SMZ yaiandikia barua SMT kuhusu mafuta

Waziri anaeshughulikia mambo ya Muungano Samia Suluhu

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshawasilisha barua rasmi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kutaka kutolewa katika orodha ya mambo ya Muungano suala la mafuta na gesi asilia. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame aliwaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi jana wakati akijibu masuala katika kikao hicho ambapo alisema Waziri Mkuu wa Tanzania ameahidi kulipeleka mbele suali hilo.

Waziri huyo alisema licha ya vikao vya kujadili kero ya Muungano vikiwa vinaendelea lakini yapo baadhi ya mambo ambayo utatuzi wake unahitaji baraka za viongozi wa kuu wa nchi na sio vikao vya kamati.
Hayo yameelezwa Dk Mwinyihaji katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin aliyetaka kujua masuala la kero za Muungano zimefikia wapi aktika kutatuliwa.
Katika suali lake Mwakilishi huyo alitaka kujua lini kero za Muungano zinaendelea kujadiliwa zitamalizika hasa kwa kuzingatia kero hizo zinazidi kushamiri kila kukicha na wananchi wamekwua wakiwatizama viongozi wao
Waziri huyo alisema vikao vya kujadili Muungano chini ya Uenyekiti wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muiungano wa Tanzania, vinaendelea kujadili mambo mbali mbali yanayouathiri Muungano.
Dk Mwinyihaji alisema vikao hivyo vinavyowashirikisha mawaziri na yapo baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na kufikiwa maamuzi na yapo yanaendelea kujadiliwa kupitia vikao hivyo vya kutatua kero za Muungano.
Waziri alisema yapo baadhi ya mambo tayari yalifipatiwa ufumbizi lakini pia yapo yanayohitaji uamuzi wa viongozi wakuu ambao uamuzi wake hadi wakutane vikongozi wa ngazi za juu kutokana ukubwa wa masuala hayo.
Awali akijibu suali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Mpendae (CCM) Mohammed Said Mohammed alietaka kujua Zanzibar inawezaje kuyasimamia yenyewe kama nchi kwneye jumuiya ya Afika Mashariki mambo yasiokuwa ya Muungano, Waziri alisema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeainisha kuwa mambo ya nje ni moja kati ya mambo ya Muungano.
“Nakubaliana na Mwakilishi kuwa katika shughuli za ushirikiano wa kikanda kuna mambo ambayo sio ya Muungano kama vile elimu ya msingi na kati, kilimo n.k serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imekuwa ikishirikishwa kikamilifu katika mambo yote ya ushirikiano wa kikanda” alisema Waziri huyo.

Alisema maslahi ya Zanzibar yanalindwa ipasavyo katika ushirikiano wa kikanda ambapo jamhuri ya muungano wa Tanzania ni nchi mwanachama.

