kuwa itawaporomoa kisiasa na kuonekana waongo!

  Katika hali inayoendelea sasa mtafanya watu wakubaliane na hoja kuwa “BARAZA la WAWAKILISHI sasa ni la kina Halikuniki”. Halikuniki kwenye maigizo utaona anampiga mkewe kumbe wote lao moja.

  Mjadala huu kuhusu ombi la Tibaijuka ulichukua sura ya kiutaifa lakini kumbe ilikua ni starehe za Halikuninki tu. Sisi ambao tunaitumikia nchi hii kwa kipato kidogo na bila maslahi baada ya kustaafu inatuuma sana tukiona pesa za nchi ambao raia zake wagaiwa hata vyandarua zinafujwa kujadili mambo ambayo majibu yako yanapatikana kwenye mtandao.

 6. JEE SASA UMNAONA FAIDA YA WASOMI SEREKELINI WENZENU BARA WANAAJIRI WASOMI SIO WAMAKUNDUCHI. SASA WAMAKUNDUCHI NA WADONGE WASHAUZA NCHI NA BAHARI MUTAFANYA NINI

 7. Wakati wa kuchinjana ,chuki kejeli,masimango,na kufukuzana na kuchomeana moto baina ya watanganyika na wazanzibari unakaribia,na hii itawashtua watu maana hakuna salama tena,Kma imeshsfkia kudzu lumiana kiasi hiki na hakuna dalili zozote za kupata haki basi kilichobakia ni hujma tu.shenz taip wanafik wakubwa,pumbav.

 8. Hapa ni kiini macho kimefanyika yani cc znz hatuna viongozi wakitishwa kidogo tu wanalegeza msimamo wao yani cjui hata tufanyeje Ee mungu tusaidie

 9. Waswahili walinena ‘Pesa sabuni ya roho’ na humfanya mtu hata awe mgumu namna gani alainike. Wazanzibari hatukutegemea kama ndugu yetu msomi huyu ambae tulikua na imani nae anaweza kutugeuka kwa sababu ya marupurupu ya Baraza la wawakilishi. Sawa lakini mkae mkijua kua iko siku hayo marupurupu mnayoyalilia yatakutokeeni puani kwani mnaona wazi jinsi gani Zanzibar inavyopelekwa kwenye mila, desturi na maadili ambayo kwa asilimia 99 ya Wazanzibari hayakubaliki na nyinyi ambao tumewakabidhi hii dhamana ndio mnazidi kuinakamisha. Hivi hamuoni kama Tanganyika inaimeza Zanzibar? Kwani hilo eneo lingeombwa kwa jina la Zanzibar si bado lingekua ni la TANZANIA? Endeleeni kuiuza nchi rejareja ambapo mnaona wazi na kila dalili zinaonyesha kua sasa Unguja imekwisha. Iliyobakia ni Pemba nayo imo katika mpango wa kumalizwa mnakaa kimyaaa kwa sababu ya marupurupu ya shilingi milioni 4 kwa mwezi na kitita cha milioni zaidi ya 50 baada ya miaka 5.

 10. Nakubaliana na hoja ya hapo juu. Jawabu kuhusu ombi la jamuhuri ya muungano kuongezewa eneo la baharini kumbe linajuilikana na majibu yake yanajuilikana. Hakukuwa na haja seriakali kuashiria hailijui suala hili hapo lilipoletwa barazani kama ni hoja binafsi. Ikiwa sio maneno ya waandishi wa habari awalitwambia kuwa hata makamo wa pili wa raisi alisema kuwa hakuwa na taarifa ya suala hili ndio maana wananchi wakaamini kuwa Shamuhuna alienda kinyume na wenzake. Imefikia hadi makamo wa pili wa raisi wa Zanzibar kuliomba baraza liiwachie serikalai suala hili lizunguzwe kwenye baraza la mapinduzi na baadae serikali itakuja kutoa taarifa. Tumekuja kundua baada ya muda kumbe jibu lilikuwa linajuilikana..

 11. Jambo la ajabu ni kuwa hakuna mjumbe aliehoji kwa nini taarifa lililotolewa barazani kuhusu bahari kuu haikutolewa pale pale wakati ilpokuja hoja hii. Hii nikuwaweka wananchi waamini kuwa tunaendesha shughuli zetu kienyeji mno bila ya kuzingatia kuwa huu ni wakati wa sayansi na teknologia. Taarifa zipo wataalamu wapo wanaoelewa haya mambo kwa nini isielezwe mapema.