BAABARA ZALETA MANUFAA
WAZIRI wa Afya Zanzibar, Juma Duni Haji amesema manufaa makubwa yamepatikana tangu kuanzishwa maabara ya utafiti iliyopo Wawi, Kisiwani Pemba.
Waziri huyo alieleza hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu suali la Mwakishi wa Jimbo la Muyuni (CCM) Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua tangu kuanzishwa kwa maabara hiyo serikali imenufaika vipi na utafiti unaofanywa katika kituo hicho.
Waziri Duni alitaja manufaa yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa maabara hiyo ni pamoja na kuwa maabara ya rufaa kwa utambuzi wa ugonjwa wa kifua kikuuu.
Alisema wakati ilipoanzishwa maabara hiyo miaka 11 iliyopita serikali ilitakiwa kuchangia milioni 30 kwa mwaka ili kuendeleza taasisi hiyo na kwa vile mradi wa wizara umewekwa kwenye miradi ya maendeleo na huombewa fedha kila mwaka.
Akijibu suali ni kiasi gani serikali inachangia kwa mwaka katika baabara hiyo ya utafiti iliyopo Wawi, Duni alisema kiasi cha fedha wanachopewa hutegemea kupatikana kwa fedha hizo za mgao wa miradi ya maendeleo ambapo serikali inalipa mishahara ya wafanyakazi katika taasisi hiyo kwani ni waajiri wa wizara.
Aidha waziri huyo alisema kwa kushirikiana na mradi wa malaria, maabara imekuwa ikihakiki vipimo vyote vilivyoonekana na vimalea vya maradhi hayo.
“PHL – Idc ni maabara tegemezi kwa kuangalia maradhi ya kuambukiza hasa kipindupindu kisiwani Pemba”, alisema waziri huyo.
Waziri huyo alibainisha kuwa maabada hiyo imekuwa nguzo muhimu katika kuyafanyia uchunguzi maji (biological analysis), kutoka vyanzo mbali mbali na kuishauri ZAWA juu ya namna ya kuyasafisha.
Alisema tafiti za mashuleni ziliweza kuibua miradi juu ya minyoo na kichocho na ilisaidia wananchi ikiwemo kutoa dawa za minyoo na kichocho kwa wanafunzi mbali mbali kwatika shule tofauti.
Akijibu suali la kuwepo malalamiko kuwa serikali haitoi mchango wake kwa kuzingatia muda muafaka wakati wa wizara ya afya inaidhinishiwa fedha za baraza kila mwaka kwa ajili ya taasisi ya utafiti ikiwemo maabara hiyo, Duni alisema taasisi kupitia mradi wa IDCF wanasaidia mradi wa mama na mtoto katika kituo cha Gombani kwa majengo. Dawa na huduma za ufuatiliaji kina mama na watoto vijijini.
Alisema kitengo cha upasuaji wamepata vifaa, vitendea kazi na mafunzo kupitia IDCF na kwamba PHL-IDC kupitia miradi yake mbali mbali kinatoa ajira mbali mbali za muda mfupi na muda mrefu kwa wanachi wa Zanzibar na Tanzania.
Alisema alisema kuwa tangu maabara hiyo kuanzishwa, serikali imekuwa ikiwapatia mishahara wafanyakazi wa maabara hiyo kwani ni watumishi wa umma wanaopaswa kulipwa.
Akijibu suali jengine la Mwakilishi huyo huyo Jaku Hashim Ayoub wa Jimbo la Muyuni (CCM) aliyetaka kujua serikali ina mpango gani wa kuifanyia ukarabati hospitali Chake Chake, Duni alisema hospitali ya Chake Chake ambayo imekuwa tegemeo kubwa kwa wananchi wa Pemba itafanyiwa ukarabati chini ya awamu ya pili ya mradi wa ADB.
Waziri wa Afya alisema hali ya hospitali ya Chake Chake inahitaji kufanyiwa ukarabati kila baada ya muda au yatakapotokea mahitaji ya kufanya hivyo.
“Katika mradi wa ADB katika awamu ya pili ya kuboresha huduma za afya Zanzibar hospitali ya Chake Chake inategemewa kufanyiwa marekebisho makubwa” alisema waziri huyo.

Alisema serikali imejiwekea utaratibu wa kuzifanyia ukarabati hospitali zake kila inapohitajika ambapo kamati maalum huangalia majengo ya wizara hiyo.
Akijibu suali la kupeleka wauguzi Kisiwani Pemba, Waziri alisema serikali kuamua kupeleka wafanyakazi Pemba haimaanishi kwamba tatizo limekwisha.
Alisema uhaba wa wafanyakazi bado upo kutokana na kuwa waliopelekwa ni kidogo kuliko mahitaji ya wauguzi wanaohitajika, na kutokana na tatizo hilo wagonjwa wanachukuliwa dawa zao kutoka katika vituo vya kupokea dawa au kama hazipo kununuliwa nje ya hospitali na kukabidhiwa mgonjwa.
“Mheshimiwa Spika hilo sio jambo geni kuchukua dawa katika hospiatli za nje kwa sababu wagonjwa hao hao hupewa dawa na maeleekezo ya kutumia kwa wagonjwa wa nje” alisema Waziri Duni.

MIRADI ISIYOZINGATIA WALEMAVU
NAIBU wa waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi amekiri kuwepo kwa miradi ya ujenzi isiyotoa umuhimu unaostahiki kwa jamii ya watu wenye ulemavu.
Naibu huyo alieleza hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, alipokuwa akibu suali lililoulizwa na Raya Suleiman Hamad.

Naibu huyo alisema suali la ulemavu ni mtambuka hivyo serikali itaendelea kuhakikisha kuwa ufumbuzi wa matatizo hayo yanapatikana.

Akizungumzia suala miundombinu ya barabara kutozingatia hali za walemavu, alisema wizara yake inasubiri matokeo ya uchambuzi na uchunguzi unaoendelea kufanywa na Benki ya Dunia kwa barabara za mjini.

Alitoa wito kwa madereva na watumiaji wa wengine wa barabara kuheshimu sheria ili kufanikisha utekelezaji wa matumizi ya barabara.

Alisema katika utaratibu wa kuziheshimu sheria ni pamoja na kuwapa nafasi ya matumizi ya barabara kwa walemavu wenye kutumia fimbo nyeupe hasa katika maeneo ambayo barabara imetiwa zebra.