 12. kum ma zao serikali ni madhilimu na wanatuda ngaya na niwoongo wanafik wana firw…na hatuwasamehe duniani mpaka akera na SHAMUHUNA M/akuangamize wewe na wote mnao shirikiana kuiuza zanzibar kwa makafiri wa tanzania bara

 13. kama mambo ya Muungano hayajadiliwi hiyo Tume iishie Chumbe haina maana kuja Zanzibar kwani sisi upande wa Zanzibar kinachotukwaza ni MMUNGANO hatuutaki hata kuusikia. Kama haumo katika mjadala kikwete atunge katiba yake lakini ajue kua WAZANZIBARI HATUTAKI MUUNGANO HUU WA KIJINGA NA IKO SIKU UTAVUNJIKA TU.ATAKE ASITAKE YEYE NA CCM WENZAKE.

 14. Ndugu zangu Wajumbe hawa wamo kwewnye fungate ya “Umoja wa Kitaifa” ndomana kila waambiwalo husema haiwezekani. Kama umoja huu ulikuja kulinda ufisadi na mambo mengine basi bora Mungu aumalize. Watoto wetu ambaoo ni kizazi cha Facebook.com watapigana siku za mbele kisha wataunda umoja wa kweli. Huu umoja wa Baraza la Mawaziri ambao ni very ceremonial is doing more harm than good! Wawapi wanaokalipia kweli kweli Masheha wawanyimao Zanids vijana, Wawapi wakalipiao kweli kweli watu watumiao taasisi za Serikali vibaya miongoni mwao waliotisha mkutano wa CCM wakawalani UAMSHO ni nani asiejuwa kuwa miongoni mwao waliongoza usajili wa wanafunzi bomu Chuo cha Kiislamu mpaka ikawa issue pale. Serikali hii imekaa kimya ikitumia “wait and see approach”. Binadamu ni tofauti na mnyama akifanya kosa usipomuanya huamini kuwa yu sahihi. Tujirekebishe

 15. HAYA NI MAPAMBANO WATANGANYIKA NA RAISI WAO KIKWETE WANAFAIDIKA MNO NA MUUNGANO ULIOPO SASA KUPITIA JUU YA MGONGO WA ZANZIBAR. NDO MAANA WAO HUWASIKII WAKILALAMIKIA MUUNGANO HUU. WANAOUMIZWA NA MUUNGANO HUU MBOVU NI ZANZIBAR LAKINI VIONGOZI WETU WAKO KIMYA KWA SABABU WAO NA FAMILIA ZAO KULA HAIWAPI TABU. SISI WANANCHI NDIO TUNAOUMIZWA NA MUUNGANO HUU MBOVU NA TUNASEMA WAZI KUA HATUUTAKI NA LAZIMA UJADILIWE. VIONGOZI WA ZANZIBAR WANAJUA KUA WANAOFAIDIKA NA MUUNGANO NI TANGANYIKA NDO MAANA KIKWETE KAMA MTANGANYIKA NASEMA USIJADILIWE. HILI HALIKUBALIKI NA VIONGOZI WA ZANZIBAR MJUE KUKAA KWENU KIMYA JUU YA HILI TUNAAPA UCHAGUZI UJAO NYOTE TUTAWANG’OA. HIVI NANI KAMA SIO WAZANZIBARI AMBAO NDIO UPANDE WA PILI WA MUUNGANO WAUJADILI MUUNGANO? KAMATI YA KERO AMBAYO NI YA CCM? WAJUMBE WOTE NI KUTOKA CCM 1)BILALI 2)SEFU IDDI 3)SAMIA 4)MOH’D ABOUD MNACHOKIFANYA NI KUTEKELEZA SERA ZA CCM AMBAZO LENGO LAKE NI KUONA KUA ZANZIBAR INAFUTIKA KATIKA RAMANI YA DUNIA. TUNAKWAMBIENI KUA NYINYI PAMOJA NA CHAMA CHENU NI MAADUI WAKUBWA WA ZANZIBAR NA VIBARAKA WA TANGANYIKA KATIKA KUIKANDAMIZA ZANZIBAR LAKINI KWA UWEZO WA ALLAH HAKI ITATAWALA NA BATIL ITAANGAMIA NA JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR ITASIMAMA TU MTAKE MSITAKE KWANI M/MUNGU YU PAMOJA NA WANAOLINGANIA DINI YAKE.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s