Wakati huo huo, Wizara hiyo imeeleza kwa kupitia shirika la Bandari upo mpango wa kuijenga banadari ya Mkokotoni ili iweze kutoa huduma kwa vyombo na mizigo.

Naibu waziri alisema katika kutimiza azma hiyo tayari shirika la banadari imeiomba kampuni ya Road and Bridge ya nchini China kuifanyia utafiti wa namna bora ya ujenzi wa banadari hiyo na gharama zinazohitajika.
KITUO CHA MAFUNZO KUJENGWA
NAIBU wa Waziri wa Elimu na Mafunzo, Zahra Ali Hamad amesema kituo cha mafunzo ya Amani kisiwani Pemba kitajengwa kupitia awamu ya pili ya mradi wa elimu mbadala na amali.

Naibu huyo alilieleza Baraza la Wawakilishi linaloendelea na kikao chake alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambwe (CUF) Salim Abdulla Hamad alitaka kujua ni lini kituo cha amali kitajengwa hasa ikizingatiwa kwenye kampeni Rais wa Zanzibar alitoa ahadi hiyo.
Zahra alisema ujenzi wa kituo hicho utafanyika katika jimbo la Mtambwe utatekelezwa kwa pamoja baina ya serikali na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB).
Alisema mkataba wa makubaliano ua utekelezwaji wa mradi huo umeshatiwa saini na utekelezwaji utachukua miaka mitano kuanzia mwakani.
Naibu Waziri huyo alisema ujenzi wa kituo hicho bado haujazindiliwa rasmi hasa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu za kibenki ambapo unatarajiwa kufanyika baada ya miezi 15.
Alisema kabla ya kazi ya ujenzi kuanza, wizara ilitangaza zabuni ya kupata mshauri wa ujenzi ambaye atafanyakazi za tayarishaji wa michoro.
Aidha alisema baada ya hatua kukamilika itatangazwa zabuni ya mshauri wa ujenzi na baadae kutafutwa mkanadarasi atakayejenga kituo hicho.
“Wizara itatangaza zabuni ya kupata mshauri wa ujenzi ‘consultant’ ambaye atafanya kazi za utayarishaji michoro na mara michoro itakapokamilika, wizara itatangaza zabuni ya kupata mshauri wa ujenzi amabye atatangaza zabuni ya kumpata mkadharasi atakayejenga kituo hicho na vyengine” alisema Naibu Waziri huyo.
Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba taratibu za sheria za manunuzi ‘procurement’ ambazo zinatumika zitachukulia mwaka mmoja na miezi mitatu hadi kupatikana mkadharasi wa ujenzi.
Akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hija Hassan hija aliyetaka kujua wanafunzi wangapi waliofanya mitihani na walimu wangapi wameteuliwa kufanya kazi ya usainishaji mitihani, Naibu Waziri huyo alisema walimu walikuwa ni 333.

Alisema kwa mtihani wa darasa la saba kati yao walimu 325 ni wa skuli za Unguja na walimu wanane wa skuli za Pemba ambapo kwa uapnde wa mitihani ya kidato cha pili, walimu 417 walishiriki katika usahihishaji wa mitihani kati yao walimu 401 walitoka katika skuli za Unguja na walimu 16 walitoka skuli za Pemba.
Zahra akijibu kuhusu wanafunzi waliofanya mithani alisema wanafunzi wa skuli za Zanzibar waliofanya mitihani katika mwezi wa Novemba 2011 kwa darasa la saba walikuwa 23,798 kati yao wanafunzi 15,556 walikuwa wa skuli za Unguja na wanafunzi 14,642 ni wa skuli za Pemba.

Advertisements

2 responses to “SMZ yaiandikia barua SMT kuhusu mafuta

  1. Pingback: SMZ yaiandikia barua SMT kuhusu mafuta·

  2. Hapa naona kama tunadanganyana kuhusu suala zima la kero za Muungano. Kero hizi kwa nini ziwe ni za upande mmoja tu? Na siku zote washughulikiaji wakuu wa hizi kero ni Wazanzibari ambao ni VIBARAKA wa Tanganyika ambao hawawezi kufanya lolote kwa vile wamepewa nafasi hizo na Muungano. Kwa mantiki hiyo, kero hizo maisha hazitakwisha. Suala la msingi ni kua kero hizo kama wana nia ziishe basi wawaingize na watu wa upinzani ndani ya hizo kamati kwani wanaokerwa na muungano ni wazanzibari wote na sio wa chama tawala CCM tu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s